Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?


Kuna katuni ilichorwa na mwandishi wa Kenya ikiwaonyesha wana habari wa TZ wakimlamba miguu JK,na waandishi wetu walilalamika sana kwa kudai mwandishi huyo wa Kenya aliwakosea heshima!

sasa kwa uandishi kama huu wa akina Maggid walilalamikia nini kama wanadhalilishwa ili hali wanajidhalilisha wenyewe kwa kujikomba kwa JK kwa habari zisofanyiwa uhakiki wa kisayansi ili kumpamba JK;ambapo mwandishi Maggid kakurupuka tu kutoka kitandani,kuvuta kompyuta yake na kuanza kuandika madudu yake?
 

Umepewa assignment na Sheikh?

Kamuambie umefeli
 
Well said...even Muhammad Ali can beat any opponent today in the ring....provided that you are a fannatic of him
 
Hao ndio mkakatati waliopanga, hata lipupunda nae natamka hilo hilo kuwa atakuwa wa 2,TBC 1 nao naona wanacover vitu vidodo vidogo vya CUF ukilinganisha na Chadema, tujiandae kwa mapambanooooooo,
 
Hii ni kazi maalum, ni kazi kama inayofanywa na Radio One na ITV, au TBC1 na TBC Taifa, ni kazi ambayo main stream media zimepewa zimuonyeshe mgombea wa CCM na CCM kuwa ndiye mshindi na kuwa CCM ndicho chama tawala baada ya 31 October 2010.
ITV/Radio One au TBC wanaporipoti ahadi za mgombea urais wa CCM utawasikia wakisema serikali imesema au rais amesema, huu ni upotoshaji wa makusudi, wanajua Kikwete huenda akakosa ridhaa y kuunda serikali baada ya uchaguzi, wanajua kuwa Kikwete hafai kuendelea kuongoza kwa sababu hana uwezo. Hawafanyi kwa bahati mbaya bali ni kazi maalum ya kujaribu kuwaghiribu wapiga kura hasa hasa wa kijijini kuwa pale watakapokuwa wanapiga kura wakimuona Kikwete wajue huyu ndiye rais na wengine ni wapinzani, wakorofi, wazushi na wasiostahili kupigiwa kura.
Wanawaambia wapiga kura kuwa hata wakiwapa kura Chadema/CUF hawataunda serikali.
Hata kwenye uchaguzi mkuu wa 2005, kuna theory kwamba CCM walipotosha makusudi kura za mgombea urais wa Chadema ili zionekane kuwa licha ya kuungwa mkono na mikutano yake kukusanya wasikilizaji wengi kuliko wote si lolote. Ni kweli kuwa Mbowe hakushinda lakini kusema kuwa hakushika nafasi ya pili ni upotoshaji, waliona wakiripoti kama kura zilivyokuwa zimepigwa ingeonyesha kupunguza nguvu ya chama chao. Na hili hawakulitaka, CCM wanajua kuwa mpinzani wao kwa Tanzania Bara tangu 2005 ni Chadema na hili lilidhihirishwa na wabunge/madiwani waliopata. Kusema kuwa Chadema walipata wabunge wengi kuliko CUF bara harafu ukasema kuwa mgombea urais wao ameshika nafasi ya tatu ni kutupotsha.
HATUDANGANYIKI!!!!
 
Huyu ni hao hao tu hakuna jipya hizi ni kampeni za kwenye mitandao, huyu na mfananinisha na mhariri wa daily news la tr23/9/2010 uk wa 22
 
kaka majid umeanza kuchakachua sasa, au mafisafi wamekuchakachua tayari.
 

Asante Malafyale kwa kumjibu na konesha kinachomsukuma Maggid. Maggid amejidhalilisha sana kuandika kama vile anaowandikia ni wajinga. Mfano anaposema:"Wote wawili, Salma Kikwete na Ridhiwani Kikwete wana mvuto wa kisiasa unaoongezewa nguvu na wao kuwa wanafamilia ya Rais aliye madarakani na ambaye bado, kiukweli, ana mvuto kwa Watanzania walio wengi," anajidhalilisha kabisa.

Hayo anayoyasema hapo juu sikubaliani nayo kabisa. Kwanza hao anaowataja wanatembea sehemu mbalimbali nchini kwa maagizo ya Ikulu kupitia kwa wakuu wa Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri. Kuanzia Ikulu hadi huko wanakofika wanatumia raslimali za nchi (msiniambie nithibitishe). Wenyeji wanawapokea siyo kwasababu wana mvuto kwao bali wanaogopa kibarua kisiote nyasi. Huo uzushi wa mwandishi kwamba Salma na Ridhwani wana mvuto kwa watu unatoka wapi?

Kwa taarifa, mtu yoyote aliye na macho ya kuona na akili ya kuchambua mambo anajua kuwa badala ya hao kuwa na mvuto kwa watu kumbe ndiyo wanamwangusha JK katika harakati zake
 
huyu mdudu karudi tena. Bora mmleta hii utabiri wake hapa manake wengine hatutembelei tena liblogo lake la kifedhuli. Huyu jamaa amepewa mikofia na tshirt au heinkein kama tendwa 2005.simuelewi kabisa yeye anatuletea data za yeye na familia yake hapa?? Kakusanya wapi hizo detailszii vijiji vingapi yeye mjengwa kaenda?? Niana hakikaa hata kijiji chagu hajawahi kukisikia sasa/kule hata vibibi kizee wote wanakwambia Chadema MWANZo MwIsHO. Huyu mjinga anaongea nini , aua anatakaa watu tuhaki kablog kake? Kwanza bora kigazeti chake kilikosa soko akajitoa. Na nina uhakika hiki kijamaa kimeandika hii makala kikilenga wadau wa humu JF anajua kabila ss tutammind, sasa mpeni taarifa kuwa asikurupuke. Watanzania hawapo kwenye kakichwa kake na asirudie tena .
 
Huyu nae nyoko tupu. Anajifanya makini lakini hana mvuto huo na ndio maana hafanikiwi. Si alianzisha jarida juzi likafa? Hata nashindwa kumfafanua. Huyu bwana ni malaria sugu tu
 
siku matokeo yatakapotaganzwa aibu itakukubwa, maggid
umeichukulia negative... hakuna haja ya aibu bali kuna haja ya wapinzani kuchukua chambuzi hii na kuifanyia kazi constructively

Not every challenge you meet/face aims at degrading or defeating you

kafu na chadema chukueni hii muiwekee mbinu za ku-address
 
Maggid, Uchambuzi wako nimeupenda na umelenga pande zote muhimu.... Hakika huo ndio ukweli wenyewe ni kwamba Chadema hawana hawafiki popote na mbio zao za miti....Ni vizuri sana watu wakakubali ukweli na kuacha ubishi.... Saa sita usiku, unabisha unasema ni mchana mbona jua linawaka.
 
sidanganyikiii, the truth shall set us freei;
 

Majidi ..uchambuzi murwa sana huu. Ila sidhani kama ni utabiri kwani kama alivyogusia mchangiaji mmoja humu ndani kama mtabiri Tanzania ni mmoja tu naye ni.....!
 
Uchambuzi wa Mjengwa unaongozwaa na hisia zaidi na mazoea..Anaogopa mabadiliko na mwangi wake.
Anatambua nguvu Ya Dr Slaa na Cahdema kwa sasa na yeye kama makada wengine wana hofu ya pamojaa..

inashangazaa mchambuzii wa kiwango chake kuogopa mabadiliko hata yale yanayoonekaa kuletaa ukombozi wa maisha ya watu kama anavyopenda kutufundisha kupitia picha za blogu yake kuhusu maisha ya watanzaniaa vijijini..

najiulizaa sana je watanazania tatizo letu kubwa hasa wenye upeo wa mambo (wasomi wa darasana na wasio wa darasani) ni ukosefu wa KUNDI LA KATI KIUCHUMI AU NI KUTOJIAMINI HATA KWA UELEWAA TULIO NAO????????????
 

Sijui hata anaelewa anachosema. Upembuzi wake unachukuliwa kuwa historia ya 2005 itajirudia bila ya kutoa matongotongo kwanza na kujionea hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini ni tofauti na ile ya mwaka 2005. Vile vile inaonyesha hana uhakika pale anaposema labda Chadema ikijipanga vizuri..............sasa namweleza Chadema wamejipanga vizuri sana

Mimi sijui yupo humu nchni kweli?
 

as good as nothing....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…