Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Msanii,
Hawa ndio wanaoitwa establishment journalists ambao wako comfortable na status quo na hawataki kuona inabadilika. Nilishangazwa na hamaki ya Mkumbwa Ally, lakini baadaye nikafikiria nikaona u-CCM wake ulivyomweka ndani ya box. Pili kuna njama pia za chama tawala za kuonyesha kwamba juhudi za Dr. Slaa hazitamfikisha kokote na sasa zinaanza kuandikwa makala kuonyesha hivyo ili ifikapo Oktoba 31 CCM ifanye mipango yake ya kuchakachua. Hawataki kuona CHADEMA inakuja juu. Wako comfortable na Lipumba kwa sababu huyu wanajua limits zake. Ushindi wa Slaa utakuwa revolutionary na hawa establishment types watajikuta nje ya mapinduzi na comfort zone yao imetobolewa.
 
Siku matokeo yatakapotaganzwa aibu itakukubwa, maggid
 
Mjengwa, vijiji gani anazungumzia?

Labda vya kusini na pwani, ninakotoka mimi (Manyara) CCM vikao haviishi hadi saa 7 usiku kwa kuwa upepo wa JK na CCM ni mbaya, wanataka kuchakachua kura.
Nafikiri Mjengwa ni sawa na Sheikh Yahaya, tofauti ni kwamba Mjengwa anajua kutumia komputa kuandika mawaazo yake wakati Sheikh Yahaya anatumia nyota.

CCM hata kama CCM ikishinda, si kwa sababu ya K 3 za Jengwa mbali Uwizi wa kura, Ubabe wa kifisadi na matumizi mabaya Madaraka.

Mjengwa kama analamba miguu ya JK na CCM atuambie
 
Majidi kaolewe na Kikwete uwe mke wa tatu....Mjengwa si yule wa Global kila siku?Wale wale Wanaotafuta kujikomba kwa Kikwete kama MICHUZI....Viherehere wakubwa...tired of CCM...eti tathmni yako pwani...what about Arusha and other regions?

Bora umwambie hivyo, kule kwetu hatawasiojua kusoma na kuandika wanahamasishana kuleta mabadiliko lakini Majidi anakuja na ndoto za kuzimu kutupumbaza.

Nafikiri akili za Majidi ziko likizo ili ashiriki kwenye vituko vya kina Makamba ili apewe U-DC.
 
Hivi gazeti lake alilolianzisha limeishia wapi, lilikuwa linaitwa something ..Jamii>

Hakuna ubaya kutoa analysis kama hii. Tatizo ni pale inapokosa basis, analysis imekaa kitabiri wakati tunajua mtabiri tunaye mmoja tu nchi hii. Angetuambia amewahoji watu kadhaa sehemu kadhaa au angetumia matokeo fulani, lakini sasa unalala leo unapata hisia kwamba CUF itakuwa ya kwanza, kesho unapata hisia zingine kwamba CHADEMA itakuwa ya nne, then unaandika makala, ebo!!

Mbona wanaoota wapo wengi tu, lakini hawawezi kuandika kwa sababu ndoto haziwezi kuwa basis ya makala!!
 
Matokeo ya uchaguzi mwaka huu yatawashangaza wengi, hasa hao wanaoishi na takwimu za chaguzi ya nyuma.
 
Kwako Magid

Kwa jinsi ulivyo rudia hii post yako ya pili, Imedhihirisha kuwa wewe uko upande gani.
Na kuna linganishi tunazotoa zisizo na uhalisia. Kati ya wachangiaji na wewe nani ambaye ametoa linganishi zisizo na uhalisia?.
Kamtafute Michuzi akufundishe jinsi ya kujenga hoja za kitoto. kwa jinsi Mafisadi walivyojazana CCm we unadhani hata katiba ikibadilishwa
itakusaidia kapuku kama wewe.
 
Mimi huwa sisomi makala za huyu bwana maana huwa sioni kama kuna JIPYA.
 

Lilikuwa linaitwa 'KWANZA JAMII" na lilikufa kutokana na ukosefu wa wasomaji kwani lilikuwa ni kama vile linatayarishwa na taasisi moja ya CCM au serikali yeke!!!!
 
Mkuu Jasusi
amini nakwambia kwamba hawa CCM wapo radhi kuangusha mibuyu kadhaa ili tu wapate uhalali wa kuongoza. huyu maggid ameona mwenzake salva amekwaa ubosi pale ikulu na yeye anatafuta pa kutokea. Alipokuwa RAI alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanampamba sana JK na kutoa makala shededezi. hatimaye gazeti liliponunuliwa na RA alihama baada ya kuona jenerali kaja na new gazeti. tusimlaani bali tuwe waangalifu naye huyu spinner.

Mkumbo,
wapo wengi hawa. naamini hizi wiki za mwisho mwisho tutawafahamu zaidi.
 
Ombi naomba kujua Maggid Mjengwa ni nani na anafanya nini? nina sababu kubwa tuu ya kumfahamu huyu mtu.
 
Na sababu ya Dr Slaa kuondoka nafasi ya Pili kufikia ya Tatu ni nini?

Gaijin;
Hamna sababu yeyote ya kisayansi ambayo Mjengwa kaitaja zaidi ya kusema tu kuwa JK ana mtaji mkubwa wa kura utakaovuna kutokana na umaarufu wa mtoto wake Ridhiwani na first Lady Mama Salma

Kwa kuandika habari za kishabiki kwa wana habari wetu wa TZ;sikushangaa mwaka juzi ambapo mwana katuni mmoja nchini Kenya alipochora katuni kuwaonyesha waandishi wa TZ wakilamba miguu ya Rais JK na kujipendekeza;Waandishi wa TZ labda akiwemo hata Mjengwa na Michuzi walichukia kweli kweli kwa picha ile na kumtaka mchora katuni yule wa Kenya awaombe radhi;sina kumbukumbu kama radhi iliombwa!

Sasa mwandishi yule wa Kenya awaombe radhi waandishi wa model hii ya akina akina Mjengwa na Michuzi?
 
Je, wewe ni professional political analyst? Tendwa alitoa utabiri wake, Sheikh Yahya alitoa na anaendelea kutoa utabiri wake, na wengi tu wanaendelea kutoa utabiri wao na wengine kama serikali kupitia Daily News kutoa matokeo ya uchaguzi ngazi ya Urais. Ruksa kwani ndio freedom of expression hiyo ili mradi isiingize vitisho. Wewe basis yako ni uchaguzi wa serikali za mitaa. Je, ni watanzania wote walitilia umuhimu uchaguzi huo kama uchaguzi huu mkuu? Mbali na uchaguzi wa serikali za mitaa, information gani unatumia na unazipata wapi kufikia hizo theses zako?

It looks that you are a CCM fanatic/ bigot!
 
Unaota!!! Vijijini watu wamebadilika sana juzi nilikuwa naongea na rafiki yaku kutoka kyela anasema kabisa wanavijiji wanamwambia Mwakyembe ubunge tunakupa lakini swala la Urais kikwete si chaguo letu safari hii. Geita vijijini wananchi wanasema kabisa safari hii ni Dr. Slaa. Musoma vijijini walimu wanasema waziwazi kuwa tunampa Dr. Slaa. Sasa wewe unatoa tu maelezo bila data.
 
CCM wamesha chakachua kura kabla hazijapigwa, wanachofanya sasa ni kuanza kuwaandaa wananchi wakubali uchakachuaji huo, na amini analysis ya magid ni handout toka TISS ya jinsi matokeo yatakavyotangazwa na NEC. ANGALIZO: Ole wenu CCM NA VYOMBO VYENU DHALIMU , SAFARI HII TANZANIA HAITATOSHA.
 
Poor Majidi,
Umejikita sana kutabiri nani atashinda au nani (very selected topic for you) atakuwa wa kwanza wa pili au wa tatu, old story! ulishaongelea zamani; sasa hivi umefanya number changes ..... number 2 anakuwa wa tatu na namba 3 anakuwa wa pili... lakini message kwetu JK ni mshindi wa wa Uchaguzi huu. That is your message; First what is your motive on all this analysis to us; maybe if we know your motive then I can comment! But for sure, i am very convinced with other writers above; our journalists are too cheap; you 're making ELECTION TIME as a capital for you to get known to acheve something as you 're making your "gamble".
By the way unge"combine" kidogo hata hizi topic ambazo una-comment; hii ya nani atashinda ulishasema zamani; unaonaje (ingawa ni uhuru wako) ungetoa maoni yako kuhusu the following:
Dr Slaaa will never be the 5th President - By Daily NEWS
NEC/Usalama wa Taifa/Tendwa etc
Matumizi ya mapesa; SALMA/JK/MTOTO na zile HELKOPTA za MAFISADI
MIkutano ya wapinzani kuvamiwa etc

You have many to comment to see that you're not biased; but as long as your have that motive (a hidden motive); you're stuck at this irrelevant topic. This infact will be known only on that date, 31st of October; but what we have to discuss now is about the "going" to that date!
 
mjengwa nahisi kinachomsumbua ni siasa fulani zenye chembe ya udini nakutokukubali ukweli lakini pia ni swahiba wa michuzi naiona synopsis katika utararatibu wao wa kutoa habari, ni wa kumpuuza tu anajua kilicho moyoni mwake huyu.
 
Hawa ni wale wanaowakuwadia mafisadi, wakichumia matumbo yao, na kutarajia kupata vyeo. Ukuu wa Wilaya, Ukuu wa Mkoa, Ukatibu Mkuu, na kadhalika!

Unaweza kumpeleka ng'ombe kisimani, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji ya kisima KAMA HATAKI!

Basi, tutawapeleka wananchi kupiga kura, lakini hatuwezi kuwalazimisha kuwachagua tunaowataka sisi. KAMWE usimdharau mtu aliye masikini, akihisi HANA CHA KUKOSA utakiona cha mtemakuni!
 
Mimi nawaomba Watanzania wenzangu mzichukulie hizi tathmini za akina Maggid Mjengwa kwa tahadhari kubwa kwani hazitolewi kwa nia nzuri au kwa bahati mbaya. Watanzania tunatayarishwa mapema kisaikologia kupokea matokeo ya huu Uchaguzi ambayo mpaka sasa dalili zote zaonyesha kuwa hayatawakislisha maamuzi sahihi ya wapiga kura. Watu kama Maggid Mjengwa na Mkumbwa Ally ni kama vyombo tu (tools) ambazo zinatumika kutuchanganya na kutuvunja moyo (break our will) mapema kabla ya kujikuta uso kwa uso na mbinu zinazoandaliwa za kimafia.

Juzi tumeshuhudia gazeti la Umma linaloendeshwa kwa kodi ya wananchi likitamka wazi wazi kuwa Dr. Slaa hawezi kuwa Raisi wa nchi hii si kwa sasa wala baadaye. Pamoja na kelele na malalamishi ya wazalendo dhidi ya matamshi haya ya hatari tumeshuhudia vyombo vilivyopewa mamlaka ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi na kudhibiti vurugu vikikaa kimya bila kuwakemea wahusika. Mathalan hivi sasa magazeti mawili ya Umma, Daily News na Habari Leo yameamua kuandika habari za wagombea wa CUF na CCM na inapobidi za Chadema pale tu inapohusu mgongano au kashfa.

Ni wazi kuna mipango mahsusi ya kukidhoofisha chama cha Chadema na mgombea wake Dr. Slaa na vyombo vikuu vinavyotumika mpaka sasa ni vya dola/Umma . Nina hakika tunavyozidi kukaribia uchaguzi ndivyo hizi tathmini uchwara kama hii ya Maggid Mjengwa zitakavyoshika kasi. Lengo ni kututayarisha kisaikolojia kwa mchezo mchafu wenye baraka za dola na hivyo kupunguza hasira za wananchi dhidi ya kitendo kama hicho. Mfano moja mzuri ni kufichwa kwa matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Synovate yaliyompa Dr. Slaa ushindi. Hatudanganyiki !
 
Maggid,hapo huna jipya na hoja zako zinashikilia CUF kubakia nafasi ya pili,kiukweli kwa jinsi hali inavyoendelea CHADEMA YA KWANZA,CCM YA PILI,CUF YA TATU.Mimi binafsi ni kati ya wengi ambao tulimpigia Kikwete kura 2005,but this time kura yangu kwa CHADEMA.Ni chama pekee enzi hizi ambacho kinaweza kuendesha gurudumu la mabadiliko.CUF CCM i say no,hukuna jipya mtakaloweza letea watanzania.Afu makala yako ni hafifu sana,hivi wewe hujaiona mikoa ya mwanza,arusha,manyara,singida,kilimanjaro,musoma,morogoro,iringa,mbeya,dar es slaam,rukwa,kigoma na kagera ambako CHADEMA jinsi hali inavyoendelea inaelekkea kuchukua majimbo mengi ktk mikoa hii.Hali ya siasa inavyoendeleam ktk maeneo haya ni kwamba wananchi wanayo kiu kubwa ya mabadiliko.Na kwa uchunguzi wa wanaharakati wetu ktk maeneo haya CHADEMA ina zaidi ya 50% supoti kutoka kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…