1. Huu ndiyo ulio ukweli mchungu wenye kuakisiwa vyema nyuma ya jitihada zote za Afrika Kusini hadi ICJ huko dhidi ya Israel.
2. Kwamba kuna mpenda haki wapi kwetu aliyebakia CCM, CHADEMA, ACT, UDSM au wapi wa aina ya mjukuu huyu wa Mandela?
3. Kwamba nani anaweza kuthubutu kwa na hakika kusema Nyerere angesema nini? Kwani haijulikani au ni unafiki, umbumbumbu, ujuha, ushabiki, uchawa, na vya namna hiyo tu, uliowajaa watu hadi kina makongorosi huko kiasi cha kutokuwa na dira wala mwelekeo?
4. Kwani Nyerere, Mandela, Castro, Tutu, Che Guevara, Mtikila, Maalim Seif, Chavez, Gaddafi nk au wa namna hiyo walikuwa na nini spesheli ambacho wengine wameshindwa kujitanabaisha navyo? Si kuwa walikuwa wenye kuendeshwa kwa nguvu za hoja?
5. Kwamba mambo sisi, si ni ushabiki na mihemko tu? Hivi hadi aseme nani ndipo tugutuke ya kuwa kwa hakika tumepotea njia; na kuwa tuliko na tuendako si kwenyewe?
6. Kwamba hata nyomi tuzionazo duniani kote nyuma ya HAMAS na Palestina si sauti za Mungu tena? Kwamba aje malaika kutokea wapi kutugatua wapi tutoke usingizini? Hivi hata tunajihurumia japo kidogo kuwa ndani ya umbumbumbu huu uliopitiliza mno, tuliomo?
7. Kwamba tumefeli wapi sisi Yarabi? Hivi sisi leo hata tunajuq kama Nyerere angekuwapo hata angesema nini? Ya kwamba hatukumsoma Wala kumwelewa? Ya kwamba aliondoka na yake yote? Na inakuwa jioni inakuwa asubuhi, tuko vizuri; maisha yanaendelea? "No wonder huwa tuko vizuri kugombea mali alizoacha marehemu!"
9. Kwamba mjukuu wa Mandela anajua Babu yake angesema nini, hata leo? Vipi contemporary, watoto, vijana, mabinti, wafuasi; wake, nk? "No wonder Afrika Kusini wanawakilisha wa aina ya kina Shivji, Ulimwengu na wachache mno wenye akili zao waliobakia hapa nchini, ambao pia nao wanaendelea kutoweka!"
9. Bila shaka baada ya kizazi cha kina Shivji na kina Ulimwengu, tutakuwa na "taifa la hovyo proper," kwa tunavyoshindana kuzidiana kuwa hovyo zaidi ya mwingine!
10. Alisema Prof. Chachage: "Babu zetu wakiwamo kina Kinjekitile, Mkwawa, Nyerere, Milambo, Sina, Isike, nk wangefufuka wakatukuta leo tulivyo komaa kuwashadadia mabeberu na wakoloni (wazungu kwa waarabu), watatukataa kuwa sisi si wajukuu zao!"
10. Kwamba wao katika uhai wao walipigana na kutupigania sisi wakipinga kutawaliwa na kwa nguvu zao wakiukataa ukoloni na utumwa? wengi wao hadi kupoteza maisha? Ya kuwa sisi leo ndiyo Hawa?
a) mkoloni na mlowezi ni wawekezaji, wafadhili au wahisani?!
b) Baina yetu tuna Arsenal, Chelsea, Man U, City, Real, Barca, nk; damu?!
c) Tunalazimishwa kwenda Rwanda tukipatikana kutaka hifadhi Uingereza ambako nako haturudi katu, kwa ridhaa zetu?!
d) tumekuwa wafuasi wa dini zao kuliko wao?!
e) Tunagombea kwenda ulaya na arabuni kwenda kuwa hata watumwa; wengine wakifia kwa maelfu baharini?
f) kwamba tumekuwa mabalozi wao hadi wanatushangaa?
g) kwamba tunaona heri tukawe magerezani kwao kuliko kuwa huru nchini?
h) kwamba tunatamani mkoloni angeendelea kuwapo kuliko yaliyotukuta baada ya uhuru?
i) Nk.
11. Kwa hakika washupavu hao (#10) wangesema: "katu sisi siyo wajukuu zao!"