Mjadala; Ni yupi anaestahili mazishi yake kugharamiwa na serikali kati ya kiongozi na mwananchi maskini?

Acha ujinga! Mjadala uko open! Kuhusu mwananchi masikini kustahili msahama wa selikali uwe rasm...wewe unaleta mihemko ya kijinga hapa! Hujui hata hapo unaweza system ikakutema ukarudi kundi la masikini mbuzi wewe
Tatizo lako nimegundua wewe ni dudumizi. Hivyo lazima upelekwe taratibu upate utelezi.

Kwamba wananchi masikini wanatakiwa kulipiwa usafiri wa mwili hadi eneo lao kisa tu ni masikini? Suala la matibabu na kukatalia mwili waziri si alitolea ufafanuzi uliweka wapi masikio yako usisikie alisema nini.

Usipende ofa jitahidi ujitegemee yaani serikali itoe mwili wa dmkali kutoka Muhimbili kwenda Ukerewe kisa tu ni masikini. Yaani uko comfortable unaona umaskini ni njia ya kuhurumiwa?

Huwezi kutaka upewe huduma sawa na mtumishi wa serikali wewe nani uzikwe na serikali na pilau serikali ilipie.
 
Nauweka mjadala huru kwenu!

Mazishi mengi ya viongozi kuanzia matibabu hadi mazishi hugharamiwa na serikali, lakini Msiba wa mwananchi maskini hupitia misukosuko kuanzia upatikanaji wa mwili hospitali hata namna ya kuusafilisha!

Je; Ni yupi anaestahili kujigharamia mazishi kati ya kiongozi wa umma au mwananchi wa kawaida ambaye hana ajira wala bima?

KARIBUNI
kwakweli hata mimi hapa pananipa kigugumizi sana, utafikiri wananchi ni kundi lingine na waajiriwa serikalini ni kundi lingine, serikalini kuna mishahara ambayo ndizo kodi za wananchi wote, ila linapokuja tatizo mtaani mtu asiye mfanyakazi wa serikali huwa mtu anapambana binafsi sana, linapotokea mtu wa kitengo cha serikali amepata tatizo basi mali za serikali hutumika kumsaidia huyo mtu anayelipwa na mshahara unaotoka kwenye kodi za wote. Imefika mahala unakuta wananchi wa hali ya chini wanawaombea yawakute mabaya walioko serikalini ili tu nao wawe wanapata hekaheka nyingi japokuwa serikali inakuwa inajichovya humo kuwasaidia, chuki baina ya makundi haya mawili hukua siku hadi siku. Wananchi wa hali ya chini na, au wananchi ambao si wafanyakazi wa serikali hujikuta wakijitenga hata mitaani wakijisemea kuwa tupo tofauti kati ya wale wa serikali na wasio. KUNA MMOJA ANAJISIKIA KUWA YEYE NDIO YEYE NA WENGINE WASIOKUWEMO KWENYE SERIKALI NI KAMA MBWA TU, samahani kwa maneno hayo. kwa ufupi UONGOZI UNAOSHIKA HATAMU UNAKUWA NI BINAFSI SANA hasa katika nchi kama yetu hii

nakuja kwa swali lako; yupi anastahiri kujigharamia?...Nafikiri serikali ingejitahidi kuweka usawa kusaidia wananchi wote na si baadhi. Kwasababu si wote wanaweza kuwa watumishi wa umma, na hii tabia ya upendeleo imekua kubwa kiasi kwamba ili uwe mtumishi wa umma watu wanatoa rushwa ili waingie humo, wengine wenye nafasi huwaweka nduguze katika vitengo ili tu wajazane kindugu ndugu waendeleze ubinafsi huo wa kihuduma kati ya masikini na watumishi wa umma.

NB: serikali makini ingekuwa inasaidia wananchi wote kwa usawa, kama ni kweli kuna upendeleo!!
 
Wewe ni kama nyani tu! Haoni utupu wake! Ungekuwa na akili timamu ungewaza! Tofautisha mazishi ya wananchi wanaozikwa na serikali kutokana na majanga kama corona!
Ni ninazungumzia utaratibu wa kawaida, iweje mwananchi masikini adaiwe gharama za tiba na kulipia maiti kuitoa mochwari?
Serikali haitoi bure huduma za afya hivyo kuna michango hutakiwa pale mgonjwa anapofika hospitali na bahati mbaya akafariki. Yaani kwa akili zako unataka mtumishi wa serikali ajilipie matibabu wakati anakatwa pesa kwa ajili ya matibabu kila mwezi.

Kama uko karibu na kuku ipe simu niieleweshe kisha itakusaidia kutafsiri nachosema.
 
kwakweli hata mimi hapa pananipa kigugumizi sana, utafikiri wananchi ni kundi lingine na waajiriwa serikalini ni kundi lingine, serikalini kuna mishahara ambayo ndizo kodi za wananchi wote, ila linapokuja tatizo mtaani mtu asiye mfanyakazi wa serikali huwa mtu anapambana binafsi sana, linapotokea mtu wa kitengo cha serikali amepata tatizo basi mali za serikali hutumika kumsaidia huyo mtu anayelipwa na mshahara unaotoka kwenye kodi za wote. Imefika mahala unakuta wananchi wa hali ya chini wanawaombea yawakute mabaya walioko serikalini ili tu nao wawe wanapata hekaheka nyingi japokuwa serikali inakuwa inajichovya humo kuwasaidia, chuki baina ya makundi haya mawili hukua siku hadi siku. Wananchi wa hali ya chini na, au wananchi ambao si wafanyakazi wa serikali hujikuta wakijitenga hata mitaani wakijisemea kuwa tupo tofauti kati ya wale wa serikali na wasio. KUNA MMOJA ANAJISIKIA KUWA YEYE NDIO YEYE NA WENGINE WASIOKUWEMO KWENYE SERIKALI NI KAMA MBWA TU, samahani kwa maneno hayo. kwa ufupi UONGOZI UNAOSHIKA HATAMU UNAKUWA NI BINAFSI SANA hasa katika nchi kama yetu hii

nakuja kwa swali lako; yupi anastahiri kujigharamia?...Nafikiri serikali ingejitahidi kuweka usawa kusaidia wananchi wote na si baadhi. Kwasababu si wote wanaweza kuwa watumishi wa umma, na hii tabia ya upendeleo imekua kubwa kiasi kwamba ili uwe mtumishi wa umma watu wanatoa rushwa ili waingie humo, wengine wenye nafasi huwaweka nduguze katika vitengo ili tu wajazane kindugu ndugu waendeleze ubinafsi huo wa kihuduma kati ya masikini na watumishi wa umma.

NB: serikali makini ingekuwa inasaidia wananchi wote kwa usawa, kama ni kweli kuna upendeleo!!
Umenena vyema kabisa ; Kwa mfano ni utaratibu upi unafaa kufanikisha hilo?
 
Mazishi ya kiongozi yafanywe na serikali sawa
Mwananchi apewe huduma zote stahiki na muhimu na serikali kabla hajafariki dunia📌📌🔨🔨🔨
 
Serikali haitoi bure huduma za afya hivyo kuna michango hutakiwa pale mgonjwa anapofika hospitali na bahati mbaya akafariki. Yaani kwa akili zako unataka mtumishi wa serikali ajilipie matibabu wakati anakatwa pesa kwa ajili ya matibabu kila mwezi.

Kama uko karibu na kuku ipe simu niieleshe kisha itakusaidia kutafsiri nachosema.
Kwahiyo malipo yote hutokana na mchango wake, magari ya serikali Kwa akili ya kusafilisha msiba na mazishi ni mchango ,usafili wa ndege, majeneza, vyakula n.k zote hutokana na michango! We chizi kwelikweli,!!! Una ushabiki wa kishamba sana! Tambua Mimi ni mtumishi level ya Senior naelewa kila kitu!
 
Suala la utumishi wako katika level ya senior ni la kumwambia msichana wako kikojozi sio mimi.

Ni watumishi wangapi miili yao hupandishwa ndege kwenda kuzikwa. Hujui hata katika utumishi kuna VIP LEADERS hao unataka wakifa serikali iwapeleke kwenye maeneo ya maziko yao kama wewe mkamua ng'ombe.

Uliwahi kuona mwalimu amepandishwa ndege kwenda kuzika Tukuyu kisa ni mtumishi wa serikali. Unajilinganisha na VIP?

Una kuku hapo karibu uipe simu niilekeze jambo kisha ikupe ufafanuzi?
 
Umenena vyema kabisa ; Kwa mfano ni utaratibu upi unafaa kufanikisha hilo?
ingekuwa serikali ina fedha ningeshauri, kwakuwa mtu akifariki harudi tena kuwafilisi fedha
1. kwa wanaofariki mbali na nyumbani; serikali ingewasafirishia maiti hadi nyumbani kwao wafiwa, ili wafiwa waendelee na taratibu zingine

2. kwa wanaofariki karibu na nyumbani kwao; serikali ingehudumia chakula kwa siku mbili tu msibani. Hapa ni lazima serikali ishauri wananchi wazike ndani ya mda huo ili wahudumiwe

Nilikuwa nawaza hivyo kwa upande wa mazishi na kifo.
 
Hususani namba moja serikali ikiamua inaweza! Hata isipotumia gari ya serikali, lakini inaweza toa Pesa hata nusu gharama umbali usiozidi kanda maalum!!
 
Nauweka mjadala huru kwenu!

Mazishi mengi ya viongozi kuanzia matibabu hadi mazishi hugharamiwa na serikali, lakini Msiba wa mwananchi maskini hupitia misukosuko kuanzia upatikanaji wa mwili hospitali hata namna ya kuusafilisha!

Je; Ni yupi anaestahili kujigharamia mazishi kati ya kiongozi wa umma au mwananchi wa kawaida ambaye hana ajira wala bima?

KARIBUNI
Kiuhalisia msaada ilitakiwa apatiwe mtu ambae hana uwezo wa kuifikia ile huduma either kutokana na maumbile,kipato,elimu n.k lakini mifumo tuliyonayo/tuliojiwekea duniani kwetu mingi sana inakinzana na uhalisia wa mambo na maisha yetu
 
Huko Libya jamaa mbona aliweza mambo mengi tu! Kupanga no kuchagua! Kama kweli wenye mamlaka ni wacha Mungu wanashindwaje kufanya hivyo?
 
Hususani namba moja serikali ikiamua inaweza! Hata isipotumia gari ya serikali, lakini inaweza toa Pesa hata nusu gharama umbali usiozidi kanda maalum!!
wanaweza saidia mojawapo, maana serikali ina magari kila mkoa/wilaya...ina coster na land cruiser za kusaidia shughuri
 
Kuna mhubiri mmoja alituambia huko mbinguni utaishi kwa matendo yako hapa duniani. Huko ni mij na una nyumba, hadhi ya kazi na nyumba yako itatokana na malipo yaa matendo yako ya duniani.

unaweza kukuta JF Kennedy ni shamba boy wa kuuza chapati.
 
Back
Top Bottom