Mjue mnyama Simba kiundani zaidi

Mjue mnyama Simba kiundani zaidi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,873
Simba takribani wote duniani wanapatikana Africa tu lakini kwa uchache sana wapo India ,Simba anaepatikana Africa ni mkubwa kiumbo kuliko Simba wa Asia ,Simba anafikia uzito wa kilo 190 akiwa wa kiume na wakike hazidi kilo 126.

Simba ni predators pekee wanaokaa pamoja na kuwinda kwa pamoja (predators ni wanyama wawindao) tofauti na wanyama wenzie wote waasili yake kama chui,tiger,jaguar ambao wao hawafungamani pamoja isipikua wanafanya mapenzi au analea mtoto ..ila simba jike akizaa basi lazima ajitenge kwa muda fulani maana madume hua hawaelewi somo na kuwala watoto.

Manyoya ya simba dume hufikia urefu wa sentimita 16 na huanza kua meusi pale umri unavyozidi kwenda ,pia huyatumia kama kuwavutia majike pia kama ulinzi kwenye shingo zao.

Kwakua Simba huishi kwa pamoja basi hata watoto wao huweza kwenda kunyonya kwa mama mwingine yaani hata mama mzazi akifa basi mtoto wa simba atalia kama kinda la ndege bali uenda kwa mama mwingine anaenyonyesha na maisha uendelea ,simba wadogo huzaliwa wakiwa na madoa madogo madogo kama chui lakini hupotea kutokana na jinsi wakuavyo.

Simba haishi msituni Bali huishi maeneo ya usavana yani ,ukame kiasi na nyasi chache chache. Ukiona simba anakula majani usifikiri kakosa chakula, simba anakula majani ili kujipatia maji yaliyo katika mimea kama ana kiu sana.

Pia simba ana uwezo wa kula kilo 4 za nyama kwa mlo mmoja ambapo ni sawa na robo ya mwili wake wote ,kwahyo ukiamua kufuga simba ujipange, na pia ndimi zao zina ncha kali ziitwazo papillae ambazo hutumia kukwangulia nyama wanazokula.

Simba anakimbia kwa speed ya km 60 kwa saa hivyo binadamu hauna namna yoyote ile yakuweza kumkimbia hata akikimbia kwa km 20 kwa saa, pia watu husema dume hawindi anawinda jike ,ni kweli na yote ni kwasabu ya uzito wa simba dume lakini ukijichanganya ndo utaelewa anawinda au hawindi.

Simba wamebakia 23,000 wamepungua asilimia 40% kwa kipindi cha miongo mitatu tu.

FB_IMG_1627854510066.jpg
 
Kwenye kula kilo 4 uongo
Simba jike anahitaji kula kilo 4 mpaka 5 kwa siku ingawaje Simba wana uwezo wa kula kilo 20 mpaka 30 kwa mara moja na akila hivyo inamchukua wiki moja tena kutafuta chakula...emu tupe ukweli Mkuu hapa tupo kujifunza..
 
Back
Top Bottom