Kuyumba na kufa kwa UCC, Chuo Kikuu UDSM chatoa ufafanuzi

akukudanger

Member
Jan 3, 2011
26
10
UCC.PNG
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) KUJIBU TAARIFA YA PROF. MAKENYA A. H. MABOKO (MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA UCC) ALIYOTOA KWA UMMA HAPO TAREHE 1 OKTOBA 2018

1. UTANGULIZI
Taasisi ya University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC) inamilikiwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa asilimia mia moja.UCC ilianzishwa na UDSM kwa madhumuni ya kutoa mafunzo, huduma za ushauri, na kufanya utafiti kuhusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji haya kwa jamii, UCC ililazimika kutanua huduma hizi kwa jamii na Taifa kwa ujumla kuanzia mwaka 2001 baada ya kusajiliwa na Ofisi ya Usajili wa Makampuni. Uamuzi huu uliwezesha kuipatia UCC fursa ya kubaki na majukumu ya kubuni mafunzo ya ufundi ya muda mfupi na mrefu ambayo yatakidhi maendeleo na ukuaji wa tasnia ya TEHAMA na yanayoendana na ukuaji wa mahitaji ya soko pamoja na kutoa huduma nyingine ambazo zitanufaisha mahitaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla katika nyanja zifuatazo: Huduma ya mtandao, kutengeneza mifumo ya kompyuta (softwares), Ushauri wa kitaalam katika tasnia ya TEHAMA, usanifu na uwekaji wa miundo mbinu ya TEHAMA.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya TEHAMA hapa nchini na duniani kwa ujumla, UCC iliendelea kupanua na kutoa huduma zake kulingana na ongezeko la mahitaji. Tangu kuanzishwa kwake, UCC ina matawi katika mikoa ifuatayo: Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha na matawi mawili kwa sasa yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam (moja likiwa makao Makuu-UDSM na tawi lingine City Centre).

Hapo tarehe 1 Oktoba 2018, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UCC, Profesa Makenya A.H. Maboko alitoa Taarifa kwa Umma kwa alichokiita ukweli kuhusu uendeshaji wa UCC na hali ya kibiashara ya kampuni. Taarifa hiyo kwa ujumla ilizungumzia “Hali ya utendaji wa Kampuni na hatua zilizochukuliwa na Urekebishaji Muundo wa Biashara na kujenga UCC mpya”. Taarifa hiyo Wafanyakazi wa UCC tuliipata kupitia mitandao ya kijamii na Ubao wa Matangazo wa UCC Makao Makuu.

Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi katika taarifa yake kwa Umma imekiri kuwa kumekuwa na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikizungumzia kuhusu UCC. Tunatambua kuwa ndani ya vyombo hivyo vya habari menejimenti ya UCC chini ya Dkt. Ellinami J. Minja ndiyo imekuwa ikilalamikiwa na wafanyakazi kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji.

Tulitarajia Bodi ya Wakurugenzi mara baada ya kupata taarifa hizo kuhusu UCC kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ingekutana na sisi Wafanyakazi ili kutumia nafasi hiyo kutusikiliza mbali na taarifa anazopata kutoka kwa Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Jambo hilo halikufanyika na hivyo taarifa iliyotolewa na Bodi kwa Umma ni mawazo ya Menejimenti ya UCC inayolalamikiwa.

Kwa malengo inayoyajua, Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikutenda haki kwa kuwa imezungumzia mambo machache sana miongoni mwa mambo lukuki ambayo wafanyakazi wanailalamikia Menejimenti chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. EllinamiJj. Minja.

Mambo hayo ambayo Bodi ya Wakurugenzi haikuyatolea maelezo pamoja na kwamba yamekuwa yakiandikwa kwenye vyombo hivyo vya habari, tumeamua kuyaeleza kwa kina ili umma uyafahamu kama ifuatavyo:

2. MALALAMIKO YA WAFANYAKAZI DHIDI YA MENEJIMENTI CHINI YA DKT. ELLINAMI J. MINJA
Tumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja ambayo Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikuyaweka wazi katika taarifa yake kwa umma kama yalivyoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii. Mambo hayo ni pamoja na KWANZA(1) Kusabisha uharibifu wa mali zilizokuwa Tawi la Mbezi Beach, PILI(2) Kubagua wafanyakazi kwa vigezo vya uanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) ,TATU(3) Usimamizi mbovu wakati wa kuhamisha matawi, NNE(4) Ukiukaji wa haki na maslahi ya Wafanyakazi, TANO(5) Notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi, SITA(6) Kutokutenda haki sawa kwa wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza kielimu, SABA(7) Kushindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kwa ufasaha mifumo ya kazi za UCC, NANE (8) Kufuja na kutumia vibaya fedha za Taasisi, TISA (9) Kushindwa kujipanga vizuri kiuendeshaji na kimkakati kwa maslahi ya wateja wetu na kwa ajili ya mafanikio ya UCC na KUMI (10) Dkt. Minja hataathiriwa na kuyumba au kufa kwa UCC.

2.1 KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI ZA UCC ZILIZOKUWA TAWI LA MBEZI BEACH DAR ES SALAAM
Mwezi Agosti 2016, Dkt. Ellinami Minja, Mkurugenzi Mtendaji wa UCC, alifanya maamuzi ya kufunga tawi la Mbezi Beach DSM lililokuwa likitoa mafunzo ya kompyuta ya muda mfupi na mrefu. Wakati maamuzi hayo yanafanyika tawi hilo lilikuwa na wanafunzi wapatao mia tatu. Maamuzi ya kufunga tawi la Mbezi Beach Dar es Salaam yalichukuliwa kiholela bila kuwashirikisha wafanyakazi (ambao ni wadau wakubwa) na ya kukurupuka kiasi cha kusababisha vifaa vya tawi hilo kupelekwa UCC makao makuu-UDSM na kuachwa viharibike kwa jua na mvua kwa sababu havikutunzwa mahali salama.

Dr. Ellinami Minja kama Mkurugenzi Mtendaji (Accounting Officer) wa Taasisi (UCC) alifanya uzembe wa hali ya juu kwa kutokuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha mali mbalimbali (physical assets) zilizotoka Tawi la Mbezi Beach DSM zinatunzwa mahali salama. Kutokana na uzembe huo mali hizo hazikutunzwa vizuri na hivyo ziliharibika na zinazidi kuharibika na kusababisha hasara kubwa kwa Taasisi yetu na ushahidi wa suala hili upo wazi. Mali hizo ni meza, viti, kompyuta, UPS, viyoyozi (ACs), Fire Extinguishers na Rack Cabinets ambavyo vinazidi kuozea nje kwa kunyeshewa na mvua na kupigwa na jua.

Kwa uzembe huo, na hasa kwa kuwa hakuna hatua zozote za uwajibishwaji zilizochukuliwa na Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja, tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina wa jambo hili ili kubaini kiwango cha hasara halisi kilichojitokeza na kiongozi huyu awajibishwe kwa kusababisha hasara hiyo.

Sisi Wafanyakazi tunaona busara ilikuwa ni kutoa msaada wa mali hizo kwenye shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2016 alipoomba taasisi mbali mbali na wananchi kwa ujumla kutoa misaada ya madawati na viti kwa shule hizo kuliko kuziacha zikiharibika na zikiendelea kuharibika.

Kwa kufanya hivyo Dkt. Ellinami Minja kwa namna moja au nyingine angekuwa ameitikia au ameunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na ndoto yake ya kuona wanafunzi kusoma bure zinatimia.

2.2 KUWABAGUA WAFANYAKAZI WALIO WANACHAMA WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI - THTU
Dkt. Minja ametengeneza ufa (utengano) mkubwa kati ya wafanyakazi walio wanachama wa Chama cha wafanyakazi (THTU) na wasio wanachama wa THTU. Wafanyakazi walio wanachama wa THTU kwake wanaonekana wasiofaa bali wanaofaa ni wale ambao sio wanachama. Amefikia hatua ambayo ili upate kuteuliwa katika nafasi ya Uongozi sharti uache uanachama wa THTU kama wewe ni mwanachama wa THTU. Ushahidi wa jambo hili upo kwa kuwa wapo wafanyakazi walioandikiwa barua za kuwataka kuacha uanachama wa THTU kama sharti la kuendelea na nafasi za Uongozi walizo nazo. Kwa lugha nyingine walio wanachama wa THTU kwake siyo wazalendo bali wazalendo ni wafanyakazi wasio wanachama wa THTU.

Hali hii imeleta utengano mkubwa kati ya makundi haya mawili ya wafanyakazi ndani ya UCC. Wafanyakazi tunaamini kuwa tendo hili liko kinyume na sheria, kanuni na taratibu za Ajira. Ifahamike kuwa Dr. Minja ndiye Mkurugenzi Mtendaji pekee ambaye ameleta utengano kwa msingi wa huyu ni mwenzetu (asiye mwanachama wa THTU) na huyu siyo mwenzetu (aliye mwanachama wa THTU) tangu UCC ilipoanzishwa.

Tunaamini pia kwamba dhamira ya Menejimenti ya kupunguza wafanyakazi ni janja tu inayolenga kuwapa uwezo wa kuwaondoa wanachama wa THTU UCC na kwa minajili ya kuondoa kikwazo cha matendo yao na pia kusimika hofu ya wale wanaobaki dhidi ya kujiunga na chama hicho (THTU).

2.3 MAAMUZI MABOVU WAKATI NA BAADA YA KUHAMISHA MATAWI KUTOKA MAJENGO YA WATU BINAFSI KWENDA KUPANGA MAJENGO YANAYOMILIKIWA NA UMMA
Katika kutekeleza agizo la Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2016 la kuitaka UCC kuhama kutoka kupanga kwenye majengo ya watu binafsi na kwenda kupanga kwenye majengo ya umma, wafanyakazi tunaamini kuwa utawala wa Dr. Minja ulitekeleza agizo hilo kwa kukurupuka na hivyo kusababisha mkanganyiko kiundeshaji na kibiashara ambao umesababisha na utasababisha hasara kubwa iwapo kusudio lake la kufunga matawi ya Mwanza, Mbeya na Arusha litatekelezwa. Sisi wafanyakazi tunahoji yafuatayo juu ya kusudio la kufungwa kwa matawi tajwa hapo juu:

a) Moja ya faida kubwa ya kuhama kutoka kupanga majengo ya watu binafsi na kupanga kwenye majengo ya umma ni kupungua kwa kodi ya pango (rental fee) iliyokuwa ikilipwa na UCC. Kodi kubwa ya pango ilikuwa ni sababu ya matawi kupata faida ndogo. Hivyo, ilikuwa ni matarajio yetu wafanyakazi kuwa baada ya matawi ya Arusha, Mbeya na Mwanza kuhamia kwenye majengo ya umma, BASI, utawala wa Dr. Minja ungetoa muda wa kutosha kwa matawi haya kuendelea kutoa huduma kwa umma ili kutumia fursa hiyo ya kushuka kwa kodi ya pango. Badala yake Menejimenti imehamisha matawi husika na kufanya maamuzi ya kuyafunga bila ya kutoa muda wa matawi hayo kufanya biashara chini ya uangalizi maalum (grace period) ili kubaini kama yataweza kutengeneza faida au la. Kwa mfano, Tawi la Mbeya lilihamia kwenye jengo la UDSM hivyo kiwango cha malipo ya pango ni nafuu sana ukilinganisha na hapo awali hivyo wangepewa muda wa angalizo kama watatengeneza faida au la.​

Hivyo basi kitendo cha kutokutoa muda wa angalizo kwa matawi haya kufanya biashara baada ya kupata unafuu wa kodi ya pango ni nia ovu na hakikubaliki na kinashangaza kwa mtu mwenye weledi wa kiuongozi.​

b) Kulikuwa na ulazima upi wa kuhama Tawi la Arusha kutoka jengo la Summit Centre (private building) na kwenda jengo la NSSF Plaza (public building) mwishoni mwaka 2017 iwapo tawi hilo linafungwa Oktoba 2018? Ikumbukwe kuwa kuhama kwa tawi la Arusha kumesababisha UCC kuingia gharama za kuhamisha vifaa/mali (relocation costs) na gharama za kutengeneza ofisi na madarasa (office & training rooms partitioning costs). Gharama zote hizi ni hasara ambayo UCC imepata kama tawi litafungwa Oktoba 2018. Ilikuwa ni busara tawi libaki lilikokuwa likisubiri kufungwa!​

c) Kwa hiyo maamuzi hayo chini ya Menejimenti ya Dr. Ellinami Minja siyo sahihi. Kuhama kutoka majengo binafsi na kwenda majengo ya umma na akiwa anajua fika kwamba atayafunga hayo matawi katika muda mfupi ujao ni matumizi mabaya ya fedha za Taasisi. Izingatiwe kuwa mchakato huo wa kuhama umegharimu pesa nyingi na kwa mantiki hiyo matumizi mabaya ya fedha za taasisi. Hatimaye gharama hizi za kuhama huingizwa kwenye matumizi ya matawi husika na mwisho wa siku inaonekana matawi husika yameleta HASARA (LOSS), kumbe chanzo ni maamuzi yasiyo sahihi ya utawala wa Dr. Minja.​

d) Wafanyakazi tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusiana na maamuzi haya yasiyo sahihi yaliyofanywa na Menejimenti hii juu ya kuhamisha matawi na hatimaye kuchukua maamuzi ya kuyafunga bila ya kuyapa muda wa angalizo wa kutoa huduma.​

2.4 UNYANYASAJI NA UKIUKAJI WA HAKI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi tunanyanyaswa sana na Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Yafuatayo ni mambo ambayo yamekuwa sugu na ambayo malalamiko yake hayajawahi kutatuliwa na Menejimenti chini ya Dr. Minja.

a) Mikataba ya wafanyakazi inayotolewa na Utawala wa Dr. Minja ni ya kiunyanyasaji ambayo haifuati sheria za kazi
  • Mikataba inayotolewa ni ya muda maalum hata kwa kazi ambazo ni endelevu kwa miaka yote ambayo shirika/taasisi imekuwepo.
  • Wakati wa ku-renew mkataba, muda na vigezo vya mkataba wa mfanyakazi unaweza kubadilishwa (kwa kupunguzwa) kiholela. Imetokea wafanyakazi wenye mikataba ya miaka 3 imebadilishwa muda na kupewa mikataba ya miezi 6 au 9 bila mawasiliano ya awali. Au mfanyakazi mwenye mkataba wa miaka mitano ukabadilishwa na kushushwa kiholela ukawa wa miaka mitatu. Hawa ni wafanyakazi ambao wamekuwa wakiitumikia UCC kwa zaidi ya miaka kumi!
  • Utaratibu wa kupewa mkataba mwingine (ku-renew) umewekewa vikwazo vingi – ikiwamo:

i. Recruitment committee (ambayo inahusisha watu wengine ambao hawafanyi kazi na mfanyakazi husika). Hii ni kinyume na miongozo ya sheria za kazi.​
ii. Kutakiwa kujaza upya KPI (Key Performance Indicators) pale unapoandika barua ya kuomba ku-renew mkataba. Hii haijalishi kwamba KPI hujazwa kwa mwaka na kwa hiyo imewekwa mahsusi kutoa mwanya kwa kiongozi wako kuku-grade vibaya pale anapoona inafaa au anapokuwa amepokea maagizo ya kufanya hivyo. Hii ni kinyume na sheria za kazi,​
iii. Kuwekwa vigezo vya muda maalum wa kuzingatia unapotaka ku-renew mkataba lakini mwajiri hajali kukujibu ndani ya muda huo alioweka.​

b) Kutokufuatwa kwa Scheme of Service (SoS) ya UCC na kutokuwa na mlinganyo mzuri wa mishahara
UCC inayo Scheme of service iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 na utawala wa Dkt. Minja bila ya kushirikisha chama cha Wafanyakazi. Mwaka 2017 ikafanyiwa tena marekebisho na Menejimenti ya Dr. Minja bila ya kuwahusisha wafanyakazi na kupeleka mapendekezo ya marekebisho moja kwa moja kwenye Bodi ya UCC. Hata hivyo, wafanyakazi tuna malalamiko kama ifuatavyo kuhusiana na jambo hili:

i. Baadhi ya wafanyakazi kuongezewa mishahara kwa upendeleo bila kuzingatia mwongozo wa Scheme of Service kwa kuwa ni wateule wake

ii. Wafanyakazi walio wengi mishahara yao haijaongezeka kwa zaidi ya miaka sita

iii. Baadhi ya wafanyakazi kuandikiwa barua kuwa mishahara waliyonayo sasa inastahili kupunguzwa

iv. Vigezo vya kupandisha madaraja ya wafanyakazi havifuatwi au havifanyiwi kazi.

v. Wafanyakazi wanalazimishwa kujiendeleza kwa kujigharamia wenyewe. Hawapandishwi madaraja kama inavyoainishwa kwenye scheme of service.

vi. Mfanyakazi anajaza KPI kila mwaka na mara zote hizo anapata alama za juu. Lakini hata mfanyakazi anapofanya vema mfululizo hapandishwi daraja wala kuwa motivated.

c) Wafanyakazi wanaofanya kazi yao kwa weledi na maadili ya kazi zao kuondolewa kwenye nafasi zao kwa vigezo visivyoridhisha

Haijalishi iwapo unafanya kazi yako kwa weledi na kwa kufuata maadili ya kazi hiyo, unatarajiwa pia kukiuka yote hayo pale unapopokea maagizo ya kufanya hivyo kutoka kwa Dr. Minja kama mkuu wa taasisi. Hayo yamewakuta baadhi ya wafanyakazi wenzetu ikiwamo Afisa Manunuzi. Wengine wametolewa kwenye nafasi zao kwa sababu wao ni wanachama wa THTU na kwa hiyo ni wapelelezi; wanachukua habari za ndani ya vikao na kuzipeleka THTU. Kwenye Taasisi yetu THTU imekuwa ni adui mkubwa wa Menejimenti ya Dkt. Minja

2.5 KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI BILA KUWASHIRIKISHA WAFANYAKAZI NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI NA YANAYOENDELEA KUFANYIKA BAADA YA NOTISI YA KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ulitoa notisi ya kukusudia kupunguza wafanyakazi kwa msingi kuwa UCC imekuwa ikipata hasara. Hii ni uthibitisho kuwa weledi wake wa kuongoza UCC umefika mwisho kwa kuwa ameshindwa kuwa na maono ya namna ya kuifanya taasisi kujiendesha kibiashara. Hata hivyo sisi wafanyakazi tunahoji kwa kuwa tuna ushahidi wa yafuatayo:

a) Kama ana nia njema na zoezi hili kwa nini hakushirikisha wafanyakazi na chama cha wafanyakazi (THTU) kama sheria inavyoagiza juu ya jambo hili kabla ya kufikia hatua ya kutoa notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi?
b) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya kwenye nafasi zisizokuwa za uzalishaji na kuwalipa mishahara mikubwa baada ya kutoa notisi ya kupunguza wafanyakazi. Mfano kuna umuhimu gani wa kuajiri hivi karibuni Finance & Administration Manager (FAM) na Human Resources Officer mwingine na kuwapa mishahara minono kama UCC haifanyi vizuri na inadhamiria kupunguza wafanyakazi wake?! Watu hawa wanakuja kumsimamia nani?!
c) Kuajiri baada ya notisi baadhi ya wafanyakazi ambao Job Titles zao hazipo kwenye Scheme of Service. Mfano Finance & Administration Manager (FAM)
d) Kuwaongezea mishahara kwa upendeleo baadhi ya wafanyakazi tena baada ya notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi
e) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya wenye mishahara minono kwenye idara ya Software Engineering kabla na baada ya Notisi ya kupunguza wafanyakazi. Ni ajabu kuona mishahara minono inalipwa kwa waajiriwa hawa wapya wakati Menejimenti na Bodi wamekiri kwenye taarifa kwa umma kuwa UCC inapata hasara. Kama inapata hasara fedha hizi wanazolipwa zinatoka wapi!

2.6 UTAWALA USIOTENDA HAKI KWA WAFANYAKAZI WANAOTAKA KUJIENDELEZA KIELIMU
Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ni utawala usiotenda haki. Kwa mfano wapo wafanyakazi ambao walitaka kujiendeleza kimasomo wakaomba ruhusa ya kusoma bila malipo (leave without pay) au ruhusa ya kusoma yenye malipo (leave with pay) wakanyimwa ruhusa na kuambiwa waache kazi kama wanataka kujiendeleza kimasomo. Wakati huo huo wapo wafanyakazi walioruhusiwa kujiendeleza kimasomo na kuendelea kupata asilimia 80% ya mishahara yao chini ya utawala wake. Kiongozi mwenye double standards hatufai sisi wafanyakazi wa UCC.

Ifahamike ya kuwa ni utawala wa Dr. Ellinami Minja tu ambao umewanyima wafanyakazi wenye scholarship kwenda kusoma na kuendelea kupata mishahara yao hata kwa asilimia fulani. Awamu zote zilizopita ziliheshimu umuhimu wa mfanyakazi kujiendeleza kielimu hasa pale anapokuwa amepata ufadhili (scholarship). Ndiyo maana ndani ya UCC iliwezekana kupata wafanyakazi wenye shahada za uzamivu watano (5) waliotokana na tawala zilizopita kuwaruhusu kwenda kusoma na wakati huo huo wakiwa wanalipwa asilimia 80% ya mishahara yao. Ushahidi wa jambo hili upo.

2.7 KUSHINDWA KUMILIKI, KUDHIBITI NA KUENDESHA KIUFASAHA MIFUMO YA KAZI ZA UCC
Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami Minja imeshindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kiufasaha mifumo ya kazi za UCC. Tatizo hili ni dhahiri zaidi katika huduma za mafunzo ambazo pia ndio zinazoajiri zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wote wa UCC. Hii ni kama ifuatavyo:

a) Ukosefu wa vifaa muhimu na mazingira mabovu ya kufundishia
Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutafuta namna ya kupata vitendea kazi vya kutosha kwa ajili ya huduma za mafunzo. Kwa mfano:
  • Kukosekana kwa kompyuta madarasani limekuwa ni jambo la kawaida sana ndani ya huduma hii. Kwenye vipeperushi vyetu vyote tumeahidi kwamba kila mwanafunzi anatumia kompyuta yake mwenyewe lakini sio mara moja au mbili wanafunzi wanalazimika ku-share kompyuta.
  • Projectors ni vifaa ya muhimu sana katika huduma ya mafunzo lakini kwa sasa chini ya Dkt. Minja vifaa hivi ni vya kugombania na kunyang’anyana! Wanafunzi mara zote wanakuwa wahanga wa mvutano huo pale mwalimu wao wanaposhindwa kupata Projector.
  • Tumeahidi kwa wateja kuwa tuna Stand-by Generator na kwamba umeme unapokatika mwanafunzi hapotezi muda wake, LAKINI hili nalo sasa ni kitendawili chini ya utawala wa Dr. Minja. Ni kawaida kwa sasa wanafunzi kukaa bila kusoma pale umeme unapokatika kwa sababu umeme unapokatika Generator hazifanyi kazi. Hali hii ipo hata Training HQ ambapo angalau tungetarajia kuwa Generator itumike mara moja baada ya umeme kukatika.
  • Mazingira ya ufundishiaji yenyewe yanakosa vifaa muhimu kwa ajili ya kuweka vizuri huduma hii. Kwa mfano katika Jiji la Dar es Salaam ambalo hali yake ya hewa ni ya joto kali unakuta madarasa hayana madirisha yanayotosheleza idadi ya wanafunzi wanaoingia humo na AC hazifanyi kazi. Mwalimu anafundisha yeye mwenyewe anabubujikwa jasho. Wanafunzi wanajipepea kwa kutumia vitabu vya kufundishia wanavyotakiwa kuwa wanavisoma kufuata maelekezo ya somo husika.
  • Huu ni unyanyasaji mkubwa wa wateja pamoja na walimu husika na ni kushindwa kutambua athari za mwenendo huu katika mustakabali wa huduma zetu! Kwa mfano Tawi la City Centre lina AC ofisini kwa Meneja tu.!
Izingatiwe kuwa ukosefu wa vifaa muhimu vya kufundishia limekuwa tatizo sugu wakati wote wa Awamu ya uongozi wa Dkt Minja. Kipindi cha tawala zilizopita Menejimenti husika zilikuwa zikifanya jitihada za makusudi na kushirikiana na Wafanyakazi katika kutatua changamoto hizo kwa kuwa walikuwa na maono na nia nzuri katika kuboresha huduma za mafunzo. Hivyo, siyo ajabu sasa kukimbiwa na wateja na kwenda kuzitafuta kwenye taasisi zenye vifaa vya kisasa na mazingira bora ya kusomea.

b) Kushindwa kutangaza huduma za mafunzo za UCC
Uongozi wa Dkt. Minja umeshindwa kabisa kuwa na mwongozo thabiti wa kujitangaza kwenye soko. Suala hili limekuwa la kisiasa sana na limekuwa linachezewa sana. Bajeti ya kujitangaza haieleweki! Katika ulimwengu huu wa matangazo ambao tunawaona hata vyuo vidogo kama Zoom Polytechnic vinajitangaza sana ni nadra kuona tangazo la UCC. Mara zote kisingizio ni hakuna hela. Njia kuu ya kujitangaza kwa UCC imekuwa ni kufundisha vizuri ili wateja warudi tena na pia wawalete na ndugu zao.

c) Hakuna jitihada za Menejimenti ku-connect na Wafanyakazi
Dkt.Minja ameweka stop kwa mfanyakazi yeyote kwenda ofisini kwake bila kwanza kupitia kwa viongozi wa kati aliowateua. Wafanyakazi wanapokuwa na dukuduku “sugu” la ki-taasisi au la binafsi wanalazimika kusubiri mpaka wakati wa Mkutano Mkuu wa taasisi ambao unatakiwa ufanyike kila nusu ya mwaka lakini nao unafanyika mara chache mno na unakuwa na mambo mengi huku Menejimenti ikiuharakisha kwa kigezo cha muda hautoshi. Pale shida inapokuwa ya binafsi ya siri basi mfanyakazi anajitahidi kumeza machungu yake. Sio wafanyakazi wengi wenye uwezo hata tu wa kuongea shida zao hadharani. Zuio hili la kumuona Dkt. Minja na kuongea naye limeleta fadhaa kubwa sana ndani ya taasisi. Tunafikiri kiongozi wa Taasisi anapaswa kuwa wazi kwa wafanyakazi kuweza kumuona hata kama ni kwa kutenga siku na muda maalum.

d) Kuvuruga na Kufunga Matawi ya UCC ambayo ndiyo kimbilio la huduma za Mafunzo ya TEHAMA
Uvurugaji na kufunga matawi umefanywa na Menejimenti ya Dkt. Minja katika mambo makubwa yafuatayo:
i. Uamuzi wa kufunga matawi ya mikoani umefanywa na menejimenti kibabe, bila upembuzi yakinifu na bila kushirikisha Wafanyakazi.
ii. Kunyanyapaa huduma za mafunzo za UCC na kufanya njama za kuziua/kuzifunga
iii. Kuhamisha Tawi la City Centre kwenda eneo finyu kuliko lilipokuwa mwanzo
iv. Kupuuzia au kudharau kurejea maamuzi au maono ya watangulizi wake wa tawala zilizopita na sababu zake.

2.8 UBADHIRIFU NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA TAASISI
(a) Menejimenti ya Dkt. Minja imekuwa na usiri mkubwa kwenye maamuzi ya fedha za Taasisi.
Wafanyakazi hawaambiwi undani wa matumizi hayo isipokuwa tu kupewa bajeti ya matumizi yanayoitwa “Overhead” katika Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi. Overhead hii inajumuisha matumizi ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na ofisi za Fedha na Meneja Rasilimali Watu (HR).
Matumizi ya Overhead huwa yanagawanywa kwa vitengo vyote vinavyozalisha kwa uwiano wa uwezo wao. Tatizo ni kuwa matumizi haya huwa ni makubwa mno kuzidi hata matumizi ya hayo matawi yenyewe ambayo idadi ya wafanyakazi wao ni kubwa mara dufu kuliko hao wa ofisi hizo. Kiasi kwamba hata pale ambapo tawi husika lilipata faida kwa uwiano wa mapato na matumizi basi hudaiwa limepata hasara pale gawio hilo la Overhead linapojumlishwa.
Wafanyakazi wanapohoji kuhusu kupewa mnyumbulisho wa matumizi husika hawapewi isipokuwa kuahidiwa kupewa katika kikao kijacho. Kwa usiri huo wa Overhead hakuwi na uwezekano wa kuhoji kuhusu matumizi hayo na hata kuchangia kuhusu kupunguza matumizi hayo. Na hakuna namna ambayo mfanyakazi anaweza kusema kuna jitihada za makusudi za kupunguza matumizi hayo ya Overhead.

(b) Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutunza na kudhibiti vizuri mali zinazotokana na jasho la wafanyakazi wake.
Katika maamuzi yake ya utata ya kufunga matawi kiholela wamediriki kuacha samani na vifaa vya mamilioni ya shilingi vikiharibika kwa mvua na jua bila kujali kwamba zimetokana na jasho la wafanyakazi hao hao ambao sasa wanataka kuwapunguza. Vifaa vilivyotoka Mbezi Beach viliachwa kuharibika bila uwajibikaji. Hakuna hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika maana yake ni kuwa ulikuwa ni uamuzi wa Menejimenti yenyewe.
(c) Menejimenti ya Dkt. Minja inadiriki kuwaambia wafanyakazi kwamba eti hasara tunayopata imetokana na wateja kutolipia huduma.
Hivi ni nani anayeajiri wakusanyaji wa madeni na malipo ya huduma nyingine zilizotolewa na UCC na kudhibiti mapato hayo? Ni mwalimu au Programmer au Dereva?! Hivi ni nani anayepaswa kuwawajibisha maofisa hao kama wanashindwa kufanya kazi zao? Ni mwalimu, Programmer, Dereva au Human Resource Officer au mafanyakazi mwingine?!

Menejimenti chini ya Dr. Minja wanadiriki kudai kwamba mamilioni ya shilingi hayajalipwa kwa UCC na hakuna anayewajibishwa kwa hili! Dkt. Minja anadiriki hata kusema kwamba huduma ya mafunzo ingeleta faida kama wateja wote wangelipa vizuri. Mbona taasisi nyingine wateja wanalipa, UCC kulikoni? Je UDSM nako wanafunzi hawalipi? Inakuwaje?
(d) Kuwa na Chief Accountants wawili ambao taasisi inagharimia mishahara yao. Kwa sasa UCC kuna Machief Accountants wawili kwa sasa. Kuna umuhimu gani wa kuendelea kuwa na Chief Accountants wawili? Sisi Wafanyakazi tulitazamia baada ya mchakato wa kupata Chief Accountant mpya mwezi Novemba 2017 yule aliyekuwepo mwanzo (ambaye katika mojawapo wa vikao vya UCC alitambulishwa kama Ag. Chief Accountant) angerudi UDSM immediately alikokuwa awali lakini bado yupo mpaka sasa na anaendelea kulipwa mshahara na UCC. Kama UCC inapata hasara kama ilivyotamkwa kwenye taarifa ya Bodi kwa Umma, pesa za kulipa Machief Accountants wawili tangu Novemba 2017 mpaka sasa zinatoka wapi? Huu ni ubadhirifu wa dhahiri unaofanywa na Dkt. Minja.

2.9 KUSHINDWA KUJIPANGA VIZURI KIUENDESHAJI NA KIMKAKATI KWA MASLAHI YA WATEJA WETU NA UCC KWA UJUMLA
Kwa ujumla Menejimenti chini ya Dkt. Minja imeshindwa kuendesha taasisi kimkakati ili kuleta tija kwa wateja wote wakahudumiwa vizuri na wakaridhika na UCC ikapata mapato yake. UCC ni taasisi ambayo imejikita katika mioyo ya Watanzania kama kimbilio lao kwa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) na huduma nyingine. Kushindwa kujipanga kwa Menejimenti ya Dkt. Minja na utendaji wao wa kutokushirikisha Wafanyakazi kumetusababishia hasara hiyo Menejimenti na Bodi inayoitangaza kwa umma. Hii ni kwa kuzingatia Menejimenti husika imegubikwa na utendaji mbovu, maamuzi mabovu yanayoiletea Taasisi hasara, na kushindwa kujipanga vizuri.
Taasisi ya UCC inahitaji Menejimenti thabiti inayoamini katika kuboresha ufanisi wa huduma zilizopo za UCC na kubuni huduma mpya kwa kuwaunganisha Wafanyakazi na kuwaelekeza katika kuongeza bidii, utaalamu na weledi huku ikijitahidi kuchukua hatua za dhati katika kutatua changamoto zinazokabili huduma tulizozitaja na nyinginezo zinazojitokeza. Tunahitaji Menejimenti yenye uchungu na wafanyakazi katika shida zao ha hivyo kuweza kupata ushirikiano wa kina (sympathy and cooperation) wa Wafanyakazi hao. Tunahitaji Menejimenti inayoinua ari na dhamira ya Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na hapo wateja watatuona tena na kurudi UCC kwenye viwango vyake.

2.10 DKT. MINJA HAATHIRIWI NA KUYUMBA AU KUFA KWA UCC
Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Minja amekuwa akiweka bayana katika mikutano mbalimbali ya wafanyakazi kwamba yeye ni mwajiriwa wa UDSM na hivyo hata UCC ikifa ajira yake iko salama. Japo maneno hayo yanaweza kuwa yanalenga kuwapa nguvu wafanyakazi kuchukua mustakabali wa Taasisi mikononi mwao, maneno haya pia yanaweka bayana kwamba maamuzi yoyote yale anayoyachukua hayamuathiri yeye mwenyewe moja kwa moja. Maamuzi yake yanaidhoofisha, kuiyumbisha na kuhatarisha mustakabali wa UCC na hayamweki yeye katika hali ya hatari. Ni sisi tu wafanyakazi ambao hatima zetu na za familia zetu ziko UCC ndio tunaohatarishwa. Yeye atakosa “posho” tu ya Ukurugenzi wa UCC. Hata kama posho hiyo ni kubwa kuliko mshahara wa mfanyakazi yeyote yule wa UCC lakini ni posho tu!

3. HITIMISHO
Tunaomba umma utambue kwamba Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami J. Minja imeshindwa kazi yake. Jitihada zake za kufunga baadhi ya huduma na hasa huduma ya mafunzo ni njia ya Menejimenti yake kujipa muda zaidi kabla kansa ya kushindwa kwake haijaenea na kuiteketeza kabisa UCC.Ifahamike kwamba huduma ya Mafunzo itolewayo na UCC ndiyo inayowahudumia watanzania wengi zaidi. Hii ni huduma inayofaa kuboreshwa na kutolewa kwa ufanisi zaidi. Huduma hii pia inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wa UCC. Haiwezi kuachwa ikauwawa hivi hivi tu! Menejimenti ya Dkt. Minja imeliteka nyara Taasisi na kuamua ya kwao yanayolenga kuathiri vibaya maslahi ya umma wa watanzania na Wafanyakazi wa UCC.

Menejimenti ya Dkt. Minja hujiamulia wanayotaka kwa gharama ya kuvuruga huduma za mafunzo kwa watanzania na kufuja haki na maslahi ya Wafanyakazi walio wengi. Wanaamua kufumbia macho familia zote za wafanyakazi hawa wanaofanya kazi kwa bidii kubwa huku wao wakijikita kwenye kufuja fedha za Shirika.
Tunaomba Mamlaka zinazohusika zitambue kuwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Ellinami J. Minja amekuwa UCC kwa kipindi cha miaka mitatu tu kati ya miaka takriban ishirini ya uhai wa UCC. Katika kipindi hiki tu cha miaka mitatu yake ya uongozi uharibifu wote na matatizo yote yaliyotajwa hapo juu ameyafanya yeye na Menejimenti yake. Je, Dkt. Ellinami Minja akiendelea kuongoza Menejimenti ya UCC nini hatima ya UCC?
IMETOLEWA NA
WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC)
TAREHE 12 OKTOBA 2018
 
Attachments

  • DOC-20181102-WA0008.pdf
    266.1 KB · Views: 73
imeandaliwa na Wafanyakazi wa Kitengo cha Kompyuta pale Chuo Kikuu (UCC)
 
Attachments

  • DOC-20181102-WA0008.pdf
    266.1 KB · Views: 17
Chuo kikuu kikongwe kinashindwa kuendesha shirika lao. Nahisi ni mabaki ya uongozi mbovu wa VC aliyepita. UDSM ya watu waliojiamini ilitoweka siku nyingi!! Wanafunzi wakapigwa mkwara hadi kuwa kama sekondari. Kukosana imekuwa ni mtindo wa staff wa UD. Kuna centre moja pale pia nilisikia inakufa kwa sababu hizo hizo! Ni ile iliyojiita ya climate, huku ikiwa imejaa wapiga dili.
 
Sasa kama wanashindwa kuendesha ishu ndogo kama UCC wanawezaje kuendesha mambo mazito ya kitaifa??
Vyuo vikuu vinatakiwa viwe icon ya kitaifa kwa kuwa ina hazina kubwa sana ya rasilimali watu.

Lilikuwa ni suala la muda tu, staff wengi sana wa UDSM hasa Computer Science wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye ishu zao binafsi na hii UCC waliifanya kama chaka lao la kupiga extra income.

Hivi bado Zalongwa ipo??
 
Imetolewa na Wafanyakazi wa kitengo cha Kompyuta Chuo Kikuu DSM
Dr Minja anafahamu sana Finance hasa ya structure Finance,

Mambo options contracts,Derivatives yupo vizuri sana

Tatizo hapa Bongo matumizi ya hivi vitu bado sana sana havitumiki kivile

Acha tuendelee kushindwa kuuza mahindi internationally

Matumizi ya hizi Derivative wakulima wasingelialia
 
Kwahiyo mkuu nikasome wapi sasa na nilitaka niapply hapo mwakani?
 
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) KUJIBU TAARIFA YA PROF. MAKENYA A. H. MABOKO (MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA UCC) ALIYOTOA KWA UMMA HAPO TAREHE 1
OKTOBA 2018

1. UTANGULIZI
Taasisi ya University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC) inamilikiwa na Chuo kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) kwa asilimia mia moja.UCC ilianzishwa na UDSM kwa madhumuni ya kutoa mafunzo, huduma za ushauri, na kufanya utafiti kuhusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji haya kwa jamii, UCC ililazimika kutanua huduma hizi kwa jamii na Taifa kwa ujumla kuanzia mwaka 2001 baada ya kusajiliwa na Ofisi ya Usajili wa Makampuni. Uamuzi huu uliwezesha kuipatia UCC fursa ya kubaki na majukumu ya kubuni mafunzo ya ufundi ya muda mfupi na mrefu ambayo yatakidhi maendeleo na ukuaji wa tasnia ya TEHAMA na yanayoendana na ukuaji wa mahitaji ya soko pamoja na kutoa huduma nyingine ambazo zitanufaisha mahitaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla katika nyanja zifuatazo: Huduma ya mtandao, kutengeneza mifumo ya kompyuta (softwares), Ushauri wa kitaalam katika tasnia ya TEHAMA, usanifu na uwekaji wa miundo mbinu ya TEHAMA.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya TEHAMA hapa nchini na duniani kwa ujumla, UCC iliendelea kupanua na kutoa huduma zake kulingana na ongezeko la mahitaji. Tangu kuanzishwa kwake, UCC ina matawi katika mikoa ifuatayo: Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha na matawi mawili kwa sasa yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam (moja likiwa makao Makuu-UDSM na tawi lingine City Centre).

Hapo tarehe 1 Oktoba 2018, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UCC, Profesa Makenya A.H. Maboko alitoa Taarifa kwa Umma kwa alichokiita ukweli kuhusu uendeshaji wa UCC na hali ya kibiashara ya kampuni. Taarifa hiyo kwa ujumla ilizungumzia “Hali ya utendaji wa Kampuni na hatua zilizochukuliwa na Urekebishaji Muundo wa Biashara na kujenga UCC mpya”. Taarifa hiyo Wafanyakazi wa UCC tuliipata kupitia mitandao ya kijamii na Ubao wa Matangazo wa UCC Makao Makuu.

Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi katika taarifa yake kwa Umma imekiri kuwa kumekuwa na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikizungumzia kuhusu UCC. Tunatambua kuwa ndani ya vyombo hivyo vya habari menejimenti ya UCC chini ya Dkt. Ellinami J. Minja ndiyo imekuwa ikilalamikiwa na wafanyakazi kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji.

Tulitarajia Bodi ya Wakurugenzi mara baada ya kupata taarifa hizo kuhusu UCC kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ingekutana na sisi Wafanyakazi ili kutumia nafasi hiyo kutusikiliza mbali na taarifa anazopata kutoka kwa Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Jambo hilo halikufanyika na hivyo taarifa iliyotolewa na Bodi kwa Umma ni mawazo ya Menejimenti ya UCC inayolalamikiwa.

Kwa malengo inayoyajua, Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikutenda haki kwa kuwa imezungumzia mambo machache sana miongoni mwa mambo lukuki ambayo wafanyakazi wanailalamikia Menejimenti chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. EllinamiJj. Minja.

Mambo hayo ambayo Bodi ya Wakurugenzi haikuyatolea maelezo pamoja na kwamba yamekuwa yakiandikwa kwenye vyombo hivyo vya habari, tumeamua kuyaeleza kwa kina ili umma uyafahamu kama ifuatavyo:

2. MALALAMIKO YA WAFANYAKAZI DHIDI YA MENEJIMENTI CHINI YA DKT. ELLINAMI J.
MINJA

Tumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja ambayo Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikuyaweka wazi katika taarifa yake kwa umma kama yalivyoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii. Mambo hayo ni pamoja na KWANZA(1)
Kusabisha uharibifu wa mali zilizokuwa Tawi la Mbezi Beach, PILI(2) Kubagua wafanyakazi kwa vigezo

vya uanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) ,TATU(3) Usimamizi mbovu wakati wa kuhamisha matawi, NNE(4) Ukiukaji wa haki na maslahi ya Wafanyakazi, TANO(5) Notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi, SITA(6) Kutokutenda haki sawa kwa wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza kielimu, SABA(7) Kushindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kwa ufasaha mifumo ya kazi za UCC, NANE (8) Kufuja na kutumia vibaya fedha za Taasisi, TISA (9) Kushindwa kujipanga vizuri kiuendeshaji na kimkakati kwa maslahi ya wateja wetu na kwa ajili ya mafanikio ya UCC na KUMI (10) Dkt. Minja hataathiriwa na kuyumba au kufa kwa UCC.

2.1 KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI ZA UCC ZILIZOKUWA TAWI LA MBEZI BEACH DAR ES SALAAM
Mwezi Agosti 2016, Dkt. Ellinami Minja, Mkurugenzi Mtendaji wa UCC, alifanya maamuzi ya kufunga tawi la Mbezi Beach DSM lililokuwa likitoa mafunzo ya kompyuta ya muda mfupi na mrefu. Wakati
maamuzi hayo yanafanyika tawi hilo lilikuwa na wanafunzi wapatao mia tatu. Maamuzi ya kufunga taw i la Mbezi Beach Dar es Salaam yalichukuliwa kiholela bila kuwashirikisha wafanyakazi (ambao ni wadau
wakubwa) na ya kukurupuka kiasi cha kusababisha vifaa vya tawi hilo kupelekwa UCC makao makuu-
UDSM na kuachwa viharibike kwa jua na mvua kwa sababu havikutunzwa mahali salama.

Dr. Ellinami Minja kama Mkurugenzi Mtendaji (Accounting Officer) wa Taasisi (UCC) alifanya uzembe wa hali ya juu kwa kutokuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha mali mbalimbali (physical assets) zilizotoka Tawi la Mbezi Beach DSM zinatunzwa mahali salama. Kutokana na uzembe huo mali hizo hazikutunzwa vizuri na hivyo ziliharibika na zinazidi kuharibika na kusababisha hasara kubwa kwa Taasisi yetu na ushahidi wa suala hili upo wazi. Mali hizo ni meza, viti, kompyuta, UPS, viyoyozi (ACs), Fire Extinguishers na Rack Cabinets ambavyo vinazidi kuozea nje kwa kunyeshewa na mvua na kupigwa na jua.

Kwa uzembe huo, na hasa kwa kuwa hakuna hatua zozote za uwajibishwaji zilizochukuliwa na Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja, tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina wa jambo hili ili kubaini kiwango cha hasara halisi kilichojitokeza na kiongozi huyu awajibishwe kwa kusababisha hasara hiyo.

Sisi Wafanyakazi tunaona busara ilikuwa ni kutoa msaada wa mali hizo kwenye shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2016 alipoomba taasisi mbali mbali na wananchi kwa ujumla kutoa misaada ya madawati na viti kwa shule hizo kuliko kuziacha zikiharibika na zikiendelea kuharibika.

Kwa kufanya hivyo Dkt. Ellinami Minja kwa namna moja au nyingine angekuwa ameitikia au ameunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na ndoto yake ya kuona wanafunzi kusoma bure zinatimia.

2.2 KUWABAGUA WAFANYAKAZI WALIO WANACHAMA WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI - THTU
Dkt. Minja ametengeneza ufa (utengano) mkubwa kati ya wafanyakazi walio wanachama wa Chama cha wafanyakazi (THTU) na wasio wanachama wa THTU. Wafanyakazi walio wanachama wa THTU
kwake wanaonekana wasiofaa bali wanaofaa ni wale ambao sio wanachama. Amefikia hatua ambayo ili upate kuteuliwa katika nafasi ya Uongozi sharti uache uanachama wa THTU kama wewe ni
mwanachama wa THTU. Ushahidi wa jambo hili upo kwa kuwa wapo wafanyakazi walioandikiwa barua za kuwataka kuacha uanachama wa THTU kama sharti la kuendelea na nafasi za Uongozi walizo nazo.
Kwa lugha nyingine walio wanachama wa THTU kwake siyo wazalendo bali wazalendo ni wafanyakazi
wasio wanachama wa THTU.

Hali hii imeleta utengano mkubwa kati ya makundi haya mawili ya wafanyakazi ndani ya UCC. Wafanyakazi tunaamini kuwa tendo hili liko kinyume na sheria, kanuni na taratibu za Ajira. Ifahamike kuwa Dr. Minja ndiye Mkurugenzi Mtendaji pekee ambaye ameleta utengano kwa msingi wa huyu ni mwenzetu (asiye mwanachama wa THTU) na huyu siyo mwenzetu (aliye mwanachama wa THTU) tangu UCC ilipoanzishwa.

Tunaamini pia kwamba dhamira ya Menejimenti ya kupunguza wafanyakazi ni janja tu inayolenga kuwapa uwezo wa kuwaondoa wanachama wa THTU UCC na kwa minajili ya kuondoa kikwazo cha matendo yao na pia kusimika hofu ya wale wanaobaki dhidi ya kujiunga na chama hicho (THTU).

2.3 MAAMUZI MABOVU WAKATI NA BAADA YA KUHAMISHA MATAWI KUTOKA MAJENGO YA WATU BINAFSI KWENDA KUPANGA MAJENGO YANAYOMILIKIWA NA UMMA

Katika kutekeleza agizo la Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2016 la kuitaka UCC kuhama kutoka kupanga kwenye majengo ya watu binafsi na kwenda kupanga kwenye majengo ya umma, wafanyakazi tunaamini kuwa utawala wa Dr. Minja ulitekeleza agizo hilo kwa kukurupuka na hivyo kusababisha mkanganyiko kiundeshaji na kibiashara ambao umesababisha na utasababisha hasara kubwa iwapo kusudio lake la kufunga matawi ya Mwanza, Mbeya na Arusha litatekelezwa. Sisi wafanyakazi tunahoji yafuatayo juu ya kusudio la kufungwa kwa matawi tajwa hapo juu:
a) Moja ya faida kubwa ya kuhama kutoka kupanga majengo ya watu binafsi na kupanga kwenye majengo ya umma ni kupungua kwa kodi ya pango (rental fee) iliyokuwa ikilipwa na UCC. Kodi
kubwa ya pango ilikuwa ni sababu ya matawi kupata faida ndogo. Hivyo, ilikuwa ni matarajio yetu
wafanyakazi kuwa baada ya matawi ya Arusha, Mbeya na Mwanza kuhamia kwenye majengo ya umma, BASI, utawala wa Dr. Minja ungetoa muda wa kutosha kwa matawi haya kuendelea kutoa huduma kwa umma ili kutumia fursa hiyo ya kushuka kwa kodi ya pango. Badala yake Menejimenti imehamisha matawi husika na kufanya maamuzi ya kuyafunga bila ya kutoa muda wa matawi hayo kufanya biashara chini ya uangalizi maalum (grace period) ili kubaini kama yataweza kutengeneza faida au la. Kwa mfano, Tawi la Mbeya lilihamia kwenye jengo la UDSM hivyo kiwango cha malipo ya pango ni nafuu sana ukilinganisha na hapo awali hivyo wangepewa muda wa angalizo kama watatengeneza faida au la.

Hivyo basi kitendo cha kutokutoa muda wa angalizo kwa matawi haya kufanya biashara baada ya kupata unafuu wa kodi ya pango ni nia ovu na hakikubaliki na kinashangaza kwa mtu mwenye weledi wa kiuongozi.

b) Kulikuwa na ulazima upi wa kuhama Tawi la Arusha kutoka jengo la Summit Centre (private building) na kwenda jengo la NSSF Plaza (public building) mwishoni mwaka 2017 iwapo tawi hilo linafungwa Oktoba 2018? Ikumbukwe kuwa kuhama kwa tawi la Arusha kumesababisha UCC kuingia gharama za kuhamisha vifaa/mali (relocation costs) na gharama za kutengeneza ofisi na madarasa (office & training rooms partitioning costs). Gharama zote hizi ni hasara ambayo UCC imepata kama tawi litafungwa Oktoba 2018. Ilikuwa ni busara tawi libaki lilikokuwa likisubiri kufungwa!

c) Kwa hiyo maamuzi hayo chini ya Menejimenti ya Dr. Ellinami Minja siyo sahihi. Kuhama kutoka majengo binafsi na kwenda majengo ya umma na akiwa anajua fika kwamba atayafunga hayo matawi katika muda mfupi ujao ni matumizi mabaya ya fedha za Taasisi. Izingatiwe kuwa mchakato huo wa kuhama umegharimu pesa nyingi na kwa mantiki hiyo matumizi mabaya ya fedha za taasisi. Hatimaye gharama hizi za kuhama huingizwa kwenye matumizi ya matawi husika na mwisho wa siku inaonekana matawi husika yameleta HASARA (LOSS), kumbe chanzo ni maamuzi yasiyo sahihi ya utawala wa Dr. Minja.

d) Wafanyakazi tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusiana na maamuzi haya yasiyo sahihi yaliyofanywa na Menejimenti hii juu ya kuhamisha matawi na hatimaye kuchukua maamuzi ya kuyafunga bila ya kuyapa muda wa angalizo wa kutoa huduma.

2.4 UNYANYASAJI NA UKIUKAJI WA HAKI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi tunanyanyaswa sana na Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Yafuatayo ni mambo ambayo yamekuwa sugu na ambayo malalamiko yake hayajawahi kutatuliwa na Menejimenti chini ya Dr. Minja.

a) Mikataba ya wafanyakazi inayotolewa na Utawala wa Dr. Minja ni ya kiunyanyasaji ambayo haifuati sheria za kazi
· Mikataba inayotolewa ni ya muda maalum hata kwa kazi ambazo ni endelevu kwa miaka yote ambayo shirika/taasisi imekuwepo.
· Wakati wa ku-renew mkataba, muda na vigezo vya mkataba wa mfanyakazi unaweza kubadilishwa (kwa kupunguzwa) kiholela. Imetokea wafanyakazi wenye mikataba ya miaka 3 imebadilishwa muda na kupewa mikataba ya miezi 6 au 9 bila mawasiliano ya awali. Au mfanyakazi mwenye mkataba wa miaka mitano ukabadilishwa na kushushwa kiholela ukawa wa miaka mitatu. Hawa ni wafanyakazi ambao wamekuwa wakiitumikia UCC kwa zaidi ya miaka kumi!
· Utaratibu wa kupewa mkataba mwingine (ku-renew) umewekewa vikwazo vingi – ikiwamo:

i. Recruitment committee (ambayo inahusisha watu wengine ambao hawafanyi kazi na mfanyakazi husika). Hii ni kinyume na miongozo ya sheria za kazi.
ii. Kutakiwa kujaza upya KPI (Key Performance Indicators) pale unapoandika barua ya kuomba ku-renew mkataba. Hii haijalishi kwamba KPI hujazwa kwa mwaka na kwa hiyo imewekwa mahsusi kutoa mwanya kwa kiongozi wako kuku-grade vibaya pale anapoona inafaa au anapokuwa amepokea maagizo ya kufanya hivyo. Hii ni kinyume na sheria za kazi,
iii. Kuwekwa vigezo vya muda maalum wa kuzingatia unapotaka ku-renew mkataba lakini mwajiri hajali kukujibu ndani ya muda huo alioweka.

b) Kutokufuatwa kwa Scheme of Service (SoS) ya UCC na kutokuwa na mlinganyo mzuri wa mishahara
UCC inayo Scheme of service iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 na utawala wa Dkt. Minja bila ya kushirikisha chama cha Wafanyakazi. Mwaka 2017 ikafanyiwa tena marekebisho na Menejimenti
ya Dr. Minja bila ya kuwahusisha wafanyakazi na kupeleka mapendekezo ya marekebisho moja kwa
moja kwenye Bodi ya UCC. Hata hivyo, wafanyakazi tuna malalamiko kama ifuatavyo kuhusiana na jambo hili:
i. Baadhi ya wafanyakazi kuongezewa mishahara kwa upendeleo bila kuzingatia mwongozo wa Scheme of Service kwa kuwa ni wateule wake
ii. Wafanyakazi walio wengi mishahara yao haijaongezeka kwa zaidi ya miaka sita
iii. Baadhi ya wafanyakazi kuandikiwa barua kuwa mishahara waliyonayo sasa inastahili kupunguzwa
iv. Vigezo vya kupandisha madaraja ya wafanyakazi havifuatwi au havifanyiwi kazi.
v. Wafanyakazi wanalazimishwa kujiendeleza kwa kujigharamia wenyewe. Hawapandishwi madaraja kama inavyoainishwa kwenye scheme of service.
vi. Mfanyakazi anajaza KPI kila mwaka na mara zote hizo anapata alama za juu. Lakini hata mfanyakazi anapofanya vema mfululizo hapandishwi daraja wala kuwa motivated.
c) Wafanyakazi wanaofanya kazi yao kwa weledi na maadili ya kazi zao kuondolewa kwenye nafasi zao kwa vigezo visivyoridhisha
Haijalishi iwapo unafanya kazi yako kwa weledi na kwa kufuata maadili ya kazi hiyo, unatarajiwa pia kukiuka yote hayo pale unapopokea maagizo ya kufanya hivyo kutoka kwa Dr. Minja kama
mkuu wa taasisi. Hayo yamewakuta baadhi ya wafanyakazi wenzetu ikiwamo Afisa Manunuzi.
Wengine wametolewa kwenye nafasi zao kwa sababu wao ni wanachama wa THTU na kwa hiyo ni wapelelezi; wanachukua habari za ndani ya vikao na kuzipeleka THTU. Kwenye Taasisi yetu THTU imekuwa ni adui mkubwa wa Menejimenti ya Dkt. Minja

2.5 KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI BILA KUWASHIRIKISHA WAFANYAKAZI NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI NA YANAYOENDELEA KUFANYIKA BAADA YA NOTISI YA KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ulitoa notisi ya kukusudia kupunguza wafanyakazi kwa msingi kuwa UCC imekuwa ikipata hasara. Hii ni uthibitisho kuwa weledi wake wa kuongoza UCC umefika mwisho kwa kuwa ameshindwa kuwa na maono ya namna ya kuifanya taasisi kujiendesha kibiashara. Hata hivyo sisi wafanyakazi tunahoji kwa kuwa tuna ushahidi wa yafuatayo:
a) Kama ana nia njema na zoezi hili kwa nini hakushirikisha wafanyakazi na chama cha wafanyakazi (THTU) kama sheria inavyoagiza juu ya jambo hili kabla ya kufikia hatua ya kutoa notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi?
b) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya kwenye nafasi zisizokuwa za uzalishaji na kuwalipa mishahara mikubwa baada ya kutoa notisi ya kupunguza wafanyakazi. Mfano kuna umuhimu gani wa kuajiri hivi karibuni Finance & Administration Manager (FAM) na Human Resources Officer mwingine na kuwapa mishahara minono kama UCC haifanyi vizuri na inadhamiria kupunguza wafanyakazi wake?! Watu hawa wanakuja kumsimamia nani?!
c) Kuajiri baada ya notisi baadhi ya wafanyakazi ambao Job Titles zao hazipo kwenye Scheme of
Service. Mfano Finance & Administration Manager (FAM)
d) Kuwaongezea mishahara kwa upendeleo baadhi ya wafanyakazi tena baada ya notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi
e) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya wenye mishahara minono kwenye idara ya Software
Engineering kabla na baada ya Notisi ya kupunguza wafanyakazi. Ni ajabu kuona mishahara

minono inalipwa kwa waajiriwa hawa wapya wakati Menejimenti na Bodi wamekiri kwenye taarifa kwa umma kuwa UCC inapata hasara. Kama inapata hasara fedha hizi wanazolipwa zinatoka wapi!

2.6 UTAWALA USIOTENDA HAKI KWA WAFANYAKAZI WANAOTAKA KUJIENDELEZA KIELIMU

Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ni utawala usiotenda haki. Kwa mfano wapo wafanyakazi ambao walitaka kujiendeleza kimasomo wakaomba ruhusa ya kusoma bila malipo (leave without pay) au ruhusa ya kusoma yenye malipo (leave with pay) wakanyimwa ruhusa na kuambiwa waache kazi kama wanataka kujiendeleza kimasomo. Wakati huo huo wapo wafanyakazi walioruhusiwa kujiendeleza kimasomo na kuendelea kupata asilimia 80% ya mishahara yao chini ya utawala wake. Kiongozi mwenye double standards hatufai sisi wafanyakazi wa UCC.

Ifahamike ya kuwa ni utawala wa Dr. Ellinami Minja tu ambao umewanyima wafanyakazi wenye scholarship kwenda kusoma na kuendelea kupata mishahara yao hata kwa asilimia fulani. Awamu zote zilizopita ziliheshimu umuhimu wa mfanyakazi kujiendeleza kielimu hasa pale anapokuwa amepata ufadhili (scholarship). Ndiyo maana ndani ya UCC iliwezekana kupata wafanyakazi wenye shahada za uzamivu watano (5) waliotokana na tawala zilizopita kuwaruhusu kwenda kusoma na wakati huo huo wakiwa wanalipwa asilimia 80% ya mishahara yao. Ushahidi wa jambo hili upo.

2.7 KUSHINDWA KUMILIKI, KUDHIBITI NA KUENDESHA KIUFASAHA MIFUMO YA KAZI ZA UCC
Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami Minja imeshindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kiufasaha mifumo ya kazi za UCC. Tatizo hili ni dhahiri zaidi katika huduma za mafunzo ambazo pia ndio zinazoajiri zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wote wa UCC. Hii ni kama ifuatavyo:
a) Ukosefu wa vifaa muhimu na mazingira mabovu ya kufundishia
Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutafuta namna ya kupata vitendea kazi vya kutosha kwa ajili ya huduma za mafunzo. Kwa mfano:
· Kukosekana kwa kompyuta madarasani limekuwa ni jambo la kawaida sana ndani ya huduma hii.
Kwenye vipeperushi vyetu vyote tumeahidi kwamba kila mwanafunzi anatumia kompyuta yake mwenyewe lakini sio mara moja au mbili wanafunzi wanalazimika ku-share kompyuta.
· Projectors ni vifaa ya muhimu sana katika huduma ya mafunzo lakini kwa sasa chini ya Dkt. Minja vifaa hivi ni vya kugombania na kunyang’anyana! Wanafunzi mara zote wanakuwa wahanga wa mvutano huo pale mwalimu wao wanaposhindwa kupata Projector.
· Tumeahidi kwa wateja kuwa tuna Stand-by Generator na kwamba umeme unapokatika mwanafunzi hapotezi muda wake, LAKINI hili nalo sasa ni kitendawili chini ya utawala wa Dr. Minja. Ni kawaida kwa sasa wanafunzi kukaa bila kusoma pale umeme unapokatika kwa sababu umeme unapokatika Generator hazifanyi kazi. Hali hii ipo hata Training HQ ambapo angalau tungetarajia kuwa Generator itumike mara moja baada ya umeme kukatika.
· Mazingira ya ufundishiaji yenyewe yanakosa vifaa muhimu kwa ajili ya kuweka vizuri huduma hii.
Kwa mfano katika Jiji la Dar es Salaam ambalo hali yake ya hewa ni ya joto kali unakuta madarasa hayana madirisha yanayotosheleza idadi ya wanafunzi wanaoingia humo na AC hazifanyi kazi.
Mwalimu anafundisha yeye mwenyewe anabubujikwa jasho. Wanafunzi wanajipepea kwa kutumia
vitabu vya kufundishia wanavyotakiwa kuwa wanavisoma kufuata maelekezo ya somo husika.
Huu ni unyanyasaji mkubwa wa wateja pamoja na walimu husika na ni kushindwa kutambua athari za mwenendo huu katika mustakabali wa huduma zetu! Kwa mfano Tawi la City Centre lina AC ofisini kwa Meneja tu.!
Izingatiwe kuwa ukosefu wa vifaa muhimu vya kufundishia limekuwa tatizo sugu wakati wote wa Awamu ya uongozi wa Dkt Minja. Kipindi cha tawala zilizopita Menejimenti husika zilikuwa zikifanya jitihada za makusudi na kushirikiana na Wafanyakazi katika kutatua changamoto hizo kwa kuwa walikuwa na maono na nia nzuri katika kuboresha huduma za mafunzo. Hivyo, siyo ajabu sasa kukimbiwa na wateja na kwenda kuzitafuta kwenye taasisi zenye vifaa vya kisasa na mazingira bora ya kusomea.
b) Kushindwa kutangaza huduma za mafunzo za UCC
Uongozi wa Dkt. Minja umeshindwa kabisa kuwa na mwongozo thabiti wa kujitangaza kwenye soko. Suala hili limekuwa la kisiasa sana na limekuwa linachezewa sana. Bajeti ya kujitangaza haieleweki! Katika
ulimwengu huu wa matangazo ambao tunawaona hata vyuo vidogo kama Zoom Polytechnic vinajitangaza
sana ni nadra kuona tangazo la UCC. Mara zote kisingizio ni hakuna hela. Njia kuu ya kujitangaza kwa UCC
imekuwa ni kufundisha vizuri ili wateja warudi tena na pia wawalete na ndugu zao.

c) Hakuna jitihada za Menejimenti ku-connect na Wafanyakazi
Dkt.Minja ameweka stop kwa mfanyakazi yeyote kwenda ofisini kwake bila kwanza kupitia kwa viongozi wa kati aliowateua. Wafanyakazi wanapokuwa na dukuduku “sugu” la ki-taasisi au la binafsi wanalazimika kusubiri mpaka wakati wa Mkutano Mkuu wa taasisi ambao unatakiwa ufanyike kila nusu ya mwaka lakini nao unafanyika mara chache mno na unakuwa na mambo mengi huku Menejimenti ikiuharakisha kwa kigezo cha muda hautoshi. Pale shida inapokuwa ya binafsi ya siri basi mfanyakazi anajitahidi kumeza machungu yake. Sio wafanyakazi wengi wenye uwezo hata tu wa kuongea shida zao hadharani. Zuio hili la kumuona Dkt. Minja na kuongea naye limeleta fadhaa kubwa sana ndani ya taasisi. Tunafikiri kiongozi wa Taasisi anapaswa kuwa wazi kwa wafanyakazi kuweza kumuona hata kama ni kwa kutenga siku na muda maalum.
d) Kuvuruga na Kufunga Matawi ya UCC ambayo ndiyo kimbilio la huduma za Mafunzo ya
TEHAMA

Uvurugaji na kufunga matawi umefanywa na Menejimenti ya Dkt. Minja katika mambo makubwa yafuatayo:
i. Uamuzi wa kufunga matawi ya mikoani umefanywa na menejimenti kibabe, bila upembuzi yakinifu na bila kushirikisha Wafanyakazi.
ii. Kunyanyapaa huduma za mafunzo za UCC na kufanya njama za kuziua/kuzifunga iii. Kuhamisha Tawi la City Centre kwenda eneo finyu kuliko lilipokuwa mwanzo
iv. Kupuuzia au kudharau kurejea maamuzi au maono ya watangulizi wake wa tawala zilizopita na sababu zake.

2.8 UBADHIRIFU NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA TAASISI
(a) Menejimenti ya Dkt. Minja imekuwa na usiri mkubwa kwenye maamuzi ya fedha za
Taasisi.

Wafanyakazi hawaambiwi undani wa matumizi hayo isipokuwa tu kupewa bajeti ya matumizi yanayoitwa “Overhead” katika Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi. Overhead hii inajumuisha matumizi ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na ofisi za Fedha na Meneja Rasilimali Watu (HR).
Matumizi ya Overhead huwa yanagawanywa kwa vitengo vyote vinavyozalisha kwa uwiano wa uwezo wao. Tatizo ni kuwa matumizi haya huwa ni makubwa mno kuzidi hata matumizi ya hayo matawi yenyewe ambayo idadi ya wafanyakazi wao ni kubwa mara dufu kuliko hao wa ofisi hizo. Kiasi kwamba hata pale ambapo tawi husika lilipata faida kwa uwiano wa mapato na matumizi basi hudaiwa limepata hasara pale gawio hilo la Overhead linapojumlishwa.
Wafanyakazi wanapohoji kuhusu kupewa mnyumbulisho wa matumizi husika hawapewi isipokuwa kuahidiwa kupewa katika kikao kijacho. Kwa usiri huo wa Overhead hakuwi na uwezekano wa kuhoji kuhusu matumizi hayo na hata kuchangia kuhusu kupunguza matumizi hayo. Na hakuna namna ambayo mfanyakazi anaweza kusema kuna jitihada za makusudi za kupunguza matumizi hayo ya Overhead.
(b) Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutunza na kudhibiti vizuri mali zinazotokana na jasho la wafanyakazi wake.
Katika maamuzi yake ya utata ya kufunga matawi kiholela wamediriki kuacha samani na vifaa vya mamilioni ya shilingi vikiharibika kwa mvua na jua bila kujali kwamba zimetokana na jasho la wafanyakazi hao hao ambao sasa wanataka kuwapunguza. Vifaa vilivyotoka Mbezi Beach viliachwa kuharibika bila uwajibikaji. Hakuna hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika maana yake ni kuwa ulikuwa ni uamuzi wa Menejimenti yenyewe.
(c) Menejimenti ya Dkt. Minja inadiriki kuwaambia wafanyakazi kwamba eti hasara tunayopata imetokana na wateja kutolipia huduma.
Hivi ni nani anayeajiri wakusanyaji wa madeni na malipo ya huduma nyingine zilizotolewa na UCC na kudhibiti mapato hayo? Ni mwalimu au Programmer au Dereva?! Hivi ni nani anayepaswa kuwawajibisha maofisa hao kama wanashindwa kufanya kazi zao? Ni mwalimu, Programmer, Dereva au Human Resource Officer au mafanyakazi mwingine?!
Menejimenti chini ya Dr. Minja wanadiriki kudai kwamba mamilioni ya shilingi hayajalipwa kwa UCC na hakuna anayewajibishwa kwa hili! Dkt. Minja anadiriki hata kusema kwamba huduma ya mafunzo ingeleta faida kama wateja wote wangelipa vizuri. Mbona taasisi nyingine wateja wanalipa, UCC kulikoni? Je UDSM nako wanafunzi hawalipi? Inakuwaje?
(d) Kuwa na Chief Accountants wawili ambao taasisi inagharimia mishahara yao. Kwa sasa UCC kuna Machief Accountants wawili kwa sasa. Kuna umuhimu gani wa kuendelea kuwa na Chief Accountants wawili? Sisi Wafanyakazi tulitazamia baada ya mchakato wa kupata Chief Accountant

mpya mwezi Novemba 2017 yule aliyekuwepo mwanzo (ambaye katika mojawapo wa vikao vya UCC alitambulishwa kama Ag. Chief Accountant) angerudi UDSM immediately alikokuwa awali lakini bado yupo mpaka sasa na anaendelea kulipwa mshahara na UCC. Kama UCC inapata hasara kama ilivyotamkwa kwenye taarifa ya Bodi kwa Umma, pesa za kulipa Machief Accountants wawili tangu Novemba 2017 mpaka sasa zinatoka wapi? Huu ni ubadhirifu wa dhahiri unaofanywa na Dkt. Minja.

2.9 KUSHINDWA KUJIPANGA VIZURI KIUENDESHAJI NA KIMKAKATI KWA MASLAHI YA WATEJA WETU NA UCC KWA UJUMLA

Kwa ujumla Menejimenti chini ya Dkt. Minja imeshindwa kuendesha taasisi kimkakati ili kuleta tija kwa wateja wote wakahudumiwa vizuri na wakaridhika na UCC ikapata mapato yake. UCC ni taasisi ambayo imejikita katika mioyo ya Watanzania kama kimbilio lao kwa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) na huduma nyingine. Kushindwa kujipanga kwa Menejimenti ya Dkt. Minja na utendaji wao wa kutokushirikisha Wafanyakazi kumetusababishia hasara hiyo Menejimenti na Bodi inayoitangaza kwa umma. Hii ni kwa kuzingatia Menejimenti husika imegubikwa na utendaji mbovu, maamuzi mabovu yanayoiletea Taasisi hasara, na kushindwa kujipanga vizuri.

Taasisi ya UCC inahitaji Menejimenti thabiti inayoamini katika kuboresha ufanisi wa huduma zilizopo za UCC na kubuni huduma mpya kwa kuwaunganisha Wafanyakazi na kuwaelekeza katika kuongeza bidii, utaalamu na weledi huku ikijitahidi kuchukua hatua za dhati katika kutatua changamoto zinazokabili huduma tulizozitaja na nyinginezo zinazojitokeza. Tunahitaji Menejimenti yenye uchungu na wafanyakazi katika shida zao ha hivyo kuweza kupata ushirikiano wa kina (sympathy and cooperation) wa Wafanyakazi hao. Tunahitaji Menejimenti inayoinua ari na dhamira ya Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na hapo wateja watatuona tena na kurudi UCC kwenye viwango vyake.

2.10 DKT. MINJA HAATHIRIWI NA KUYUMBA AU KUFA KWA UCC
Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Minja amekuwa akiweka bayana katika mikutano mbalimbali ya wafanyakazi kwamba yeye ni mwajiriwa wa UDSM na hivyo hata UCC ikifa ajira yake iko salama. Japo maneno hayo yanaweza kuwa yanalenga kuwapa nguvu wafanyakazi kuchukua mustakabali wa Taasisi mikononi mwao, maneno haya pia yanaweka bayana kwamba maamuzi yoyote yale anayoyachukua hayamuathiri yeye mwenyewe moja kwa moja. Maamuzi yake yanaidhoofisha, kuiyumbisha na kuhatarisha mustakabali wa UCC na hayamweki yeye katika hali ya hatari. Ni sisi tu wafanyakazi ambao hatima zetu na za familia zetu ziko UCC ndio tunaohatarishwa. Yeye atakosa “posho” tu ya Ukurugenzi wa UCC. Hata kama posho hiyo ni kubwa kuliko mshahara wa mfanyakazi yeyote yule wa UCC lakini ni posho tu!
3. HITIMISHO
Tunaomba umma utambue kwamba Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami J. Minja imeshindwa kazi yake. Jitihada zake za kufunga baadhi ya huduma na hasa huduma ya mafunzo ni njia ya Menejimenti yake kujipa muda zaidi kabla kansa ya kushindwa kwake haijaenea na kuiteketeza kabisa UCC.Ifahamike kwamba huduma ya Mafunzo itolewayo na UCC ndiyo inayowahudumia watanzania wengi zaidi. Hii ni huduma inayofaa kuboreshwa na kutolewa kwa ufanisi zaidi. Huduma hii pia inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wa UCC. Haiwezi kuachwa ikauwawa hivi hivi tu! Menejimenti ya Dkt. Minja imeliteka nyara Taasisi na kuamua ya kwao yanayolenga kuathiri vibaya maslahi ya umma wa watanzania na Wafanyakazi wa UCC.

Menejimenti ya Dkt. Minja hujiamulia wanayotaka kwa gharama ya kuvuruga huduma za mafunzo kwa watanzania na kufuja haki na maslahi ya Wafanyakazi walio wengi. Wanaamua kufumbia macho familia zote za wafanyakazi hawa wanaofanya kazi kwa bidii kubwa huku wao wakijikita kwenye kufuja fedha za Shirika.
Tunaomba Mamlaka zinazohusika zitambue kuwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Ellinami J. Minja amekuwa UCC kwa kipindi cha miaka mitatu tu kati ya miaka takriban ishirini ya uhai wa UCC. Katika kipindi hiki tu cha miaka mitatu yake ya uongozi uharibifu wote na matatizo yote yaliyotajwa hapo juu ameyafanya yeye na Menejimenti yake. Je, Dkt. Ellinami Minja akiendelea kuongoza Menejimenti ya UCC nini hatima ya UCC?
IMETOLEWA NA​
WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) TAREHE 12 OKTOBA 2018
 
Hivi wanashindwa UCC wataweza kuwa na Campus's nchi nzima kama wenzao wa Jomo Kenyatta
 
Ninachoona hapo ni kama mtiririko wa majungu na kupakana matope unaochagizwa na kundi moja dhidi ya kundi jingine. Hakuna jipya hapo ni maslahi tu.
 
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC) KUJIBU TAARIFA YA PROF. MAKENYA A. H. MABOKO (MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA UCC) ALIYOTOA KWA UMMA HAPO TAREHE 1 OKTOBA 2018

1. UTANGULIZI
Taasisi ya University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC) inamilikiwa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa asilimia mia moja.UCC ilianzishwa na UDSM kwa madhumuni ya kutoa mafunzo, huduma za ushauri, na kufanya utafiti kuhusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji haya kwa jamii, UCC ililazimika kutanua huduma hizi kwa jamii na Taifa kwa ujumla kuanzia mwaka 2001 baada ya kusajiliwa na Ofisi ya Usajili wa Makampuni. Uamuzi huu uliwezesha kuipatia UCC fursa ya kubaki na majukumu ya kubuni mafunzo ya ufundi ya muda mfupi na mrefu ambayo yatakidhi maendeleo na ukuaji wa tasnia ya TEHAMA na yanayoendana na ukuaji wa mahitaji ya soko pamoja na kutoa huduma nyingine ambazo zitanufaisha mahitaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla katika nyanja zifuatazo: Huduma ya mtandao, kutengeneza mifumo ya kompyuta (softwares), Ushauri wa kitaalam katika tasnia ya TEHAMA, usanifu na uwekaji wa miundo mbinu ya TEHAMA.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya TEHAMA hapa nchini na duniani kwa ujumla, UCC iliendelea kupanua na kutoa huduma zake kulingana na ongezeko la mahitaji. Tangu kuanzishwa kwake, UCC ina matawi katika mikoa ifuatayo: Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha na matawi mawili kwa sasa yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam (moja likiwa makao Makuu-UDSM na tawi lingine City Centre).

Hapo tarehe 1 Oktoba 2018, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UCC, Profesa Makenya A.H. Maboko alitoa Taarifa kwa Umma kwa alichokiita ukweli kuhusu uendeshaji wa UCC na hali ya kibiashara ya kampuni. Taarifa hiyo kwa ujumla ilizungumzia “Hali ya utendaji wa Kampuni na hatua zilizochukuliwa na Urekebishaji Muundo wa Biashara na kujenga UCC mpya”. Taarifa hiyo Wafanyakazi wa UCC tuliipata kupitia mitandao ya kijamii na Ubao wa Matangazo wa UCC Makao Makuu.

Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi katika taarifa yake kwa Umma imekiri kuwa kumekuwa na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikizungumzia kuhusu UCC. Tunatambua kuwa ndani ya vyombo hivyo vya habari menejimenti ya UCC chini ya Dkt. Ellinami J. Minja ndiyo imekuwa ikilalamikiwa na wafanyakazi kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji.

Tulitarajia Bodi ya Wakurugenzi mara baada ya kupata taarifa hizo kuhusu UCC kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ingekutana na sisi Wafanyakazi ili kutumia nafasi hiyo kutusikiliza mbali na taarifa anazopata kutoka kwa Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Jambo hilo halikufanyika na hivyo taarifa iliyotolewa na Bodi kwa Umma ni mawazo ya Menejimenti ya UCC inayolalamikiwa.

Kwa malengo inayoyajua, Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikutenda haki kwa kuwa imezungumzia mambo machache sana miongoni mwa mambo lukuki ambayo wafanyakazi wanailalamikia Menejimenti chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. EllinamiJj. Minja.

Mambo hayo ambayo Bodi ya Wakurugenzi haikuyatolea maelezo pamoja na kwamba yamekuwa yakiandikwa kwenye vyombo hivyo vya habari, tumeamua kuyaeleza kwa kina ili umma uyafahamu kama ifuatavyo:

2. MALALAMIKO YA WAFANYAKAZI DHIDI YA MENEJIMENTI CHINI YA DKT. ELLINAMI J. MINJA
Tumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja ambayo Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi haikuyaweka wazi katika taarifa yake kwa umma kama yalivyoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii. Mambo hayo ni pamoja na KWANZA(1) Kusabisha uharibifu wa mali zilizokuwa Tawi la Mbezi Beach, PILI(2) Kubagua wafanyakazi kwa vigezo vya uanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) ,TATU(3) Usimamizi mbovu wakati wa kuhamisha matawi, NNE(4) Ukiukaji wa haki na maslahi ya Wafanyakazi, TANO(5) Notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi, SITA(6) Kutokutenda haki sawa kwa wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza kielimu, SABA(7) Kushindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kwa ufasaha mifumo ya kazi za UCC, NANE (8) Kufuja na kutumia vibaya fedha za Taasisi, TISA (9) Kushindwa kujipanga vizuri kiuendeshaji na kimkakati kwa maslahi ya wateja wetu na kwa ajili ya mafanikio ya UCC na KUMI (10) Dkt. Minja hataathiriwa na kuyumba au kufa kwa UCC.

2.1 KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI ZA UCC ZILIZOKUWA TAWI LA MBEZI BEACH DAR ES SALAAM
Mwezi Agosti 2016, Dkt. Ellinami Minja, Mkurugenzi Mtendaji wa UCC, alifanya maamuzi ya kufunga tawi la Mbezi Beach DSM lililokuwa likitoa mafunzo ya kompyuta ya muda mfupi na mrefu. Wakati maamuzi hayo yanafanyika tawi hilo lilikuwa na wanafunzi wapatao mia tatu. Maamuzi ya kufunga tawi la Mbezi Beach Dar es Salaam yalichukuliwa kiholela bila kuwashirikisha wafanyakazi (ambao ni wadau wakubwa) na ya kukurupuka kiasi cha kusababisha vifaa vya tawi hilo kupelekwa UCC makao makuu-UDSM na kuachwa viharibike kwa jua na mvua kwa sababu havikutunzwa mahali salama.

Dr. Ellinami Minja kama Mkurugenzi Mtendaji (Accounting Officer) wa Taasisi (UCC) alifanya uzembe wa hali ya juu kwa kutokuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha mali mbalimbali (physical assets) zilizotoka Tawi la Mbezi Beach DSM zinatunzwa mahali salama. Kutokana na uzembe huo mali hizo hazikutunzwa vizuri na hivyo ziliharibika na zinazidi kuharibika na kusababisha hasara kubwa kwa Taasisi yetu na ushahidi wa suala hili upo wazi. Mali hizo ni meza, viti, kompyuta, UPS, viyoyozi (ACs), Fire Extinguishers na Rack Cabinets ambavyo vinazidi kuozea nje kwa kunyeshewa na mvua na kupigwa na jua.

Kwa uzembe huo, na hasa kwa kuwa hakuna hatua zozote za uwajibishwaji zilizochukuliwa na Menejimenti ya Dkt. Ellinami Minja, tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina wa jambo hili ili kubaini kiwango cha hasara halisi kilichojitokeza na kiongozi huyu awajibishwe kwa kusababisha hasara hiyo.

Sisi Wafanyakazi tunaona busara ilikuwa ni kutoa msaada wa mali hizo kwenye shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2016 alipoomba taasisi mbali mbali na wananchi kwa ujumla kutoa misaada ya madawati na viti kwa shule hizo kuliko kuziacha zikiharibika na zikiendelea kuharibika.

Kwa kufanya hivyo Dkt. Ellinami Minja kwa namna moja au nyingine angekuwa ameitikia au ameunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na ndoto yake ya kuona wanafunzi kusoma bure zinatimia.

2.2 KUWABAGUA WAFANYAKAZI WALIO WANACHAMA WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI - THTU
Dkt. Minja ametengeneza ufa (utengano) mkubwa kati ya wafanyakazi walio wanachama wa Chama cha wafanyakazi (THTU) na wasio wanachama wa THTU. Wafanyakazi walio wanachama wa THTU kwake wanaonekana wasiofaa bali wanaofaa ni wale ambao sio wanachama. Amefikia hatua ambayo ili upate kuteuliwa katika nafasi ya Uongozi sharti uache uanachama wa THTU kama wewe ni mwanachama wa THTU. Ushahidi wa jambo hili upo kwa kuwa wapo wafanyakazi walioandikiwa barua za kuwataka kuacha uanachama wa THTU kama sharti la kuendelea na nafasi za Uongozi walizo nazo. Kwa lugha nyingine walio wanachama wa THTU kwake siyo wazalendo bali wazalendo ni wafanyakazi wasio wanachama wa THTU.

Hali hii imeleta utengano mkubwa kati ya makundi haya mawili ya wafanyakazi ndani ya UCC. Wafanyakazi tunaamini kuwa tendo hili liko kinyume na sheria, kanuni na taratibu za Ajira. Ifahamike kuwa Dr. Minja ndiye Mkurugenzi Mtendaji pekee ambaye ameleta utengano kwa msingi wa huyu ni mwenzetu (asiye mwanachama wa THTU) na huyu siyo mwenzetu (aliye mwanachama wa THTU) tangu UCC ilipoanzishwa.

Tunaamini pia kwamba dhamira ya Menejimenti ya kupunguza wafanyakazi ni janja tu inayolenga kuwapa uwezo wa kuwaondoa wanachama wa THTU UCC na kwa minajili ya kuondoa kikwazo cha matendo yao na pia kusimika hofu ya wale wanaobaki dhidi ya kujiunga na chama hicho (THTU).

2.3 MAAMUZI MABOVU WAKATI NA BAADA YA KUHAMISHA MATAWI KUTOKA MAJENGO YA WATU BINAFSI KWENDA KUPANGA MAJENGO YANAYOMILIKIWA NA UMMA
Katika kutekeleza agizo la Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2016 la kuitaka UCC kuhama kutoka kupanga kwenye majengo ya watu binafsi na kwenda kupanga kwenye majengo ya umma, wafanyakazi tunaamini kuwa utawala wa Dr. Minja ulitekeleza agizo hilo kwa kukurupuka na hivyo kusababisha mkanganyiko kiundeshaji na kibiashara ambao umesababisha na utasababisha hasara kubwa iwapo kusudio lake la kufunga matawi ya Mwanza, Mbeya na Arusha litatekelezwa. Sisi wafanyakazi tunahoji yafuatayo juu ya kusudio la kufungwa kwa matawi tajwa hapo juu:

a) Moja ya faida kubwa ya kuhama kutoka kupanga majengo ya watu binafsi na kupanga kwenye majengo ya umma ni kupungua kwa kodi ya pango (rental fee) iliyokuwa ikilipwa na UCC. Kodi kubwa ya pango ilikuwa ni sababu ya matawi kupata faida ndogo. Hivyo, ilikuwa ni matarajio yetu wafanyakazi kuwa baada ya matawi ya Arusha, Mbeya na Mwanza kuhamia kwenye majengo ya umma, BASI, utawala wa Dr. Minja ungetoa muda wa kutosha kwa matawi haya kuendelea kutoa huduma kwa umma ili kutumia fursa hiyo ya kushuka kwa kodi ya pango. Badala yake Menejimenti imehamisha matawi husika na kufanya maamuzi ya kuyafunga bila ya kutoa muda wa matawi hayo kufanya biashara chini ya uangalizi maalum (grace period) ili kubaini kama yataweza kutengeneza faida au la. Kwa mfano, Tawi la Mbeya lilihamia kwenye jengo la UDSM hivyo kiwango cha malipo ya pango ni nafuu sana ukilinganisha na hapo awali hivyo wangepewa muda wa angalizo kama watatengeneza faida au la.​

Hivyo basi kitendo cha kutokutoa muda wa angalizo kwa matawi haya kufanya biashara baada ya kupata unafuu wa kodi ya pango ni nia ovu na hakikubaliki na kinashangaza kwa mtu mwenye weledi wa kiuongozi.​

b) Kulikuwa na ulazima upi wa kuhama Tawi la Arusha kutoka jengo la Summit Centre (private building) na kwenda jengo la NSSF Plaza (public building) mwishoni mwaka 2017 iwapo tawi hilo linafungwa Oktoba 2018? Ikumbukwe kuwa kuhama kwa tawi la Arusha kumesababisha UCC kuingia gharama za kuhamisha vifaa/mali (relocation costs) na gharama za kutengeneza ofisi na madarasa (office & training rooms partitioning costs). Gharama zote hizi ni hasara ambayo UCC imepata kama tawi litafungwa Oktoba 2018. Ilikuwa ni busara tawi libaki lilikokuwa likisubiri kufungwa!​

c) Kwa hiyo maamuzi hayo chini ya Menejimenti ya Dr. Ellinami Minja siyo sahihi. Kuhama kutoka majengo binafsi na kwenda majengo ya umma na akiwa anajua fika kwamba atayafunga hayo matawi katika muda mfupi ujao ni matumizi mabaya ya fedha za Taasisi. Izingatiwe kuwa mchakato huo wa kuhama umegharimu pesa nyingi na kwa mantiki hiyo matumizi mabaya ya fedha za taasisi. Hatimaye gharama hizi za kuhama huingizwa kwenye matumizi ya matawi husika na mwisho wa siku inaonekana matawi husika yameleta HASARA (LOSS), kumbe chanzo ni maamuzi yasiyo sahihi ya utawala wa Dr. Minja.​

d) Wafanyakazi tunaomba Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusiana na maamuzi haya yasiyo sahihi yaliyofanywa na Menejimenti hii juu ya kuhamisha matawi na hatimaye kuchukua maamuzi ya kuyafunga bila ya kuyapa muda wa angalizo wa kutoa huduma.​

2.4 UNYANYASAJI NA UKIUKAJI WA HAKI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi tunanyanyaswa sana na Menejimenti chini ya Dkt. Minja. Yafuatayo ni mambo ambayo yamekuwa sugu na ambayo malalamiko yake hayajawahi kutatuliwa na Menejimenti chini ya Dr. Minja.

a) Mikataba ya wafanyakazi inayotolewa na Utawala wa Dr. Minja ni ya kiunyanyasaji ambayo haifuati sheria za kazi
  • Mikataba inayotolewa ni ya muda maalum hata kwa kazi ambazo ni endelevu kwa miaka yote ambayo shirika/taasisi imekuwepo.
  • Wakati wa ku-renew mkataba, muda na vigezo vya mkataba wa mfanyakazi unaweza kubadilishwa (kwa kupunguzwa) kiholela. Imetokea wafanyakazi wenye mikataba ya miaka 3 imebadilishwa muda na kupewa mikataba ya miezi 6 au 9 bila mawasiliano ya awali. Au mfanyakazi mwenye mkataba wa miaka mitano ukabadilishwa na kushushwa kiholela ukawa wa miaka mitatu. Hawa ni wafanyakazi ambao wamekuwa wakiitumikia UCC kwa zaidi ya miaka kumi!
  • Utaratibu wa kupewa mkataba mwingine (ku-renew) umewekewa vikwazo vingi – ikiwamo:

i. Recruitment committee (ambayo inahusisha watu wengine ambao hawafanyi kazi na mfanyakazi husika). Hii ni kinyume na miongozo ya sheria za kazi.​
ii. Kutakiwa kujaza upya KPI (Key Performance Indicators) pale unapoandika barua ya kuomba ku-renew mkataba. Hii haijalishi kwamba KPI hujazwa kwa mwaka na kwa hiyo imewekwa mahsusi kutoa mwanya kwa kiongozi wako kuku-grade vibaya pale anapoona inafaa au anapokuwa amepokea maagizo ya kufanya hivyo. Hii ni kinyume na sheria za kazi,​
iii. Kuwekwa vigezo vya muda maalum wa kuzingatia unapotaka ku-renew mkataba lakini mwajiri hajali kukujibu ndani ya muda huo alioweka.​

b) Kutokufuatwa kwa Scheme of Service (SoS) ya UCC na kutokuwa na mlinganyo mzuri wa mishahara
UCC inayo Scheme of service iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 na utawala wa Dkt. Minja bila ya kushirikisha chama cha Wafanyakazi. Mwaka 2017 ikafanyiwa tena marekebisho na Menejimenti ya Dr. Minja bila ya kuwahusisha wafanyakazi na kupeleka mapendekezo ya marekebisho moja kwa moja kwenye Bodi ya UCC. Hata hivyo, wafanyakazi tuna malalamiko kama ifuatavyo kuhusiana na jambo hili:

i. Baadhi ya wafanyakazi kuongezewa mishahara kwa upendeleo bila kuzingatia mwongozo wa Scheme of Service kwa kuwa ni wateule wake

ii. Wafanyakazi walio wengi mishahara yao haijaongezeka kwa zaidi ya miaka sita

iii. Baadhi ya wafanyakazi kuandikiwa barua kuwa mishahara waliyonayo sasa inastahili kupunguzwa

iv. Vigezo vya kupandisha madaraja ya wafanyakazi havifuatwi au havifanyiwi kazi.

v. Wafanyakazi wanalazimishwa kujiendeleza kwa kujigharamia wenyewe. Hawapandishwi madaraja kama inavyoainishwa kwenye scheme of service.

vi. Mfanyakazi anajaza KPI kila mwaka na mara zote hizo anapata alama za juu. Lakini hata mfanyakazi anapofanya vema mfululizo hapandishwi daraja wala kuwa motivated.

c) Wafanyakazi wanaofanya kazi yao kwa weledi na maadili ya kazi zao kuondolewa kwenye nafasi zao kwa vigezo visivyoridhisha

Haijalishi iwapo unafanya kazi yako kwa weledi na kwa kufuata maadili ya kazi hiyo, unatarajiwa pia kukiuka yote hayo pale unapopokea maagizo ya kufanya hivyo kutoka kwa Dr. Minja kama mkuu wa taasisi. Hayo yamewakuta baadhi ya wafanyakazi wenzetu ikiwamo Afisa Manunuzi. Wengine wametolewa kwenye nafasi zao kwa sababu wao ni wanachama wa THTU na kwa hiyo ni wapelelezi; wanachukua habari za ndani ya vikao na kuzipeleka THTU. Kwenye Taasisi yetu THTU imekuwa ni adui mkubwa wa Menejimenti ya Dkt. Minja

2.5 KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI BILA KUWASHIRIKISHA WAFANYAKAZI NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI NA YANAYOENDELEA KUFANYIKA BAADA YA NOTISI YA KUSUDIO LA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ulitoa notisi ya kukusudia kupunguza wafanyakazi kwa msingi kuwa UCC imekuwa ikipata hasara. Hii ni uthibitisho kuwa weledi wake wa kuongoza UCC umefika mwisho kwa kuwa ameshindwa kuwa na maono ya namna ya kuifanya taasisi kujiendesha kibiashara. Hata hivyo sisi wafanyakazi tunahoji kwa kuwa tuna ushahidi wa yafuatayo:

a) Kama ana nia njema na zoezi hili kwa nini hakushirikisha wafanyakazi na chama cha wafanyakazi (THTU) kama sheria inavyoagiza juu ya jambo hili kabla ya kufikia hatua ya kutoa notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi?
b) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya kwenye nafasi zisizokuwa za uzalishaji na kuwalipa mishahara mikubwa baada ya kutoa notisi ya kupunguza wafanyakazi. Mfano kuna umuhimu gani wa kuajiri hivi karibuni Finance & Administration Manager (FAM) na Human Resources Officer mwingine na kuwapa mishahara minono kama UCC haifanyi vizuri na inadhamiria kupunguza wafanyakazi wake?! Watu hawa wanakuja kumsimamia nani?!
c) Kuajiri baada ya notisi baadhi ya wafanyakazi ambao Job Titles zao hazipo kwenye Scheme of Service. Mfano Finance & Administration Manager (FAM)
d) Kuwaongezea mishahara kwa upendeleo baadhi ya wafanyakazi tena baada ya notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi
e) Kuendelea kuajiri wafanyakazi wapya wenye mishahara minono kwenye idara ya Software Engineering kabla na baada ya Notisi ya kupunguza wafanyakazi. Ni ajabu kuona mishahara minono inalipwa kwa waajiriwa hawa wapya wakati Menejimenti na Bodi wamekiri kwenye taarifa kwa umma kuwa UCC inapata hasara. Kama inapata hasara fedha hizi wanazolipwa zinatoka wapi!

2.6 UTAWALA USIOTENDA HAKI KWA WAFANYAKAZI WANAOTAKA KUJIENDELEZA KIELIMU
Utawala wa Dkt. Ellinami Minja ni utawala usiotenda haki. Kwa mfano wapo wafanyakazi ambao walitaka kujiendeleza kimasomo wakaomba ruhusa ya kusoma bila malipo (leave without pay) au ruhusa ya kusoma yenye malipo (leave with pay) wakanyimwa ruhusa na kuambiwa waache kazi kama wanataka kujiendeleza kimasomo. Wakati huo huo wapo wafanyakazi walioruhusiwa kujiendeleza kimasomo na kuendelea kupata asilimia 80% ya mishahara yao chini ya utawala wake. Kiongozi mwenye double standards hatufai sisi wafanyakazi wa UCC.

Ifahamike ya kuwa ni utawala wa Dr. Ellinami Minja tu ambao umewanyima wafanyakazi wenye scholarship kwenda kusoma na kuendelea kupata mishahara yao hata kwa asilimia fulani. Awamu zote zilizopita ziliheshimu umuhimu wa mfanyakazi kujiendeleza kielimu hasa pale anapokuwa amepata ufadhili (scholarship). Ndiyo maana ndani ya UCC iliwezekana kupata wafanyakazi wenye shahada za uzamivu watano (5) waliotokana na tawala zilizopita kuwaruhusu kwenda kusoma na wakati huo huo wakiwa wanalipwa asilimia 80% ya mishahara yao. Ushahidi wa jambo hili upo.

2.7 KUSHINDWA KUMILIKI, KUDHIBITI NA KUENDESHA KIUFASAHA MIFUMO YA KAZI ZA UCC
Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami Minja imeshindwa kumiliki, kudhibiti na kuendesha kiufasaha mifumo ya kazi za UCC. Tatizo hili ni dhahiri zaidi katika huduma za mafunzo ambazo pia ndio zinazoajiri zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wote wa UCC. Hii ni kama ifuatavyo:

a) Ukosefu wa vifaa muhimu na mazingira mabovu ya kufundishia
Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutafuta namna ya kupata vitendea kazi vya kutosha kwa ajili ya huduma za mafunzo. Kwa mfano:
  • Kukosekana kwa kompyuta madarasani limekuwa ni jambo la kawaida sana ndani ya huduma hii. Kwenye vipeperushi vyetu vyote tumeahidi kwamba kila mwanafunzi anatumia kompyuta yake mwenyewe lakini sio mara moja au mbili wanafunzi wanalazimika ku-share kompyuta.
  • Projectors ni vifaa ya muhimu sana katika huduma ya mafunzo lakini kwa sasa chini ya Dkt. Minja vifaa hivi ni vya kugombania na kunyang’anyana! Wanafunzi mara zote wanakuwa wahanga wa mvutano huo pale mwalimu wao wanaposhindwa kupata Projector.
  • Tumeahidi kwa wateja kuwa tuna Stand-by Generator na kwamba umeme unapokatika mwanafunzi hapotezi muda wake, LAKINI hili nalo sasa ni kitendawili chini ya utawala wa Dr. Minja. Ni kawaida kwa sasa wanafunzi kukaa bila kusoma pale umeme unapokatika kwa sababu umeme unapokatika Generator hazifanyi kazi. Hali hii ipo hata Training HQ ambapo angalau tungetarajia kuwa Generator itumike mara moja baada ya umeme kukatika.
  • Mazingira ya ufundishiaji yenyewe yanakosa vifaa muhimu kwa ajili ya kuweka vizuri huduma hii. Kwa mfano katika Jiji la Dar es Salaam ambalo hali yake ya hewa ni ya joto kali unakuta madarasa hayana madirisha yanayotosheleza idadi ya wanafunzi wanaoingia humo na AC hazifanyi kazi. Mwalimu anafundisha yeye mwenyewe anabubujikwa jasho. Wanafunzi wanajipepea kwa kutumia vitabu vya kufundishia wanavyotakiwa kuwa wanavisoma kufuata maelekezo ya somo husika.
  • Huu ni unyanyasaji mkubwa wa wateja pamoja na walimu husika na ni kushindwa kutambua athari za mwenendo huu katika mustakabali wa huduma zetu! Kwa mfano Tawi la City Centre lina AC ofisini kwa Meneja tu.!
Izingatiwe kuwa ukosefu wa vifaa muhimu vya kufundishia limekuwa tatizo sugu wakati wote wa Awamu ya uongozi wa Dkt Minja. Kipindi cha tawala zilizopita Menejimenti husika zilikuwa zikifanya jitihada za makusudi na kushirikiana na Wafanyakazi katika kutatua changamoto hizo kwa kuwa walikuwa na maono na nia nzuri katika kuboresha huduma za mafunzo. Hivyo, siyo ajabu sasa kukimbiwa na wateja na kwenda kuzitafuta kwenye taasisi zenye vifaa vya kisasa na mazingira bora ya kusomea.

b) Kushindwa kutangaza huduma za mafunzo za UCC
Uongozi wa Dkt. Minja umeshindwa kabisa kuwa na mwongozo thabiti wa kujitangaza kwenye soko. Suala hili limekuwa la kisiasa sana na limekuwa linachezewa sana. Bajeti ya kujitangaza haieleweki! Katika ulimwengu huu wa matangazo ambao tunawaona hata vyuo vidogo kama Zoom Polytechnic vinajitangaza sana ni nadra kuona tangazo la UCC. Mara zote kisingizio ni hakuna hela. Njia kuu ya kujitangaza kwa UCC imekuwa ni kufundisha vizuri ili wateja warudi tena na pia wawalete na ndugu zao.

c) Hakuna jitihada za Menejimenti ku-connect na Wafanyakazi
Dkt.Minja ameweka stop kwa mfanyakazi yeyote kwenda ofisini kwake bila kwanza kupitia kwa viongozi wa kati aliowateua. Wafanyakazi wanapokuwa na dukuduku “sugu” la ki-taasisi au la binafsi wanalazimika kusubiri mpaka wakati wa Mkutano Mkuu wa taasisi ambao unatakiwa ufanyike kila nusu ya mwaka lakini nao unafanyika mara chache mno na unakuwa na mambo mengi huku Menejimenti ikiuharakisha kwa kigezo cha muda hautoshi. Pale shida inapokuwa ya binafsi ya siri basi mfanyakazi anajitahidi kumeza machungu yake. Sio wafanyakazi wengi wenye uwezo hata tu wa kuongea shida zao hadharani. Zuio hili la kumuona Dkt. Minja na kuongea naye limeleta fadhaa kubwa sana ndani ya taasisi. Tunafikiri kiongozi wa Taasisi anapaswa kuwa wazi kwa wafanyakazi kuweza kumuona hata kama ni kwa kutenga siku na muda maalum.

d) Kuvuruga na Kufunga Matawi ya UCC ambayo ndiyo kimbilio la huduma za Mafunzo ya TEHAMA
Uvurugaji na kufunga matawi umefanywa na Menejimenti ya Dkt. Minja katika mambo makubwa yafuatayo:
i. Uamuzi wa kufunga matawi ya mikoani umefanywa na menejimenti kibabe, bila upembuzi yakinifu na bila kushirikisha Wafanyakazi.
ii. Kunyanyapaa huduma za mafunzo za UCC na kufanya njama za kuziua/kuzifunga
iii. Kuhamisha Tawi la City Centre kwenda eneo finyu kuliko lilipokuwa mwanzo
iv. Kupuuzia au kudharau kurejea maamuzi au maono ya watangulizi wake wa tawala zilizopita na sababu zake.

2.8 UBADHIRIFU NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA TAASISI
(a) Menejimenti ya Dkt. Minja imekuwa na usiri mkubwa kwenye maamuzi ya fedha za Taasisi.
Wafanyakazi hawaambiwi undani wa matumizi hayo isipokuwa tu kupewa bajeti ya matumizi yanayoitwa “Overhead” katika Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi. Overhead hii inajumuisha matumizi ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na ofisi za Fedha na Meneja Rasilimali Watu (HR).
Matumizi ya Overhead huwa yanagawanywa kwa vitengo vyote vinavyozalisha kwa uwiano wa uwezo wao. Tatizo ni kuwa matumizi haya huwa ni makubwa mno kuzidi hata matumizi ya hayo matawi yenyewe ambayo idadi ya wafanyakazi wao ni kubwa mara dufu kuliko hao wa ofisi hizo. Kiasi kwamba hata pale ambapo tawi husika lilipata faida kwa uwiano wa mapato na matumizi basi hudaiwa limepata hasara pale gawio hilo la Overhead linapojumlishwa.
Wafanyakazi wanapohoji kuhusu kupewa mnyumbulisho wa matumizi husika hawapewi isipokuwa kuahidiwa kupewa katika kikao kijacho. Kwa usiri huo wa Overhead hakuwi na uwezekano wa kuhoji kuhusu matumizi hayo na hata kuchangia kuhusu kupunguza matumizi hayo. Na hakuna namna ambayo mfanyakazi anaweza kusema kuna jitihada za makusudi za kupunguza matumizi hayo ya Overhead.

(b) Menejimenti ya Dkt. Minja imeshindwa kutunza na kudhibiti vizuri mali zinazotokana na jasho la wafanyakazi wake.
Katika maamuzi yake ya utata ya kufunga matawi kiholela wamediriki kuacha samani na vifaa vya mamilioni ya shilingi vikiharibika kwa mvua na jua bila kujali kwamba zimetokana na jasho la wafanyakazi hao hao ambao sasa wanataka kuwapunguza. Vifaa vilivyotoka Mbezi Beach viliachwa kuharibika bila uwajibikaji. Hakuna hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika maana yake ni kuwa ulikuwa ni uamuzi wa Menejimenti yenyewe.
(c) Menejimenti ya Dkt. Minja inadiriki kuwaambia wafanyakazi kwamba eti hasara tunayopata imetokana na wateja kutolipia huduma.
Hivi ni nani anayeajiri wakusanyaji wa madeni na malipo ya huduma nyingine zilizotolewa na UCC na kudhibiti mapato hayo? Ni mwalimu au Programmer au Dereva?! Hivi ni nani anayepaswa kuwawajibisha maofisa hao kama wanashindwa kufanya kazi zao? Ni mwalimu, Programmer, Dereva au Human Resource Officer au mafanyakazi mwingine?!

Menejimenti chini ya Dr. Minja wanadiriki kudai kwamba mamilioni ya shilingi hayajalipwa kwa UCC na hakuna anayewajibishwa kwa hili! Dkt. Minja anadiriki hata kusema kwamba huduma ya mafunzo ingeleta faida kama wateja wote wangelipa vizuri. Mbona taasisi nyingine wateja wanalipa, UCC kulikoni? Je UDSM nako wanafunzi hawalipi? Inakuwaje?
(d) Kuwa na Chief Accountants wawili ambao taasisi inagharimia mishahara yao. Kwa sasa UCC kuna Machief Accountants wawili kwa sasa. Kuna umuhimu gani wa kuendelea kuwa na Chief Accountants wawili? Sisi Wafanyakazi tulitazamia baada ya mchakato wa kupata Chief Accountant mpya mwezi Novemba 2017 yule aliyekuwepo mwanzo (ambaye katika mojawapo wa vikao vya UCC alitambulishwa kama Ag. Chief Accountant) angerudi UDSM immediately alikokuwa awali lakini bado yupo mpaka sasa na anaendelea kulipwa mshahara na UCC. Kama UCC inapata hasara kama ilivyotamkwa kwenye taarifa ya Bodi kwa Umma, pesa za kulipa Machief Accountants wawili tangu Novemba 2017 mpaka sasa zinatoka wapi? Huu ni ubadhirifu wa dhahiri unaofanywa na Dkt. Minja.

2.9 KUSHINDWA KUJIPANGA VIZURI KIUENDESHAJI NA KIMKAKATI KWA MASLAHI YA WATEJA WETU NA UCC KWA UJUMLA
Kwa ujumla Menejimenti chini ya Dkt. Minja imeshindwa kuendesha taasisi kimkakati ili kuleta tija kwa wateja wote wakahudumiwa vizuri na wakaridhika na UCC ikapata mapato yake. UCC ni taasisi ambayo imejikita katika mioyo ya Watanzania kama kimbilio lao kwa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) na huduma nyingine. Kushindwa kujipanga kwa Menejimenti ya Dkt. Minja na utendaji wao wa kutokushirikisha Wafanyakazi kumetusababishia hasara hiyo Menejimenti na Bodi inayoitangaza kwa umma. Hii ni kwa kuzingatia Menejimenti husika imegubikwa na utendaji mbovu, maamuzi mabovu yanayoiletea Taasisi hasara, na kushindwa kujipanga vizuri.
Taasisi ya UCC inahitaji Menejimenti thabiti inayoamini katika kuboresha ufanisi wa huduma zilizopo za UCC na kubuni huduma mpya kwa kuwaunganisha Wafanyakazi na kuwaelekeza katika kuongeza bidii, utaalamu na weledi huku ikijitahidi kuchukua hatua za dhati katika kutatua changamoto zinazokabili huduma tulizozitaja na nyinginezo zinazojitokeza. Tunahitaji Menejimenti yenye uchungu na wafanyakazi katika shida zao ha hivyo kuweza kupata ushirikiano wa kina (sympathy and cooperation) wa Wafanyakazi hao. Tunahitaji Menejimenti inayoinua ari na dhamira ya Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na hapo wateja watatuona tena na kurudi UCC kwenye viwango vyake.

2.10 DKT. MINJA HAATHIRIWI NA KUYUMBA AU KUFA KWA UCC
Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Minja amekuwa akiweka bayana katika mikutano mbalimbali ya wafanyakazi kwamba yeye ni mwajiriwa wa UDSM na hivyo hata UCC ikifa ajira yake iko salama. Japo maneno hayo yanaweza kuwa yanalenga kuwapa nguvu wafanyakazi kuchukua mustakabali wa Taasisi mikononi mwao, maneno haya pia yanaweka bayana kwamba maamuzi yoyote yale anayoyachukua hayamuathiri yeye mwenyewe moja kwa moja. Maamuzi yake yanaidhoofisha, kuiyumbisha na kuhatarisha mustakabali wa UCC na hayamweki yeye katika hali ya hatari. Ni sisi tu wafanyakazi ambao hatima zetu na za familia zetu ziko UCC ndio tunaohatarishwa. Yeye atakosa “posho” tu ya Ukurugenzi wa UCC. Hata kama posho hiyo ni kubwa kuliko mshahara wa mfanyakazi yeyote yule wa UCC lakini ni posho tu!

3. HITIMISHO
Tunaomba umma utambue kwamba Menejimenti chini ya Dkt. Ellinami J. Minja imeshindwa kazi yake. Jitihada zake za kufunga baadhi ya huduma na hasa huduma ya mafunzo ni njia ya Menejimenti yake kujipa muda zaidi kabla kansa ya kushindwa kwake haijaenea na kuiteketeza kabisa UCC.Ifahamike kwamba huduma ya Mafunzo itolewayo na UCC ndiyo inayowahudumia watanzania wengi zaidi. Hii ni huduma inayofaa kuboreshwa na kutolewa kwa ufanisi zaidi. Huduma hii pia inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi wa UCC. Haiwezi kuachwa ikauwawa hivi hivi tu! Menejimenti ya Dkt. Minja imeliteka nyara Taasisi na kuamua ya kwao yanayolenga kuathiri vibaya maslahi ya umma wa watanzania na Wafanyakazi wa UCC.

Menejimenti ya Dkt. Minja hujiamulia wanayotaka kwa gharama ya kuvuruga huduma za mafunzo kwa watanzania na kufuja haki na maslahi ya Wafanyakazi walio wengi. Wanaamua kufumbia macho familia zote za wafanyakazi hawa wanaofanya kazi kwa bidii kubwa huku wao wakijikita kwenye kufuja fedha za Shirika.
Tunaomba Mamlaka zinazohusika zitambue kuwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Ellinami J. Minja amekuwa UCC kwa kipindi cha miaka mitatu tu kati ya miaka takriban ishirini ya uhai wa UCC. Katika kipindi hiki tu cha miaka mitatu yake ya uongozi uharibifu wote na matatizo yote yaliyotajwa hapo juu ameyafanya yeye na Menejimenti yake. Je, Dkt. Ellinami Minja akiendelea kuongoza Menejimenti ya UCC nini hatima ya UCC?
IMETOLEWA NA
WAFANYAKAZI WA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC)
TAREHE 12 OKTOBA 2018
I greatly dislike! Hii kitu kabisa watu wasiombe isitokee na ipishilie mbali sana kwani itapoteza ajira karibia 1000!
 
Back
Top Bottom