Mjadala wa lugha ya kufundishia ungefungwa rasmi kama Ndalichako na timu yake "wasingemsaliti" Hayati Magufuli

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
222
529
Ni suala linaloendelea kubishaniwa, kiswahili au Kiingereza kipi kitumike kuhamishia maarifa kwa vijana wa kitanzania (transfer of knowledge).

Huu ubishi kuna wakati mwamba mmoja (Mungu amrehemu) alitaka kuwaonyesha watu kuwa inawezekana kwa vitendo.

Tukubali tukatae, hakuna mkamilifu dunia wala hakuna anayekosea kila kitu. Kinachotugharimu binadamu mabaya yetu yanatabia ya kufunika kila jema tulilofanya! Hili Mwamba geu lilimkosti sana.

Kati ya vitu nilivyokuwa nasubiri kwa hamu ni somo la historia ya Tanzania kufundishwa kwa kiswahili

Nafahamu huenda watunzi wangeweka mbwembwe kibao za kusifia watawala kulingana na aina ya upepo uliokuwepo lakini hilo lingebaki kuwa umaamuma wa watunzi kutozingatia weledi wao.

Hivi somo Kama history kuna haja gani ya kufundishwa kwa lugha ya kigeni? Wanasema kiswahili hakina misamiati ya kutosha, history ina misamiati gani isiyokuwepo kwenye kiswahili?

Somo la civics au General study, linashindikana nini kufundishwa kwa kiswahili? Hali kadhalika kwenye geography?

Ukiangalia haya masomo ndo msingi mkubwa wa kujenga kujitambua tulikotoka na tunakoelekea Jambo ambalo ndio msingi mkubwa wa kujenga uzalendo wa mtu kulipenda taifa lake.

Ukiangalia ufaulu wa somo la historia na civics unazidi kudidimia kila mwaka.

Kama watu hawajui historia yao wataanzia wapi kulipenda na kulipigania Taifa lao?

Ukiangalia mataifa yaliyoendelea Kama china tamthilia na movie zao nyingi zinasimulia historia yao. Hii huwajenga watoto kulipenda na kulipigania Taifa lao. Huku kwetu tumekazana kuwapeleka watoto wetu English medium waweze kusema mummy na dady wanaporudi na tunawasifia kwa kudhani hiyo ndo elimu

Mama Ndalichako atwambie vile vitabu na ule mtaala wa historia ya Tanzania uliotakiwa kuanza kufundishwa siku chache kabla ya kifo cha Magufuri uko wapi!? Tulitakiwa tuanzie hapo masomo mengine yangefuata baadae
 
Hakukuwa na mtaala Wala vitabu vya historia bali kuliandaliwa kijitabu chakutukuza na kupromoti utawala wa Magufuli tu!!
 
Nyie wakeleketwa wa kutumia lugha ya kiswahili mnachoshindwa kutueleza ni faida tutakao pata tukitumia kiswahili, jamii yetu itabadika kiuchumi au ni kuonyesha utaifa tu.

Tupate dakitari PhD wa kiswahili ili aongeze nini ambacho kimemshinda kuongeza, kama mpaka leo lugha ya kiswahili inao fundisha kwa lugha hiyo hiyo bado wanafaili kwa 40%, leta hoja muache uzalendo wa kishamba.
 
Nyie wakeleketwa wa kutumia lugha ya kiswahili mnachoshindwa kutueleza ni faida tutakao pata tukitumia kiswahili, jamii yetu itabadika kiuchumi au ni kuonyesha utaifa tu. Tupate dakitari PhD wa kiswahili ili aongeze nini ambacho kimemshinda kuongeza, kama mpaka leo lugha ya kiswahili inao fundisha kwa lugha hiyo hiyo bado wanafaili kwa 40%, leta hoja muache uzalendo wa kishamba.
Kwamba kufundisha kwa kiswahili ni hoja za kishamba lakini kufundishwa kwa kiingereza ndo hoja za kijanja?

Lengo la Elimu ni kuhamisha maarifa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Na ili maarifa hayo yaeleweke kwa ufasaha lazima anayehusika kuhamisha maarifa hayo atumie lugha na mbinu itakayoeleweka kwa urahisi kwa mpokeaji.

Swali ni je, lugha ya kiingereza watoto wetu wanaimudu vizuri kupokelea hayo maarifa?

Walimu/Wataalam wetu wanaimudu vizuri kuhamisha maarifa kutoka kwao kwenda kwa wengine?

Hapa ndo pa kutafutia tiba mbadala! Kama ni kiingereza kianzie toka mwanzo wa elimu hadi mwisho! Na Kama ni kiswahili kiwe hivyo hivyo
 
Kwamba kufundisha kwa kiswahili ni hoja za kishamba lakini kufundishwa kwa kiingereza ndo hoja za kijanja?

Lengo la Elimu ni kuhamisha maarifa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Na ili maarifa hayo yaeleweke kwa ufasaha lazima anayehusika kuhamisha maarifa hayo atumie lugha na mbinu itakayoeleweka kwa urahisi kwa mpokeaji...
Mkuu bado hujajibu hoja yangu, je tukifundisha kwa lugha ya kiswahili kutoa hayo maalifa what will be the value added kama taifa that we are missing now?, economically tutaogezeka nini? au tufindishe kwasbb wa China wana fundisha kwa kichina.
 
Tunataka maarifa tunayowapa watoto wetu wayaelewe vyema, ndio maana tunahimiza matumizi ya kiswahili kama lugha ya kufundishia. Kwa Sasa watoto wetu hawaelewi maarifa tunayowapa Kwa kuwa tunatumia lugha ngeni kwao
 
Mkuu bado hujajibu hoja yangu, je tukifundisha kwa lugha ya kiswahili kutoa hayo maalifa what will be the value added kama taifa that we are missing now?, economically tutaogezeka nini? au tufindishe kwasbb wa China wana fundisha kwa kichina.
Sina hakika Kama unachouliza hata we mwenyewe umekitafakari vizuri

Shida kubwa ni kwamba matokoea ya elimu huwa hayaonekani ndani ya kipindi kifupi kwa hiyo hata hiyo value added unayouliza huwezi kuiona ndani ya miaka minne au kumi ijayo.

Hasara za kukosa maarifa sahihi ni makubwa sana na moja wapo ni hii ya kudharua tamaduni zenu na kutukuza za wengine

Na faida za kuwa na maarifa sahihi vizazi kwa vizazi ni kubwa ikiwemo kuthamini tamaduni zetu, kujitambua na kuweza kujiamini na kuamini kuwa tunaweza kufanya chochote tofauti na sasa ambapo kutojua kuongea kiingereza tu kunamshushia mtu confidence na kujiona hawezi na watu wengine kumuona hana anachoweza
 
Ni suala linaloendelea kubishaniwa, kiswahili au Kiingereza kipi kitumike kuhamishia maarifa kwa vijana wa kitanzania (transfer of knowledge).

Huu ubishi kuna wakati mwamba mmoja (Mungu amrehemu) alitaka kuwaonyesha watu kuwa inawezekana kwa vitendo.

Tukubali tukatae, hakuna mkamilifu dunia wala hakuna anayekosea kila kitu. Kinachotugharimu binadamu mabaya yetu yanatabia ya kufunika kila jema tulilofanya! Hili Mwamba geu lilimkosti sana.

Kati ya vitu nilivyokuwa nasubiri kwa hamu ni somo la historia ya Tanzania kufundishwa kwa kiswahili

Nafahamu huenda watunzi wangeweka mbwembwe kibao za kusifia watawala kulingana na aina ya upepo uliokuwepo lakini hilo lingebaki kuwa umaamuma wa watunzi kutozingatia weledi wao.

Hivi somo Kama history kuna haja gani ya kufundishwa kwa lugha ya kigeni? Wanasema kiswahili hakina misamiati ya kutosha, history ina misamiati gani isiyokuwepo kwenye kiswahili?

Somo la civics au General study, linashindikana nini kufundishwa kwa kiswahili? Hali kadhalika kwenye geography?

Ukiangalia haya masomo ndo msingi mkubwa wa kujenga kujitambua tulikotoka na tunakoelekea Jambo ambalo ndio msingi mkubwa wa kujenga uzalendo wa mtu kulipenda taifa lake.

Ukiangalia ufaulu wa somo la historia na civics unazidi kudidimia kila mwaka.

Kama watu hawajui historia yao wataanzia wapi kulipenda na kulipigania Taifa lao?

Ukiangalia mataifa yaliyoendelea Kama china tamthilia na movie zao nyingi zinasimulia historia yao. Hii huwajenga watoto kulipenda na kulipigania Taifa lao. Huku kwetu tumekazana kuwapeleka watoto wetu English medium waweze kusema mummy na dady wanaporudi na tunawasifia kwa kudhani hiyo ndo elimu

Mama Ndalichako atwambie vile vitabu na ule mtaala wa historia ya Tanzania uliotakiwa kuanza kufundishwa siku chache kabla ya kifo cha Magufuri uko wapi!? Tulitakiwa tuanzie hapo masomo mengine yangefuata baadae
Katika kitu sintofanya ni kuruhusu mtoto wangu kusoma shule yenye mitaala ya kiswahili. Magufuli alikuwa anajifanya anakiheshimu kiswahili huku akiongea kiswanglish, tena kibovu. Uzalendo wa kijinga hauna maana yoyote.
 
Transfer of Knowledge....mhhhh?????

Maana yake nini?

Kuna Ulazima gani? wa hilo ""Transfer of Knowledge"

Kwani tumekosa maarifa? Au Maarifa ya Mwafrika yamekandamizwa?

Unajua yaliyotokea Congo wakati wa Mfalme Dhalimu Leopold? Unajua Yaliyotokea Katika maktaba kubwa na inayosadikika kuwa ya kwanza kuwa na taarifa ambazo Wazungu hawakuwa nazo Egypt?

Unajua nini yaliyotokea kwenye maktaba ya Timbuktu? Afrika magharibi?

Lugha za Mwafrika zinaeleweka sana tu.

Mnakuja na maneno maneno ati 'Transfer of Knowledge' kama vile kuna maana yeyote ile muhimu.

Haiwezekani mpaka leo mtu anakuwa na fikra za 'Kusaidia' Waafrika ....kwa kumlazimisha kupokea Maadili maovu ya Ufalme wa Mwingereza, wakati anajua Umejaa Uwongo, na Udhalimu.

Hakuna cha kujifunza, hakuna maarifa mazuri kutoka kwa Mkoloni aliye Ua, kubaka, na kukandamiza binadamu. zaidi ya kutufundisha Ushetani.
 
Dondosheni vitu vya maana kujadiliwa.
Tabia zenu za kumbandika 'you know who' imekuwa ni Biashara kwenu, hamwezi kupasua au kutoboa bila ya kutumia jina lake kidhalimu, kama mnavyotumia dini kusambaza udahlimu Duniani.

Badilisheni hayo Ma Id lakini Lugha zenu zimebaki pale pale. Mtaeleweka.

BiBi yenu Malikia Elizabeth amezikwa na Ukimbari wake huko. mkazikwe nae huko na Ukimbari wenu
 
Nani anapigia chapuo lugha hii ya kidwanzi kuwa lugha ya kufundishia? Lugha inayokataliwa mpaka na shetani ya nn hii?
 
Dondosheni vitu vya maana kujadiliwa.
Tabia zenu za kumbandika 'you know who' imekuwa ni Biashara kwenu, hamwezi kupasua au kutoboa bila ya kutumia jina lake kidhalimu, kama mnavyotumia dini kusambaza udahlimu Duniani.

Badilisheni hayo Ma Id lakini Lugha zenu zimebaki pale pale. Mtaeleweka.

BiBi yenu Malikia Elizabeth amezikwa na Ukimbari wake huko. mkazikwe nae huko na Ukimbari wenu
Tunajadili swala zima la Elimu, naona umepotea njia kwa kujadili yasiyoeleweka hapa
 
Nyie wakeleketwa wa kutumia lugha ya kiswahili mnachoshindwa kutueleza ni faida tutakao pata tukitumia kiswahili, jamii yetu itabadika kiuchumi au ni kuonyesha utaifa tu.

Tupate dakitari PhD wa kiswahili ili aongeze nini ambacho kimemshinda kuongeza, kama mpaka leo lugha ya kiswahili inao fundisha kwa lugha hiyo hiyo bado wanafaili kwa 40%, leta hoja muache uzalendo wa kishamba.
Ni MTU mpumbavu Tu anayeweza kutoa elimu Kwa lugha ambayo watu hawaielewi na na watu ambao wanatakiwa wahudumie na hao wenye Elimu hawaijui.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Mkawaelimishe Neanderthral.

Nikupe msamiati mwingine wa Kutumia? Kisujudu cha Malikia. wee? au?
Umefunzwa Udhalimu, unategemea kusema au kuandika lipi lisilo na hujuma, unyanyasaji...Uhasama??
 
Mleta mada maneno mengiiii lakini pumba. Hata mfano wako wa Historia tena ukitetea historia ya Tanzania, una mapungufu! Je ni histiria ya Tz tu ndio itafundishwa?? Hawatafundishwa masomo mengine? Je vitabu vyake vipo tayari?? Zingatia vitabu vingi vya sayansi viko patented (sio vyetu na hatuwezi kuvizalisha wala kuvitafasiri).

Hakuna kufunga mjadala. Mie nasema tusijifunze kwa kiingereza tu, tujifunze hata kwa kiarabu, kifaransa, kireno, kihispania, kichina nk.

Mfano wangu mdogo sana!! Kama palivo na limitations za kutumia lugha zetu za kimila huko vijijini kufundishia, jinsi eneo linavozidi kuwa kuwa na kuongezeka kwa muingiliano - ndivo mahitaji ya lugha iliyo-advanced yanavokuwa makubwa. Ndio kinaingia kiswahili! Na hata kiswahili kina limitations pia - ndiopo zinaingia lugha zilizokuwa advanced kuliko kiswahili.

Lugha inayoongewa zaidi kulikoz zote duniani (bila kujali ufasaha) ni kiingereza. Tuihimize kwa sababu ilo katika mifumo yetu ya elimu, bunge, mahakama na tujaribu kuondoa vikwazo vya kuingia katika ulimwengu!!!

Mtupe faida za kiswahili dhidi ya za kiingereza ndio mshinde katika mabishano haya. Sio kufunga mjadala!!!
 
Ni suala linaloendelea kubishaniwa, kiswahili au Kiingereza kipi kitumike kuhamishia maarifa kwa vijana wa kitanzania (transfer of knowledge).

Huu ubishi kuna wakati mwamba mmoja (Mungu amrehemu) alitaka kuwaonyesha watu kuwa inawezekana kwa vitendo.

Tukubali tukatae, hakuna mkamilifu dunia wala hakuna anayekosea kila kitu. Kinachotugharimu binadamu mabaya yetu yanatabia ya kufunika kila jema tulilofanya! Hili Mwamba geu lilimkosti sana.

Kati ya vitu nilivyokuwa nasubiri kwa hamu ni somo la historia ya Tanzania kufundishwa kwa kiswahili

Nafahamu huenda watunzi wangeweka mbwembwe kibao za kusifia watawala kulingana na aina ya upepo uliokuwepo lakini hilo lingebaki kuwa umaamuma wa watunzi kutozingatia weledi wao.

Hivi somo Kama history kuna haja gani ya kufundishwa kwa lugha ya kigeni? Wanasema kiswahili hakina misamiati ya kutosha, history ina misamiati gani isiyokuwepo kwenye kiswahili?

Somo la civics au General study, linashindikana nini kufundishwa kwa kiswahili? Hali kadhalika kwenye geography?

Ukiangalia haya masomo ndo msingi mkubwa wa kujenga kujitambua tulikotoka na tunakoelekea Jambo ambalo ndio msingi mkubwa wa kujenga uzalendo wa mtu kulipenda taifa lake.

Ukiangalia ufaulu wa somo la historia na civics unazidi kudidimia kila mwaka.

Kama watu hawajui historia yao wataanzia wapi kulipenda na kulipigania Taifa lao?

Ukiangalia mataifa yaliyoendelea Kama china tamthilia na movie zao nyingi zinasimulia historia yao. Hii huwajenga watoto kulipenda na kulipigania Taifa lao. Huku kwetu tumekazana kuwapeleka watoto wetu English medium waweze kusema mummy na dady wanaporudi na tunawasifia kwa kudhani hiyo ndo elimu

Mama Ndalichako atwambie vile vitabu na ule mtaala wa historia ya Tanzania uliotakiwa kuanza kufundishwa siku chache kabla ya kifo cha Magufuri uko wapi!? Tulitakiwa tuanzie hapo masomo mengine yangefuata baadae
Kiswahili ni lugha changa sana kwenye medani za kimataifa, sayansi na technolojia. Unataka ufundishe sayansi- physics, chemistry, biology etc kwa kiswahili, vitabu utapata wapi? Je sheria za hati miliki zinaruhusu kutafsiri vitabu ambavyo viko kwa lugha ya kiingereza kwenda kiswahili? Na kama inaruhusiwa, itachikua miaka mingapi kufanya kazi hiyo?
Tutapata faida gani lugha ya kufundishia ikiwa ni kiswahili?
Tunahitaji kuingiliana na watu wa mataifa mengine, na lugha zinazotumika kimataifa (zile kubwa) ni English, french, Chinese, Spanish etc. Kiswahili hakipo.
Watanzania wengi wanakosa kujiamini wanapokutana na watu wa mataifa mengine sababu ya lugha. Mfano, wakati mahakama ya ictr iliyokuwa pale Arusha, raia wa Kenya, Uganda, etc waliweza kupata ajira pale kwa wingi. WaTz tukabaki kuambulia zile kazi za chini eg udereva, ulinzi na usafi. Hi ni kwa sababu kwenye usaili waTz hawawezi kujieleza kwa ufasaha kwa lugha zinazokubalika ktk mfumo wa UN.
Mfano meingine, angalia idadi ya watanzania wanaofanyakazi ktk mfumo wa UN na makampuni ya kimataifa hko duniani, ni wachache sana kulinganisha na say, ndugu zetu wa Kenya. Tatizo letu lugha.
Vile vile hawa wanasiasa wetu wanaotuimbia 'tuienzi lugha yetu adhimu', wao watoto wao wanawapeleka english medium schools , au nje ya nchi kabisa. Wanyonge wanahimizwa kupeleka watoto wao za kata (shule za kina kayumba).
Hatuwezi kulazimisha kutumia kiswahili eti ni uzalendo, sijui kuhifadhi utamaduni wetu, hii itazidi kutufanya tushindwe kushindana na wenzetu wa mataifa mengine.
Tunapaswa kufundisha watoto wetu kwa kiingereza kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu.
 
Back
Top Bottom