MJUE Lowasa

Mkapa aliwaita watu kama nyie: wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.

Huyo Lowassa kama ana hizo nguvu angeacha kujiuzulu uwaziri mkuu!!

Mlishaambiwa Richmond ni nani! Ila hamtaki sasa tuwafanyeje enyi wadanganyika?

Ndo maana nawaambiaga Chadema hata wafanyeje kwa wapiga kura kama mwanzisha mada na muunga mkono! Kamwe hawaingii ikulu.

Maanani ni mbilikimo wa mawazo na wavivu wa kufikiri.
 
Hebu nisaidie Ikulu kwako unaielewaje?.Maana naona mawazo yako yote yako IKULU.
 
Aiiiiii Lowassa wewe ni kiboko......... Manake wakati mwingine haya mabaya yasemwayo juu yako yanageuka kuwa mazuri...
 

Nimecheka sana lakini mwisho nikagundua nimecheka kilofa!!!
 



Umetisha Boss.
 

Hongera kwa kumsafisha. Lakini hata utumie vim hawezi kutakata.
 
Tulidhani unataka kutueleza anazo hela ngapi katika Swiss Banks,kumbe unaandika rubbish.
 
..... Umeleta mada ambayo inaonyesha chuki binafsi yako binafsi na Mh. EL, ki msingi kila mtu ana uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa hii inamaanisha anatumia haki yake kama M TZ, isitoshe nyinyi ambao mko safi jitokezeni mgombee watanzania watakuwa na uamuzi wa nini kifanyike,.... na kama atashinda hajichagui yeye mwenyewe bali.....wananchi wapiga kura ndio wanaochagua...... swala la kujiandaa kwa ajili ya kugombea urais ni la mapema... kama anajipanga kwa kutumia rushwa ..... jamani si takukuru wapo? kwani kazi ya takukuru ni nini... mi nasema Mh. EL aendelee na mikakati yake ya kujipanga..... na kama mwanasiasa mkomavu hataogopa manene kwani hata kwenye kanga yapo...........
 
Itakuwa ni maajabu ngamia kupita kwenye tundu la sindano
 
We Pilau acha kudandia hoja zawenzako wewe humfahamu huyo fisadi,tena sitaki hata kusikia habari zake mamvi aende zake Monduli,naongezea sifa nyingine ni mwizi wa ng'ombe wamasai wanalijua hilo waulize tu.Unaongelea takukuru ambayo alikwisha ilambisha mikwanja.Achahako kazee kazeeke vibaya,Eti mbunge asiyechangia Vicoba anyimwe kura jimboni kwake,Je kanajua kila Mbunge kashawaibia wananchi hivyo anamapesa ya bure ya kugawa kila kona ya mguu.Mwacheni yeye aendelee kugawa siku zikiisha atafyaata.
 
kuwa mmeru siyo issue. hata hivyo wameru-wamasai ni wengi mno. nenda arusha kafanye utafiti. hata hivyo hakuwahi kuuonyesha umeru wake kwa wamasai. wamasai wanalijua umeru-wake na wala siyo issue kwao kwa vile alichowasidia wamasai huko kwao kinatambulika. hata hivyo wameru na wamasi wanakaribiana.
 

Baada ya Mwl.Nyerere..., hajatokea, hayupo na wala hatotekea mwenye sifa izo ndani ya Nchi hii ya Tanzania labda ashuke Malaika kuingoza.!!!
 
ukiwa na chaguo lako kichwani la mgombea urais na ukataka watu wamuunge mkono hakika EL atakunyima usingizi na atakutia baridi utabaki unatunga ngonjera za uongo na kujifurahisha nafsi. EL songa mbele timiza malengo yako.
 
Mbona mazuri yake hujayaweka hapa. Ni waziri mkuu pekee aliyewahi kufanya maamuzi yanayoonekana kufanywa na kiongozi wa nchi. Big up EL!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…