Mjerumani Aponzwa na Mbwa Wake


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280


Mjerumani aliyekuwa akiwakimbia polisi na kujificha kwenye kabati ndani ya nyumba yake, aliponzwa na mbwa wake aliyewaongoza polisi hadi kwenye sehemu aliyojificha. Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani aliponzwa na mbwa wake mwenyewe baada ya kuwakimbia polisi waliofika nyumbani kwake na kwenda kujificha kwenye kabati la nguo.

Wakati polisi walipogonga mlango wa nyumba yake iliyopo kwenye kitongoji cha Euskirchen karibu na mji wa Cologne, mlango ulifunguliwa na mwanaume mwingine ambaye alisema hajui mwanaume anayetafutwa ameenda wapi.

Lakini mwanaume huyo alipomuachia mbwa aliyekuwa amemshikilia, mbwa huyo moja kwa moja alienda kwenye kabati alilojificha mmiliki wake na kuanza kutingisha mkia.

Kitendo hicho kiliwashtua polisi ambao waliamua kulisachi kabati hilo lenye unene wa mita moja na urefu wa sentimeta 80.

Polisi walipolifungua kabati hilo, Mwanaume huyo alikutwa amejikunja ndani yake. Walimkamata na kumtia mbaroni.

Polisi hawakusema walikuwa wakimtafuta mwanaume huyo kwa kosa gani na walikataa kutaja umri wala jina la mtuhumiwa huyo.
 
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,945
Likes
239
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,945 239 160
Kama ndio mimi namtimulia mbali huyo mbwa.
 
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,849
Likes
29
Points
145
Emanuel Makofia

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,849 29 145
Hahaaa ahaaaaa "mtoto,baba kaniambia nikuambie hayupo kaenda shamba":D
 
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Messages
408
Likes
4
Points
35
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2009
408 4 35
maumbwa mengine hayana mpango
 

Forum statistics

Threads 1,251,233
Members 481,615
Posts 29,763,433