Uchaguzi Mkuu 2020: Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU awaonya Wafanyabiashara na Wanasiasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
1594983028436.png

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) nchini Tanzania, imetahadharisha wafanyabishara kutojihusisha na vitendo vya rushwa, kupitia dhana ya ufadhili wa gharama za uchaguzi ndani ya vyama vya siasa.

Hayo amesema Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 wakati anafungua warsha ya wadau wa uchaguzi, kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, jijini Dar es Salaam.

Brigedia Mbungo amesema, gharama za uendeshaji uchaguzi ndio chanzo cha vitendo vya rushwa, ambapo baadhi ya wafanyabiashara hutumia mwaya huo, kujinufaisha baada ya wagombea waliowafadhili, kupata uongozi serikalini.

“Lakini wapo wagombea wa vyama ambavyo vimekuwa vikichangiwa na watu wenye fedha na hasa wafanyabiashara ili kudhamini mchakato wa uchaguzi na baada ya uchaguzi watu hao wachache wenye uwezo hujipatia manufaa zaidi pindi wagombea hao wanapoingia kwenye madaraka,” amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Mbungo amesema, kitendo hicho kinasababisha viongizi kufanya maamuzi ya kisera yenye maslahi kwa watu wachache.

“Mara nyingi chanzo kikuu cha rushwa katika uchaguzi ni gharama za uchaguzi. Jambo hili husababisha wagombea au watia nia kutumia ushawishi pamoja na nguvu ya fedha ili kurubuni wapiga kura wawachague. Mgombea au wagombea wenye uwezo wa kifedha, hutumia kigezo hicho cha fedha kuwarubuni wananchi ili wawachague,” amesema Brigedia Mbungo.

Kuhusu warsha hiyo, Brigedia Mbungo amesema, Takukuru imeamua kukutana na wadau wa uchaguzi, ili kuunga mkono azma ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ya kutaka uchaguzi huo unafanyika kwa haki, huru na usawa.

Mkurugenzi huyo wa Takukuru amesema, tarehe 16 Juni 2020 wakati Rais Magufuli anavunja shughuli za Bunge la 11, alisisitiza wadau wa uchaguzi waepukane na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

“Ningependa tujikumbushe kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kupambana na rushwa bila uoga wala upendeleo katika nyanja zote ikiwemo katika uchaguzi. Kwa kuzingatia katiba ya nchi inayoelekeza taasisi na vyombo vyote kuelekeza nguvu na juhudi kuhakikisha tunaondoa rushwa katika janii yetu, Takukuru imeelekeza nguvu katika hilo,” amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Mbungo amesema rushwa ina athari kubwa katika mchakato wa uchaguzi na kwamba ni lazima idhibitiwe.

Ametaja athari zake kuwa ni; wananchi kukosa viongozi wawajibikaji, waadilifu na wazalendo, uvunjifu wa amani kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya kisiasa na taifa kugubikwa na rushwa.

Pia, rushwa inadidimiza uchumi wa taifa kutokana na ukosefu wa mipango thabiti ya maendeleo, kukosekana kwa uwazi katika maamuzi, utawala bora pamoja na wananchi kukosa imani na serikali yao.

Baadhi ya wahudhuliaji wa warsha hiyo ni viongozi wa dini, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahozi na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda.

=====

MAELEZO YA BRIGEDIA JENERALI JOHN JULIUS MBUNGO, MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU, KATIKA WARSHA YA WADAU YA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

PCCB HOUSE UPANGA DAR ES SALAAM

TAREHE 17/07/2020

Ndugu Viongozi mbalimbali wa Serikali;

Ndugu Viongozi wa Vyama vya Siasa;

Ndugu Viongozi wa Dini;

Ndugu Viongozi kutoka Asasi za Kiraia

Ndugu Wageni waalikwa;

Ndugu Watumishi wa TAKUKURU

Ndugu Waandishi wa Habari;

Mabibi na Mabwana.

Habari ya Asubuhi.

Ndugu Washiriki

Awali ya yote napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mwingi wa huruma na upendo kwa kutujalia afya njema na kutukutanisha mahali hapa kwa ajili ya kushiriki katika tukio hili muhimu la Kujadili kwa pamoja NAMNA TUTAKAVYOWEZA KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020.

Pili, natoa shukrani zangu za dhati kwenu kwa kuitikia wito wetu na kuja kushiriki katika warsha hii muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu. Kufika kwenu kunaonesha ni kwa jinsi gani mmedhamiria kushirikiana na Serikali katika kupambana na rushwa – hususan katika kipindi cha mchakato wote wa Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge pamoja na Rais, uliopangwa kufanyika Oktoba - 2020.

Dhamira na Ari mliyonayo ni muhimu sana kwa uimarishaji wa Utawala Bora, Demokrasia pamoja na Usalama katika Taifa letu. Hii inatokana na ukweli kuwa rushwa katika Uchaguzi ni hatari sana na inaweza kuleta madhara kwa Taifa ikiwemo uvunjifu wa amani kwani Viongozi wala rushwa hawataweza kuisimamia nchi hii na kuiongoza katika misingi ya Demokrasia, Utawala Bora, Haki, Usawa, Uwazi, Uwajibikaji na Uzalendo.

Ndugu washiriki,

Juni 16, 2020, Watanzania tulimshuhudia Rais wetu, Mheshiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihitimisha shughuli za Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Magufuli alifanya hivyo kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 90(2) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuhitimishwa kwa shughuli za Bunge la kumi na moja kulikofanywa na Rais wetu ni kielelezo cha kuanza kwa mbio za Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba, 2020. Uchaguzi huu ni ule ambao utahusisha nafasi za kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi, Mbunge wa Viti Maalum pamoja na Diwani wa Kata husika.

Ndugu washiriki,

Ni imani yangu kuwa nyote mnatambua wazi kuwa rushwa ni adui mkubwa wa uchaguzi huu kwani pamoja na kuminya haki, usawa, uhuru na demokrasia, rushwa katika uchaguzi husababisha madhara yafuatayo:

Kukosa Viongozi wawajibikaji, waadilifu na wazalendo;

Uvunjifu wa amani kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya kisiasa;

Taifa kugubikwa na rushwa;

Uchumi wa Taifa kudidimia kwa kukosa mipango ya maendeleo;

Viongozi kufanya maamuzi ya Kisera yenye maslahi kwa wachache;

Kukosekana kwa Uwazi katika maamuzi;

Kukosekana kwa Utawala Bora; na vilevile

Wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Ndugu washiriki

Ni kutokana na sababu hiyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, imeona ni vema kama ilivyo utaratibu wetu, tukutane nanyi wadau wetu muhimu ili kwa pamoja tujadili na tushauriane namna bora tutakavyoweza kushirikiana katika kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Oktoba 2020, unafanyika kwa haki na bila ya kugubikwa na vitendo vya rushwa.

TAKUKURU iliona ni vema sisi pamoja na ninyi wadau, tungeshirikiana kuhakikisha kuwa Watanzania wanafahamu kwamba uchaguzi ni:-

Ni fursa au mchakato ambao watu wa eneo la uchaguzi wanaitumia kutafakari mustakabali wa maendeleo yao katika eneo lao.

Ni fursa ya kuainisha changamoto zote zinazoikabili jamii inayoishi kwenye eneo hilo kwa kuangalia mahitaji ya eneo lao kwa mfano wanahitaji barabara, maji, zahanati au kuongeza madarasa katika shule iliyopo kwenye eneo lao.

Ni fursa ya kutathimini uwezo wa viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi uliopita endapo walikuwa na mchango wowote katika kuwaletea maendeleo tajwa.

Ni fursa ya kukubaliana kuhusu changamoto zilizopo kwenye eneo lao na kufanya tafakari ya namna ya kuzipatia ufumbuzi kupitia Mbunge na Diwani mwenye sifa ya uongozi, mwadilifu, asiyependa Rushwa na anayependa wananchi wake.

Ninasema hivi kwani ninatambua kuwa tafakari hiyo na uchambuzi huo wa changamoto ndiyo utakaowawezesha wananchi hao kutambua sifa na uwezo wa kiongozi wanayemtaka awaongoze.

Ndugu washiriki

Mara nyingi chanzo kikuu cha Rushwa katika uchaguzi ni gharama za uchaguzi. Jambo hili husababisha wagombea au watia nia kutumia ushawishi pamoja na nguvu ya fedha ili kurubuni wapiga kura wawachague; Mgombea au wagombea wenye uwezo wa kifedha, hutumia kigezo hicho cha fedha kuwarubuni wananchi ili wawapigie kura.

Lakini pia, wapo wagombea au vyama ambavyo vimekuwa vikichangiwa na watu wenye fedha na hasa wafanyabiashara ili kudhamini mchakato wa uchaguzi na baada ya uchaguzi watu hao wachache wenye uwezo, hujipatia manufaa pindi wagombea hao watakapoingia kwenye madaraka.

Ndugu washiriki

Ningependa tujikumbushe kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imedhamiria kupambana na tatizo la rushwa bila woga wala upendeleo katika Nyanja zote ikiwemo katika uchaguzi.

Kwa kuzingatia Ibara ya 9 (h) ya Katiba ya Tanzania inayoielekeza Taasisi na Vyombo vyote kuelekeza nguvu na juhudi kwenye kuhakikisha tunaondoa rushwa katika jamii yetu, zipo jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kuwa Rushwa katika Uchaguzi – INADHIBITIWA ikiwemo kutunga sheria mbalimbali za kusimamia jambo hili ambazo ni pamoja na:

Sheria ya Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya Mwaka 2010 (The Election Expenses Act No. 6 of 2010);

Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (Sura ya 343);

Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992; na

Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

HIVYO, kwa mujibu wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007, TAKUKURU imeendelea kufanya yafuatayo:

Kuelimisha wananchi juu ya rushwa na madhara katika uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi waadilifu. Elimu hii imekuwa ikitolewa kwa njia ya Semina, Vipindi vya Radio pamoja na Warsha kama hii.

Tunafanya kazi za utafiti na udhibiti kwa lengo la kubainisha mianya ya rushwa katika chaguzi zetu na kushauri namna bora ya kuiziba;

Tumekuwa tukichukua hatua za haraka na za kisheria kwa waliobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ndugu Washiriki

Kama nilivyoeleza hapo awali, TAKUKURU imewakutanisha hapa leo – viongozi wa kutoka maeneo na sekta mbalimbali, kwa lengo la kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa mwaka huu.

Mkusanyiko huu ni fursa kwenu ninyi kama viongozi na wawakilishi wa wananchi - kujadili na kutoa maoni yatakayosaidia kuleta ufumbuzi wa tatizo la rushwa katika uchaguzi.

Ni matumaini yetu kuwa, tukielewana sisi katika ngazi ya viongozi itakuwa ni rahisi sana kufikisha elimu hiyo kwa wananchi na kubadili fikra na mitazamo yao kuhusu rushwa katika uchaguzi.

Hatua hiyo itamwezesha mwananchi kuipinga na kuikataa rushwa kwa nguvu zake zote na hapo tutakuwa tumefanikiwa kupata viongozi waadilifu watakaoliletea Taifa letu maendeleo endelevu ndani ya muda mfupi.

Ndugu washiriki

Ushirikiano huu wa wadau ni muhimu sana katika kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU pekee hatuwezi kufanikiwa kuidhibiti rushwa katika Taifa letu.

Nina imani kwamba Warsha hii itatuwezesha kuwa na uchaguzi usiogubikwa na vitendo vya rushwa na ambao utatupatia viongozi waadilifu, wachapakazi, wazalendo na watakao endeleza kwa dhati - mapambano dhidi ya Rushwa nchini. Hii itawezekana kwa kuwa katika mkusanyiko huu wapo wawakilishi kutoka takriban kila sekta ndani na nje ya Serikali.

Tafadhali tuwe huru, kila mdau katika eneo lake aeleze ni kwa namna gani anadhani tunaweza kudhibiti vitendo au mianya ya rushwa katika uchaguzi.

Ndugu washiriki

Baada ya maelezo hayo, ninatamka kwamba WARSHA YA WADAU YA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI, imefunguliwa rasmi.

AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA

NAOMBA NISOME MAJUMUISHO YALIYOFIKIWA KUPITIA WARSHA HII

MAJUMUISHO YA MAJADILIANO KATIKA WARSHA YA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI RUSHWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

Washiriki wamekiri kuwa rushwa katika uchaguzi ni tatizo na kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni jukumu la kila mmoja hivyo:

Kushirikisha umma katika mapambano dhidi ya rushwa kupitia:

  • Kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vipindi vya Redio/TV, mikutano ya wanasiasa na kupitia jukwaa la kitaifa la mjadala wa rushwa katika uchaguzi.
  • Taasisi za elimu kuimarisha elimu ya uraia mashuleni na kupitia elimu ya watu wazima.
  • Kuwe na usiri kati ya TAKUKURU na mtoa taarifa.
  • Kuwe na zawadi au motisha kwa watoa taarifa.
  • TAKUKURU kuongezewa watumishi hasa kipindi hiki cha uchaguzi ili kuwafikia wapiga kura wa ngazi ya chini.
  • Kuwepo na ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa kwani jukumu hili si la TAKUKURU peke yake.
  • Kujenga uelewa wa pamoja kuhusu vitendo gani vinavyochukuliwa ni rushwa katika uchaguzi.

  • Kuimarisha maadili ya wananchi, hasa kwa wagombea na wapiga kura kwa:
  • Kuwa na mfumo wa wazi wa taratibu za kugombea ndani ya vyama ili kukabiliana na rushwa ya ngono
  • Kutoa elimu ya madhara ya rushwa kwa wagombea na wapiga kura kupitia majukwaa na mijadala ya wazi.
  • Taasisi za dini kuimarisha maadili ya umma kupitia mahubiri kwa kujenga hofu ya Mungu.
  • Kuwe na semina za wagombea katika ngazi mbalimbali za uchaguzi ndani ya vyama vya siasa.
  • Wanasiasa wanaoshiriki katika uchaguzi waeleze mali wamezipata wapi.
  • Uongozi wa kiasiasa na Serikali vitenganishwe ili kuleta ushindani sawa nyakati za uchaguzi.

  • Kuchukua hatua za kisheria na kiutendaji kukabiliana na rushwa katika uchaguzi kwa kufanya yafuatayo:

  • Kuwe na mfumo wa kutoa haki na uwazi kwa kila chama.
  • Kuchukua hatua za kisheria/kiutendaji katika kudhibiti rushwa kwa kuimarisha uchunguzi kwa njia mbalimbali ikiwemo kudhibiti utunzaji wa siri.
  • Kuja na mbinu mpya za kupambana na rushwa kwani wagombea na wapiga kura wana mbinu mpya za kuomba na kupokea rushwa katika uchaguzi (muda, kesi na maboya).
Ndugu Washiriki,

Ni imani yangu kuwa haya yote tuliyokubaliana yakisimamiwa na kutekelezwa kwa Weledi tutafanikiwa KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI – KABLA, WAKATI na hata BAADA ya uchaguzi.
 
Asipate tabu, atege mitego yake Lumumba na ofisi zote za chama cha veggies (vegiteble) huko ndiyo rushwa inafanyika.
 
Hili jahazi mwaka huu sijui maana kila utingo anajitokeza kutaka kuingiza gia
 
1.Tumesitisha uchunguzi dhidi ya Kibajaji, mwenye ushahidi aendelee.
2.Tumemwachia Serukamba maana alikamatwa kwa amri ya TAKUKURU Kigoma na siyo sisi Dodoma.
3.Mpaka sasa hatujaona rushwa kwa watia nia wa CCM.
4*Kuna rushwa kwenye uchaguzi hasa wafanyabiashara kukunua wagombea wa vyama Fulani ili wanufaike nao wakipata ubunge.
Bla bla bla bla!
 
View attachment 1509325

Sitashangaa huyu Brigadier akichukua form kugombea ubunge kwa ticket ya CCM
 
Back
Top Bottom