Mjue Edward Lowassa: Hii ni CV yake

Mjue Edward Lowassa: Hii ni CV yake

Hatakama angekuwa na afya kama jiwe hafai huo.

Lowassa hafai kwa mujibu wa katiba ipi? Huo Ufisadi wake umeuthibitisha wapi? Au kwakuwa alichukua Maamuzi magumu kujiuzulu ndio kawa Ng'ombe wa kafara? Kama ni hivyo acha Muhongo ang'ang'anie Madaraka maana ukijiuzulu ndio waBongo washakutuhumu tayari.
 
Mnatafutza maneno ya kumpamba "chura chura2" hata umuogeshe kw sabun hatakan! Nafas aliyonayo&fursa bado angefanya hayo
 
ndan ya kwa ze best of ze best #PR .MWANDOSYA fananisha kila k2 na lowassa utaona tofaut n uroho wa madaraka na umaarufu
 
Elimu na Tabia ni vitu viwili tofauti tabia nzuri hufanya matumizi mazuri ya elimu; tabia isiyo nzuri hufanya matumizi mabaya ya elimu.
 
Edward Lowassa ‘MwanaCCM Mtiifu’

Edward Ngoyai Lowassa, ni mmoja kati ya wanachama -wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) nchini Tanzania. Jina lake linatajwa kuwa miongoni mwa watu wenye nafasi kubwa ya kuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania.

Mengi yanazungumzwa, mengi yanasemwa juu ya sifa na uwezo wake, makala haya hayalengi kujadili uwezo wake kama kiongozi ila nafasi yake kama mwanachama halali na mtii kwa Chama Cha Mapinduzi.

Februari 18, 2014, Edward Lowassa pamoja na makada wengine wa Chama Cha Mapinduzi walipewa adhabu ya miezi 12-kwa kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i). Kifungo hicho kimemalizika siku chache zilizopita.

Maswali mengi waliyonayo watanzania ni je nini hasa hatma ya Lowassa? Na je kihistoria Lowassa ni nani hasa ndani ya chama cha mapinduzi?

Bahati mbaya sina majibu ya swali la kwanza, hata hivyo nina majibu ya swali la pili na hilo linaweza kutusaidia kujibu lile la kwanza. Je Lowassa ni mwanachama wa aina gani wa CCM?

Jibu rahisi ni Lowassa ni ‘Mwana CCM Mtiifu’. Hebu tuitazame kidogo historia yake ndani ya chama. Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 na katika Kijiji Cha Ngarash huko Monduli, Lowassa ni mtoto mkubwa wa kiume kwa mzee Ngoyai Lowassa.

Kielimu, Lowassa ana Shahada ya Uzamivu (masters degree) katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu Cha Bath nchini Uingereza aliyohitimu mwaka 1984, na kabla ya hapo alihitimu shahada ya kwanza katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1977.

Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM na serikali yake. Lowassa amejiunga na CCM akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Huko alikuwa mwanachama hai na baadae kiongozi wa Tanganyika African National Union (TANU) Youth League (baadae CCM Youth League). Mara baada ya kuhitimu masomo, aliajiriwa na CCM kama katibu msaidizi na baadaye katibu wa wilaya.

Hili pekee linatosha kuonyesha kuwa Lowassa amekulia katika misingi ya chama, ameanza kuaminiwa na chama akiwa kijana mdogo (bila shaka baada ya viongozi wa chama kujua weledi, uzalendo na utiifu wake) na ameshiriki toka ujana wake kwenye ujenzi wa CCM na Tanzania kwa ujumla. Akiwa kijana ndani ya CCM alipata kuwa msaidizi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago na Horace Kolimba.

Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika na Tanzania, mmoja wa waasisi wa chama na taifa letu. Bila shaka Lowassa alijifunza mengi kutoka kwake, na kama sio utiifu wa hali ya juu na uzalendo wake kwa chama na taifa, asingekweza kufanya kazi na mzee Kawawa,anayesifika kuwa na misimamo ya hali ya juu.

Pia Lowassa ni Luteni wa jeshi, licha ya kupigana vita dhidi ya Idd Amin nchini Uganda mwaka 1978/1979, pia akiwa jeshini alifanya kazi kwa ukaribu na Rais Jakaya Kikwete pamoja na katibu mkuu wa CCM wa sasa Mh Abdulrahman Kinana ambao wote ni makada wa CCM kwa miaka mingi. Wote tunajua kuwa jeshini ndiko kulikobobea kwa kufunzwa uzalendo na utiifu wa hali ya juu.

Mwaka 1985,Lowassa aliteuliwa kuwa Mbunge kupitia Umoja Wa vijana CCM (UVCCM), sambamba na Mama Anne Makinda (Spika wa Bunge la sasa) na Jenerali Ulimwengu.-Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli akipeperusha bendera ya CCM ambako amekuwa mwakilishi hadi leo.

Toka mwaka 1977 Lowassa amekuwa akiaminiwa na CCM na hakuwahi kukiangusha, amekwisha kabidhiwa dhamana nyingi za uongozi zenye kumpa dhamana ya kusimamia na kutekeleza ilani za chama, nyadhifa ambazo kila wakati alizitekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu. Lowassa amekwisha kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania (2005-2008), Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005), Ardhi na Makazi (1993-1995), -Haki na Mambo ya Bunge (1990-1993), na Mazingira na Mapambano dhidi ya umasikini katika ofisi ya Makamu wa Rais.

Utiifu wa Lowassa kwa chama ulijidhihirisha wazi mwaka 2008 alipokubali kwa ridhaa yake kuachia nafasi yake ya Uwaziri Mkuu ili kulinda heshima ya serikali nzima, Chama tawala-CCM-na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi. Huu ni uungwana na uzalendo wa hali ya juu, wenye moja ya vielelezo vya utawala bora.

Mwaka 2014 tumeshuhudia sakata la Escrow ambapo pamoja na kuwa na ushahidi wa wazi wa pesa kwenye akaunti zao, baadhi ya Mawaziri waligoma kuwajibika kwa hiari yao na wengine kusimamishwa kazi na Rais. Lowassa alijiuzuru kwa tuhuma tu, ambazo hazikuwa na mashiko wala ushahidi yakinifu, wala walau kupewa nafasi kuhojiwa na kamati teule ya bunge.

Kwa maelezo hayo nachelea kusema kuwa, Lowassa amekuwa mwanachama mtiifu kwa Chama Cha Mapinduzi kwa miaka mingi na hajawahi kukiangusha chama wala serikali wala taifa kwa namna yoyote ile. Watu kama hawa wanastahili pongezi na ni mfano wa kuigwa ndani na nje ya chama.
 
Kwenye wizi ni mtiifu kweli lakini hana sifa za kuwa raisi
 
thanx kwa uchambuzi the man iz da general in liberating racism come our next president wa ukweli
 
Kizuri cha jiuza!Kibaya cha jitembeza!TAFAKARI
....
 
ndan ya kwa ze best of ze best #PR .MWANDOSYA fananisha kila k2 na lowassa utaona tofaut n uroho wa madaraka na umaarufu

Kumbe shida ni Lowassa? Hivi tunaweza kutoa ule mfano wa kuzunguka uwanja kwa Mwandosya?
 
CHA KUOKOTA SIO CHA KUIBA.
0,,16052859_303,00.jpg

Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.

Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa.

Kwa utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU KWELIKWELI sio masihara.
1551527_577265145701642_2136377614_n.jpg

Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.

Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu".

Hatutaki kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu,fitna,kuchongeana,uchu wa madaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA. kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandikakwa facts and figures kama anavyosemaga Prof.Muhongo.

1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
Nianze na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa BRN.Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI,MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaan we want things to happen now.

Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweli LOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.

Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi.

HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.
Naamini huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye point ya tatu.

2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.

Jamani Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye dawati,alivyoshusha ada n.k Tusisahau kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu.

Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie.

Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL.

3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS)
Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".

Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.

Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges.

Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT.

A FOCUSED MAN 4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua LOwassa ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga chini.

Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi itakayotukomboa Tanzania.

Na ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA ....(nitamuongelea wakati mwingine)

5.LOWASSA ANASIKILIZIKA,ANAFUATILIA,SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
Hii ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha nyuma.

Rais anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa kiongozi anataka hili lifanyike.

LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.
KUTOKA Burudan Mwanzo - Mwisho: SIFA TANO ZA LOWASSA KUWA NIA URAIS 2015 ZATAJWA

Mkuu
Hata mie na kubaliana nawe, swali langu ni je hatuwezi kupata sura mpya?.
Maana hao kina Lowasa,Membe,Wasira n.k ni walewale.
Usije shanga kesho akija pewa Chenge nchi hii.
Pili kwanini Lowasa yuko tayari kulipa gharama kubwa (mamilioni) ilimradi tu apate Urais ana ajenda gani?.
Wakuu tujifunze kwa yaliyotokea tulipo pata wapambe wa chaguo la Mungu!!!.
Wapambe sikuzote huwa ni hatari sana, sasa jamvi hili linaanza kujaa wapambe wa urais(mtu) badala ya kuangalia nani kwa hakika ni mzalendo na atatukwamua hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom