Mji gani mzuri kati ya Lindi na Singida?

Mji gani mzuri kati ya Lindi na Singida?

Mimi nmefika Lindi na singida, naijua vizuri lindi pamoja na singida

Lindi ni miongoni mwa miji ya zamani hapa tz, kwa kweli kwa sasa lindi mjini hapana ishu yoyote, ukiangalia majengo ni yake ya kale na mengine mpaka yanabomoka,

Shughuli ya kiuchumi kwa lindi ni uvuvi (japo unafanywa kijivu), pia kilimo (nani,ufuta) biashara sio sana, watu wa lindi niwavivu sana na kunauswahili wa kufa mtu

Usafiri sio shida kama miaka ya nyuma, fulsa za biashara zipo, inategemea na mfanyaji biashara

Singida ni mji ambao unakuwa kwa kasi sana, Kuna fulsa nyingi sana za biashara na kilimo, ukiwa mchakarikaji singida unatoka

Nakushauri nenda Singapore
 
kijographia mji wa lindi upo vizuri sana kwasababu upo jirani sana na bahari. bahari ni kiungo muhimu ktk uwekezaji wa biashara ya utalii.

shida ya mji wa lindi ni umwinyi usio wa kawaida. tabia za umwinyi na uswahili zimetamalaki sana lindi kiasi cha kuwaogopesha hata wageni wahamiaji wanaotaka kuwekeza ndani ya mji ule.

ni jambo la kawaida kawaona vijana kwa wazee wakicheza mchezo wa bao vibarazani mida ambayo walitakiwa waitumie ktk uzalishaji mali.

nasikia huwezi kujenga jengo zuri ndani ya mji wa lindi bila kuwaona wazee wa kimatumbi. usipofanya hivyo jengo lako halifiki hata ghorofa moja. hiyo ndiyo lindi.
Hahahahahahahah jamani umetusingizia wamatumbi.... Lindi wapo wamwera
 
Lindi bana acheni masiharaa...
Paris of Africa according to mzungu enzi zilee
Lindi life yake ni rahisi kimtindo, hayo mengine unayoambiwa hapa changanya na zako
Unakumbuka takwimu za TACAIDS Lindi ndo mkoa pekee Tz bara kuwa na % ndogo ya maambukizi ya HIV
Lindi sio pazuuri ninachokipenda Lindi ni zile barabara za lami mpaka vichochoroni na bahari tu
 
Tatizo la singida ushamba mwingi,kuna kajamaa kanamiliki kagloclery mitaa ya stendi kuu( ukitoka lango la stendi kuu upande wa kushoto) na kagari kake toyota mark11, full "mashauzi", kaglocery kenyewe kadogo utadhani choo cha apa kwangu.
Kiufupi acheni kufananisha Lindi na vitu vya kijinga.
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
naomba unielimishe, wazawa/wenyeji wa mji lindi ni nani?. maana mimi siku zote najua ni wamatumbi.
Lindi ina wilaya sita....

Kilwa
Liwale
Nachingwea
Rwangwa
Lindi mjini
Lindi vijijini
.....

Ndani ya wilaya ya kilwa Kuna makabila mawili kama sio matatu
Wamatumbi.. Kilwa kaskazini pamoja na wangindo
Kilwa kusini wapo wasiojua kabila lao[emoji23]

Liwale Kuna wangindo pia
Rwangwa Kuna wamwera
Nachingwea Kuna wamwera
Lindi mjini wamwera
Lindi vijijini wamwera
 
U
Lindi ni mji wa Kisultani. Kibiashara hauko vizuri ila totoz pale ni balaa! Makombo ya kiarabu sijui...watoto wazuri. Maisha ya Lindi pia ni rahisi, ndiyo maana ukioa mtoto wa Lindi ukampeleka bara, atajigombanisha tu ili arudi kwao akale tambi, pweza, ngisi, madafu, wali wa nazi, vibua, Bagia, kalimati na kuattend vigodoro.
Umenichoma mkuki wa moyo
 
Lindi bana acheni masiharaa...
Paris of Africa according to mzungu enzi zilee
Lindi life yake ni rahisi kimtindo, hayo mengine unayoambiwa hapa changanya na zako
Unakumbuka takwimu za TACAIDS Lindi ndo mkoa pekee Tz bara kuwa na % ndogo ya maambukizi ya HIV
Siyo Kigoma ?
 
Tatizo la singida ushamba mwingi,kuna kajamaa kanamiliki kagloclery mitaa ya stendi kuu( ukitoka lango la stendi kuu upande wa kushoto) na kagari kake toyota mark11, full "mashauzi", kaglocery kenyewe kadogo utadhani choo cha apa kwangu.
Kiufupi acheni kufananisha Lindi na vitu vya kijinga.
Ha ha ha

Smart guy
 
Back
Top Bottom