Sipendi kuonekana mbaya kwenye maisha

Status
Not open for further replies.

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
174
618
Lakini ili la leo limenisikistisha zaidi, though muhusika nimemuelekeza huku nacheka, kuna staff mwezangu anafikaga kuiacha familia yake home kwangu mimi naishi karibu na maeneo ya kazi, dah wananipa mazingira magumu sana jamani.

Tuliwaigi kufanya dili la elfu 60,000 yeye ndo alifanya dili zima, na mimi ndo nilikuwa source ya iyo ela,bila Mimi ingeshindikana kwaiyo tukagawana elfu 30 per mtu. tumegawana kama Leo kesho yake akaniambia nimuazime elfu 20 katika ile tuliyogawana mimi nikampa elfu 10 nikamwambia elfu 20 nimeitumia.

Nasemaje hela kaiazima tangu mwezi wa saba hadi leo ajanipa, na anafika home kwangu kila siku kuacha familia na wala hazungumzii ile ela ambayo nilimuazima, gesi yangu wanatumia kupikia chakula asubuhi chai mchana wanajua wao wanachopika maana mimi huwa nakuwa kazini japo narudi kula saa nne.

Viberti wananimalizia, niliwanunulilia vya gesi mara mbili wameviharibu kule juu kwa kutachia, vimepasuka vyote haviwaki tena, nilinunua vya gesi kwasababu utakuta kiberiti umekiacha kipya Asubuhi ukirudi kazini jioni kimebaki nusu, sijui binti hawezi tumia gesi ivyo inamlazimu kutumia njiti nyingi hata sielewi.

Nikaanza kuwawekea vya gesi labda vitakaa hata siku mbili havijamaliza vimepasuka vyote juu pakuwashia, na viberiti vikiisha hawanunui wao ni kutumia tu, sukari yangu wanatumia ikiisha wanasubiri niweke tena.

Kuna mkaa niliacha pindi nimesafiri pamoja na gesi vyote niliviacha mana niliwaachia funguo nimekuta mkaa wamebeba nyumbani kwao, wakaniambia ule mkaa tulichukua kwenda nao home tulienda kupikia maharage, kama kawaida nawachekeaga tu nawaambia sawa haina shida, na hapa gesi inaelekea kukata nilitegemea atasema tuchangiane lakini yupo kimya tu.

Kilichonikera leo binti yake anayemwachia mtoto kachukua ndoo ninalowekea maji ya kunywa dogo kamuingiza mtoto na kuanza kumuogeshea mule ndani ya ndoo nimepatwa na hasira lakini kama kawaida yangu nimemwelekeza binti huku nacheka huku moyoni nina hasira na macho yalojaa machozi.

Nimemwambia kistaarabu siku nyingine chukua besenii Dada lile ninalofulia umwogeshee mtoto, japo najitahidi kumuelekeza kila Siku, kuna siku nikamkuta anachukua kopo ninaloogea anakinga maji bombani amwagie mtoto eti mtoto anasikia joto, anachota maji bombani yale ya kwanza kabisa kutoka yanakuaga na moto kwasababu sasa hivi kuna jua Kali nikamwambia Dada usitumie ilo kopo sio nzuri ni chafu, infact ni chafu usiku nakojoleaga halafu naliosha nilimwambia tu chafu though sikumwambia chafu kwanini.

Sasa na mama mtoto nae ambae ni mfanyakazi mwezangu kuna siku nae kachukua sufulia lenye chakula ndani kaliingiza ndani ya beseni ambalo huwa nafulia nguo za ndani na za kawaida pia kupooza chakula cha mtoto ndani ya dishi kaweka maji ili chakula kipoe haraka na anajua nafuliaga nguo, na anamlisha mtoto viazi vya kupondwa hata miezi sita ajatimiza anampondea viazi anamlisha akiona watu wanapita anakificha kile chakula.

Mimi sikumkataza asije ona kama staki atumie vitu vyangu japo naweza kuwa sahihi, kwasabu mtoto ni mdogo sio sawa kushare vyombo na watu wazima, ukijifanya mjuaji mnaweza gombana bure mi naishiaga kumuangalia tu! Kwasababu sio mtoto wa kwanza kusema anajifunza kulea hapana, aisee naitamani likizo nirudi mkoani nikapumzike tu!
 
Last edited:
Kwanza kwa nini mpaka wakuletee wewe nyumbani kwako watoto?. Kuna mambo mengine hata kama urafiki isiwe ule urafiki wa kumkera mwingine. Mwambie wazi usilete watoto kwangu au funga mlango tembea. Kama unashindwa vyote kama umepanga hama hapo. Hivyo vitu vidogo,watakuja kufanya kitu kikubwa kama kuunguza nyumba. Wahi kabla ya hatari
 
Mtoto mdogo hawezi muacha home bado ananyonya ajatimiza miezi sita sina urafiki nae Mimi ni work mate tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom