Mjadala waDowans(ITV) na Audi alteram partem | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala waDowans(ITV) na Audi alteram partem

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KAUMZA, Jan 14, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nimeupenda sana mjadala wa leo lakini nadhani ningeupenda zaidi kama kanuni ya audi alteram partem"hear the other side" ingefuata. Kwangu mimi naona mjadala huu umekuwa ni wa upande mmoja sana na hivyo unatufanya tushindwe ku-balance hoja mbili zinazovutana. Hii inaonesha wazi inawezekana mjadala huu umeandaliwa na watu fulani kwa ajili ya kuwakandamiza watu fulani. Kiutaalamu, katika mada kama hizi ni vema sauti za pande mbili zingesikika.

  Tujadili uhalali wa mjadala wa upande mmoja
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mmh, hivi kwani mkuu ukiambiwa 1+1=2, ni lazima upate na hoja ya upande wa pili ili kujua kama hesabu ni sahihi?
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wamealikwa wamekacha si unajua kikaango
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  NIngependa kama ungechangia kwenye mjadala wenyewe sio kujaza upupu na kujaza server

   
 5. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Miss Judith!! katika sheria haki ya asili"natural justice" ni kitu muhimu sana na ukitoa hukumu bila kuzingatia haki ya asili ya kusikiliza pande zote basi uamuzi wako utakuwa batili na utatupwa tu. Na ndio maana hata mtu akikamatwa ndani ya nyumba ya mtu akiiba, mahakama haiwezi kumfunga mpaka isikilize utetezi wake.

  Kilichotokea leo ITV swali la kipima joto lilikuwa JE SABABU ZA KUILIPA DOWANS NI ZA MSINGI?? Binafsi nimeshindwa kutoa jibu japo kimoyo moyo kwa kuwa sijausikia utetezi wa upande wa pili
   
 6. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Rejea majibu yangu kwa Miss Judith. King of kings, tumia lugha nzuri. Hii ni sheria kaka, no blah blah
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mjadala wa television si mahakama, ila kla kitu kwenye mjadala is judged on its own merit. nijuavyo mimi pamoja na haki ya kusikilizwa, kuna wakati mahakama huwa inasikiliza upande mmoja na katika hali kama hiyo nakuna guarantee kuwa anayesikilizwa atashinda.mfano licha ya kusikilizwa peke yake akisema kwa mfano 1+1=3 mbele ya jaji wa hakihawezi kushinda na kama ni jela atenda!
   
 8. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Swali la kipima joto lilitutaka sisi watazamaji tuamue kama sababu za kuilipa Dowans ni za msingi au la! Niambie Miss Judith, ungeweza vipi kutoa uamuzi bila kuusikiliza upande wa pili? Kma wewe ni mwanasheria nadhani unafahamu kuwa katk kutoa uamuzi huwa tunapima hoja zinazowasilishwa na wahusika wa pande zinazovutana na wala huwa hatuangalii tukio. Ndo maana mtu anaweza kubaka kabisa na umati wa watu ukashuhudia lakini mbele ya hakimu akatoka kidedea kwa kuwa tu ametoa hoja nzito kuliko upande wa mashtaka.

  Labda unielekeze maana hakuna ajuae kila kitu. Ni mazingira gani natural justice haipewi uzito? Naomba unipe na authorities
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kaumza, kwa upandee wangu ule haukuwaa mjadala ingawa uliitwa mjadala, kilichokuwa kinajadiliwa ni nini? Ni kuwa Dowans ilipwe au isilipwe? sasa wale wote waliokaa pale wanasema isilipwe, kuna mjadaala hapo? In my view, sio mjadala.
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  unadhani RA au EL au NK wangeitwa aje hapo wangeweza kuja?
   
 11. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waziri Ngeleja aliitwa lakini kasafiri yuko China. Angekuwa na busara za kutosh angetuma muwakilishi ila hakufanya hivyo. Ulitaka waairishe mdahalo?
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wangekuwepo wa size yao pale wangekuja, vile vi feather weight vilivyowekwa pale hata wanachokiongea hawakielewi ukawapambanishe na miji heavy weight? ustake ncheke!
   
 13. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ulijaa ushabiki. Hata hivyo Rugemereza alikuwa mwangalifu sana katika ku draw conclusions. Tunataka hao ambao 'hawakutendewa haki wajibu mapigo" nao.
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  upande wa pili unaotaka ni upi?matamko ya serikali yako wazi na hukumu ya icc walikuwanayo,wamejadili hayo matamko kama yako right or not.usilete porojo na spin za ajabu ajabu,wasaliti kama nyinyi na wamiliki wa dowans mnastahili adhabu ya kunyongwa mpaka mfe.
   
 15. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Mkuu KAUMZA, upande wa pili unaousema wana kiwanja chao kinaitwa TBC, wajadili huko wakitaka (of course hawawezi diriki), sisi wananji tuta-balance wenyewe mbele kwa mbele!
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mkuu hakuna ushabiki pale bali ni hisia kali za watu waliochoshwa na udhalimu!yaonekana wewe ni mmoja ya wale mnaokula mkate kwa jam!
   
 17. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nddo maana nikasema tujadili facts in issue na si facts tu. Kamati ya Bunge liliilazimisha serikali ivunje mkataba na pia isinunue mitambo ya Dowans. Wanaoona mbali pamoja na Zitto Kabwe wakasisitiza ni bora serikali iinunue mitambo hiyo. Na kwa kuwa serikali ilikuwa imeingia uaoga hasa kutokana na minyukano ndani ya Bunge na Mwakyembe ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati kuitisha serikali kuwa "tutakutana bungeni", ikaamua kutoinunua mitambo hiyo. Leo tunailazimisha serikali isilipe hizo sh 94bl, na tukuchelewa kulipa ndani ya siku chache zijazo tutalipa sh 94bl+7.5%. Tulishafanya kosa kwa kukubali vipengele vigumu na vinavyotubana ktk mkataba. Ushauri wangu ni kuwa tulipe baada ya hapo tuwe makini ktk kuingia mikataba hasa inayohusu biashara za kimataifa. Kwa sasa hata tukimjua mchawi ni nani haitasaidia. Tuweke siasa pembeni, tudili na sheria
   
 18. m

  mams JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35


  Ktk mjadala kuna upande huelemewa na hivyo kuishiwa point. Wanaotetea dowans ilipwe wanaongea kwa vificho au kuongelea pembeni. Kulikuwa na nafasi nyingi za kuitetea dowans hata kwa kupiga simu hawakufanya hivyo ukiwamo wewe!
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jan 15, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kisheria ni moja ya nguzo ya Kanuni za Haki za msingi (Principles of Natural Justice)!
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu r u siriazi? yaanni watu wafanye uzembe makusudi kutusababishia hasara yote hiyo halafu tuwaache tu? Kuna trend nimeiona kuhusu watu wote wanaokubaliana na Dowans ilipwe kwa kisingizio cha rule of law hakuna anayesuggest hatua kali kuchukuliwa kwa waliotusababishia upuuzi huu. As such tunafika mahali et "tusitafute mchawi'. Who is this so called mchawi? na kwa nini asitafutwe? Tutajifunzaje kama mambo yenyewe ni free ride tu namna hii?. Kwa nini tusitengeneze utaratibu as such mtu akiona majukumu ya kazi anayopewa yanamzidi uwezo akatae?

  Yaani Dowans walipwe halafuj maisha yaendelee tuj kama kawaida kwa wale waliotuingizia hasara hii? Who r we tring to protect here?
   
Loading...