Mizinga ya nyuki nyuma ya UCC (UDSM) ni hatari kwa watu wanaopita maeneo hayo

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
Wadau nimepita maeneo ya UDSM nikaona mizinga ya nyuki imetundikwa kwenye miti iliyotanda nyuma ya jengo la UCC eneo ambalo lilizoeleka kwa wanafunzi kujipumzisha na kujisomea kwa sababu ya kuwepo kwa utulivu na nyasi nzuri.

Nyuki ni wadudu hatari sana kwa binadamu hasa pale wanapochokozwa. Huwa hatari zaidi wanapokuwa wameivisha asali, kipindi hicho huwa wanatabia ya kujihami sana kwa kumuuma yeyote anayepita karibu yao kwa hofu ya kuibiwa asali yao.

Ni maoni yangu tu na maneno yangu si sheria.
 
Kwa hiyo una wasiwasi kuwa wanafunzi watawachokoza nyuki??..hofu yako ni kuwa kunaweza kutokea ugomvi mkali kati ya nyuki na wanafunzi au sio bro!
 
Mimi kwenye nyumba yangu ya shamba nimetundika mizinga ya nyuki kadhaa, mimewawekea na maji ili wasisumbuke. Maisha yanaenda vizuri tuu huku nikijipatia asali na nta kiulaini tuu. Pia kwa mwafunzi wa chuo Nilitegemea ndo angekuwa na understanding ya kutosha ya jinsi ya kuwa handle nyuki.
 
Mkuu sorry kwani palikua pametangwaza kwamba ni sehemu ya kusomea ama mlijiongeza kutokana na nyasi??? Sehemu tulivu nenda library kiongozi
Library ni mahali pa kuchota maarifa mapya ndio maana pamesheheni vitabu sio mahala pa kukazia maarifa uliyoyachota kwenye mihadhara na kuyahifadhi kwenye madaftari yako. Lakini pia eneo husika lipo karibu sana na watu labda kama huwajui nyuki muziki wake.
 
Kwa hiyo una wasiwasi kuwa wanafunzi watawachokoza nyuki??..hofu yako ni kuwa kunaweza kutokea ugomvi mkali kati ya nyuki na wanafunzi au sio bro!
Nyuki huchokozwa hata pasipo mchokozi kujuwa, mathalan ukipita umejipaka mafuta yenye harufu kali huo pia ni uchokozi kwao na muziki wao si wa kitoto
 
Mimi kwenye nyumba yangu ya shamba nimetundika mizinga ya nyuki kadhaa, mimewawekea na maji ili wasisumbuke. Maisha yanaenda vizuri tuu huku nikijipatia asali na nta kiulaini tuu. Pia kwa mwafunzi wa chuo Nilitegemea ndo angekuwa na understanding ya kutosha ya jinsi ya kuwa handle nyuki.
Sawa Ila siku wakivurugwa ndio utajua nyuki ni hatari kiasi gani
 
Mkuu sorry kwani palikua pametangwaza kwamba ni sehemu ya kusomea ama mlijiongeza kutokana na nyasi??? Sehemu tulivu nenda library kiongozi
Pale pana ukoka mzuri sana na kipindi cha boom, likikata unapiga usingizi mkali sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom