Mjadala wa Ushauri na tiba ya maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Jamani, girlfriend wangu anasumbuliwa sana na tatizo la maumivu kipindi cha bleeding, kwa wanaojua kama kuna tiba yoyote ambayo inaweza kumsaidia huyu binti, naombeni mawazo. Maana huwa anapata maumivu makali sana. Nawakilisha.

Naombeni ushauri wenu wa kitabibu

Asanteni
1580456617206.png



WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI
Habari zenu wana jf.

Jaman mimi nasumbuliwa na tumbo nikiwa katika hedhi linauma saaana hadi naweka maji ya moto kwenye chupa napitisha kwenye tumbo panachemka ndio naweza kulala.

Hii hutokea siku ile ya kwanza, maumivu hupungua kadri siku zinavyokua zinasogea.

Tangu nakua sikuwa na shida hii sasa nashangaa na pia nimeolewa ni miezi tisa sasa sijapata ujauzito msaada tafadhali.
---
Hi Doctor,

Naomba msaada kwa hili Doctor. Nina mchumba ambae nategemea kufunga nae ndoa siku chache zijazo. Mchumba wangu huyu ana tatizo la kuumwa na tumbo sana (hadi analia na kugaragara) pindi anapoingia period. Huumwa kwa muda wa siku mbili. Je, tatizo hili linatokana na nini? Na tiba yake ni nini? Naomba msaada wako nimuokoe kwenye maumivu haya. Asante sana
---
Habari wanaJF,

ninaomba msaada wenu. Mimi ni mwanamke aged 37, kawaida katika mzunguko wangu wa hedhi huwa napatwa na maumivu makali sana hasa day1 na 2. sasa naona tatizo limeongezeka maana ikishapita wiki moja baada ya hedhi ninapatwa na maumivu makali sana ambayo yanaweza kudumu kwa siku nzima au masaa zaidi ya 12.

Maimivu haya huwa chini ya kitovu ni makali kiasi nashindwa kusimama au kunyanyua mguu. Nimetibiwa hospitali mbalimbali lakini naona hakuna alieweza kunipa sababu kamili ya maumivu haya zaidi ya kuhisi labda hutokea kipindi cha kupevuka yai au. Mimi sijabahatika kupata mtoto japo mimi na mume wangu tumepimwa na kuonekana hakuna mwenye tatizo kati yetu na tatizo la maumivu wakati wa hedhi niliambiwa labda baada yakupata mtoto yangeisha.

Naombeni msaada wenu doctors wa jf na yeyote aliekutana na tatizo hili hata ushauri tu utafaa ninateseka sana. huwa natumia diclopar kupunguza maumivu wakati mwingine nazidisha dose ili niweze kupata usingizi.

Nisaidieni niondokane na tatizo hili

===

USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU
KILA mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika.



DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.


MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.
Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.



JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.


Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho Apiol ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.


TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.


UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.



Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.



PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na stress au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)
---
View attachment 713534
Katika mfululizo wa mada zetu za leo, tutazungumziia matatizo yanayoambana na hedhi. Wanawake wengi hupata matatizo kabla ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi na mara ya baada ya kukoma hedhi. Nafikiri ni wakati muafaka wa kulizungumzia pia tatizo la kukosa kabisa hedhi. Katika kila moja ya hayo, tutajaribu kuona sababau za tatizo na jinsi ya kuepuka tatizo hilo.

Tunaanza kwa kulitazama tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (Premenstrual syndrome). Premenstrual syndrome ni hali ambayo humwathiri mwanamke kihisia, afya yake aya mwili na tabia yake katika kipindi fulani cha mzunguko wake wa hedhi, kwa kawaida kabla tu ya kuingia mwezini. Tatizo hili ni la kawaida kwa wanawake na huathiri karibu asilimia 85 ya wanawake wanaopata hedhi. Maumivu huanza siku 5 hadi 11 kabla ya kuanza hedhi.

Kuna mlolongo wa dalili za tatizo hili la maunmivu kabla ya hedhi, lakini mwanamke anaweza kupata baadhi ya dalili zifuatazo:

Dalili Za Kihisia Na Kitabia

RpsQeM6TIjsmEj2Qnxrpl-M-te20nmjyQjcbkzYARHh_Se54EGTonYInzxZjuRxxj0o2oGFFDW2_7Oj4cZrjmr1B_4_8AoFK-fUxNo_SE-vVYt1f6oBL82ihdxCPuaK_JXxCRC44rzboPhEu=s0-d


. Kuwa na msongo wa mawazo au wasiwasi
. Kuwa na mfadhaiko
. Kulialia
. Madadiliko ya mara kwa mara ya kihisia na hasira
. Mabadiliko ya ulaji na kupenda sana kula
. Matatizo ya kupata usingizi
. Kujitenga na jamii
. Kushindwa kutuliza mawazo

Dalili Na Mabadiliko Katika Maumbile ya Mwili

. Maumivu kwenye maungio ya mifupa na misuli
. Kuumwa kichwa
. Uchovu
. Kunenepa
. Maumivu kwa mbali maziwa yakiguswa
. Kuchipuka kwa chunusi
. Kukosa choo au kuharisha
Kwa baadhi ya wanawake, madadiliko haya ya kitabia na maumivu ya mwili yanaweza kuwa makubwa kiasi cha kuathiri shuguli zao. Pamoja na kuwa wengine huathirika sana, matatizo haya huisha ndani ya siku nne baada ya kuanza hedhi.
Kwa wanawake wachache, maumivu haya ya kabla ya hedhi huwafanya washindwe kabisa kuendelea na shughuli zao za kila siku, na huwatokea kila mwezi. Aina hii ya PMS huitwa premenstrual dysphoric disorder (PMDD).
Dalili za premenstrual dysphoric disorder ni pamoja na mfadhaiko, hisia za ghafla zinazobadilika, hasira, wasiwasi, kushindwa kufikiri, hasira za ghafla na kuwa na msongo wa mawazo.

Chanzo Cha Maumivu Ya Kabla Ya Hedhi – Premenstrual Syndrome

Chanzo kamili cha tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi hakijathibitika, lakini sababu zifuatazo zimeonyesha kuwa na mchango mkubwa:
. Mabadiliko Katika Mzunguko Wa Homoni. Dalili za maumivu kabla ya hedhi zinabadilika na mabadiliko ya homoni katika mzunguko wa hedhi. Viwango vya homoni ya estrogen na progesterone huongezeka wakati fulani katika mwezi. Mwongezeko huu husababisha mabadiliko ya mara kwa mara ya namna mwanamke atakavyojisikia, kuleta wasiwasi na kusababisha hasira za haraka.
. Mabadiliko ya viwango vya kemikali katika ubongo. Mabadiliko katika viwango vya serotinin katika ubongo vinaaminika kusababisha premenstrual syndrome. Viwango vya Serotinin huathiri namna mwanamke atakavyojisikia. Serotinin ni kemikali katika ubongo inayoamsha namna ya kujisikia, hisia na mawazo. Kuwa na kiwango kidogo cha serotinin kunasababisha mfadahiko, uchovu, kupenda kula sana na kukosa usingizi.
. Mfadhaiko. Wanawake wengine waliobanika kuwa na matatizo mazito ya maumivu kabla ya hedhi, walikuwa na mfadhaiko, ingawa mfadhaiko huo haukuwa sababu ya matatizo yao yote.

Mambo Ya Kufanya Kupunguza Maumivu Ya Kabla Ya Hedhi

Unaweza kuondokana na au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hedhi kwa kufanya mabadiliko katika namna ya kula, kufanya mazoezi na namna unavyoishi kwa ujumla. Unaweza kujaribu yafuatayo:
Badili Namna Ya Kula
. Punguza mlo, kula mara nyingi zaidi kuzuia tumbo kuvimba na hali ya kujisikia tumbo limejaa
. Punguza chumvi na chakula chenye chumvi nyingi kuzuia tumbo kujaa
. Chagua chakula chenye complex carbohydrates, kama matunda, mboga za majani na nafaka nzima
. Chagua chakula chenye uwingi wa calcium
. Jizuie kutumia kahawa na pombe
Jipangie Ratiba Ya Mazoezi Ya Mwili
Panga ratiba ya kutembea angalau kwa dakika 30, kuendesha baiskeli, kuogelea au mazoezi mengine ya kukutoa jasho siku kadhaa kwa wiki. Mazoezi ya kila siku yataboresha afya yako na kukuondolea baadhi ya dalili, kama uchovu na mfadhaiko.
Punguza Msongo Wa Mawazo
. Pata usingizi wa kutosha
. Fanya mazoezi ya misuli au upumuaji mzito ili kuondoa maumivu ya kichwa, wasiwasi na matatizo ya kukosa usingizi
. Jaribu kufanya yoga au massage ili kuondoa msongo wa mawazo.

Tiba Ya Maumivu Kabla Ya Hedhi

Kwa wanawake walio wengi, kubadli mtindo wa maisha kumweza kuwasaidia kuondokana na PMS. Kulingana na ukubwa wa tatizo, daktari anaweza kukuandikia dawa moja au zaidi ya dawa za kusaidia PMS. Utendaji kazi na msaada wa dawa hizi hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine. Dawa ambazo hutolewa ni pamoja na:
.Mefenamic Acid
. Antidepressants
. Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs)

Tiba Mbadala Ya Maumivu Kabla Ya Hedhi
Kuna vitu vinafahamika kuondoa au kupunguza makali ya tatizo la maumivu kabla ya hadhi:
. Calcium. Kupata calcium ya kutosha katika mlo au matumizi ya vidonge vya calcium kunaweza kuondoa dalili za maumivu kabla ya hedhi – premenstrual syndrome.


. Magnesium. Kutumia magnesium kila siku kutasaidia kuondoa maumivu ya kwenye maziwa na kujaa kwa tumbo kunakoambatana na premenstrual syndrome.
. Vitamin E. Matumizi ya vitamini E ya kila siku yanaweza kuondoa PMS kwa kuzuia utengenezaji wa prostaglandins, namna ya homoni inayosababisha mkakamao wa misuli na maumivu kwenye maziwa.
. Tiba ya mimea. Baadhi ya wanawake wameeleza kupata nafuu ya PMS kwa kutumia mimea kama ginkgo, tangawizi, chasteberry na mingine ingawa njia hii haijathibitishwa na vyombo vya kusimamia chakula na dawa.
Katika ukurasa unaofuata, tutazungumzia tatizo la maumivu wakati wa hedhi (Dysmenorrhea). Katika kurasa za mbele tutazungumzia tatizo la kukosa hedhi (Amenorrhea) na matatizo baada ya kukoma hedhi (Menopausal syndrome).
Tunaomba mchango wako wa mawazo kuhusu mada hii, na usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (PMS).


TATIZO LA MAUMIVU KABLA YA HEDHI (Premenstrual Syndrome – PMS) - DOCTOR JOH
---
Pill to end period pain: Drug that brings relief for millions of sufferers could be available by 2010

A drug that could free women from the misery of period pain has been devised by scientists. The 'hot water bottle in a pill' is designed to tackle the cause of the crippling cramps that plague up to 90 per cent of young and middle-aged women each month.
Taken ahead of a woman's period, it could prevent the pain.

Alternatively, it could be taken when required, easing pain when it hits. Likely to be prescription only, the drug could be on the market in just four years. Its inventors at Southampton-based drug firm Vantia Therapeutics said that they are confident it will work better than any of the drugs or treatments currently available.

Period pain, or dysmenorrhea, blights the life of between 45 and 90 per cent of women of child-bearing age and is the leading cause of absenteeism from school and work in women in their teens and 20s.

The pain is caused by the womb contracting during a period.

The new drug reduces levels of vasopressin, the hormone controlling the movement of the womb's muscles. Preliminary tests on a small group of women showed it to be safe, with no side- effects, an American Chemical Society conference in California heard.

A larger trial on more than 100 British and American women with bad period pain is already under way and the results are due later this year. If the drug fulfils its promise, it could earn Vantia a large chunk of the £600million-plus spent on period pain relief each year around the world.

Current treatments range from powerful painkillers and versions of the Pill, to relaxation techniques and hot water bottles.

But some tackle the symptoms rather than the cause, others cause upset stomachs or mood swings, and none work for all.

Vantia scientist Andrzej Batt said: 'We hope that the drug will provide a more effective treatment option for millions of women worldwide with this painful condition.

'Dysmenorrhea not only diminishes the quality of life for millions of women but also has a hidden, society-wide economic cost that involves an enormous number of days lost from work and school.'

Oily fish 'prevents endemetriosis'
Eating plenty of oily fish can protect against endometriosis, a cause of infertility which may affect two million British women, say researchers.

A study of more than 70,000 nurses found that those who ate the most tuna, salmon, mackerel and other foods high in omega-3 fatty acids were 22 per cent less likely to develop the painful condition.

But those whose diets were laden with harmful trans fats found in thousands of products from cakes and biscuits to pies and chips were 48 per cent more at risk, according to the findings published online in Human Reproduction.

Source: Daily Mail
---
KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya. Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata wakina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini pale anapopatwa na tatizo hilo.

Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.

AINA YA MAUMIVU

Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Ya kwanza ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano wanasema kuwa hupata maumivu makali.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

Sababu hizo ni kama kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka damu nyingi wakati wa hedhi, wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

Endometriosis: Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kutoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo

Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.

PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.

Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

Baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. niliishia kuelezea ugonjwa wa uvimbe katika nyonga ambao husababishwa na magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya zinaa.

Dalili za ugonjwa huo ni:

1. Maumivu kuja na kuondoka, kwa kiwango tofauti (spasmodic).

2. Maumivu zaidi huwa sehemu ya chini ya tumbo na huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka mapajani.

3. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.

4. Kupata choo laini au hata kuharisha na wengine hufunga choo.

5. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.

6. Kupata maumivu ya kichwa, kujisikia kuchoka.

Kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua bila hata msaada wa daktari.

USHAURI

Iwapo mwanamke atapata maumivu makali sana ni bora akamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu nini chanzo cha maumivu hayo kuwa makali.

MATIBABU

Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS). Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.

Pia wanawake wanashauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu hayo, kama kuoga maji moto, kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo, kufanya mazoezi kama yoga, meditation, kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.

Vilevile unaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:

Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, kafeini, sodium na sukari, kufanya mazoezi ya viungo, kujiepusha na wasiwasi na mawazo na kuepuka kuvuta sigara.
---
mamii90,

Tatizo lamaumivu makali wakati wa hedhi (dysmenorrhoea) hutokea wanawake wengi tu, hasakati ya miaka 18 mpaka 25 au 26 hivi, na wengine zaidi ya miaka hiyo. Na wakatimwingine maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kuingiliana na shughuli zako zakila siku kama shule, kazi, hata shughuli za nyumbani. Ni moja ya sababu kubwa yaabsenteeism mashuleni na kazini.

Mara nyingi,kwa wanawake ambao kwanza walikuwa na siku za hedhi kawaida tu, halafu inatokeabaadae wanakuwa na maumivu makali wakati wa hedhi, basi chanzo chaweza kuwatatizo tunaita endometriosis, au fibroids, wakati mwingine njia ya uzazi wampango ambayo kuna device wanaweza ndani ya kizazi (IUD), maambukizi ya njia yauzazi, au hata msongo wa mawazo (stress, depression).

Na kwawanawake ambao wao tangu kuvunja ungo ni maumivu tu kila anapokuwa hedhi, maranyingi sababu huwa ni vichocheo (hormonal) mwilini hasa vinavyohusiana na mfumowa uzazi.

Ushauri:Jaribu kumuona daktari akuchunguze kama maumivu yako ni kwa sababu zinazotibikakama endometriosis, fibroid, IUD, infections etc. Na kama ni hormonal basiakushauri nini cha kufanya.

Unawezapunguza maumivu hayo ukiwa nyumbani kwa kulala kiupande, kunyanyua miguu wakatiumelala, kutumia chupa maalum ya maji ya moto (heating pad), massage laini yatumbo, kunywa vinywaji vya moto , relaxation techniques kama yoga, hotshower/bath, na husipokuwa kwenye hedhi kufanya mazoezi hasa ya kutembea.

Dawa maranyingi ni za kutuliza maumivu NSAIDs mfano Ibuprofen (japo haishauriwi kutumiakila mara, kila uumwapo tumbo).
 
Inabidi akacheki kama ana uvimbe kwenye mji wa uzazi (Fibroids)...moja ya dalili zake ni pain during menstruation ikiambatana na Heavy menstrual bleeding (menorrhagia).

Pia kuna wengine huexperience Pain during sex. Other symptoms are abdominal pain or pressure, changes in bladder and bowel patterns and, in some cases, infertility.

It is better to get checked from a gynacoelogist to rule out the right thing!!

Hope nimesaidia kidogo
 
Last edited:
Mkuu ni maumizvu ya tumbo au wapi?
what i know kuna wale wanaopata maumivu ya tumbo wakiwa hedhi na upande wangu nako kuna tatizo hilo naomba suluhisho pia.....
 
Mkuu ni maumizvu ya tumbo au wapi?
what i know kuna wale wanaopata maumivu ya tumbo wakiwa hedhi na upande wangu nako kuna tatizo hilo naomba suluhisho pia.....

Mazee kama maumivu yanaamabatana na dalili nilizoainisha hapo juu ni vizuri mkamwona gynacoelogist!! kama hakuna dalili zingine huenda ni Ovulation tu...lugha yepesi yai linapokuwa linatoka kwenye ovaries kuja kwenye mji wa mimba huambatana na maumivu kidogo!!

Cheers
 
Mazee kama maumivu yanaamabatana na dalili nilizoainisha hapo juu ni vizuri mkamwona gynacoelogist!! kama hakuna dalili zingine huenda ni Ovulation tu...lugha yepesi yai linapokuwa linatoka kwenye ovaries kuja kwenye mji wa mimba huambatana na maumivu kidogo!!

Cheers
yah mkuu maana mwanzoni hakuwa na tatizo hilo.......au kufanya mapenzi akiwa hedhini inasababisha pia?
 
Masa, tofauti ya "mayoma" na "Fibroids" ni ipi?

Myoma ni kama tumour na Fibroids ni uvimbe tu...

Myoma is worse zipo aina 2

* The leiomyoma occurs in the skin or gut but the common form is the uterine fibroid.
* Rhabdomyomas are rare tumors of muscles, they occur in childhood and often become malignant.

Nimekujibu?
 
Myoma ni kama tumour na Fibroids ni uvimbe tu...

Myoma is worse zipo aina 2

* The leiomyoma occurs in the skin or gut but the common form is the uterine fibroid.
* Rhabdomyomas are rare tumors of muscles, they occur in childhood and often become malignant.

Nimekujibu?

Katika hesabu tunasema UTERINE FIBROIDS ni subset ya MYOMA hivyo huwezi kutofautisha tu kwa tumour vs. uvimbe; afterall TUMOUR na UVIMBE ni kitu kilekile katika lugha tofauti.
 
Mara nyingi maumivu haya yanapotea mwanamke anapopata mtoto,ikiwa hakuna complication zozote which is possible kitakachomsaidia ni dawa za kutuliza maumivu tu hadi hapo atakapopata mtoto then ataona mabadiliko no pain ...not proffessional just from experiance. I know how you feel mimi nilikuwa silali baba ndio ukubwa huo.honestly mwanzo nilifikiri anadeka mpaka nilipopata somo.vumilia kaka.
 
Sahiba you are right. Nilikuwa na tatizoi hilo sana wakati wa usichana wangu. Kilichonisaidia ni baada ya kujifungua likaisha sasa hivi hata sijui maumivu wakati wa hedhi.

For the time being kima hana dalili ulizoorodhesha, atumie dawa za kutuliza maumivu
 
Sahiba you are right. Nilikuwa na tatizoi hilo sana wakati wa usichana wangu. Kilichonisaidia ni baada ya kujifungua likaisha sasa hivi hata sijui maumivu wakati wa hedhi.

For the time being kima hana dalili ulizoorodhesha, atumie dawa za kutuliza maumivu


Asante sana dada Caro kwa Ushuhuda wako, Maana this problem huwa linamtokea during bleeding na anakuwa na maumivu makali ya tumbo na sometimes huwa anatamani mtu amkande kwa maji ya uvuguvugu. but thank you all for sharing your experinces.
 
pole, she's not alone, wengine tunakuwa wagonjwa kabisa. unapatwa na nausea na huna raha. Tell her ajaribu painkillers, indocid works very well for me, pia akiwa nyumbani atumie hot water bottle it relieves the pain. ajitie shughuli pia sleeping makes it more painful!

Cha muhimu pia amuone Gyna afanyiwe scans etc kubaini kama ana uvimbe (fibroids etc), hayo ya maumivu kupungua baada ya kupata mtoto huwa nayasikia pia.. may be u shd try it out.. ama una mpango gani naye?????cha kufia nini zaeni mwenzako angalua apumnzike!
 
If your periods have changed, it's very important to see your doctor. There are a number of diseases which can cause heavy bleeding (see list below). The doctor will investigate possible causes and offer the appropriate treatment. But in about half the women with heavy bleeding, no cause can be found.

Some causes of heavy menstrual bleeding

Unexplained - for half of all cases no cause can be found.

Contraceptive coil (IUD) - the coil can cause heavier, longer periods.

Injectable contraception (Depo Provera) - can cause heavy or prolonged bleeding.

Pelvic disorders:
Fibroids - these benign (not cancerous) growths in the muscular wall of the uterus are a common cause of heavy bleeding.

Polyps - these benign growths of the lining of the uterus may cause heavy bleeding but more commonly lead to spotting between or after periods.

Pelvic inflammatory disease - an infection in the reproductive tract which can cause infertility and chronic pain if untreated.

Endometriosis - a painful condition in which the lining of the uterus grows outside the uterus.

Endometrial hyperplasia - thickening of the lining of the uterus, leading to heavier bleeding.

Endometrial cancer - cancer of the lining of the uterus, causing heavy periods, bleeding between periods and blood-stained vaginal discharge. Rare, but more common in women after the menopause.

Blood and hormonal conditions:

Hormone imbalances - can stop ovulation (egg release) leading to build-up of endometrium and heavier periods.

Hypothyroidism - an underactive thyroid gland can cause heavier periods.
Blood clotting disorders.

Use of anticoagulant drugs.

The menstrual cycle is affected by stress. If you are going through any kind of life crisis, it is possible that your periods may settle down once that crisis has been resolved. Meanwhile reassurance from your doctor that there is nothing seriously wrong may help you to accept this change as a common and usually temporary response to stress. For many women, however, there is no easy solution to the stress in their lives. If this is the case, you will need to decide whether you want treatment for your heavy bleeding.

In all cases, the first step to take is to visit your GP and explain that your periods have changed. Once your doctor and/or gynaecologist have carried out the preliminary tests described in the next section, and you have been given the medical all clear, what happens next will largely depend on how you feel about your heavy bleeding.
 
Pill to end period pain: Drug that brings relief for millions of sufferers could be available by 2010

A drug that could free women from the misery of period pain has been devised by scientists. The 'hot water bottle in a pill' is designed to tackle the cause of the crippling cramps that plague up to 90 per cent of young and middle-aged women each month.
Taken ahead of a woman's period, it could prevent the pain.

Alternatively, it could be taken when required, easing pain when it hits. Likely to be prescription only, the drug could be on the market in just four years. Its inventors at Southampton-based drug firm Vantia Therapeutics said that they are confident it will work better than any of the drugs or treatments currently available.

Period pain, or dysmenorrhea, blights the life of between 45 and 90 per cent of women of child-bearing age and is the leading cause of absenteeism from school and work in women in their teens and 20s.

The pain is caused by the womb contracting during a period.

The new drug reduces levels of vasopressin, the hormone controlling the movement of the womb's muscles. Preliminary tests on a small group of women showed it to be safe, with no side- effects, an American Chemical Society conference in California heard.

A larger trial on more than 100 British and American women with bad period pain is already under way and the results are due later this year. If the drug fulfils its promise, it could earn Vantia a large chunk of the £600million-plus spent on period pain relief each year around the world.

Current treatments range from powerful painkillers and versions of the Pill, to relaxation techniques and hot water bottles.

But some tackle the symptoms rather than the cause, others cause upset stomachs or mood swings, and none work for all.

Vantia scientist Andrzej Batt said: 'We hope that the drug will provide a more effective treatment option for millions of women worldwide with this painful condition.

'Dysmenorrhea not only diminishes the quality of life for millions of women but also has a hidden, society-wide economic cost that involves an enormous number of days lost from work and school.'

Oily fish 'prevents endemetriosis'
Eating plenty of oily fish can protect against endometriosis, a cause of infertility which may affect two million British women, say researchers.

A study of more than 70,000 nurses found that those who ate the most tuna, salmon, mackerel and other foods high in omega-3 fatty acids were 22 per cent less likely to develop the painful condition.

But those whose diets were laden with harmful trans fats found in thousands of products from cakes and biscuits to pies and chips were 48 per cent more at risk, according to the findings published online in Human Reproduction.

Source: Daily Mail
 
Heshima mbele wakuu,

Mimi ni mwanamke nina umri wa miaka 29, bado sina mtoto.
Ninaumwa sana wakati wa hedhi kiasa kwamba siwezi kulala, kula wala kufanya kazi yoyote, miguu inatetemeka, siwezi kula na hata nikila mara nyingine hua natapika.

Wakati nikiwa na umri wa miaka 14-na kuendelea nilikua sipati maumivu kama ninayoyapata sasa.

Jamani wana jamvi, naomba ushauri na msaada wa kitabibu maana nateseka sana na nashindwa kabisa kufanya shughuli zangu.
 
Pole sana Hope 2, nakushauri utumie dawa inayoitwa Joy inapatikana pale Ubungo plaza ground floor kwa bwana mmoja anaitwa Dr. Buberwa. Sisterz wangu wangi wameponea hapo. plz jaribu vinginevyo beba mimba...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom