Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Always remember to take your medication son, vinginevyo watakuhamishia Mirembe.

Bichwa nzima bado ukoloni mamboleo unakuandama😕 kiswahili umeona hakitoshi? Hapa ndipo namkubali 2Pac aliposema "when I come 2u mother........ ck.
 
Kabla ya Bunge Maalum la Katiba, kuna mwenyekiti mmoja wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kinondoni, wanamwita bwana Paulo Makonda, aliitisha kiako na waandishi wa habari, bila kumung'unya maneno hivi alisema nini vile kuhusu Mzee Lowassa?
Kuonyesha kwamba alikuwa anamaanisha na hakuwa pekee yake, baada ya muda kadhaa akateuliwa kuwa mjumbe wa BMK.
Isitoshe akampopoa makofi mzee wetu kipenzi Jaji Mst. Warioba, kuonyesha hakuwa pekee yake akapewa dhamana ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama hapo hapo mjini kwenu.
 
Kwi kwi kwi mataahira banaaaaa, kama hamnazo ni hamnazo tu!

Bichwa nzima bado ukoloni mamboleo unakuandama😕 kiswahili umeona hakitoshi? Hapa ndipo namkubali 2Pac aliposema "when I come 2u mother........ ck.
 
Mi namshauri lowasa aanzishe Chama chake mbona wakina bashe , Hamisi mgeja wapo?
 
Jamaa atakufa akiukisa urahisi. Yani yeye ni ile ndoto yake ndio inamsumbua. Hii ndoto ni yake si ya watanzania. Anywe wiskey na brandy nyingi kupoza moyo. Uraisi asahau!
 
Ccm sio chadema ili mtu awe rais mpaka meja general mtei na bregedia wake mbowe waseme. Hii ni ccm maamuz yake yanafanywa na vikao. Chama cha lowasa ni ccm na atagombea ccm.kama ccm ni yako njiandae kumzuia ukishindwa hama ww au kubali maamuz ya vikao.
 
CCM mwaka huu lazima ipasuke tu, na tunalisubiri hilo kwa hamu kwa sababu ili kuwasambaratisha hawa kwa urahisi, kwanza wanyukane na kufarakana wao wenyewe!!

By the way, huyu jamaa (Lowassa) ndiye aliyebeba umoja wa CCM na kiukweli wapende wasipende ni lazima wampatie tu akitakacho, au la JK akubali CCM imfie na kumsambaratikia mikononi mwake.

Hili ni bomu ambalo CCM imeliandaa siku nyingi kupitia kwa huyuhuyu Mwenyekiti wao wa chama wa sasa na wakati wa kulipuka ni sasa!

Na ishu nyingine yenye utata na ambayo naamini lazima Kikwete amhofie huyu bwana na rafiki yake wa siku nyingi ni ile kashfa ya ufisadi wa kampuni kufua umeme ya Richmond. Taifa halikuwahi kuambiwa ukweli halisi wa skendo hii nzima ya Richmond hata kama jamaa alijiuzuru wakati huo na tukumbuke maneno ya jamaa wakati anajiuzuru......"kulinda heshima ya serikali na ya chama chake"

Ni wazi ukweli wa UFISADI WA RICHMOND alio nao ni Lowassa wenyewe na rafiki yake huyu huyu Jakaya Kikwete. Hili mimi naamini kupitia uchaguzi wa mwaka huu litafufuka na kuanza upya tu iwapo CCM wataendelea kumshikia mwenzao bango la ufisadi na wengine kujifanya wasafi sana!!

Kwa CCM vita iliyopo ni kati ya KUNDI KUBWA LA LOWASSA vs MAKUNDI MADOGO MADOGO YA WATIA NIA WENGINE vs KUNDI LA MWENTEKITI WA CCM TAIFA ambalo liko ktk dilemma na hilo ndilo litakalo amua nani awe nani.

JK na kundi hataweza kumtosa Lowassa kwa sababu akichagua njia hiyo ndiyo itakuwa angamio la CCM na sisi wengine kuzijua siri zote za Royal family hata zile ambazo zipo kama tetesi tu bila kuwa comfirmed!!....The question is that; Is he ready for that??

Tusubiri tuone
 
Kikwete alipoambiwa yeye ni DHAIFU alikasirika na kuona kwamba ametukanwa.

Lakini kauli hiyo angeichukua kama changamoto na kuifanyia kazi haya yote yasingekuwa yanampata leo.

Lowassa kwa kufahamu UDHAIFU wa Kikwete sasa ameamua kumtisha waziwazi kwa kutumia magazeti.

Kwamba yeye Lowassa ndiyo ALPHA NA OMEGA (read Yeye ndiyo plan A, B, C, D) bila yeye CCM wasahau kabisa kuingia Magogoni, kwani ataondoka na kundi lake kwenda UKAWA. Hata kama yeye hatakuwa mgombea lakini atauza kura zake kwa UKAWA.

Mathalani Kikwete angeifanyia kazi hiyo kauli ya UDHAIFU na kumchukulia hatua Lowassa mapema, haya yote yasingekuwa yanaikuta leo CCM.

Sasa JINI liko nje ya chupa kulidhibiti tena Kikwete hawezi. CCM wakubari kumsimamisha Lowassa lakini watokwe na jasho la damu kumnadi au Wamtupilie mbali Lowassa, lakini Lowassa auze kura zake kwa UKAWA.

Wazungu wanasema hiyo ni catch 22 situation kwa Kikwete. I can see CCM ikimfia Kikwete mikononi mwake. Hakuna wa kumlaumu ajilaumu yeye mwenyewe.
 
Kuna wakati ilisemwa kuwa huyu mzee (EL) "angepotezwa" kabla ya uchaguzi wa mwaka huu.

Bahati njema sana kwa wanamageuzi kwamba the guy is still alive na ambitions zake zilezile tena kwa sasa zikiwa juu juu zaidi.

Kuna mdau mmoja hapo juu amesema kuwa "watampoteza huyu" huyu mzee. Sina hakika anaamanisha kupoteza kwa maana ya ataondoka CCM au kumpoteza kwa maana ya kunyang'anywa uhai wake (kuuwawa).

Kama ni kwa maana ya kumuua, kwa sasa ni IMPOSSIBLE na nadhani ina risk kubwa zaidi kuliko hata kumtosa tu (kutokumpatia nafasi ya ugombea Urais kupitia chama chao)

Mimi kwa mtazamo wangu na kwa namna jinsi jamaa alivyo na nguvu za kisiasa ndani ya CCM, iwapo ataingia ktk mchakato wa kawaida kuwania uteuzi wa chama ili kuwania tiketi, ni lazima atawabwaga wenzake wote!!...EL mwenyewe anajua hili, wafuasi wake wanajua hili, wapinzani wake ndani ya chama wanajua hili na CCM kwa ujumla wanajua hili!!

Hofu ya CCM ni namna ya kuja kumuuza kwa wananchi (voters) kwa sbb ya trails ya kashfa zinazomwandama yeye hasa ile ya Richmond ambayo kwa kweli hatujui ni kwa namna gani amejipanga kujisafisha ili umma ujue na uamini kuwa hakuhusika!!

Hili ndilo tatizo linaloiandama CCM na kwa mtazamo wao wanadhani kuwa EL ndiye fisadi pekee, kumbe kwa sisi huku nje tunajua kuwa CCM wote (the whole system) ya chama na serikali ni mbovu, imeoza!!
 

Kweli kweli nawambieni,Lowassa atastahili kupewa nishani ya ushujaa wa mchi yetu kama atahamia UKAWA. CCM itakuwa imevua gamba, na UKAWA watakuwa wamempata mwana mpotevu. Good riddance! WM
 



Hapo kuna shida gani kama Lowassa akikubaliana na ukawa kugombea uraisi?
Sio jambo la ajabu kwa wanasiasa au vyama kuungana.Hii ilishatokea Kenya vyama viliungana na kuangusha chama tawala cha KANU.Pia huko Israël,Ariel Sharon aliwahi kuhama chama chake cha likud likud na kuanzisha chama kingine cha kadima na kushinda uchaguzi. Pia Huko Malawi Raisi Bingu wa Mutharika alishawahi kuhama chama tawala, kuanzisha chama chake na kushinda uchaguzi. Haya mambo yapo na yanafanyika si kitu cha ajabu !
 
UKAWA, hamna mgombea, mko masikio na mimacho yote Dodoma, kama fisi msubiria mkono udondoke...mtasubiri sana, hamchagui mgombea wenu wa Urais, kumbe mnamsubiria Lowassa akiachwa tu na CCM, mnamchukua juu kwa juu...

Mnapoteza muda, CCM sio wapuuzi kiasi hicho, wanajua Lowassa ni lulu, dhahabu kwa sasa, fanyeni mipango yenu mmlete mgombea wenu...mnakaa hamchagui mgombea wenu wa Urais mnamsubiri Lowassa, eeehh..so funny...!!

Fanyeni yenu, sisi CCM tunafanya yetu...ila sorry, nisitukane wakunga na uzazi ungalipo, ikiwa CCM watamwacha Lowassa, UKAWA TUTAKUWA PAMOJA...ur my brothers and sisters..tuko pamoja ikiwa tu CCM itaenda kinyume na kipenzi cha wengi....Na ITAKUWA MWISHO WA CCM...hili liko wazi, so sijawapuuza ila ni UTANI WETU WA JADI...so UKAWA ENDELEENI KUTUSUBIRIA maamuzi yetu ya CCM, na nyie ndio muamue...

Vivaaa Lowassa...2015 huna hata mpinzani
 

Mamaaaaaa Aminaaaa.......! Ngoja nikatafute kigodoro na matarumbeta fasta kunogesha hii singo
 
lowasa si chochote ndani ya ccm, asisubiri kuachwa atoke tu hata sasa na ccm itapeta kama kawa, heri ya nusu shari kuliko shari kamili, lowasa ni shari kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…