Mkuu tunakushukuru kwa mara nyingine tena kwa ufafanuzi wako mzuri, ningependa kujua yafuatayo: kwanza kipi ni rahisi kati ya kujenga network ya mabomba ya gesi nchi nzima au kuwa na viwanda vya kuchakata na kujaza gesi kwenye mitungi?
Unless kama mambo yamebadilika lakini kwa ninavyofahamu, usually, kama sio always, Natural Gas inafikishwa majumbani kwa kutumia pipes na sio kwa kutumia cylinders.
Ile mitungi Iliyozagaa mitaani sio natural gas kwa maana ya Liquefied Natural Gas (LNG) bali ni LPG, yaani Liquefied Petroleum Gas (LPG).
Ipo mitungi ya Compressed Natural Gas lakini sio rafiki sana kwa sababu yenyewe inakuwa mizito mno!
Pili, kabla ya gesi ya Mtwara niliwahi kuona kwa macho yangu ujenzi wa vinu vya gesi Songosongo na pia bomba la gesi toka Songosongo kuja kijiji kinaitwa Somanga (wilaya ya Kilwa) na bomba likaelekea Dar. Baadae likajengwa bomba kutoka Mtwara (kijiji cha Msimbati) je jumla sasa gas inayosafirishwa na hili bomba kwa sasa ni kiasi gani? Ndo zile 7 TCM ulizosema awali?
The short answer is YES. Hata hivyo, lile bomba la Mtwara ni kubwa MNO kulinganisha na hizo 7 TCF... kwa maana nyingine kwa sasa lipo underutilized.
Ukubwa huo wa bomba la Mtwara haukuja kwa kukosewa bali walifanya hivyo ili taifa lisiingie gharama nyingine ya kujenga bomba lingine tutakapoanza kuchimba zile 50TCF
Tatu, je kwa hii vita inayoendea na tumesikia Ujerumani wamefunga gas supply from Russia, kweli kabisa hatuwezi kuuza hizi 50 TCM zetu zilizopo Mtwara??
TUMECHELEWA...
Ndo maana hapo kabla nilisema JPM na JK ni kama walikuwa na maono tofauti. Lau kama tungeenda kwa speed za JK, hivi sasa ingekuwa ni suala la muda tu kuanza kuuza gesi nje.
Pamoja na yote yanayosemwa kuhusu JK na kuuza gesi kwa Wachina lakini ukweli ni kwamba JK alikuwa na plan mzuri sana.
Plan ya JK kuhusu gas ilikuwa ina-include yafuatayo:-
1. Kusambaza pipeline network Tanzania nzima ili gesi itumike majumbani na viwandani kama mbadala wa mafuta, umeme, na mkaa
2. Kujenga pipeline network kuelekea nchi jirani ili tuuze gesi yetu huki
3. Kupanua Bandari ya Mtwara ili gesi isafirishwe nje ya mipaka ya nchi yetu kwakutumia tankers. Hivyo basi, hilo la kuuza gesi Ulaya lilikuwa ni moja ya plan kuu.
So, kwa mahesabu ya zamani (back in 2015), shughuli hizo zingekamilika anywhere from 2022-2023.
Lakini kwavile hadi sasa bado hatujapiga hatua kwavile Magu inaonekana haikuwa priority yake, hadi kuwa tayari ni labda 2030!!
Kutokana na ukweli huo binafsi nina mashaka sana ikiwa Russia hana mkono wake kwa yale yanayoendelea Msumbiji. Gesi ya Tanzania na Msumbiji ikiwa tayari, dependency ya Russian Gas kwa nchi za UIaya itapungua.
NOTE: Kwavile naona upo more interested na hii topic, basi nitaku-tag kwenye thread ambayo nitaelezea hii mambo kwa undani zaidi, kuanzia utafutaji, uchimbaji, fursa na sheria zilizopo zinazoongoza sekta ya mafuta na gesi.