Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Kisangura, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, ameendelea kuzigusa na kuzifikia familia mbalimbali katika kata yake kwa kushiriki nao upendo kupitia utoaji wa elimu ya kukabiliana na uhalifu pamoja na msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji ya shule.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkaguzi wa Polisi Genuine Kimario amebainisha kuwa, kutokana na ushirikiano na uwajibikaji mzuri wa wananchi wa kata hiyo, amejijengea utaratibu wa kushiriki nao pale anapopata baraka au msaada wowote, kwa kuugawa kwa wananchi wanaohitaji.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wananchi wa Kata ya Kisangura kuendelea kuuchukia na kupinga vitendo vya uhalifu ili kujiletea maendeleo wao binafsi na familia zao. Aidha, amewahimiza wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati ili kuhakikisha kata hiyo inaendelea kuwa shwari na salama wakati wote.