Mjini shule | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjini shule

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  PaDri mmoja aliyekuwa na tabia ya kutembea na mke wa mtu kila mumewe alipokuwa kazini, siku moja siri ya uzinzi ilimfikia mwenye mali na kutakiwa arudi nyumbani ghafla. Jamaa alifanya hivyo na kukuta mlango umefungwa kwa ndani. Aligonga mkewe kwa woga wa kufumaniwa akachanganyikiwa, lakini Padri kwa kujiamini alivaa nguo na kujining’iniza dalini huku miguu ikionekana kwa chini.
  Jamaa alipoingia alianza kumshutumu mkewe;
  Jamaa: Nasikia unatembea na Padri?”
  Mke: Watu waongo mume wangu, huyo Padri yupo wapi?”
  Jamaa alianza kumtafuta kila kona lakini hakumuona alisahau kuangalia juu zaidi ya uvunguni na ndani ya kabati. Baada ya kuridhika kweli hakukuwa na mtu ndani, walikaa kitandani huku mkewe akiomba asiangalie juu.
  Padri aliyekuwa akining’inia juu ya kenchi mikono yake ilichoka na kujikuta akidondoka toka na kuanguka mbele ya yule mwanaume na mkewe. Wote walishtuka kumuona Padri, jamaa aliuliza;
  “Si huyu?”
  Padri: “Huyu nani, nimesikia mkiniteta kuwa natembea na mkeo, lakini kwa uwezo wa roho mtakatifu amenileta ndani mwako ili unithibitishie kuwa mimi natembea na mke wako”
  Jamaa alipoangalia juu hakuona sehemu yenye tundu alipopitia padri.
  Jamaa: “Umepitia wapi?”
  Padri: “Ni uwezo waroho mtakatifu aliyeniingiza kwa uwezo wake bila kuharibu bati wala kitu chochote”
  Jamaa: “Samahani baba Padri”
  Padri: “Nimekusamehe wewe na mkeo kwa kuwa hamkujua mtendalo”
  Jamaa: “Asante baba Padri walimwengu ni wagombanishi”
  Baada ya kusema hayo Padri alimfungulia mlango na kutoka huku mume akiamini kuwa ni kweli Padri kaletwa na roho mtakatifu. Kweli mjini shule.
   
 2. Jeni

  Jeni Senior Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mmmhhhh malimwengu
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  janja ya njyani kula indi mbichi
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Ingekuwa mimim kibano tu sisikilizi la Padri wala nani
   
Loading...