"see e5. Je, Katika kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, iliyo funguliwa na Freeman Aikaeli Mbowe dhidi ya ndugu Makonda kama moja ya walalamikiwa, ikiwa mawakili wa upande wa malalamiko watauliza swali kuhusu elimu ya Makonda, itakuwaje?? Je, swali hilo litaruhusiwa au halihusiani na shtaka la msingi??"
Shida inakuja Freeman anamshtaki Makonda au Albert Bashite? Yaani mlalamikiwa ni Paul C. Makonda au Albert Bashite? Kwa kuwa mpaka sasa hakuna uthibitisho juu ya mlalamikiwa, ndipo hapo mahakama inatakiwa ijiridhishe kwanza ni lipi jina halali la mshtakiwa ili kuondoa utata katika hukumu itakayotolewa.
Kilaza babako,Je aliyefeli sekondari anawezaje kumudu masomo ya Chuo,Mimi mwanaume wa Dar ndio maana nimekujibu acha UPOYOYOMakonda hakupata zero aliyepata zero ni bashite yule wa kolomije misungwi mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa dar. Nampa pongezi maana hata manaume wa dar wote ni vilaza.
Kamjibu makondaNa
Kilaza babako,aliyefeli sekondari anawezaje kumudu masomo ya Chuo,Mimi mwanaume wa Dar ndio maana nimekujibu acha UPOYOYO
Siamini kama utata wa elimu yake ulikuwa 'siri'. Kuna waliojua ndiyo maana habari imejulikana mapema. Pia siamini kama kitu hulipuka ghafla; kabla ya mvua huwa kuna fukuto na pia kabla ya volcano kuna kufoka Moshi au vumbi, na kabla ya tetemeko pia huwa kuna dalili.KALAMU YA CHARLES FRANCIS KATIKA MJADALA WA ELIMU YA NDUGU "MAKONDA".
Na Charles Francis M,
Habari zenu Watanzania, nawasalimu kutoka mezani kwangu. Hapa nimeshika kalamu tayari kuingia katika mjadala wa elimu ya ndugu Makonda kwa kuandika katika misingi ya uchambuzi na siyo personal attack. Naomba "sana sana sana" ikiwa akili zako zina "mahaba" juu ya upande fulani na hauwezi kujizuia, usisome, usichangie chochote, puuza tu kuanzia hapa Kabla ya kusoma mbele zaidi maana "nitakuudhi kwa haki".
Kumekuwa na mjadala mkali na mpana sana kuhusu elimu, vyeti na majina ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ndugu Paul Makonda. Mjadala huu umejikita katika mantiki kuwa kiongozi huyo anatumia jina ambalo siyo lake na kwamba jina lake la elimu ya awali ya sekondari ni tofauti na majina yake ya elimu ya juu.
Mjadala huu umejikita katika kusudio hasa au shinikizo la kumtaka kiongozi huyo ahakikiwe elimu na majina yake. Hapa kuna mambo kadhaa lazima yawekwe bayana. Kwa mfano majina yaliyopo kwenye vyeti vyake vya kitaaluma na hasa kidato cha nne. Lakini pia ithibitike kuwa baraza la mitihani lime wahi kusajili mwanafunzi mwenye jina hilo na kwamba ndiye Makonda huyu wa sasa.
Tarehe 22.02.2017 Jumatano, Katika Gazeti la Jambo Leo, Ndugu Paul Makonda amenukuliwa na gazeti hilo akiwajibu vibaya waandishi wa habari wa gazeti hilo ambao walitaka kujua kuhusu elimu yake na sakata ambalo limebeba dhima ya mjadala wa elimu ya mkuu huyo wa mkoa. Suala la kuwajibu vibaya waandishi hao ambao walikuwa katika majukumu yao, siyo vema wala siyo maadili ya mtumishi wa umma hata kidogo.
UPANDE WA KWANZA LAZIMA UJIBU HAYA:
1. Kwanini Makonda aliwajibu vibaya (kwa hasira) waandishi hao wa habari pindi walipo hoji suala la elimu yake ikiwa hana "ukakasi katika elimu yake"??
2. Ni nani aliye ongoza zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma kwa mkoa wa Dar Es Salaam?? Je, katika zoezi hilo mkuu wa mkoa alihakikiwa na nani?? Kama hakuhakikiwa ni kwanini??
3. Je, baraza la mitihani lime wahi kutoa cheti cha uhitimu wa elimu ya awali ya sekondari kwa Makonda kwa kutumia jina lipi??
4. Je, chuo kikuu Makonda alisoma wapi na alitumia majina gani?? Ikiwa majina yana tofautiana na yale ya elimu yake ya sekondari, alidahiliwa vipi chuo kikuu??
5. Je, Katika kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017, iliyo funguliwa na Freeman Aikaeli Mbowe dhidi ya ndugu Makonda kama moja ya walalamikiwa, ikiwa mawakili wa upande wa malalamiko watauliza swali kuhusu elimu ya Makonda, itakuwaje?? Je, swali hilo litaruhusiwa au halihusiani na shtaka la msingi??
6. Ikithibitika kuwa vyeti vya elimu ya mkuu huyo wa mkoa kuwa vina dosari, Je ni hatua gani kisheria zinaweza kuchukuliwa??
UPANDE WA PILI PIA NAHOJI YAFUATAYO:
1. Hapo hapo, naomba kuhoji upande wa pili mjadala huu. Kwanini elimu ya Makonda iwe hoja kubwa kwa sasa?? Kwanini elimu yake haikuhojiwa kipindi akiwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni au kipindi akiwa kada tu wa Uvccm??
2. Ikithibitika kuwa Makonda anatumia majina halali na kwamba elimu yake haina shaka, Je ni hatua gani stahiki (kisheria) atachukua dhidi ya wale walio anza kumtuhumu?? Au nao watakuwa salama kama ambavyo alimtuhumu Asko Gwajima na kisha kukutwa hana hatia na hakumshtaki Makonda??
3. Je, mjadala huu kuhusu elimu ya Makonda tunaweza kuhusisha na vita aliyo iasisi dhidi ya dawa za kulevya katika mkoa wake?? Kwamba hii ni mbinu ya kumkomoa kisiasa?? Kwamba ni michezo ya watoto wa mjini "mwaga mboga nimwage ugali"??
4. Mjadala huu unapata nguvu kubwa sana kwa sababu ya aina ya Uongozi wa Makonda unao tuhumiwa kuwa na ubabe mwingi?? Yaani mjadala huu siyo kwa sababu ya nia na dhamira ya dhati kuhusu suala la elimu yake ila ni kwa sababu tu "tumepata nafasi" ya kumsema vizuri??
5. Tarehe 18.10.2016 siku ya Jumanne, katibu mtendaji wa baraza la mitihani (NECTA) alitoa tangazo kupitia gazeti la MTANZANIA kuwa kila mwenye taarifa ya mtu anaye tumia jina ambalo siyo lake katika ajira au mafunzo popote nchini, taarifa zake zitolewe kupitia mawasiliano ya simu 0742 48 49 55 na E-mail yenye jina "esnecta@necta.go.tz". Kwanini njia hii isitumike dhidi ya Makonda badala yake malalamiko yapo kwenye mitandao ya kijamii??
Mjadala huu siyo mdogo, ndiyo maana nimeufanya kuwa "balanced" kama mchambuzi nimehoji pande zote. Sikutaka kuwa upande wowote kwa sababu sikutaka kuumiza upande au kubagua popote ila nimefungua mjadala huu kwa kutoa nafasi pana ya majadiliano yenye hoja na ushawishi. Charles napenda sana mijadala ya aina hii. Na ndiyo maana mara kadhaa naonekana kama niko tofauti na wengi lakini ni kwa sababu ya kupenda hoja kuliko mapenzi binafsi.
NB: Je, wakuu wote wa mikoa walihakiki vyeti vyao?? Je, mamlaka zote za juu zilihakiki vyeti?? Kwa mfano: Spika na Mawaziri walihakiki lini vyeti vyao na Je, mamlaka ya uteuzi (yaani mamlaka iliyo teua mawaziri) nayo ilihakikiwa na nani?? Kulikuwa na uwazi gani katika uhakiki huo?? Kama haikuhakikiwa, ni kwanini??
KARIBUNI SANA KWA MJADALA.......
"Caytano Maytano"
Charles Francis M.
Wajina wakoBashite weka Vyeti mezani![]()

Kama hujui kaa kimyaaa. Makonda alisoma chuo kikuu miaka mingapi?Na
Kilaza babako,Je aliyefeli sekondari anawezaje kumudu masomo ya Chuo,Mimi mwanaume wa Dar ndio maana nimekujibu acha UPOYOYO
Kaulize TCU!Kama hujui kaa kimyaaa. Makonda alisoma chuo kikuu miaka mingapi?
Alibadili kozi Mara ngapi?
Kama una hoja, basi ijikite katika kuwataka wanaotuhumu wathibitishe kama kweli Mkuu wa Mkoa alisomea cheti cha mtu mwingine baada ya yeye kufeli kidato cha nne.
Lakini hoja yako eti mchango wake unaonekana au hauonekani haiwezi KUIFUTA JINAI kama aliitenda. Ukisema hivyo, ni wengi sana ambao hawapaswi kjuadhibiwa maana wapo hadi walioghushi vyeti vya taaluma pasipo hata kuzisomea lakini ukiwakuta kazini wanapiga mzigo hasa baada ya kupata uzoefu wa miaka mingi kama 5-10). Sasa kama na hawa utawaacha, hiyo safisha safisha itawakumba akina nani?
Hao wenye sifa stahiki lakini hawafanyi kazi zao sawasawa acha waondolewe na mfumo wa upimaji wa utendaji kazi (performance appraisal). kama mfumo huo hauwezi kuwabaini na kuwawajibisha, basi hakuna sababu ya kulalamika. Ila sitakubaliana na yeyote anayetaka kuhalalisha jinai eti kwa kuwa mtenda jinai anaonyesha matunda.
Hii itakuwa sawa na kubariki wizi na ujambazi kwa kuwa tu huyu jambazi akishatoka kuwaibia watu "at gun point" anatoa misaada kwa maskini, wajane, na watoto yatima..na kuchangia ujenzi wa zahanati, shule na miradi ya maji.
Je wale waliotumbuliwa mchango wao ulikuwa hauonekani?Mm sjaisoma yote ila nilipoona jina la makonda kutajwa tu nikajua ndo wale wale wapiga vuvuzera....hivi ata kama vyeti sio vyake na hana elimu hiyo mchango wake hauonekani?...tumekuwa na wasomi wangapi na hawajafanya lolote kwa taifa hili....tumewapeleka bunge la katiba badala ya kujadili rasimu wakatoka nje elimu yao wameitumia vipi?....Wewe kama unaona kalamu yako inakusahidia sana kawaandikie Chadema sera za kuombea kura 2020,sio cheap reason kama hii ishu ulokuja nayo....hii nchi kuishi kwa madili muache.Hatutaki madawa full stop na tunamtaka makonda full stop.
Ndo tatizo kuubwa Sana linalotukabili watanzania. Nilidhani tutasimamia Bashite ahakiki vyeti vyake mpaka tuujue mwisho. Wafanyakazi wa serikali wamehakikiwa vyeti vyao kwa vitisho bila kujali gharama za waliokuwa mbali ya vituo vyao vya kazi kwa sababu Kama za masomo, kuuguza nk. BASHITE KAHAKIKI VYETI VYAKOIla tumeshaichoka hii hadithi, for real
Vyeti ni kwa ajili ya muajiri tu...hakuna sheria inayomlamzimisha kiongozi au mtanzania yeyote kuonyesha vyeti mtandaoni.Nami najibu hii namba tano. Sasa kama watu wametuma na hata wanaomjua na hawaoini likifanyiwa kazi si ndio wanaamua kuingia kwenye mitandao!?
Tukumbuke hapa suala la kutaja mali za watumishi wa umma sheria ilikuwa wazi lakini ikaweka ugumu kwa mtu mwenye nia njema kuona fomu husika ili aisaidie serikali kwa wale waliodanganya.
Badala ya watu kupoteza MB zao na wino kuandika haya yote ni kwa nini mhusika (bahati nzuri ni member hapa) asiweke vyeti hadharani mjadala ukaisha!? Kumbuka huyu ni mtumishi wa umma kwa hiyo kutaja belongings zake hadharani ni lazima. Kwani Mzee Mkapa, JK na wasaidizi wao mbona walitutajia hadi kuku wanaowamiliki ...ni kwa sababu walitaka wakalie ofisi za umma kwa amani.
Lakini kwa kuwa ndiyo yaliyopo mezani .....yamenikinai
Ndio maana huyu bwana ameipa mtazamo mpyaIla tumeshaichoka hii hadithi, for real
Asante sana kwa maelezo ya kweli na mifano hai.Well said Mkuu,...sijui kwa nini watu wanakufa ganzi kwa haka katoto
Kule Colombia, alikuwepo muuza na msambazaji mkubwa wa madawa ya kulevya akiitwa Pablo Escobar, zaidi ya 80% ya madawa ya kulevya yaliyoingizwa US huyu jamaa alikuwa responsible...alikuwa na pesa ya nguvu. Huyu bwana alitumia pesa hiyo haramu kujenga mashule, mahospitali na kusomesha watu kwa kutoa scholarships....hii haikuondoa ukweli kuwa alikuwa mkosaji. Kule Jamaica kuna mtu alikuwa akiitwa Dudu...similary alifanya na alikuwa kama Escobar...sasa hivi yuko Jela kutokana na uovu wake...pamoja na kwamba pesa haramu aliyokuwa akiipata aliitumia kwa jamii yake na kwa starehe zake.
Wandugu tusiondoke kwenye mambo ya msingi na ni very very basic...na hasa kwa watu walioenda shule za uhakika...kukubali uovu wa elimu wa aina yeyote ni kujishushia heshima na kudharau umuhimu wa elimu...shame on us!
Juzi juzi tu...matamko yametoka kuhusu uhakiki wa qualification za watu waliopo mavyuoni...na maofisini....wengine walikuwa wamesha-advance...na waliondolewa...kwanini kwa watu wengine isifanyike hivyo hivyo?
Kama mnampenda sana mtu kuwa kiongozi haina shida....lakini record zake ziwekwe straight...kama mkimsamehe kwa makosa aliyofanya....hilo ni suala jingine...lakini taarifa ni muhimu zikawa sahihi. Hivi tunawafundisha nini watoto wetu tukikubali udhaifu huu?
Umesema vyema kwamba utendaji wake ni Mauro japo kwa hili kwangu no comment.suala la kuhakiki vyeti halihusiani kabisa na utendaji vinginevyo wangehakiki utendaji wa watu na sio vyeti,tunachotaka ni kuondoa double standard kwani wapo watendaji wengi wazuri wameachishwa kazi kwa sababu ya vyeti. Unalisemeaje hilo?Mm sjaisoma yote ila nilipoona jina la makonda kutajwa tu nikajua ndo wale wale wapiga vuvuzera....hivi ata kama vyeti sio vyake na hana elimu hiyo mchango wake hauonekani?...tumekuwa na wasomi wangapi na hawajafanya lolote kwa taifa hili....tumewapeleka bunge la katiba badala ya kujadili rasimu wakatoka nje elimu yao wameitumia vipi?....Wewe kama unaona kalamu yako inakusahidia sana kawaandikie Chadema sera za kuombea kura 2020,sio cheap reason kama hii ishu ulokuja nayo....hii nchi kuishi kwa madili muache.Hatutaki madawa full stop na tunamtaka makonda full stop.
Alafu tunaweza kudharau hizi habari zinazo circulate hapa JF, mimi naona ni sahihi na taasisi yoyote ya umma au binafsi inatakiwa kutolea maelezo (clear doubts) kwa habari zilizotokea hapa. wanavyodharau wanaonyesha uwezo mdogo wa kufikiri walio nao.Tunalo tatizo katika kushughulikia masuala kadhaa katika nchi yetu. Tume ya maadili kwa viongozi inawataka waorodheshe mali, madeni n.k na pia vyanzo vya mali waliyonayo. Sina uhakika kama kuna ufuatiliaji wa ukweli wa majibu yanayotolewa na viongozi wanaopaswa kuorodhesha mali zao. Uhakika nilio nao ni kwamba kama atatokea mtu asiyeridhika na majibu hayo, apeleke malalamishi yake na ushahidi kwenye hiyo Tume. Baraza la Mitihani nalo linataka lipelekewe maelezo na ushahidi ili liweze kuifuatilia taarifa kuhusu mtu kutumia vyeti visivyokuwa vyake yaani vya kugushi. Naona ingekuwa vyema kwa Taasisi hizi kufanya uchunguzi walau kidogo wapatapo tetesi kuhusiana na mambo haya ya udanganyifu ili kuonyesha kwamba wako makini katika kazi zao. Kinachojitokeza sasa watu wa chini ndio husumbuliwa sana mara tu tuhuma zikizagaa kuhusu mapungufu yao. Ni vyema kukawa na haki sawa kwa kila mwananchi katika masuala kama haya. Vinginevyo tutajenga taifa lenye tabaka katika kutoa haki kwa walionacho na wale wasiokuwa na chochote.
Umesema vyema kwamba utendaji wake ni Mauro japo kwa hili kwangu no comment.suala la kuhakiki vyeti halihusiani kabisa na utendaji vinginevyo wangehakiki utendaji wa watu na sio vyeti,tunachotaka ni kuondoa double standard kwani wapo watendaji wengi wazuri wameachishwa kazi kwa sababu ya vyeti. Unalisemeaje hilo?