Mjumbe wa CCM ajiunga UKAWA

Mjumbe wa CCM ajiunga UKAWA

Popote panapofuka moshi lazima moto uwake.
Matokeo ya hizi sarakasi za ccm kunajisi mchakato wa maana wa katiba tutayaona very soon viashiria vinaonekana na hakika na Tanganyika kupitia JK inaingia kwenye historia mpya ya kunyonga democracy na inner meaning of rule of people by the power of people.. itajidhihiri.
 
Kessy nimoja ya wabunge wa sisiem wanaotumia akili zao binafsi.
 
Wabunge wengi wa ccm akili zao wamezikabidhi kwa mwenyekiti wao ziwekwa kwenye kibuyu pale magogoni hapo dodoma wameachiwa kidogo tu za kuvukia Barbara na kuzomea tu.
 
Tunajisahaulisha kwamba katiba AFRICA uwa haitungwi ki raisi kama wengi tunavyozani,kuna njia tukipitia hiyo tuu ndo tunapata katiba mpya iliyo serious otherwise twajidanganya, tatizo ni watakaolipa gharama ya kupita njia hiyo Mungu atusamehe mana si njia ila waafrika tunaipenda sana.
 
Kwa hali hii hata kama UKAWA wangeitikia wito wa kurudi bungeni lazima wangetoka tena.
 
keissy.jpg

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ali Mohamed Kessy ambaye pia ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) akiwatangazia waandishi wa habari kuunga mkono muundo wa serikali tatu uwepo katika Katiba Mpya, mjini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya bunge hilo, Ummy Mwalimu na Makamu wake, Prof Makame Mbarawa ambao walimwita Kessy kumtaka kukanusha kuhusu taarifa yake ya kuwapo tatizo la akidi kwenye vikao vya kamati

Dodoma. Jana ilikuwa kama sinema pale viongozi wa Kamati Namba Moja ya Bunge Maalumu walipojikuta wakibishana na mjumbe wao mbele ya waandishi wa habari, huku siri za mambo ya ndani ya vikao zikianikwa hadharani.

Kamati hiyo inaongozwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na makamu wake ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, huku ikiwa imesheheni vigogo wengine wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Viongozi wengine katika kamati hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uhusiano na Uratibu), William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

Wamo pia Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana.

Jana asubuhi, Mwalimu na Profesa Mbarawa walifika mbele ya waandishi wa habari katika Hoteli ya St Gasper wakiwa wameambatana na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.

Lengo la mwenyekiti na makamu wake lilikuwa ni kumbana Keissy ili akanushe taarifa aliyoitoa juzi kwenye moja ya televisheni kwamba kamati hiyo inaongoza kwa kuvunja kanuni hasa katika suala la akidi ya vikao kutotimia.

Sinema ilivyoanza

Walipofika mbele ya waandishi wa habari, Keissy alipewa fursa ili akanushe taarifa yake, lakini alibadili mada na kuanza kuzungumzia masuala ya muundo wa Serikali na Bunge, huku akisema yeye ni muumini wa serikali tatu na siyo mambo ya serikali mbili zinazopendekezwa na wengi kutoka katika chama chake.

Kauli hiyo iliwashtua Mwalimu na Profesa Mbarawa ambao walianza kumkatisha ili asiendelee.

“Keissy sikukuitia mambo hayo, huu ni mkutano wangu, naomba ukanushe nilichokuitia, hayo utazungumza baadaye tafadhali sana,” alisema Mwalimu.

Wakati huo Profesa Mbarawa na waandishi wa habari waliokuwapo walivunjika mbavu kwa vicheko, huku yeye akiendelea kusisitiza kwamba ni muumini wa Tanganyika.

Wakati akisema hayo, Profesa Mbarawa naye aliingilia kati na kumtaka Keissy kueleza kilichompeleka hapo huku akimtaka aache kelele za kupotosha wananchi kwa kuwa anachosema siyo kweli.

Alipopewa nafasi ya kuzungumzia jambo hilo, Keissy alisema: “Jana (juzi), mimi nilihesabu mara mbili nikaona Zanzibar hawajatimia lakini kumbe mmoja nilimfanya akawa mtu wa Tanganyika, kwa hilo nilighafilika, lakini mle ndani mambo siyo mazuri,” alisema Keissy.

Kabla hajaendelea Mwalimu alidakia na kumtaka anyamaze kimya kwa kuwa huo haukuwa mkutano wake, ili yeye (Mwalimu) aendelee kueleza mambo yaliyojiri ndani ya kamati.

“Jamani waandishi si mnaona amekanusha, huu ni mkutano wangu na yeye sitaki azungumze mambo ya mle ndani kwa kuwa msemaji ni mimi au makamu wangu au mtu yeyote atakayeteuliwa na mwenyekiti, sasa tunaendelea,” alisema Mwalimu.

Mara baada ya Mwalimu kutoa taarifa ya kamati yake kwa waandishi wa habari na kumaliza kujibu maswali, alinong’ona na Profesa Mbarawa na hapo wakampa nafasi Keissy ili azungumze kwa ufupi mambo yake lakini palepale mbele yao.

Kauli za Keissy

Akitumia fursa hiyo, Keissy alisema: “Kuna mambo yanafanywa mle ndani ambayo mimi na wenzangu wengine tunalazimishwa, hatukubaliani nayo likiwamo suala la kuizika Serikali ya Tanganyika wakati wa upande wa pili (Zanzibar) wanapewa nafasi na kunufaika na rasilimali za nchi hii, ndugu zangu huu ni uonevu.”

Alisema uonevu huo umekuwa mkubwa kwa wabunge wa Tanzania Bara ukilinganisha na wenzao wa Zanzibar ambao alisema wanakula fedha nyingi za bure ilihali hawafanyi kazi za Tanganyika.

“Ndugu zangu, hapa tusidanganyane, we fikiria watu zaidi ya 50 wanatoka kule Zanzibar na kuja kutuamulia mambo yetu, hii si halali hata kidogo. Haiwezekani mtu wa Zanzibar akaja kuzungumzia masuala ya Nkasi wakati hayajui,” alisema.

Alisema kuwa msimamo wake siku zote ni serikali tatu na kwamba hatayumbishwa na vitisho au jambo la aina yoyote hata kukiwa na kulazimishwa.

Mbunge huyo alisema kuwa kutakuwa na urahisi wa kuongoza Serikali kama Tanganyika itapewa hadhi yake kuliko ilivyo sasa kwa serikali mbili zinazopigiwa upatu.

Kwa mapendekezo yake alisema ni vyema likawepo Bunge la Tanganyika, Bunge la Zanzibar na kisha miongoni mwa wabunge hao, wachaguliwe wachache kuunda Bunge la Muungano.

Aliendelea kusisitiza kuwa wabunge kutoka Zanzibar wanawanyonya wenzao wa Tanzania Bara kwa kila kitu kauli ambayo ilionekana kumkera Profesa Mbarawa na kuamua kumkatisha asiendelee kuzungumza.

Wakati akiendelea kuzungumza, viongozi hao walimkatisha tena na kumwambia akubali waondoke pamoja kuendelea na vikao vya kamati. Baada ya hapo, Mwalimu na Profesa Mbarawa walinyanyuka na kuanza kuondoka, lakini Keissy alisimama na kuendelea kuzungumza na waandishi wa habari.

Baada ya kuona anaendelea, Profesa Mbarawa alirudi na kumshika mkono Kessy huku akisema; “Mheshimiwa Keissy twende bwana, maana ukimwacha huku huyu atazungumza mambo mengi.”

Wakati akiondoka eneo hilo, Keissy alipaza sauti akiwaambia waandishi wa habari: “Angalieni tunavyodhibitiwa, lakini msimamo ni huo wala sitayumba ngoja tukaendelee lakini mimi ndiyo mtoa habari namba moja.”

Wakati huo huo Mjumbe asema Tuko Dodoma kula posho tu

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Alli Omari Juma amefuta matumaini ya Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba mpya, badala yake akabainisha kuwa wajumbe wako Dodoma kwa ajili ya kula posho tu.

“Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa ni mambo ya kulazimishana kila upande, sisi wengine tunaona bora ya Ukawa waliotoka nje kuliko mambo ya humu ndani,” alisema Juma na kuongeza:

“..Hata wale Wapemba waliokwenda Umoja wa Mataifa kudai haki ya kujitenga , naona walikuwa halali kwani hapa bungeni hakuna mwakilishi hata mmoja kutoka huko wakati tunaambiwa kuwa itakuwa Katiba ya wote, ni kudanganyana.”

Mjumbe huyo alisema kuwa Rasimu ya Warioba imetupwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuwafanya wengine waone kuwa kinachotengenezwa ni marekebisho ya Katiba ya 1977.

Alisema kuwa suala la akidi pia litakuwa ni moja ya vikwazo vitakavyosababisha kutopatikana kwa Katiba, akitolea mfano kutoka kwenye kamati yake Namba 4.

Alisema ndani ya kamati hiyo mambo mengi yanachakachuliwa kwani wajumbe wanaotakiwa kutoka Zanzibar ni 14 lakini waliopo ni 12 tu, ambao baadhi hawakubaliani na mawazo ya CCM lakini wanaambiwa mambo ni mazuri.

“Ukawa walitoka kwa uhalali kabisa nami nawaunga mkono, sisi tuliobaki humu ndani tulikuja kwa makusudi ya kuangalia kinachoendelea na sasa tunaona mambo ni ovyo,” alisema.

Kwa upande mwingine alimlaumu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Samuel Sitta kwamba amekuwa ni kinara wa kuvuruga kanuni kila wakati na kutaka mambo yake mwenyewe.

Jumba ambaye ni mtaalamu wa sheria, aliwatupia lawama pia viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba nao wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwaweka Wazanzibar pamoja ili wajue wanataka nini.

Kwa mujibu wa Juma, kila maeneo wanayojadili wanafanya kazi hiyo kwa kuboresha maslahi ya CCM kwani wanawasaidia kuwaandikia Ilani yao.

Alimtaka rais Jakaya Kikwete kukubaliana na maoni ya watu mbalimbali kwamba bunge la Katiba lisitishwe mara moja kuliko kuendelea kujadili misimamo mikali ya CCM.

Msimamo wa serikali tatu ni wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA) waliosusia Bunge.



Chanzo: Mwananchi
Kessy yuko sahihi kabisa,akina Ummy wale wanaleta uswahili wao kwenye mambo magumu na ktk picha wanaonekana wanafanya mzaha kwenye critical issue.TANGANYIKA NA MAMLAKA YAKO IPO SIKU ITAWEKWA WAZI NA ARDHI HII ITAPATA TENA SAUTI KUU.
 
Kuleni hizo posho ni zawadi kutoka kwa mheshimiwa anayemaliza muda wake, zikibaki siku kumi tu jitoeni turudie bunge na Mkulu aandae fedha nyingine. Mla ni mla leo!!!
 
Hii ni aibu kwa CCM na vibaraka wao,kuwaswaga wabunge wao kama mifugo MwanaDiwani
 
Last edited by a moderator:
Hii ni aibu kwa CCM na vibaraka wao,kuwaswaga wabunge wao kama mifugo MwanaDiwani

Hapo mwenyekiti wa kamati na naibu wake wasidhani chama chao kitawaacha hivi hivi. Lazima wawekwe kiti moto na hivi wanavyozidi kudhihirisha kwa vicheko wanadhihirisha walikusudia kukiaibisha chama.Kessy na kina Lugola wanaeleweka ni watu wenye uthubutu hasa linapokuja suala wanaloliamini. Waliona fahari gani kumtaka akanushe mbele ya waandishi jambo ambalo hata wao walishajua alimwesabia mjumbe mmoja wa visiwani kwa kumweka bora? Sasa ndo kawadhihirishia kuwa kuna wakati wanakuwepo wajumbe 12 wa visiwani badala ya 14 wanaotakiwa na akidi lakini mambo yanapitishwa tu.Huwezi kumzuia mjumbe tena mwenye jimbo kabisa kuelezea waandishi msimamo wake kwa hoja ya kuwa kikao ni chako.Hata yeye ana uwezo wa kuwaita waandishi wa habari. Matokeo ya upuuzi huu mtayaona mkianza mjadala bungeni kuchangia rasimu hizo na kuzipitisha kwa kura. Mtabaki na posho mlizojizolea ila katiba haipo.
 
Last edited by a moderator:
Hawa wote wakina Kessy ni wanafiki waliopo bungeni Kula posho. Dhambi hii wanayowafanyia wanyonge..., haha tote Yana mwisho. Mtu mzima unakuja mbele ya press na kulalamika kama hujaenda shule, simple...kama hukubaliani nao toka humo ndani kama jamaa wa ukawa walivyofanya, shenzi taipu, kubwa jinga.
Siyo kwamba ni sehemu ya sanaa!?
 
Back
Top Bottom