Wenzako wala hawajali hiki, ndio kwanza wanafikiria kuongeza ndege nyingine ya kifahari! Kazi ipo sana, sana sana..Nilishawahi sema, nimeshuhudia hayo magari ya kifahari, VX6-VX8 yanapowashwa tangu asubuhi hayazimwi mpaka wakati dereva anapolala! Yaani hata kama gari imepaki ofisi au kwenye shughuli za mheshimiwa hakuna kuzimwa, kisa eti gari liwe na baridi ndani! Yaani jamaa wanaponda hela za mlipa kodi kama hawana akili nzuri..Sasa fikiria nimeona kama 2 au 3, je yako mangapi serikalini yanafanya hivi? Si mchezo hela zinavyochomwa moto..Salaam,Ni hayo tu.
niongezee hapo vp kuhusu jose Mujika kama ni issue ya usalama?Najua kinga ni bora kuliko tiba. But, seriously kati ya Rais wa Ufaransa na wa Tanzania nani anayehitaji hilo secured car? Rais Magufuli anaogopa nini? Vipi kuhusu marais wa nchi kadhaa Ulaya ambao wanatumia tu public commuter trains?
Mimi naongelea kuhusu matumizi ya kodi na pesa za umma. Sijali kama kiongozi hata akinunua Maserati kwa pesa zake. Hiyo ni mipango yake, ili mradi tu pesa kazipata kihalali.
Naona una overplay umuhimu wa usalama hapa. Pengine ufafanue usalama gani unauongelea na una husika vipi na gari? Je, kwa Macron kutumia hiyo Peugeot Citroen DS ali-comprise usalama wake?
Na huyo mkurugenzi analo shangingi alilouziwa na serikali kwa bei che eti atalitumia kwenda kazini! Wakati fulani JPM akiwa waziri wa ujenzi alichachamaa na kujaribu kuthibiti matumizi mabaya ya magari ya umma. Amekuwa Rais, kwake hilo siyo tatizo tena. Sijui lini Watz watapata kiongozi anayewahurumia kwa dhati! Ni haki kweli kutoza nyumba ya mbavu za mbwa kodi ya majengo ili mkurugenzi anunuliwe na kutembelea shangingi? Badala ya kuimba Mungu Ibariki Tz tuanze kuomba AIOKOE!Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.
Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
JF mna maneno!Pata picha Mwakyembe anaendeshwa kwenye VW Golf. Atafika Dodoma, center bolt imekatika.
Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.
Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
ki ukweli kwa hali ya barabara zetu haya ma VX na GX haya kwepekii kabisa...
Kwenye hoja ndiyo umeona hilo tu?Umeshawahi kutafakari,ukiwa na Suzuki grande au hiyo RAV 4 unayoizungumzia,unaweza kwenda vijiji vingapi ambavyo barabara zake asilimia 80 ni rough roads,na mara ngapi ili hiyo gari angalau iweze kuishi miaka 5?Hizo gari kama Landcruiser V8 kiuhalisia ni gari ngumu sana,kwa hali ya barabara za vijijini ukipeleka gari kama Rav4,Suzuki,Xtrail,Klugger na gari za mtindo huo maisha yake yatakuwa mafupi sana.
So basically unataka wawe na magari ya kutumia mjini na ya kutumia kwenda nayo vijijini sio. Sasa hapo wanasave au watatumia gharama zaidiNipe justification ya Spika kutumia S class 500 ku-commute kati ya Uzunguni-Bungeni-Uzunguni. Au PM kutumia S class 500 au LC 200 ku-commute kati ya home and office. Ama VP kutumia GL class ya mwaka 2015 ku-commute home and office.
Kwani wakitumia VW Passat kuna shida gani kwa hizi home and office commuting?
Walishazoea kumtoa kwenye line kuna kazi kwelikweli.ni vyema Magufuli akaliangalia na hili pia. Hakuna haja ya kuishi kianasa namna hiyo.
Kwa hiyo hizo 7 series, S class na GL class ndiyo wanayatumia kwenda nayo vijijini?So basically unataka wawe na magari ya kutumia mjini na ya kutumia kwenda nayo vijijini sio. Sasa hapo wanasave au watatumia gharama zaidi
Braza ni aidha unajitoa ufahamu ama uwezo wako wa kuelewa ni mdogo. Mimi sijasema hizo Passat zitumike off road. Ebu usome na kuelewa basi mzee.Hii ni Leo bado unataka watumie Passat!! Uhalisia unakataa hayo mawazo huo Ndo ukweli wenyewe ila haina maana kwamba barabara zenye viwango hazijengwi, hadi hapo haya magari yataendelea kutumika tu sababu biashara zingine Lazima ziendelee. Hatuwezi jibana kutumia Passat eti pesa tunayosave inajenga barabara itakua wendawazimu itamaanisha sehemu zingine kama hizi viongozi hawatafika hadi hizi barabara ziwe sawa na who knows inaweza kuwa 10yrs from now
View attachment 512976
On the other hand, ulichoandika kinadhihirisha jinsi CCM isivyostahili kuendelea kuwa madarakani hata nusu saa! Haiwezekani miaka 55 ya uhuru, tuwe bado na barabara kama hizo. Sasa CCM imefanya jambo gani kwa asilimia 100 toka ishike madaraka?Hii ni Leo bado unataka watumie Passat!! Uhalisia unakataa hayo mawazo huo Ndo ukweli wenyewe ila haina maana kwamba barabara zenye viwango hazijengwi, hadi hapo haya magari yataendelea kutumika tu sababu biashara zingine Lazima ziendelee. Hatuwezi jibana kutumia Passat eti pesa tunayosave inajenga barabara itakua wendawazimu itamaanisha sehemu zingine kama hizi viongozi hawatafika hadi hizi barabara ziwe sawa na who knows inaweza kuwa 10yrs from now]
Hata kama siyo la kawaida, Ufaransa wana deserve hiyo lixury kwani angalau wameshasahau kuhusu huduma mbaya za afya, elimu, barabara, maji, umeme n.k. miaka mingi iliyopita.kufanikiwa kuwazuga wengine kwa muonekano wa gari analotumia eti ni la kawaida tu!