Mkaa VS Gesi

Gesi ni nishati ya bei rahisi sana ukilinganisha na Mkaa.

Nitolee mfano wa familia yangu::
Kukiwa hakuna gesi, hutumia mkaa wa sh 2000/= kwa siku, ambao ni wastani wa sh 60000/= kwa mwezi.

Lakini ninunuapo gesi ya Oryx kilo 15 kwa takribani shilingi 48000/=, hukaa kwa muda wa miezi miwili mpaka mitatu. Ambayo kwa wastani ningetumia mkaa ingekua ni kati ya 120,000/= - 180,000/=.

Japo ugumu wa gesi ni kuchemshia vitu vigumi mfano maharag n.k ambavyo kwangu mimi hununua mkaa hata wa 2000/= na vitu husika vikaCheshwa vingi na kuhifadhi kwa friji.

Kiujumla gesi + friji ni gharama nafuu sana.
1. Ongeza usafi
2. Muda... Mkaa hadi ukolezee....
3. Mkaa ukibaki ni loss tayari
4. Gesi moto mara moja...
5. Mara mkaa wa mwembe, siju mkorosho inawaka kama mabua

Gesi ni far better than mkaa
 
Gesi mnayoizungumzia ni kwa matumizi ya familia za mjini au hata kijijini?
Maana kuna utofauti mkubwa kati ya maisha ya mjini na kijijini
 
Gesi ni nishati ya bei rahisi sana ukilinganisha na Mkaa.

Nitolee mfano wa familia yangu::
Kukiwa hakuna gesi, hutumia mkaa wa sh 2000/= kwa siku, ambao ni wastani wa sh 60000/= kwa mwezi.

Lakini ninunuapo gesi ya Oryx kilo 15 kwa takribani shilingi 48000/=, hukaa kwa muda wa miezi miwili mpaka mitatu. Ambayo kwa wastani ningetumia mkaa ingekua ni kati ya 120,000/= - 180,000/=.

Japo ugumu wa gesi ni kuchemshia vitu vigumi mfano maharag n.k ambavyo kwangu mimi hununua mkaa hata wa 2000/= na vitu husika vikaCheshwa vingi na kuhifadhi kwa friji.

Kiujumla gesi + friji ni gharama nafuu sana.
Umeongea vyema mkuu, ila apo kwenye maharage ukiweza nunua presure cooker inasaidia sana kwa vutu vigumu.
 
Ni ufahamu tu. Lakini gesi ni rahisi sana. Ila sema haipiki maharage
Issue iko hivi, mkaa unapendwa kwa sababu mtu ananunua buku kapika siku imeisha. Watu hawana elfu 45 ya kununua mtungi mzima au 20 ya kale kadogo. Sio kwamba hawapendi, hawana accumulated income. Maisha ya kuunga unga unapata buku 5 kwa siku unakula unalala.
 
Jumlishana matumizi ya umeme mkuu, au ni friji ya mafuta? Nayo pia weka gharama zake hata kama ni kidogo.
Otherwise uko sawa.
Gesi ni nishati ya bei rahisi sana ukilinganisha na Mkaa.

Nitolee mfano wa familia yangu::
Kukiwa hakuna gesi, hutumia mkaa wa sh 2000/= kwa siku, ambao ni wastani wa sh 60000/= kwa mwezi.

Lakini ninunuapo gesi ya Oryx kilo 15 kwa takribani shilingi 48000/=, hukaa kwa muda wa miezi miwili mpaka mitatu. Ambayo kwa wastani ningetumia mkaa ingekua ni kati ya 120,000/= - 180,000/=.

Japo ugumu wa gesi ni kuchemshia vitu vigumi mfano maharag n.k ambavyo kwangu mimi hununua mkaa hata wa 2000/= na vitu husika vikaCheshwa vingi na kuhifadhi kwa friji.

Kiujumla gesi + friji ni gharama nafuu sana.
 
Ni ufahamu tu. Lakini gesi ni rahisi sana. Ila sema haipiki maharage
Hata maharage inapika vizuri tu sema labda hujui unapikaje,mchawi wa matumizi bora ya gas ni sufuria iitwayo pressure cooker,nusu saa tu maharage unakula!
 
Ndugu wali wa kupikwa na gas hauna radha hila wa mkaa ni mtamu sana asikuambia mtu mkaa unapika fresh
Labda ww mwenyewe tu haujui kutumia jiko lako la gas kupikia wali.binafsi ni mwaka wa 7 huu natumia gas pekee kwa vyakula vyangu vyote ktk level ninayoihitaji na haijawahi kuniangusha.
 
Gesi ni rahisi asikwambie mtu, Nina uzoefu wa nishati zote mbili, mkaa na gesi. Nikiwa nyumbani kwa wazazi matumizi ya mkaa kwa mwezi ilikuwa gunia mbili kwa mwezi @sh 35,000. Tena gunia si za kitoto ni zile za lumbesa. Lakini baada ya muda teknolojia ya gesi kutamalaki maeneo mengi nchini mama akajaribu kubadili, akanunua gesi tena mtungi mdogo tu wa 20,000 anapika kila kitu hadi maharage, ajabu ulikaa wiki mbili, hivyo alinunua miwili kwa mwezi jumla sh 40,000. Mi binafsi watoto wapo boarding nikinunua gesi ya sh 48,000 itakaa miezi sita nikinunua mtungi mdogo utakaa miezi mitatu, wakati hapo awali nikinunua mkaa wa sh 2,000 kila siku,

Cha kufanya
Kampuni za gesi ziwe wabunifu kuongeza wateja, ningekuwa afisa masoko ningeteua hata wilaya moja, kupita wenyeviti wa mtaa nikawasajili wamama/baba mtaa wanahitaji mtung but hawana kianzio nawakopesha mtungi complete wateja, mfano mtungi mmoja unauzwa sh 70,000 mtz hamudu, badala yake muuzie huo mtungi was sh 70,000 ndani ya kila wiki kachukue 10,000 kupitia magariyanayoabaa gesi mtaani, baada ya wiki 7 deni lemeisha mtungi ni wake. Kwani kampuni za soda zinafanyaje? Wanakupa hadi friji tena ya thamani wanajua utauza tu soda zikiwa za baridi, ..gesi sio ghali tatizo kununua complete mtungi,
 
Gesi ni bora na rahisi kwa watu wenye kipato cha kati lakini gesi ni bora ila siyo rahisi kwa watu wenye kipato cha chini, kwa mfano; kuna familia unakuta kwa siku wana uwezo wa kununua mkaa wa mia tano tu ambao hupika siku nzima kwa kujibana sana, hatahivyo hakuna gesi ya 500. Utambue kuwa watanzania wengi wana kipato cha chini na hawawezi kukusanya elfu 21 au 22 ya kununulia gesi ya mitungi midogo kila inapoisha ila wanauwezo wa kubahatisha 500 ya kununulia mkaa.
Tumekuwa tukitumia gas cooker, nakumbuka mzee wangu alikuwa akinituma kununua gas kwa sh100 (noti nyekundu) ile mitungi/vichwa vya Agip na Afrigas.
 
Back
Top Bottom