Ni dhahiri kabisa CCM wameingiwa na hofu kubwa sana baada ya kugundua kuna uwezekano wa UKAWA kuimarisha wigo wa ushirikiano kwa kumjumuisha Zitto Kabwe na ACT yake.
Viongozi wa Chadema wamekuwa wakitamka na kufanya mengi ambayo more often than not yamekuwa construed kama “uchochezi, uvunjifu wa amani, kukiuka sheria, nk”. As a result, tumeshuhudia kamata kamata za uonevu mkubwa dhidi ya viongozi na wanachama wa chama hiki.
Wakati viongozi wa Chadema wakiwa wanapata treatment hiyo kutoka kwa CCM na serekali yake, imedhihirika kuwa Zitto hakumbwi na kashi kashi kwa kiwango hicho pamoja na ukweli kwamba huwa anatoa matamko ambayo mara nyingi yanakuwa even harsher kuliko hata ya viongozi wengine wa upinzani.
Mnyetishaji mmoja ndani ya Lumumba (ambaye inasemekana yupo CCM ya kina Nape, January, nk) ametoboa siri nzito kuwa huu ni mkakati mahususi wa kutaka kudhoofisha uhusiano unaoanza kuchipuka kati ya UKAWA (hususani Chadema) na ACT ya Zitto. CCM wamedhamiria kupandikiza mbegu ya mashaka kwenye mind ya viongozi wa Chadema eti wajiulize “ kwanini Zitto hafanyiwi kama sisi, lazima atakuwa anatumiwa na CCM kutuhujumu!!”
Chanzo: mnyetishaji ndani ya CCM (Lumumba).
My take:
UKAWA (Chadema in particular) msikubali kabisa kabisa kabisa njama hizi ovu za CCM za kuwatenganisha wapinzani kama walivyofanya kupitia kwa yule propesa Lipumba.
Umoja wa wapinzani wote (incl Zitto) ni silaha mojawapo muhimu sana katika kufanikisha crusade hii dhidi ya ukandamizaji wa demokrasia.