Mjadala kuhusu kuzima simu bandia unaendelea live TBC1

Mjadala kuhusu kuzima simu bandia unaendelea live TBC1

Hii tender ya kuzima simu wangepewa TANESCO shughuli ingesha isha zaamaanii.....TCRA wanajivutavutaaa.....
 
Simu yoyote ile ya aina hiyo iwe inaenda AFRICA, ASIA, AMERICA, EUROPE, AUSTRALIA, IMEI huwa ni ile ile. Simu inaweza kuwa locked kutumia mitandao au unlocked kutumia mitandao ya nchi zote ila IMEI huwa hiyo hiyo kwa simu za aina hiyo!

International Mobile Equipment
Identity (IMEI) means International Mobile Equipment Identity. an IMEI is the unique serial number of every GSM mobile cell phone. The IMEI number is used by networks to identify valid phones and block stolen or blacklisted phones from accessing the network.
Kulikuwa na haja gani ya kuwaambia watu watume imei zao?Jipunguzie UZEZETA
 
Hivi kweli kuna watu wali amini kwa 100% kuwa eti simu zote fake zitazimwa?

asee... kweli fikra hizi za haraka haraka ndio maana hata serikali haipatagi shida kuwatawala inavyotaka wananchi wa nchi hii.

mimi natumia Tecno Y3 sio genuine na nimenunua betri mpya juzi tu hapa kwa sababu na amini hilo swala la kuzima simu feki sio swala jepesi kwa tanzania.
Na kama ujatuma imei aizimwi hiyo
 
Mjadala unaendelea TBC muda huu na wageni ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.Mjadala utaendelea mpaka saa 6 kamili usiku muda ambao ndio simu za bandia zitazimwa.

Kwa mujibu wa mtangazaji,baadae pia watafika wageni wengine kutoka TCRA kuelezea jambo hili la kuzima simu bandia ifikapo saa 6 kamili usiku wa leo.

Kuna nafasi ya watu kupiga simu na kuuliza maswali.

Fuatilia.

Moja ya jibu lilitolewa baada ya watu kuuliza maswali ni kuwa,simi yako ikizimwa,line yako itaendelea kufanya kazi kwenye simu nyingine ambayo itakuwa ni origino hivyo kama line yako ina hela za Mpesa,tigo pesa, n.k, fedha zako ziko salama.

Jambo lingine alilosema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ni kuwa,mbali na simu feki,hata tablet na moderm zinazotumia line za simu nazo zitaingia katika mkumbo huu.

Nachokiana hapa leo hii ni kuwa saa 6 kamili ya usiku wa leo itasubiriwa kama saa 6 kamili ya kukaribisha mwaka mpya.

Waziri wa Mawasiliano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wameondoka studio baada ya kumaliza session yao na sasa ameingia Meneja Mwasiliano wa TCRA,bwana Innocent Mungy na Afisa mwenzake kutoka TCRA kuendelea na mjadala huo.

NB:

Jumla ya simu(IMEI) zinazotarajiwa kuzimwa ni 630,000 na wanazizima kwa awamu kwa kuziingiza kwenye system.

Wanaondoka studio ikiwa ni saa 6:28 na wametoa ripoti kuwa zoezi la kuzima simu linaendelea na mpaka sasa wamekamilisha asilimia 70 ya kazi hiyo.

Kwakweli inasikitisha japo zoezi hili linatajwa kufanywa kwa nia njema!

Hivi mie ninachojiuliza, kama sababu kuu ni usalama, yaani sio rahisi kumjua mtumiaji wa simu, na hizo simu zinatumika kwingineko dunia na hasa China zinakotengenezwa, kwanini wasingefikiria kidogo na kuona wengine wanafanya nini? Kwa mtu anayeifahamu China, tracking ya simu iko kila mahari. Kwa wachina, simu yako lazima wanaijua na imesajiliwa kuhakikisha wanaweza kukufuatia! Hii ina maana kuwa wana uwezo wa kuzisajiri na kuzifuatilia kunapokuwa na umuhimu wa kufanya hivyo; Kwa mtazamo wangu wachina wana software ya kuweza kusajili simu yoyote iwe fake au genuine. kwa hiyo ingekuwa rahisi kwa Tanzania kwenda kwa wachina na kupata hiyo software badala ya kuzima hizi simu. Vita ya simu genuine na fake ni ya kimataifa kwa wafanyabiashara wakubwa wa magharibi na china na India ili kulinda biashara zao na si kingine. Je Tanzania inafaida na maamuzi haya au inawasaidia matajiri wa magharibi kutajirika zaidi? Kumbuka wanazima simu 630,000 na wengi wa watumiaji ni wanafunzi na maskini wenye kipato cha chini. Hii ina maana tayari umeondoa uwezo wa Watanzania hawa kutumia simu nafuu kwa masomo yao (internet) na hata shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Tayari inairudisha Tanzania nyuma zaidi, ikiwa iko nyuma ya nchi nyingine hasa katika Jumuiya ya Afrka mashariki katika matumizi ya teknolojia ya habari. Tunaweka mipango ya kupunguza digital divide (decreasing the gap between people with access to computers and the Internet and those who do not as a nation). Tungefikiria faida na hasara za zoezi hili nina hakika tungefanya utafiti wa kutosha na kuja na innovative solution ambayo itachangia kwenye maendeleo ya nchi zaidi ya kufuata mkumbo.
 
Cm wanazosema cfeki sidhani kwenye nchi zilizoendelea wanazipokea, wanatushangaa sie kuona tuna cm ya dolar 10, wao cm inaanzia dolar 200
 
Ongeeni yote,jifarijini mnavyotaka,ila leo ni leo,kama una gaka lazima liwekwe dampo
 
Ndugu mwache na ujinga wake.mi zangu zote feki na haizimwi hata moja.Mijitu mizezeta sana Tanzania yetu walipoambiwa watume imei walijua ujanja kumbe ndipo walipojimaliza wenyewe.

Ndiyo mkuu yaani wengine walikuwa wanauliza ile namba vipi mbona hawajibu ..... Hapo ndo utashangaa malalamiko simu original inafungwa..... Tanzania hii basi tena..... Hapo bado gharama ya huo mtambo,mapato yatakavyo kosekana serikalini na usumbufu kwa mwananchi wa kawaida

Wakuu kwanza mnapaswa kujua IMEI ni kitu gani na kinafanya kazi gani kwenye simu

Kama ni mtundu kidogo basi imei ni kama IP address ya kompyuta yako

Imei ndio anuani ya simu yako inayotumika kuwasiliana na SP wako ambao ni Voda, Tigo, Halotel nk nk
Unapochomeka simcard yako kwa simu basi imei ndio inatumika kurusha na kuwasiliana na mtandao husika

Ukienda kwamfano Voda kwenye mitambo yao huwa inasoma no 0754xxxx with IMEI No 35xxxxxxxxxxx, hivyo akina Voda na Tigo wala hawahitaji utume request ili waitambue emei yako sababu ndio inaambatana na no yako kuwasiliana na mitambo yao, na bila emei basi simu haiwezi kuwasiliana na mitambo ya simu

Imei za simu zinatolewa na shirika moja tu duniani, kila mtengeneza simu anawajibija kwenda kuomba imei kwaajili ya simu zake baada ya kukidhi viwango
Baada ya hapo imei hizo husambazwa kwenye mitandao yote ya simu duniani wakizihitaji, hapa tz hatukuwa tukizihitaji kabla

Kinachofanyika ni kwamba mitandao ya simu ita upload imei zote halali kwa maana ya zilizotolewa na shirika husika tu linalogawa imei kwa watengeneza simu, kisha mitambo itakuwa commended itambue imei hizo tu, imei zingine fake zitakataa kuconnect na mitambo ya simu

Hakuna miujuzi yoyote mkuu katika hili
Labda issue iwe ni je hawa tcra kushirikiana na mitandao husika mitambo hiyo ipo na inafanya kaZi ipasavyo?

Lakini sio kusema eti haiwezekani au ni jambo la miujiza
 
Yaani km kweli sim feki zitazima... Kwa kweli nitajivunia maendeleo ya technologia kwa Tanzania yetu... Maaana mie naona km hawa jamaa wanazuga tuuu.....
Hakuna cha kujivunia hapo!
Wananchi waliozimiwa simu wanapaswa kwenda mahakamani na risiti zao walizonunulia simu ili wakadai fidia serikali kwa kushindwa kumlinda mlaji (consumer)! Iweje nchi iingize bidhaa fedha huku tukiwa na vyombo lukuki vya kiuchunguzi wakiongozwa na TRA, TBS na maofisa forodha wa bandari na viwanja vya ndege!
Pia maduka yaliyouza bidhaa feki nayo yanapaswa kuwajibishwa!
 
Ahsante kwa maelezo mazuri kwahiyo tatizo si la simu feki Bali ni wizi Wa IMEI,kwa maana nyingi hizi cm zenye imei za bandia yawezekana ni original ila kwa vile hazijasajiliwa ndo maana zinaitwa feki ,na kwa vile kuna simu feki lakini zona IMEI halali basi hizo zinaitwa original lakini ukiangalia hiyo cm Union a kabsa kuwa hili ni lifeki.
Wakuu kwanza mnapaswa kujua IMEI ni kitu gani na kinafanya kazi gani kwenye simu

Kama ni mtundu kidogo basi imei ni kama IP address ya kompyuta yako

Imei ndio anuani ya simu yako inayotumika kuwasiliana na SP wako ambao ni Voda, Tigo, Halotel nk nk
Unapochomeka simcard yako kwa simu basi imei ndio inatumika kurusha na kuwasiliana na mtandao husika

Ukienda kwamfano Voda kwenye mitambo yao huwa inasoma no 0754xxxx with IMEI No 35xxxxxxxxxxx, hivyo akina Voda na Tigo wala hawahitaji utume request ili waitambue emei yako sababu ndio inaambatana na no yako kuwasiliana na mitambo yao, na bila emei basi simu haiwezi kuwasiliana na mitambo ya simu

Imei za simu zinatolewa na shirika moja tu duniani, kila mtengeneza simu anawajibija kwenda kuomba imei kwaajili ya simu zake baada ya kukidhi viwango
Baada ya hapo imei hizo husambazwa kwenye mitandao yote ya simu duniani wakizihitaji, hapa tz hatukuwa tukizihitaji kabla

Kinachofanyika ni kwamba mitandao ya simu ita upload imei zote halali kwa maana ya zilizotolewa na shirika husika tu linalogawa imei kwa watengeneza simu, kisha mitambo itakuwa commended itambue imei hizo tu, imei zingine fake zitakataa kuconnect na mitambo ya simu

Hakuna miujuzi yoyote mkuu katika hili
Labda issue iwe ni je hawa tcra kushirikiana na mitandao husika mitambo hiyo ipo na inafanya kaZi ipasavyo?

Lakini sio kusema eti haiwezekani au ni jambo la miujiza
 
Hakuna cha kujivunia hapo!
Wananchi waliozimiwa simu wanapaswa kwenda mahakamani na risiti zao walizonunulia simu ili wakadai fidia serikali kwa kushindwa kumlinda mlaji (consumer)! Iweje nchi iingize bidhaa fedha huku tukiwa na vyombo lukuki vya kiuchunguzi wakiongozwa na TRA, TBS na maofisa forodha wa bandari na viwanja vya ndege!
Pia maduka yaliyouza bidhaa feki nayo yanapaswa kuwajibishwa!
Ni kweli unalolisema...
Mimi nasemea hiyo technology kupanda
 
Bw. Killerman hivi ni kweli unaamini kwamba simu fake Tanzania zinazimilikiwa na Watanzania ni 3 katika kila simu 10, kabisaaaa??? Najiuliza maswali mengi sana kuhusu hili nakosa majibu....
Na ndio maana nikasema siamini...
Ikitokea ndo nitajuwa uwakika wa jambo hili....
 
Jamani asubuhi ndio ishafika,,, na hii ni tar 17.
Kwa yeyote anayejuwa mtu aliyezimiwa simu yake ambayo ni feki atujuze...
Ila awe mkweli tuu.....
 
Paul, IMEI siyo IP address kwani IP address hutolewa na mmilki wa mtambo, yaani sawa na namba ya simu (0754..., 078...). IMEI ni kama MAC address ya computer maana iko katika hardware (computer) yenyewe kama ilivyo IMEI kwa simu. Maelezo mengine uko sahihi! Every

Back
Top Bottom