Ni kweli suala hilo liliingizwa kwenye muungano kinyemela, na sio hilo tuu, yako mengine kibao. Tulipo ungano, mambo ya muungano yalikuwa 11, sasa yanakaribia 30. La mwisho kabisa ni la kuifanya Zanzibar mkoa.......................................................................................................................Jamani muungano wa dhati ni kama ndoa. Mkishaungana, mnakuwa kitu kimoja. Hi kwenye ndoa, ili upate kila kitu, lazima uombe?. Vile ambayo ni stahili yako, unaweza kuomba, ama ukachukua, ili mradi usende kusiko.............................................................................................................Dini ya Kiislamu inaruhusu wake mwisho wanne. Inasema kabla hujaoa tena, omba ridhaa ya mke/wake waliopo, unaweza omba ridhaa na ukakataliwa, ukioa kwa nguvu bila hiyo ridhaa bado ndoa ni halali.................................................................................................................Japo ndoa ni muungano wa hiyari, haiwezi kufika mahali mke aliyeolewa akajiamkia tuu na kusema leo sikutaki, naomba talaka yangu. Talaka atoaye ni muoaji sio muolewaji..........................................................................................................Hizi kelele za muungano ni kama ndoa, hapo kuna muoaji na aliyeolewa, inaonekena kuna kelele za kutaka talaka. Kama kweli umetendewa visivyo, talaka itatolewa, lakini kama umetendewa ndivyo, wataka talaka tuu ili uwe huru kufanya mambo yako, unajisumbua bure, talaka hakuna.............................................................................................Kwa mara ya kwanza Juzi, Karume kaomba gesi na mafuta. Hivi hamjifunzi tuu kwa makosa ya Jumbe kutaka kuipigania Zanzibar uhuru wake UN, yalimkuta yapi?.Komandoo kataka badili katiba ili kuondoa ukomo wa miaka 10, yepi yalimkuta?.........................................................................................................Leo Karume anayaomba mafuta yawe yenu, hivi ni mafuta gani hayo?. Mbona hayajapatikana bado?, au hayo mafuta ya kwenye kinibu yataka watoa roho. Hivi kweli ni mafuta ama kuna mengine?. Mesej ya Karume sent...subirini majibu ila msije kulia!
Waliopigania uhuru mara nyingi sio wanaokula matunda ya uhuru.
Kama ndoa hapa basi na iwe ya kisasa kuwa hata mwanamke ana uhuru sawa sio wa kuomba.
Shukurani sana kwa kutufananisha na wake na kwa vile tunajuwa kuwa sote ni nchi tuliokubaliana hivyo ndowa hii ni ile inayopigwa vita, ya jinsia moja. Kwenye ndowa ya jinsia moja hakuna maendeleo kwani hakuna kizazi kwa vile ni kinyume na maumbile.
Great thinkers! my foot kujilinganisha na ndowa ya jamii moja, PASCO umefika mbali sana.