Mji gani mzuri kati ya Lindi na Singida?

Mji gani mzuri kati ya Lindi na Singida?

Small Axe

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Posts
652
Reaction score
465
Hii miji ilikua nyuma sana ezi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa lakini hivi karibuni mambo sio kama zamani barabara, fursa na miundombinu mingine mingi. Je, upi mji mzuri wenye fursa nyingi na ni mzuri kwa kuishi?
 
Kijographia mji wa Lindi upo vizuri sana kwasababu upo jirani sana na bahari. Bahari ni kiungo muhimu ktk uwekezaji wa biashara ya utalii.

Shida ya mji wa Lindi ni umwinyi usio wa kawaida. Tabia za umwinyi na uswahili zimetamalaki sana lindi kiasi cha kuwaogopesha hata wageni wahamiaji wanaotaka kuwekeza ndani ya mji ule.

Ni jambo la kawaida kawaona vijana kwa wazee wakicheza mchezo wa bao vibarazani mida ambayo walitakiwa waitumie katika uzalishaji mali.

Nasikia huwezi kujenga jengo zuri ndani ya mji wa Lindi bila kuwaona wazee wa kimatumbi. Usipofanya hivyo jengo lako halifiki hata ghorofa moja. Hiyo ndiyo Lindi.
 
Lindi ni mji wa Kisultani. Kibiashara hauko vizuri ila totoz pale ni balaa! Makombo ya kiarabu sijui...watoto wazuri. Maisha ya Lindi pia ni rahisi, ndiyo maana ukioa mtoto wa Lindi ukampeleka bara, atajigombanisha tu ili arudi kwao akale tambi, pweza, ngisi, madafu, wali wa nazi, vibua, Bagia, kalimati na kuattend vigodoro.
 
Lindi bana acheni masiharaa...
Paris of Africa according to mzungu enzi zilee
Lindi life yake ni rahisi kimtindo, hayo mengine unayoambiwa hapa changanya na zako
Unakumbuka takwimu za TACAIDS Lindi ndo mkoa pekee Tz bara kuwa na % ndogo ya maambukizi ya HIV
 
Lindi bana acheni masiharaa...
Paris of Africa according to mzungu enzi zilee
Lindi life yake ni rahisi kimtindo, hayo mengine unayoambiwa hapa changanya na zako
Unakumbuka takwimu za TACAIDS Lindi ndo mkoa pekee Tz bara kuwa na % ndogo ya maambukizi ya HIV
Nadhani kwa sababu kuna watu wachache sana. Yaani mjini kati kumepooooa!!
 
Singida kibiashara pako vizuri sana ukitaka kwenda kokote mikiani unaenda kirahisi,ukitaka kwenda nchi jirani unaenda kirahisi kwa maana nyingine Singida ni hab kibiashara,Mimi nimefika kote enzi ya MWL na ya hapa kazi tu,Singida inakuja juu kwa kazi kubwa kuliko Lindi pamoja na bahari haifui dafu kwa Singida yenye vibwawa tu kindai na singidani
 
Back
Top Bottom