balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 16,513
- 15,152
Tumeshaamua jumatatu tunamburuza mahakamani
Kama kuroga ni ishu na ww kamloge Magu atengue kauli yake amg'oe Makonda....Makonda ni lulu kwa vijana wa sasa hasa mateja....lazima tumuunge mkono hasa sisi wenye uchungu na nguvu kazi.
KALAMU YA CHARLES FRANCIS KATIKA MJADALA WA ELIMU YA NDUGU "MAKONDA".
Na Charles Francis M,
Habari zenu Watanzania, nawasalimu kutoka mezani kwangu. Hapa nimeshika kalamu tayari kuingia katika mjadala wa elimu ya ndugu Makonda kwa kuandika katika misingi ya uchambuzi na siyo personal attack. Naomba "sana sana sana" ikiwa akili zako zina "mahaba" juu ya upande fulani na hauwezi kujizuia, usisome, usichangie chochote, puuza tu kuanzia hapa Kabla ya kusoma mbele zaidi maana "nitakuudhi kwa haki".
Kumekuwa na mjadala mkali na mpana sana kuhusu elimu, vyeti na majina ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ndugu Paul Makonda. Mjadala huu umejikita katika mantiki kuwa kiongozi huyo anatumia jina ambalo siyo lake na kwamba jina lake la elimu ya awali ya sekondari ni tofauti na majina yake ya elimu ya juu.
Mjadala huu umejikita katika kusudio hasa au shinikizo la kumtaka kiongozi huyo ahakikiwe elimu na majina yake. Hapa kuna mambo kadhaa lazima yawekwe bayana. Kwa mfano majina yaliyopo kwenye vyeti vyake vya kitaaluma na hasa kidato cha nne. Lakini pia ithibitike kuwa baraza la mitihani lime wahi kusajili mwanafunzi mwenye jina hilo na kwamba ndiye Makonda huyu wa sasa.
Tarehe 22.02.2017 Jumatano, Katika Gazeti la Jambo Leo, Ndugu Paul Makonda amenukuliwa na gazeti hilo akiwajibu vibaya waandishi wa habari wa gazeti hilo ambao walitaka kujua kuhusu elimu yake na sakata ambalo limebeba dhima ya mjadala wa elimu ya mkuu huyo wa mkoa. Suala la kuwajibu vibaya waandishi hao ambao walikuwa katika majukumu yao, siyo vema wala siyo maadili ya mtumishi wa umma hata kidogo.
UPANDE WA KWANZA LAZIMA UJIBU HAYA:
1. Kwanini Makonda aliwajibu vibaya (kwa hasira) waandishi hao wa habari pindi walipo hoji suala la elimu yake ikiwa hana "ukakasi katika elimu yake"??
2. Ni nani aliye ongoza zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma kwa mkoa wa Dar Es Salaam?? Je, katika zoezi hilo mkuu wa mkoa alihakikiwa na nani?? Kama hakuhakikiwa ni kwanini??
3. Je, baraza la mitihani lime wahi kutoa cheti cha uhitimu wa elimu ya awali ya sekondari kwa Makonda kwa kutumia jina lipi??
4. Je, chuo kikuu Makonda alisoma wapi na alitumia majina gani?? Ikiwa majina yana tofautiana na yale ya elimu yake ya sekondari, alidahiliwa vipi chuo kikuu??
5. Je, Katika kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, iliyo funguliwa na Freeman Aikaeli Mbowe dhidi ya ndugu Makonda kama moja ya walalamikiwa, ikiwa mawakili wa upande wa malalamiko watauliza swali kuhusu elimu ya Makonda, itakuwaje?? Je, swali hilo litaruhusiwa au halihusiani na shtaka la msingi??
6. Ikithibitika kuwa vyeti vya elimu ya mkuu huyo wa mkoa kuwa vina dosari, Je ni hatua gani kisheria zinaweza kuchukuliwa??
UPANDE WA PILI PIA NAHOJI YAFUATAYO:
1. Hapo hapo, naomba kuhoji upande wa pili mjadala huu. Kwanini elimu ya Makonda iwe hoja kubwa kwa sasa?? Kwanini elimu yake haikuhojiwa kipindi akiwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni au kipindi akiwa kada tu wa Uvccm??
2. Ikithibitika kuwa Makonda anatumia majina halali na kwamba elimu yake haina shaka, Je ni hatua gani stahiki (kisheria) atachukua dhidi ya wale walio anza kumtuhumu?? Au nao watakuwa salama kama ambavyo alimtuhumu Asko Gwajima na kisha kukutwa hana hatia na hakumshtaki Makonda??
3. Je, mjadala huu kuhusu elimu ya Makonda tunaweza kuhusisha na vita aliyo iasisi dhidi ya dawa za kulevya katika mkoa wake?? Kwamba hii ni mbinu ya kumkomoa kisiasa?? Kwamba ni michezo ya watoto wa mjini "mwaga mboga nimwage ugali"??
4. Mjadala huu unapata nguvu kubwa sana kwa sababu ya aina ya Uongozi wa Makonda unao tuhumiwa kuwa na ubabe mwingi?? Yaani mjadala huu siyo kwa sababu ya nia na dhamira ya dhati kuhusu suala la elimu yake ila ni kwa sababu tu "tumepata nafasi" ya kumsema vizuri??
5. Tarehe 18.10.2016 siku ya Jumanne, katibu mtendaji wa baraza la mitihani (NECTA) alitoa tangazo kupitia gazeti la MTANZANIA kuwa kila mwenye taarifa ya mtu anaye tumia jina ambalo siyo lake katika ajira au mafunzo popote nchini, taarifa zake zitolewe kupitia mawasiliano ya simu 0742 48 49 55 na E-mail yenye jina "esnecta@necta.go.tz". Kwanini njia hii isitumike dhidi ya Makonda badala yake malalamiko yapo kwenye mitandao ya kijamii??
Mjadala huu siyo mdogo, ndiyo maana nimeufanya kuwa "balanced" kama mchambuzi nimehoji pande zote. Sikutaka kuwa upande wowote kwa sababu sikutaka kuumiza upande au kubagua popote ila nimefungua mjadala huu kwa kutoa nafasi pana ya majadiliano yenye hoja na ushawishi. Charles napenda sana mijadala ya aina hii. Na ndiyo maana mara kadhaa naonekana kama niko tofauti na wengi lakini ni kwa sababu ya kupenda hoja kuliko mapenzi binafsi.
NB: Je, wakuu wote wa mikoa walihakiki vyeti vyao?? Je, mamlaka zote za juu zilihakiki vyeti?? Kwa mfano: Spika na Mawaziri walihakiki lini vyeti vyao na Je, mamlaka ya uteuzi (yaani mamlaka iliyo teua mawaziri) nayo ilihakikiwa na nani?? Kulikuwa na uwazi gani katika uhakiki huo?? Kama haikuhakikiwa, ni kwanini??
KARIBUNI SANA KWA MJADALA.......
"Caytano Maytano"
Charles Francis M.
Kwa kweli....Ila tumeshaichoka hii hadithi, for real
UPANDE WA KWANZA LAZIMA UJIBU HAYA:
1. Kwanini Makonda aliwajibu vibaya (kwa hasira) waandishi hao wa habari pindi walipo hoji suala la elimu yake ikiwa hana "ukakasi katika elimu yake"??
2. Ni nani aliye ongoza zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma kwa mkoa wa Dar Es Salaam?? Je, katika zoezi hilo mkuu wa mkoa alihakikiwa na nani?? Kama hakuhakikiwa ni kwanini??
3. Je, baraza la mitihani lime wahi kutoa cheti cha uhitimu wa elimu ya awali ya sekondari kwa Makonda kwa kutumia jina lipi??
4. Je, chuo kikuu Makonda alisoma wapi na alitumia majina gani?? Ikiwa majina yana tofautiana na yale ya elimu yake ya sekondari, alidahiliwa vipi chuo kikuu??
5. Je, Katika kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, iliyo funguliwa na Freeman Aikaeli Mbowe dhidi ya ndugu Makonda kama moja ya walalamikiwa, ikiwa mawakili wa upande wa malalamiko watauliza swali kuhusu elimu ya Makonda, itakuwaje?? Je, swali hilo litaruhusiwa au halihusiani na shtaka la msingi??
6. Ikithibitika kuwa vyeti vya elimu ya mkuu huyo wa mkoa kuwa vina dosari, Je ni hatua gani kisheria zinaweza kuchukuliwa??
Unaweza kuthibitisha kiongozi? Natamani kuona mtu anatoa evidence beyond reasonable doubt kuwa jamaa amenunua jina baada ya kuzungusha.Makonda alipata zero kwa jina la Albert
Constructive arguments hazihitaji watu kama wewe, wanaume wa Dar wameingia vipi kwenye hoja yako??Makonda hakupata zero aliyepata zero ni bashite yule wa kolomije misungwi mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa dar. Nampa pongezi maana hata manaume wa dar wote ni vilaza.
Soma previous argument zangu za nyuma kwenye huu uzi ndyo uelewe. Usikurupke mkuuConstructive arguments hazihitaji watu kama wewe, wanaume wa Dar wameingia vipi kwenye hoja yako??
Mkuu Elli, unataka uthibitisho gani?Unaweza kuthibitisha kiongozi? Natamani kuona mtu anatoa evidence beyond reasonable doubt kuwa jamaa amenunua jina baada ya kuzungusha.
Unaweza kuthibitisha kiongozi? Natamani kuona mtu anatoa evidence beyond reasonable doubt kuwa jamaa amenunua jina baada ya kuzungusha.
Wangapi waliokuwa wakizipenda kazi zao na kutumia vyema nafasi zao lakin walipojulikana tuh wamefoji vyeti hawakupewa mafao yao pindi walipo stafu.. Unataka yeye haachwe haki isitendeke kwake, yeye Nabii auMm sjaisoma yote ila nilipoona jina la makonda kutajwa tu nikajua ndo wale wale wapiga vuvuzera....hivi ata kama vyeti sio vyake na hana elimu hiyo mchango wake hauonekani?...tumekuwa na wasomi wangapi na hawajafanya lolote kwa taifa hili....tumewapeleka bunge la katiba badala ya kujadili rasimu wakatoka nje elimu yao wameitumia vipi?....Wewe kama unaona kalamu yako inakusahidia sana kawaandikie Chadema sera za kuombea kura 2020,sio cheap reason kama hii ishu ulokuja nayo....hii nchi kuishi kwa madili muache.Hatutaki madawa full stop na tunamtaka makonda full stop.
Umeichoka wewe usitusemee wote, site lhatuchoki mpaka utata wa vyeti vyake utatuliwe.Ila tumeshaichoka hii hadithi, for real
Shuhuli anazofanya za kukushuhulikia chumbani sisi tutaonaje Ndugu ? Tuone vyeti ili tujue Nani Bashite na nani PaulMm sjaisoma yote ila nilipoona jina la makonda kutajwa tu nikajua ndo wale wale wapiga vuvuzera....hivi ata kama vyeti sio vyake na hana elimu hiyo mchango wake hauonekani?...tumekuwa na wasomi wangapi na hawajafanya lolote kwa taifa hili....tumewapeleka bunge la katiba badala ya kujadili rasimu wakatoka nje elimu yao wameitumia vipi?....Wewe kama unaona kalamu yako inakusahidia sana kawaandikie Chadema sera za kuombea kura 2020,sio cheap reason kama hii ishu ulokuja nayo....hii nchi kuishi kwa madili muache.Hatutaki madawa full stop na tunamtaka makonda full stop.
Mbona na wewe una jina fake unalotumia humu?Makonda alipata zero kwa jina la Albert
Okay, Bashite em' lete hivyo vyeti hapo kwenye droo ya chiniUmeichoka wewe usitusemee wote, site lhatuchoki mpaka utata wa vyeti vyake utatuliwe.