Mjadala Maalum: Wanaosaka ajira nje ya Tanzania

Botswana kulikua kuzuri miaka ya nyuma, ajira zilikua nyngi sana, na mshahara ulikua mzuri kwa kazi za kawaida kama ualimu, clinical officer an manesi walikua wanalipa around pula 20000, kwa mwezi sawa na 4m ya Tz, ila wazimbabwe wameshaharibu maana wameingia kwa windi sana na kusababisha ajira kuwa ngumu sana. Hata ajira za kada ya afya imekua ngumu sana kupata.
Mimi huko ndo nataka kwendaaa kusakaaa ajira mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Mimi huko ndo nataka kwendaaa kusakaaa ajira mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTEKama una fani ya uhasibu au IT kapambane unaweza pata, na sio gharama sana kufika huko, unachukua zako busi mpaka tunduma,b aada ya Tunduma unaunga bus la Lusaka , from Lusaka unachukua gari mpaka kazungura ferry ukishavuka tayari upo republic of Botswana, sasa hapo inategemea unaenda Wpi GB, franctown, mahuni au Natla?Kilo Tano unasafiri confortable
 
Habari wananchi na wasio wananchi lakin mko Tanzania,

Kwa makusudi nimeamua kuanzisha thread hii iwape mwongozo vijana wanaosaka ajira Nje ya Tanzania na Nje ya Africa kwa ujimla,

Ili upate ajira nchi yoyote au fursa zingatia yafuatayo kabla hujakurupuka kwenda uko,
1. GDP na money circulation katika nchi husika na mzunguko Wa fedha ,
Hapa patakusaidia kujua je uko uendako uwezekano Wa kupata ajira itakayokulipa vema upo?

2. Employment and un employment rate,
Hii itakusaidia kujua kama huendi kuzurula na bahasha kwa muda mrefu bila mafanikio. Hii itakupa mwanga kama uende au lah,

3. Life expenses and earnings , hii pia itakupa mwanga kujua kama utakachopata kama ujira na ukatumia , utaweza kubakiza kuja kuwekeza kwenu?
Mfano
A. Gharama ya bed spaces au vyumba vya kupanga
B. Usafiri
C. Chakula
D. Matumizi mengine

Watu wengi hupata sifa kuwa anaish ulaya wakati anachopata akilipa matumizi anazidiwa na MTU anayeish Tanzania, na akija likizo anawakimbia aliowaacha maana kimaendeleo wanakuwa mbali,

4. Employment policy for foreigners,
Hapo chunguza , yafuatayo
A. Kodi ya wageni kufanya Kazi katika nchi hiyo
B. Mishahara ya wageni
C. Muda Wa kupata working permit kwa wageni na gharama Zake kwa mwaka,
D. Mikataba kwa wageni,

5. Gharama za kufika nchi husika na gharama za kuishi wakati ukisaka ajira, ni muhimu kujua gharama husika za kusafiri na kuishi,

6. Aina ya Visa unayohitaji kwenda nchi hiyo,

Wengi huwa na visiting visa, MUHIMU VISA IWE MIEZ MITATU NA ZAID NDO UTAFANIKIWA , ya mwezi mmoja haitasaidia labda urudi na uende upya, inaweza kukuchukua miez 4 kupata Kazi, yaan visa ikaisha ukarudi au ukafanya RUN VISA SYSTEM,

7. Epuka kuwa na one way ticket , utarudishiwa uwanja Wa ndege maana wanataka wajue ni lini utarudi kwenu , japo zipo airports ambazo hawasumbui kuwa na one way or onward ticket, kama vile Kuala Lumpur. Changi Singapore, bole Ethiopia, Kathmandu's Nepal, alander Sweden, lakin ili kujiweka Vema kuwa na outbound tickets,

8. Epuka ma agents Wa online, jiandae ufike eneo husika , usiwaamini ma agents Wa online watakula hela yako na utaishia kulia tu. Hasa ma agent Wa Dubai na uarabuni wengi ni wanaigeria wahuni sana, USHAURI chukua visa yako, ticket yako pata utakapofikia , saka ajira Mwenyewe zipo sana na inahitaji uvumilivu kama miezi mitatu, japo kuna wanaopata ndani ya wiki moja,

9. UBAGUZI
Haikwepeki muafrica dunian huwa anabaguliwa ila cha muhimu ni kuchagua sehem nzuri ya ubaguzi Wa kawaida, napendelea MTU kama anaenda asiende Urusi, India , Nepal, German , Spain, huko ubaguzi ni Nje Nje, ambao hauvumiliki. Hata Kazi kupata ni ngumu sana,

10. Maeneo hatarishi
A.Nepal, sri Lanka, na Bangladesh wanatoa kafara watu wehusi
B. India hasa Mumbai wanaua waafrica
C. Syria,turkey,ukraine kuna mapigano makali huwez pata kazi


11. Maeneo mazuri kufanya Kazi
A. Malaysia
B. Sweden
C. USA, earnings ni kubwa
D. Denmark
E. Estonia
F. Singapore
G. New Zealand
H. Australia
I. Canada, hapa visa yake ngumu kupata
J. Finland ila mshahara Mdogo
K. Japan
L. Norway
M. Luxembourg
N. Botswana
O. Seychelles
P. England japo ngumu kupata Kazi

12. MWISHO NA MUHIMU set mind set yako kupata Kazi yeyote, andaa CV za Kazi mbali mbali, yaan CV tofauti tofauti kama tano, yaan hata za kudanganya ila uhakikishe unakuwa na kumbu kumbu ya ni CV aina gan umepeleka wapi usije kujichanganya wakati Wa interview, kwa kazi nyingi hawajali umesomea nini, ila kwa udaktari , ualimu, engineer , lazima uwe umespecialize, ila kwa nyinginezo ngazi za chini wanajali experience uliyoandika kwenye CV husika,

Ushauri watanzania jaribuni hata Nje ya Tanzania inawezekana, tafteni hata kufagia na kufanya mauzo supermarket inalipa, mshahara wao si chini ya 1500 dollars per month take Home,

Watanzania wanaogopa kuonekana ana degree lakin anafagia, au analinda au anafua mashuka au analea wazee au anasajili lain mtaani hapana unachohesabu ni umeingiza ngapi

Aina ya Kazi zinazopatikana ulaya na mshahara waka
1. Sales and marketing 2500 USD per month
2. Security guard huyu ni Wa kuchezea camera za usalama kwenye mitaa na nyumba. 3000 USD
3. Watchman 1800 USD
4. Teachers ni 20,000 USD ila huwez pata kama ni mwafrica Kazi ya ualimu ni kitu sensitive sana,
5. Kitchen helper 1500 USD free transport, house allowance na food
6. Steward 2000 USD
7. Gardner 1700 USD
8. Room attendants kwenye hotels 2000 USD
9. House keeping 2300 USD
10. Waiter and waitress 2000 usd
11. Dish washer. 1600 USD wanaosha vyombo kwa Mashine maalum
12. Laundry and dry cleaner 1200 USD
13. Tax Driver 5000 usd hawa ni nchi chache lakin waganda wakenye na Wa Nigeria wanapata hizi Kazi
14. Cashier and accountants 6000 USD
15. Cleaners wanaooperate Mashine za usafi mtaani 2000 USD
16. Cook walio specialize 3000 USD
17. Houseboy / housegirls and nany ni 1300 USD , malazi na chakula bule,


Note that anayekulipia work permit ni mwajiri wako
Vp netherland/Holland yenyewe ikoje kwa job seeker ninadreams za kwenda huko nipe raman kama hakueleweki nijipange kwingine mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok sasa cha kufanya kuwa na yafuatayo
Kuna options 2

Ya kwanza
Kuwa na
1. Passport
2. Two passport photo zenye background nyeupe
3. Fee ya visa 150 USD
4. Kuwa na ticket ya kwenda na kurudi almost 780 USD
5. Kuwa na hotel booking kuonesha utakapokaa 30 days ni kama 1500 USD
6. Hela ya kuweka kama deposits ya kukudhamini ubalozin dollar 3000 ili ukizamia bila vibali waitumie kulipa faini,
7. Pia barua ya mwaliko kama una mtembelea MTU,


Njia ya pili ni simple kidogo

1. Mpate MTU aliyeko nchi unapotaka kwenda,
Scan passport yako mtumie kwenye email,
Mtumie ticket ya kwenda na kurudi ya kuambatanisha kwenye documents za kukuombea visa,
Mtumie 150 dollar za visa fee,
Mtumie passport size photo,

Yeye ndo awe mdhamini wako hakuna haja ya kuweka hela ya kukudhamini, ili ukioverstay wanambana yeye maana ndo mwenyeji wako,
Na hakuna haja ya hotel maana ataandika kuwa utakaa Kwake ,

Hii ya pili ni njia rahis,
Ndani ya week unakuwa sehem husika,
Na atakupa.mwongozo pa kuanzia maana utakuwa.na mwenyeji
Njia ya pili ni nzuri Sana....
 
Habari yako mkuu, mi nafanya kuunganisha watu wanaotaka kazi Nje,

Gharama zangu siyo nyingi

Kukutaftia nafasi na kukuweka ni 100 USD

Kukutaftia visa na kwenda 300 USD

Gharama za usafiri inategemea na unapoenda

Alafu malipo yangu nu kuwa utakatwa 5% kwenye mshahara wako kwa miez mitatu,

Nafanya na waganda na wakenya

Ila tahadhari nafasi yeyote unapaswa kuikubali, iwe mwanzo wako wa kutafta Nyingine

Nchi nazofanya connection
1. UAE
2. Turkey
3. Botswana
4. Scandinavian countries
5. Na Asia zingine.
Bado unaconnect
 
Mkuu moxec, nimeishi na kufanya kazi Namibia for almost 7 years. wale jamaa wana rank kwenye second world countries na wako vizuri kuliko kawaida. hawana longolongo na kila mtu yuko busy na mambo yake. Currency yao ina thamani sawa na Rand ya South Africa na hata ukienda supermarket na Rand inapokelewa the same uwe na NAD (Namibian Dollar). Ni sehemu nzuri ya kutafutia maisha..
Mkuu namibia
 
Vp kuhusu nauli kwa gharama za gari mpk ndege! !

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu, sikushauli uende kwa ndege. unaweza kwenda kwa kutumia basi na ukafika vizuri tu. Nauli ya one way kwa kutumia basi inaweza kuwa ina-range kati ya TSH. 300,000-350,000/- na itategemea na mtu mwenyewe na jinsi alivyo connect magari. kwa mwenye low budget unaweza panda magari ya Taqwa ya kwenda Bulawayo. shukia Livingstone (Zambia). panda shuttles (Noah) za kwenda sesheke (Border ya zambia na Namibia) na kama utaweza mwombe akupeleke mpaka custom kabisa. Ukimaliza kugongesha passport, panda tax (10 NAM $) mpaka centre (Katima Mulilo). then subiria magari ya kwenda windhoek (Though hapa itategemeana unataka kwenda mji gani) kwani huku miji yote inalingana kwa maendeleo na uzuri/usafi.

I hope maelezo haya machache yatasaidia. All the best and God bless
 
Ubarikiwe sn mkuu
mkuu, sikushauli uende kwa ndege. unaweza kwenda kwa kutumia basi na ukafika vizuri tu. Nauli ya one way kwa kutumia basi inaweza kuwa ina-range kati ya TSH. 300,000-350,000/- na itategemea na mtu mwenyewe na jinsi alivyo connect magari. kwa mwenye low budget unaweza panda magari ya Taqwa ya kwenda Bulawayo. shukia Livingstone (Zambia). panda shuttles (Noah) za kwenda sesheke (Border ya zambia na Namibia) na kama utaweza mwombe akupeleke mpaka custom kabisa. Ukimaliza kugongesha passport, panda tax (10 NAM $) mpaka centre (Katima Mulilo). then subiria magari ya kwenda windhoek (Though hapa itategemeana unataka kwenda mji gani) kwani huku miji yote inalingana kwa maendeleo na uzuri/usafi.

I hope maelezo haya machache yatasaidia. All the best and God bless

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom