Mjue Edward Lowassa: Hii ni CV yake

Mjue Edward Lowassa: Hii ni CV yake

CHA KUOKOTA SIO CHA KUIBA.
0,,16052859_303,00.jpg

Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.



Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa.


Kwa utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU KWELIKWELI sio masihara.
1551527_577265145701642_2136377614_n.jpg

Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.

Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu".


Hatutaki kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu,fitna,kuchongeana,uchu wa madaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA. kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandikakwa facts and figures kama anavyosemaga Prof.Muhongo.

1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
Nianze na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa BRN.Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI,MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaan we want things to happen now.


Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweli LOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.


Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi.

HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.
Naamini huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye point ya tatu.


2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.

Jamani Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye dawati,alivyoshusha ada n.k Tusisahau kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu.


Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie.


Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL.


3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS)
Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".


Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.

Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges.


Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT.


A FOCUSED MAN 4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua LOwassa ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga chini.


Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi itakayotukomboa Tanzania.


Na ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA ....(nitamuongelea wakati mwingine)

5.LOWASSA ANASIKILIZIKA,ANAFUATILIA,SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
Hii ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha nyuma.

Rais anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa kiongozi anataka hili lifanyike.

LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.
KUTOKA Burudan Mwanzo - Mwisho: SIFA TANO ZA LOWASSA KUWA NIA URAIS 2015 ZATAJWA

Mbona sifa ya mikakati ya wizi wa mali za umma hujaweka? Kama alivyosimamia Richmond na sasa kuna la viwanja vya posta oyster bay
 
Nakerwa na watu wanaolitetea hili fisadi la kutupwa! Sisi watanzania tumerogwa na nani jamani?


Mwizi namba moja ni mkuu wa kaya
Richmond mwakyembe kwa kauli take alisema kuna baadhi ya mambo ameyaficha kwa maslahi ya taifa na Edo alivohojiwa na cc akasema wazi ilitekeleza maagzo ya mkuu.

Escrow katibu was rais ndiye aliye ruhusu miamala kufanyika na huyu ametekelsza maagizo ya mkuu

Miamala ya stanbic mkuu na familia take no wahusika no moja
 
Ilan, huyo huyo alosoma degree ya mazingaombwe tunaemtaka maana ujasiri, uchapakazi,maamuzi,na uzalendo wake niwakimazingaombwe kiukweli alitakiwa achukue masters kabisa ya mazingaombwe maana nizaidi ya faida kwa Tanzania! Lowassa ni mtiifu hilo haliitaji compliment wala shout out coz ni sifa yake ya ndani sio yakugeza, hao walokula escrow hata ule utii wakinafki wakujiuzulu wamekosa..mnaomuita fisadi hamjielewi, wala hamuitambua Siasa hata theluthi yake,ila hiyo sumu Mlonyweshwa kuhusu Richmond tutawatapisha na MUAROBAINI...mtaelewa tu!
 

[TD="align: center"][/TD]
[TD="width: 20%"][/TD]
[TD="width: 5%, align: center"][/TD]
[TD="width: 14%"][/TD]


SalutationHonourable
First Name: Edward
Middle Name:Ngoyai
Last Name:Lowassa
Constituent:Monduli
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 139, Monduli
Office Phone: +255 754 800000
Ext.:
Office Fax: +255 22 2452037
Office E-mail: elowassa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 26 August 1953

[TH="colspan: 3, align: left"] GENERAL [/TH]

[TD="align: center"] Member picture
1021.jpg
[/TD]

[TD="width: 20%"] Member Type: [/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
School Name/Location Course/Degree/Award
University of Bath, UK
University of Bath, UK
University of Dar Es Salaam
Milambo Secondary School
Arusha Secondary School
Monduli Primary School

[TH="colspan: 5, align: left"] EDUCATION [/TH]

[TH="width: 15%, align: center"] Start Date [/TH]
[TH="width: 13%, align: center"] End Date [/TH]
[TH="width: 10%, align: center"] Level [/TH]

[TD="align: center"]MSc. (Development Studies)[/TD]
[TD="align: center"]-[/TD]
[TD="align: center"]-[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]

[TD="align: center"]MSc.[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]1984[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]

[TD="align: center"]BA (Edu) Hons.[/TD]
[TD="align: center"]1974[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]

[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1972[/TD]
[TD="align: center"]1973[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]

[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1968[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]

[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1961[/TD]
[TD="align: center"]1967[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
Company Name
Tanzania GovernmentPrime Minister
Ministry of Water and Livestock DevelopmentMinister
State, Vice President's OfficeMinister for Environment & Poverty
The Parliament of TanzaniaMember - Monduli Constituency
Ministry of Lands, Human Settlement DevelopmentMinister
State, Prime Minister's Office and First Vice PresidentMinister (Judiciary &Parliamentary Affairs)
Arusha International Conference CentreManaging Director

[TH="colspan: 4, align: left"] EMPLOYMENT HISTORY [/TH]

[TH="align: center"] Position [/TH]
[TH="align: center"] From [/TH]
[TH="align: center"] To [/TH]

[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]2/8/2008[/TD]

[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]2005[/TD]

[TD="align: center"]1997[/TD]
[TD="align: center"]2000[/TD]

[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]

[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]

[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]

[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember
Chama Cha Mapinduzi, CCMParty Executive-District, Regional &Head Office

[TH="colspan: 4, align: left"] POLITICAL EXPERIENCE [/TH]

[TH="class: text_menu"]Ministry/Political Party/Location[/TH]
[TH="class: text_menu, align: center"]Position[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]

[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]Todate[/TD]

[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]


Kutokana na CV hii kwa nini huyu kiongozi asiwe Rais wetu ajae wa taifa hili ukizingatia kwamba ana uwezo wa hali ya juu kwenye masuala ya kiutawala na uongozi. Nawasilisha

nakubaliana nawewe kua lowassa ana CV nzuri, na pia ni mchapakazi ( ndomana ni tajiri, yani huwezi kua tajiri bila kua mchapakazi unless uwe umerithi na mi sidhani kama amerithi ). Sasa kwanini asiwe raisi wa Tanzania? majibu yake ni mepesi mno, 1. Kwanza Tanzania tunahitaji maendeleo ya haraka sana ( mfumo ambao utatusukuma kupata maendeleo fasta fasta ), ieleweke hapa sio mtu atakae leta maendeleo haraka bali mfumo ( simuoni lowassa kama mtu atakae weka huo mfumo ) 2. Tunahitaji modern economy, tunaweza kua na raisi mwema, mchapakazi, mtu wa watu etc lakini tukakosa mipango ya kisasa ya kiuchumi ( uchumi wa sasa hivi umebadilika sana duniani, ile stable economy ya mataifa mbali mbali sio kitu kilichojiweka chenyewe ni ufahamu juu ya zama mpya za kiuchumi na mimi simuoni lowassa kama mtu anaeweza kutambua mambo haya ya kitaalamu katika uchumi unless awe anategemea watendaji ndo wamfanyie na kama ndo hivyo kwanini watendaji wasiwe maraisi kwasababu wanajua mambo mengi ya kimaendeleo kuliko rais?) 3. Tolerance, katika nchi ambayo asilimia kubwa ya watu hawajasoma/elimu yao haiwasaidii kupambanua changamoto walizonazo katika maeneo yanayowazunguka ni lazima kiongozi awe tolerant ( tukubaliane tu wote hatujaliona hilo kwa lowassa ) 4. Speech, lowassa uwezo wa speech ni mdogo ( sio sana, thou ni mdogo ) na ndo maana kumekua na kashfa nyingi zinamuandama za kutumia pesa kuwashawishi watu ( neno muhimu hapa ni kashfa ), unaweza hata kufuatila interviews na matamko yake mbalimbali utaona uwezo wake wa speech ulivo chini, umuhimu wa uwezo mkubwa wa speech kwa kiongozi mkubwa wa taifa ni pale ambapo patatokea janga, wananchi watahitaji comfort sio ya pesa tu bali hata maneno yawatulize ( simuoni lowassa kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza ) 5. Lengo, kwanini lowassa awe raisi? sababu kubwa hapa ni kuonesha kua alionewa, alidhalilishwa na nia ni kuprove wrong wale wote waliokua wanafikiria yeye ni fisadi ( maelezo hapa ni yeye si fisadi bali mtendaji mzuri sana na ameisaidia nchi yetu vizuri katika nyazifa zilizopita, nakubali ) lakini kwa kigezo cha kutaka kuudhihirishia umma kua yeye ni msafi je anafaa kua raisi? hapana kwakweli, lowassa ni mzee wetu tunamheshimu sana na tunathamini mchango wake kwene ujenzi wa taifa hili, ila katika kipindi hichi ambapo tunahitaji mabadiliko makubwa ya mfumo simuoni kama anafit.

Nimalizie kwa kum-quote Jerry Muro ( Tz highly acclaimed/renowned reporter ) kwene mkasiTV alisema, " tunahitaji mfumo ambao hata ukiweka jiwe lituongoze mambo hayaharibiki "...naomba kuwasilisha
 
Pamoja na yote Eddo boy ni mchapa kazi anafuatilia jambo hahawah kulia kwa uongo mbele za watu na mjiandae kusikia ukweli mwaka huu mbaya ya watu yatatokea sana na uzuri pia tutasikia kikubwa ni kufanya uchaguzi wa viongozi walio bora tujiandikishe na kuwakumbusha pia wengine kujiandikisha katika daftari la kupiga kura
 
Huyu ndio rais anayetarajiwa,kuibadili tanzania kiutandaji,uzalendo na misingi
ya uwajibikaji
 
BA (Education) ni mwalimu. Hivi Edo kweli ni mwalimu? Ninavyojua huyu ni msanii fine art, ualimu kaupata wapi?
Mbona ile shahada ya Mapambo na mazingaombwe haionekani.Shahada ya Kwanza ilikua Education Kweli?Huu ni ufisadi wa kitaaluma nao
 
SalutationHonourable
First Name: Edward
Middle Name:Ngoyai
Last Name:Lowassa
Constituent:Monduli
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 139, Monduli
Office Phone: +255 754 800000
Ext.:
Office Fax: +255 22 2452037
Office E-mail: elowassa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 26 August 1953

[TH="colspan: 3, align: left"] GENERAL [/TH]

[TD="align: center"] Member picture
1021.jpg
[/TD]

[TD="width: 20%"] Member Type: [/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
Company Name
Tanzania GovernmentPrime Minister
Ministry of Water and Livestock DevelopmentMinister
State, Vice President's OfficeMinister for Environment & Poverty
The Parliament of TanzaniaMember - Monduli Constituency
Ministry of Lands, Human Settlement DevelopmentMinister
State, Prime Minister's Office and First Vice PresidentMinister (Judiciary &Parliamentary Affairs)
Arusha International Conference CentreManaging Director

[TH="colspan: 4, align: left"] EMPLOYMENT HISTORY [/TH]

[TH="align: center"] Position [/TH]
[TH="align: center"] From [/TH]
[TH="align: center"] To [/TH]

[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]2/8/2008[/TD]

[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]2005[/TD]

[TD="align: center"]1997[/TD]
[TD="align: center"]2000[/TD]

[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]

[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]

[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]

[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember
Chama Cha Mapinduzi, CCMParty Executive-District, Regional &Head Office

[TH="colspan: 4, align: left"] POLITICAL EXPERIENCE [/TH]

[TH="class: text_menu"]Ministry/Political Party/Location[/TH]
[TH="class: text_menu, align: center"]Position[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]

[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]Todate[/TD]

[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]

EL Team 2015 naomba maelezo. Je Lowassa amepata wapi utajiri alionao hivi sasa ingawa historia ya ajira yake inaonyesha kuwa yeye amefanya kazi CCM, AICC (mwaka 1) na Serikalini tu ambako kote mishahara yake ni midogo na yeye ana familia na watoto? Je si ni vema akatufahamisha siri ya ujasirimali wake, ili tusije kumuona kuwa ni mwizi asiyefaa uraisi wakati anapita kuomba kura zetu?
 
EL Team 2015 naomba maelezo. Je Lowassa amepata wapi utajiri alionao hivi sasa ingawa historia ya ajira yake inaonyesha kuwa yeye amefanya kazi CCM, AICC (mwaka 1) na Serikalini tu ambako kote mishahara yake ni midogo na yeye ana familia na watoto? Je si ni vema akatufahamisha siri ya ujasirimali wake, ili tusije kumuona kuwa ni mwizi asiyefaa uraisi wakati anapita kuomba kura zetu?
Labda na wewe utusaidie ukiambiwa uelezee mali za lowasa unaweza kuziainisha kuwa ni hizi na hizi ? Au unazungumzia utajiri usioujua wala kuuona?
 
Lowassa ni nani?

Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953, na kukulia katika Kijiji cha Ngarash huko Monduli, akiwa ni mtoto mkubwa wa kiume kwa mzee Ngoyai Lowassa.

Alisoma Shule ya Msingi ya Monduli (1967-1971), Shule ya Sekondari Arusha kwa kidato cha nne (1967-1971) na Shule ya Sekondari Milambo kwa kidato cha tano na sita (1971-1973). Ana shahada ya elimu na sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyohitimu mwaka 1977, na Shahada ya Uzamivu katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Bath nchini Uingereza aliyohitimu mwaka 1984 kwa udhamini wa British Council.

Ni mume wa Regina Lowassa na wamejaliwa watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike.

Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM na serikali yake. Mara baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliajiriwa na CCM kama Katibu Msaidizi na baadaye Katibu wa Wilaya. Alipata kuwa msaidizi wa mzee Rashidi Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago na Horace Kolimba. Alifanya kazi pia jeshini sambamba na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Abdulrahman Kinana na aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni.

Jambo moja ambalo watu wengi hatukulijua kabla ni kwamba Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa wanajeshi waliopigana vita nchini Uganda mwaka 1978/1979.

Kwa nchi nyingi duniani, hii ni sifa muhimu ya ziada kwa mtu yeyote anayewania uongozi wa nchi kwa sababu kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo kwa kuwa tayari kuifia nchi.

Aliingia katika siasa za kiserikali mwaka 1985 alipoteuliwa kuwa mbunge wa vijana, sambamba na Anne Makinda na Jenerali Ulimwengu. Akiwa bado mbunge mwaka 1989 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC) ambako alidumu hadi mwaka 1990 alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Monduli hadi leo.

Aliteuliwa kuwa waziri katika ofisi ya makamu wa kwanza wa rais akishughulikia Mahakama na Bunge 1990-1993, na baadaye aliteuliwa kuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya mijini 1993-1995.

Mwaka 1997 aliteuliwa na rais Benjamin Mkapa kuwa waziri katika ofisi ya makamu wa rais akishughulikia mazingira na umasikini.

Mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo.

Aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa waziri mkuu Desemba 30, 2005, nafasi aliyodumu nayo hadi Februari 7, 2008 alipojiuzulu kwa kile kinachojulikana kama kashfa ya Richmond, lakini yeye mwenyewe akieleza kama kitendo cha kuwajibika katika kulinda maslahi ya chama chake kwa makosa yaliyofanywa na watendaji wa chini yake.

Uhalisiawa taswira ya uchapa kazi wa Lowassa

Ili kufanya tathimini kuhusu uhalisia wa taswira ya Lowassa kwamba ni mchapa kazi inabidi kumuangalia katika maeneo makubwa matatu alikofanyia kazi, ambayo ni katika chama chake cha CCM, AICC na serikali alipokuwa waziri na baadaye waziri mkuu. Msingi wa uchapa kazi wa Lowassa unaelezwa katika aina ya maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya kama kiongozi. Nitaanisha baadhi ya maeneo haya.

Mzee mmoja aliyepata kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM na serikalini na ambaye amefanya naye kazi kwa karibu, anamweleza Lowassa kikazi kama ‘frontliner'.

Kwamba Lowassa siku zote alikuwa mbele akitaka kuhakikisha kwamba anatekeleza jambo mlilokubaliana na kuona matunda yake kwa haraka iwezekanavyo. Kichama, mzee huyu alimwelezea Lowassa kama mtu anayeijua CCM ya sasa kuliko mtu mwingine yeyote aliyeko madarakani ndani ya CCM na serikalini. Kwa mujibu wa mzee huyu, ambaye mwenyewe anajibainisha kuwa ni CCM asili, Lowassa "ndiye mchawi anayefaa kuilea CCM ya sasa"!!

Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) aliyepata kufanya kazi na Lowassa anakiri kwamba ni mchapa kazi, lakini kwa maoni yake ni kwamba aliivuruga sana AICC. Hii ni kwa sababu kwa muda mfupi aliokaa pale AICC alibinafisisha vitega uchumi vya AICC vikiwamo duka la zawadi (gift shop) lililokuwa Uwanja wa Ndege sambamba na kampuni ya magari ya watalii na hoteli.

Mfanyakazi huyu anamueleza Lowassa kama mtu mwenye maamuzi ya ‘kiMagufuli' na ‘kiMrema' yasiyozingatia umakini na utaratibu.

Hata hivyo, mfanyakazi mwingine aliutetea uamuzi wa Lowassa wa kubinafisisha vitega uchumi vya AICC kwa maelezo kwamba vilikuwa vinaendeshwa kwa hasara. Pengine uamuzi huu wa Lowassa wa kubinafisisha vitega uchumi vya AICC inatupa mwanga kidogo juu ya falsafa yake kiuchumi, ambayo tutaijadili katika sehemu ya tatu ya makala hii.

Mifano mingine inayotajwa kuwa ni uwezo alionao wa kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia yanahusishwa na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata, kuvunjwa kwa mkataba wa City Water na mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria. Tuitazame kidogo mifano hii.

Pamoja na kwamba wazo la kujenga Chuo Kikuu kipya cha Dodoma lilitolewa na Rais Kikwete katika kampeni zake za mwaka 2005, inajulikana kwamba Lowassa ndiye aliyesukuma utekelezaji wake kwa kutafuta fedha za ujenzi wa chuo hicho kupitia mifuko ya pensheni.

Kuna ‘hadithi' kwamba mwanzoni alipowaita makatibu wakuu wa wizara walionyesha ugumu wa kutekeleza mradi ule katika muda ambao Rais alikuwa anataka utekelezwe. Hata hivyo, inaelezwa Lowasa aliwakaripia na kuwaambia kuwa Katibu Mkuu yeyote anayeamini kwamba mradi huu hautekelezeki ampelekee barua ya kujiuzulu na yeye angeifikisha kwa Rais.

Ni katika hatua hii ndipo makatibu wakuu walipokuja na wazo la kutafuta fedha kutoka mifuko ya pensheni. Panaweza pakawa na ubishi juu ya chanzo hasa cha wazo la kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini hakuna ubishi mkubwa kuhusu ukweli kwamba Lowassa ndiye aliyesukuma utekelezaji wake na kuhakikisha kwamba fedha za ujenzi wa chuo hicho zinapatikana.

Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata ni jambo la kisera ambalo limeanishwa vizuri katika Sera ya Elimu ya Mwaka 1995 iliyotengenezwa wakati Profesa Philemon Sarungi akiwa waziri wa elimu.

Katika sera hiyo, ujenzi wa Shule za Kata umeelezwa kama mkakati sahihi wa kupanua elimu ya sekondari nchini. Utekelezaji wa sera hii ulianza mwaka 1997. Hata hivyo, ufanisi wake ulikuwa wa kusuasua hadi baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 ambapo Rais Kikwete alihimiza zaidi kama sehemu ya mpango wake wa kupanua elimu ya sekondari na elimu ya juu nchini na hapa ndipo tunapomuona tena Lowassa. Hakuna ubishi kwamba ni yeye aliyesimamia kwa kasi zaidi ujenzi wa shule hizi alipokuwa waziri mkuu.

Baadhi yetu katika tasnia ya elimu hatuamini kwamba ilikuwa ni uamuzi wa maana kujenga shule hizi kwa mkupuo na kwa muda mfupi kiasi kile kana kwamba dunia inaisha kesho.

Kasi ya ujenzi wa shule hizi ndani ya muda mfupi ulisabisha kupatikana majengo mengi yakiitwa shule lakini pasipo elimu ya maana ndani yake.

Hata hivyo, shule hizi sasa zipo na maelfu ya watoto wa Kitanzania wanasoma, pamoja na kwamba elimu waipatayo inatia shaka ya kutosha.

Uamuzi mwingine unaoelezwa kwamba ni mgumu uliofanywa na Ndugu Lowassa ni kumshauri Rais kufuta umiliki wa kiwanja Mikocheni mwaka 1995 kwa mfanyabiashara maarufu wakati huo akiitwa Bipin Raichada.

Uamuzi huu ulisababisha kushtakiwa kwa Lowassa na mfanyabiashara huyu kwa madai kwamba alimshauri Rais vibaya. Uamuzi huu ulienda sambamba na raia kadhaa wenye asili ya kihindi kunyang'anywa viwanja katika eneo la mnazi mmoja ambalo walikuwa wamelivamia bila kujali kwamba ni eneo la wazi kwa kutumia fursa ya ‘ruksa'.

Akiwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo, Lowassa alivunja mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya City Water iliyokuwa imekabidhiwa jukumu la kuendesha shirika la maji Dar es Salaam.

Kampuni hii baadaye iliishtaki serikali, kesi ambayo ilikuwa imemuweka pabaya Lowassa kwa maelezo kwamba alivunja mkataba husika kimakosa na alikuwa anakwenda kuisababishia serikali hasara kubwa. Bahati nzuri serikali ilishinda kesi hiyo na pengine hiyo ikawa ndiyo pona ya Lowassa.

Moja ya sifa za kikazi za urais nilizoeleza katika makala zilizopita ni bidii, weledi na umakini katika kazi. Nilibainisha kuwa "tunahitaji Rais ambaye ana historia ya bidii katika kazi popote huko alikopita, na tukimfuatilia tunaweza kuona alama yake alipopita".

Jambo la wazi ambalo halihitaji mjadala sana ni kuwa popote alipofanya kazi Lowassa aliacha alama. Pengine jambo ambalo tunaweza kulijadili ni umakini wa maamuzi yake na kiwango ambacho alama alizoacha zilikuwa chanya na kwa manufaa ya Taifa.

Kwa upande mmoja unaona umuhimu wa kiongozi wa aina ya Lowassa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka yenye kuzingatia matokeo zaidi kuliko mchakato wa kupata matokeo husika. Hii ni taswira njema kwa kiongozi, hasa kama kuna mtu juu yake wa kuweza kudhibiti kasi ili kuhakikisha kwamba matokeo chanya yanapatikana bila kuathiri haki za watu.

Kwa upande mwingine, unaweza kumuogopa kiongozi wa aina ya Lowassa katika nafasi ya juu sana kwa kuwa kwa mtindo wake wa kufanya maamuzi makubwa kwa haraka na bila kuzingatia mchakato wa kimaamuzi anaweza kuirudisha nchi nyuma katika utawala bora na ujenzi wa demokrasia. Yote hii itategemea na nchi inahitaji kiongozi wa aina gani kwa wakati husika, maana mzee Ali Hassan Mwinyi alishatuonya kitambo kuwa kila zama na kitabu chake. Nawaachia wasomaji wafanye tathmini juu ya uhalisia wa taswira ya uchapa kazi wa- Lowassa.
 
Wasifu wa Edward Lowassa

Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.

Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.

Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.

Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, kumebadilisha kabisa upepo wa kisiasa nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.

Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzuLu wadhifa huo kufuatia sakata la kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond Development Company LLC ya Houston Texas.

Hata hivyo wakati anatangaza kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa' walio juu yake.

"Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze" alisema Lowassa

"Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze" alisema Lowassa

Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.

Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya kuongoza nchi.

Lowassa amekimbilia upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote 42. Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu waliomuunga mkono.

Wakati chama cha CCM kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.

Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia'
"Nitakuwa mnafki nikisema bado nina imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia", alisema, na kuongeza "kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM"

Wakati sakala la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakama Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.

Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘mzee wa maamuzi magumu'.

Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Moja ya mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.

Lowassa ni mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.

Mtoto wa Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo. Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo

Ulipofika uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.

Chanzo: BBC
 
Kwenye msafara wa mamba kenge wapo.Sasa tusione kipya kwa kina Prof na Dr.Slaa kupingia chocho
 
Kwa Vyama Hivi Vya Upinzani Ndio Maana WanaCCM Wanasema Watatawala Milele. Prof. Lipumba na Dr. Slaa Mbona Mmewaangusha

Watanzania.Kwa Kitendo Mlichokifanya Hata siku Moja Mstegemee Kuaminiwa na WaTZ, Usali Usio na Mfano. Hakika Heshima yenu Imeporomoka. Haitakaa Itokee Ku-gain any Political trust.
 
Kwa Vyama Hivi Vya Upinzani Ndio Maana WanaCCM Wanasema Watatawala Milele. Prof. Lipumba na Dr. Slaa Mbona Mmewaangusha

Watanzania.Kwa Kitendo Mlichokifanya Hata siku Moja Mstegemee Kuaminiwa na WaTZ, Usali Usio na Mfano. Hakika Heshima yenu Imeporomoka. Haitakaa Itokee Ku-gain any Political trust.

Usipende kuhukumu,sikiliza pande zote ndo uongee mawazo yako,Siamin kwamba Lipumba anaweza kuhangaika na cuf toka mwaka 1995 mpaka leo hii ndio ajiondoe uanachama bila sababu???Hata Slaa ajiondoe tu bila sababu? Naamin wote wanapenda mabadiliko but kuna kitu ambacho kimo ndan ya ukawa kilichowakera
 
Mbona ile shahada ya Mapambo na mazingaombwe haionekani.Shahada ya Kwanza ilikua Education Kweli?Huu ni ufisadi wa kitaaluma nao
Kwani kaka imekuwaje tena? Au haupo tena CDM na .UKAWA. Tunaposhangaa ya firauni, tusubiri kuona Musa
 
Back
Top Bottom