Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,342
- 5,536
Nipo hapa stand ya mabasi Moshi mjini ambapo dada mmoja amepata msaada kutoka kwa konda aliyemwingiza kwenye basi (kosta) ili kumwokoa kutoka kwenye kundi la vijana waliokuma wakimzomea na kumzodoa kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa. Dada huyo aliyekuwa amevaa skin tight inayopita magotini na t shirt iliyombana na inafunika nusu ya makalio alijikuta hana la kufanya hadi alipookolewa na konda kwa kumwingiza kwenye gari yake iliyokuwa kwenye foleni na kufunga vioo vyote. Nilichokigundua baada ya kuuliza mwenyeji nimegundua hilo ni jambo la kawaida kwa mji wa Moshi na limekuwa likifanyika karibu kila siku. Waathirika wakuu ni wageni maana wenyeji wanafahamu. Kina dada mkija Moshi mjipange sawasawa!