Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Mjadala unaendelea TBC muda huu na wageni ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.Mjadala utaendelea mpaka saa 6 kamili usiku muda ambao ndio simu za bandia zitazimwa.
Kwa mujibu wa mtangazaji,baadae pia watafika wageni wengine kutoka TCRA kuelezea jambo hili la kuzima simu bandia ifikapo saa 6 kamili usiku wa leo.
Kuna nafasi ya watu kupiga simu na kuuliza maswali.
Fuatilia.
Moja ya jibu lilitolewa baada ya watu kuuliza maswali ni kuwa,simi yako ikizimwa,line yako itaendelea kufanya kazi kwenye simu nyingine ambayo itakuwa ni origino hivyo kama line yako ina hela za Mpesa,tigo pesa, n.k, fedha zako ziko salama.
Jambo lingine alilosema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ni kuwa,mbali na simu feki,hata tablet na moderm zinazotumia line za simu nazo zitaingia katika mkumbo huu.
Nachokiana hapa leo hii ni kuwa saa 6 kamili ya usiku wa leo itasubiriwa kama saa 6 kamili ya kukaribisha mwaka mpya.
Waziri wa Mawasiliano na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wameondoka studio baada ya kumaliza session yao na sasa ameingia Meneja Mwasiliano wa TCRA,bwana Innocent Mungy na Afisa mwenzake kutoka TCRA kuendelea na mjadala huo.
NB:
Jumla ya simu(IMEI) zinazotarajiwa kuzimwa ni 630,000 na wanazizima kwa awamu kwa kuziingiza kwenye system.
Wanaondoka studio ikiwa ni saa 6:28 na wametoa ripoti kuwa zoezi la kuzima simu linaendelea na mpaka sasa wamekamilisha asilimia 70 ya kazi hiyo.
Kwakweli inasikitisha japo zoezi hili linatajwa kufanywa kwa nia njema!