Mjadala wa Ushauri na tiba ya maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)

Vigeuze maandishi yaonekane.
Maandishi madogo sana hayawezi kuonekana, box lake hilo waweza angalia.

1573318337319.jpeg
 
Kunywa chai ya mchaichai. Kunywa maji vugu yenye unga wa mlonge. Kunywa maji yenye uwatu.
 
Wakuu habari.

Ni muda mrefu sana nasumbuliwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Yaani nikiingia tu napata maumivu makali na kutapika juu kila siku.

Nmeenda hospitali wanasema ni hali ya kawaida napewa tu dawa za kutuliza maumivu but nikinywa siku nyingine zinadunda kabisa hazitulizi.

Mazoezi nafanya na maji ya moto najikanda sioni nafuu nimechoka jamani anayejua dawa ambayo itaniponya maana natamani hata ikifika siku zangu maumivu nimuhamishie mtu maana shughuli hazifanyiki na hata ikiwa siku ya kazi siwezi kwenda kazini kabisa.

Msaada jamani.
 
Habari zenu wakuu.

Nina mpenzi ambaye mara nyingi anapokuwa katika siku zake analalamika sana maumivu makali sana ya tumbo
naona hali hii imekuwa kama mazoea.

Niliwahi mpeleka hospital kwa vipimo nilikuwa nikihofia afya yake ya uzazi lakini Dr alisema mfumo wa uzazi upo vizuri akatupatia vidonge fulani.

Lakini naona hali imekuwa ile ile sasa anasema kuna wamama wamemshauri abebe ujauzito itamsaidia so sasa hivi ananisumbua anataka ujauzito.

Naombeni mniambie hii inatokana na nini? Na ni vipi naweza msaidia
 
hili tatizo lipo na linatesa wanawake wengi, anaefahamu tiba yake au jinsi yakuweza kupata dawa tafadhali anisaidie
 
mkuu tunaweza kuwasiliana au kunisaidia?
Mkuu nenda sehemu inaitwa Kihurio (bagamoyo) kwa wapare huko,kuna mzee ana dawa si ya kubahatisha bora tu mke ana na mayai na wewe uwe na uwezo wa kutia mimba.Huyu mzee akikupa dawa havuki mwezi.nilikuwa na rafiki yangu alihangaika miaka 4 bila mimba alivyoenda kwa babu hakuvuka mwezi,mzee dawa zake sio za ramli bali ni za kunywa tu.chango ni sumu ambazo mwanamke anakuwa nazo,husababishwa na dawa zote za uzazi wa mpango au vyakula vyenye sumu.
 
Habarini wakuu wangu, natumai mu wazima.

Pamoja na kwamba mimi nikachepukaji kazuri lakini kuna sehemu nilisha wekeza mtoto mmoja mzuri sana

Sasa yule mtoto bhana ananiambia kuwa tumbo humuuma sana kila anapo ingia piriodi. Sasa anasema amejaribu kuomba ushauri wa dawa ya kutumia ili walau kutuliza maumivu. Watu wengi wamemwambia hako ka tatizo hakana dawa

Sasa wakuu naombeni ushauri juu ya hili nipate kumwokoa huyu binti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom