Mjadala: Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Wanasiasa kutoa Zawadi kwa Wananchi, ni Rushwa au ni Kutimiza ahadi?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
Salaam Wakuu,

Kuelekea Uchaguzi mkuu, Wanasiasa wamekuwa wakivalia nguo za vyama na kisha kuzunguka huku na huku kutoa Zawadi na kudaiwa kwamba wanatimiza ahadi walizozitoa 2015.

Na hii imekuwa na pande mbili:
jamiiforums_20200601_1.jpg

1). Anayetoa Msaada kama sio Mbunge au kiongozi yoyote wa Kuchaguliwa huwa wanakamatwa na kudaiwa wanatoa rushwa. Mfano Aden Rage. Hii haijalishi una uwezo au huna.
Tabora: TAKUKURU kuwakamata Wanasiasa walioanza Kampeni kabla ya muda, Aden Rage kashadakwa

2). Ukiwa mtu aliyechaguliwa mfano Mbunge, Diwani, Rais pia ukiwa ni Kiongozi wa kuteuliwa kama Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa, Wao wanaruhusiwa kutoa misaada kwa kile kinachodaiwa ni kutekeleza ahadi za Uchaguzi.

Je, Wananchi hii hali mnaichukuliaje? Wote waruhusiwe kutoa misaada au endelee kama ilivyo? Sababu wanaotegemea kugombea, Wanalalamika kwamba hawapewi nafasi ili waonekane.

Hapa chini ni Picha ya Mbunge ya Eng. Stella Manyanya aliyeipost kwenye Page yake ya facebook akatoa zawadi ya Pikipiki kwa Viongozi wa Chama.

1591013906952.png

Eng. Stella Manyanya: "Leo nagawa pikipiki kwa viongozi wa chama, kwa kila kata katika jimbo langu la Nyasa, katibu wangu mh. Cosmas Nyoni(Lindongo) alipokuwa anazihakikisha. Mgeni rasmi ni mwenyekiti CCM mkoa wa Ruvuma ndugu Oddo Mwisho".

Nini maoni yako Mdau?
 
Inategemea! Kama anatoa kwa uwazi hiyo rushwa! Ila kama anatoa kwa kificho hiyo ni rushwa! Na pia inategemeana na lengo la zawadi
 
Back
Top Bottom