Mjusi anayeruka Dunia imekwisha jamani

Mjusi anayeruka Dunia imekwisha jamani

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,071
Reaction score
34,840
dragon.jpg
While participating in a herpetology study we stumbled across this female laying eggs in a nest. She was found in the Lambusango Forest reserve
 
mkuu ina maana kama wanasayansi wangemgundua popo sasa hivi ungesema dunia imeisha?..nadhani ni viumbe wa mwenyezi Mungu tu hawa na wengi wengi tu hatuwajui
Ni kweli lakini mwisho wa dunia kunatokea mambo mengine ya ajabu hatujawahi kuyaona maishani mwetu Mkuu hii ndio Dalili ya Mwisho wa Dunia.
 
Ya kawaida tu Mkuu hayo. Mbona kila siku wanasayansi wanagundua viumbe vipya. Pendelea kuangalia NAT GEO CHANNEL au Animal Planet au DISCOVERY. Utaona maajabu ya viumbe duniani.
 
pia kuna nyoka warukao toka mti mmoja hadi mwingine. ni jambo la kawaida.
 
Mbona Mlima kilimanjaro au ziwa victori lilipogunduliwa,ukusema mwisho wa dunia umekaribia?
 
Hakuna cha ajabu chochote, mjusi anaruka na ana mabawa cha ajabu nini?!. Jee ungewaona nyoka warukao na hawana mabawa ungesemaje?!

Wewe google "the world of strange powers" uone mambo ya ajabu ya kweli!
 
acha woga binadamu tunachelewa kugundua mambo kwa ajili ufupi wa akili yetu tofauti na mungu,mbona bado vingi tu?
 
Kwa nini usishangazwe na vijidudu vya ukimwi ambavyo ni vidogo mno kuonekana na darubini za kawaida na vinatumaliza.
Kama huna habari kuna nyoka wanaoruka pia.
 
Nenda kule milima ya bihawana wakati wa kiangazi wako wengi sana!

hata mimi nashangaa yaani mambo ya miaka zaidi ya milioni iliyopita we ndo unajua leo. Kwa taarifa yako na ndio uhusiano uliopo kati ya ndege na reptile ulipoanzia hapo. si unaona magamba kwa ndege na nyoka! Ukimla ndege-kuku,kanga na wengineo- ujue unamla ndugu yake huyo mjusi. Uamuzi ni wako uendelee kula chips kuku au chips kavu!
 
WENGINE NAONA Mnashangaa mambo ya wanasayansi hao, wenzetu wamezekeza sana ktk utafiti. Hakuna cha mwisho wa dunia wala mdogowake mwanzo wa dunia. ondoa uoga wako
 
mkuu ina maana kama wanasayansi wangemgundua popo sasa hivi ungesema dunia imeisha?..nadhani ni viumbe wa mwenyezi Mungu tu hawa na wengi wengi tu hatuwajui

Teh teh teh. Nadhani mleta mada alikwepa somo la biolojia akiwa sekondari.
Kuna wanyama wakiwemo mamalia na reptilia, wana kawaida ya kuruka hewani. Kuruka huku ni kwa namna mbili, 'Flying' na 'gliding' Flying ni kama vile arukavyo popo na 'gliding' ni kama vile anavyofanya huyo mjusi pichani na baadhi ya jamii ya cheche (gliding squirrel). Hawa wanaruka toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutanua ngozi iliyo mbavuni mwao ambayo huwasaidia kuelea hewani. Ngozi hii inafanana kabisa na ile ya popo. Kuna nyoka pia wenye mfumo kama huo, sijajua wanaitwaje! Nimeeleweka nadhani
 
Mimi huyo mjusi nilimfahamu tangu nasoma biology of reptiles ya Prof Howell pale mlimani miaka 24 iliyopita
 
hamna cha ajabu hapo!dunia ipo na itaendelea,timiza wajibu wako uliokuleta hapa duniani.
 
Back
Top Bottom