Kama ilivyo ndoa za kiserikali, sasa ni muda serikali ije na utaratibu wa Mazishi ya Kiserikali

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
315
879
Hizi ni dini za mchongo zilizojaa unafiki na utapeli, zimekuwa zikimantain wafuasi wake kwa kuwajengea hofu ya kutokuswaliwa pindi watakapokufa.

Tumeona hili limekuwa likileta sitofahamu kubwa sana kwenye jamii pale ambapo kiongozi wa dini kwa makusudi kabisa anakataa kumfanya ibada ya msiba, kisa jambo dogo tu ambalo marehemu alipishana na hawa viongozi wa dini.

Sasa serikali iingilie kati suala hili maana waumini wengi wameshachoshwa na utapeli wa dini hizi ila hawajui wanatokaje. Cha kufanyika serikali impe mamlaka Mwenyekiti wa Kijiji kupokea malipo ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu na hivyo Mwenyekiti anahudhuria makaburini anatoa waraka wa kuishi kwa amani na upendo hapa duniani na mwisho anamuru mazishi kuendelea. Baada ya hapo shughuli inakuwa imeisha na watu wanatawanyika.

Nadhani hii itapunguza hawa viongozi wa dini kujiona miungu watu.
 
mazishi ya kiserikali mbona yapo???,,,wewe siku moja ndgu yako akifa ,,,uchune,usiende kumchukua mochwari kwa siku kadhaa,hapo ndipo utajua serikali ina kazi nyingi!!
 
Unahangaika bure.

Siku hizi kuna wachungaji kibao mitaani. Na vikanisa vidogo vidogo.

Hivyo vinakuja kukusaidia kukuzika kama katoliki ama KKKT wamekugomea kukuzika
 
mazishi ya kiserikali mbona yapo???,,,wewe siku moja ndgu yako akifa ,,,uchune,usiende kumchukua mochwari kwa siku kadhaa,hapo ndipo utajua serikali ina kazi nyingi!!
Mtoa hoja ana hoja. Tueleze sasa huo utaratibu ukoje.. ili Mimi nikifiwa au kabla sijafa naweza acha wosia nizikwe kwa utaratibu Wa Selikali.. usikumbilie kusema nifiwe halafu niuchune kivipi.. sitaki kuuchuna nataka nijue utaratibu nianzie wapi.. sitaki ndugu yangu azikwe kwa taratibu za dini ya kiislam, kikristo, kihindi sijui nini sitaki nahitaji azikwe kwa taratibu za kiselikali. Niende wapi au nimuone nani? M/kiti Wa mtaa, Kijiji, polisi au mahakama au mkuu Wa wilaya? Hii ni hoja ya msingi usilete mizaha kwenye mambo ya msingi huna majibu unakausha.
 
Utaratibu Wa Selikali sifahamu ila Dini anayosali marehem ikigoma kuendesha ibada kwa sababu yoyote Ile. Nalifahamu kanisa Moja la waadventista wasabato, Hawa wanaendesha ibada ya mazishi kwa mtu yeyote aliyeomba kufanyiwa ibada hiyo awe mlokole, mkatoliki, muislam, Hana dini wao ukitoa taarifa Tu hata kama huna Jeneza, sanda n.k watatoa na marehemu wako atafanyiwa ibada..
 
Kukataa kumzika maiti na kumfanyia ibada ni dhambi na watu wa mji husika wote wanakuwa wamefanya kosa.

Sijawahi kuona kwa upande wetu ila kuna manaswara ni wanafiki sana hata mwaka jana kule Arusha kuna mdada waliktaa kumzika..
 
Serikali tunazika vizuri sema hapo umepaongezea vizuri kwamba hawa wa wakilishi wa viongoz wa mitaa wapewe hadhi ya usimamizi wa haya mazishi ndo kitakua kipya
 
Unahangaika bure.

Siku hizi kuna wachungaji kibao mitaani. Na vikanisa vidogo vidogo.

Hivyo vinakuja kukusaidia kukuzika kama katoliki ama KKKT wamekugomea kukuzika
Hata Mwamposa anatangaza mara kwa Mara pale kawe kwamba ndugu yako akikataliwa na Mchungaji kampe taarifa atakupa Mchungaji na waumuni wakamzike ndugu yako.
Baba paroko asikutishe Mwamposa anatoa Hadi upako bure! Arise& shine
 
Back
Top Bottom