Mjusi anayeruka Dunia imekwisha jamani

Acha woga. Bado viumbe wengi hatujawahi kuwaona.
N kama vile Majini na mashetani baadhi ya watu hawawajui.

Ya kawaida tu Mkuu hayo. Mbona kila siku wanasayansi wanagundua viumbe vipya. Pendelea kuangalia NAT GEO CHANNEL au Animal Planet au DISCOVERY. Utaona maajabu ya viumbe duniani.
Ni kweli lakini si unajuwa sisi wengine hatukuenda shule.

anaruka au anapaa?
kuruka na kupaa yote sawa Mkuu

acha uoga kijana hiyo ni kazi yake mola. tatizo unadhani viumbe wote ktk ulimwengu huu wanajulikana.
Hakuna cha woga kuna baadhi ya Watu ukiwaambia kuna Viumbe wanaoitwa kwa jina Mashetani

Hakuna cha ajabu chochote, mjusi anaruka na ana mabawa cha ajabu nini?!. Jee ungewaona nyoka warukao na hawana mabawa ungesemaje?!Na Mkiambia kuwa Kuna Mashetani na Majini Mnbasema Hamjuwi Ohhhh Waislam wanafuga Majini hahahah mimi nimefanya hivyo kutaka kuwapima Watu akili zenu je mkiambia kuwa kuna Viumbe wanaoitwa Majini na Mashetani.

Wewe google "the world of strange powers" uone mambo ya ajabu ya kweli!
ok Asante

Kwa nini usishangazwe na vijidudu vya ukimwi ambavyo ni vidogo mno kuonekana na darubini za kawaida na vinatumaliza.
Kama huna habari kuna nyoka wanaoruka pia.[/QUOTENinajuwa Sana je unajuwa kuwa kuna Viumbe wanaoitwa Mashetani?na Majini?

WENGINE NAONA Mnashangaa mambo ya wanasayansi hao, wenzetu wamezekeza sana ktk utafiti. Hakuna cha mwisho wa dunia wala mdogowake mwanzo wa dunia. ondoa uoga wako
mimi Sina uoga wowote ule Mkuu

Teh teh teh. Nadhani mleta mada alikwepa somo la biolojia akiwa sekondari.
Kuna wanyama wakiwemo mamalia na reptilia, wana kawaida ya kuruka hewani. Kuruka huku ni kwa namna mbili, 'Flying' na 'gliding' Flying ni kama vile arukavyo popo na 'gliding' ni kama vile anavyofanya huyo mjusi pichani na baadhi ya jamii ya cheche (gliding squirrel). Hawa wanaruka toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutanua ngozi iliyo mbavuni mwao ambayo huwasaidia kuelea hewani. Ngozi hii inafanana kabisa na ile ya popo. Kuna nyoka pia wenye mfumo kama huo, sijajua wanaitwaje! Nimeeleweka nadhani
mimi nimesoma Zamani Chini ya Mti ikinyesha Mvua hakuna tena kusoma wala somo la biolojia silijuwi sisi ndio tuliokimbia umande wa Mvua.
Mimi huyo mjusi nilimfahamu tangu nasoma biology of reptiles ya Prof Howell pale mlimani miaka 24 iliyopita
Babu kubwa nimeweka hap makusudi ili nipate kujuwa Watu upeo wao wa Elimu kuna viumbe Wengi tu Mwenyeezi Mungu alivyo viumba hatuvijuwi sisi binadamu.

hamna cha ajabu hapo!dunia ipo na itaendelea,timiza wajibu wako uliokuleta hapa duniani.
Ninawashukuru wote waliochangia hii Thread nimeona upeo wenu wa Elimu Asanteni ila mukiambiwa kuwa kuna Viumbe wanaoitwa Majjini na Mashetani kule kwenye Thread ya Mambo ya Dini na imani muamini mimi ninajuwa kila kitu ila nilitaka Watu kuwapima uwezo wao wa Elimu Mukiambia kuwa kuna Viumbe wanaoitwa Mashetani na Majjini na Ufo jamani muamini sio kubisha pasipo na kuwa na Elimu asanteni.
 
Hapo kuna mawili,
1, huyo aliyekuwa anawafundisha hiyo course ya Herpetology hakuwatendea haki kwa kutowapa elementary information ya evolutionary lineage na diversification ya mijusi ambao wengine inasemekana lineage yake ni ancestors wa ndege
2, Particpants hamkutaka kuuliza uliza maswali matokeo yake mka conclude kuwa dunia imekwisha.
 
Back
Top Bottom