Mizinga ya demu imeua ndugu wawili

Mizinga ya demu imeua ndugu wawili

bombom

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2013
Posts
614
Reaction score
228
Niko Masomoni Nairobi, nikihudhuria kozi fupi.

Nikiwa huko mnamo tarehe 6 Januari, nilipigiwa simu na rafiki yangu wa kike akiwa anaangua kilio kuwa mama yake mdogo amefariki huko Bukoba, hivyo nimwezeshe nauli pamoja na fedha ya kutumia kwa muda wa wiki mbili hivi.

Tarehe 15 Aprili 2014, nilipigiwa simu tena kwamba yeye yuko Kampala, na hakunipa taarifa kabla ya kwenda huko kwani lilikuwa suala la dharura, kwa sababu alikwenda kumuuguza dada yake aliyekuwa akiishi Jinja, na kwa wakati alipokuwa akipiga simu hiyo, kwa bahati mbaya dada yake huyo alifariki kwenye Hospitali ya Mulago - Kampala, alikokuwa amelazwa. Aliomba kupelekewa fedha za matumizi wakati akiendelea kusubiri ndugu zake waweze kufika huko kwa ajili ya mipango ya ama mazishi au kuusafirisha mwili wa marehemu. Alieleza kuwa, kwa kuwa yeye amekaa sana huko kwa ajili ya kuuguza, ameomba kutangulia Bukoba. Kwa ajili hiyo aliomba nimtumie nauli (flight) ya MWANZA (comnnection ya Easy Jet) ili akaunganishe Bukoba kwa Basi.

Kufuatia hali hiyo ya misiba ya mfurulizo ya ndugu zake hny wangu, ilibidi nifanya kautafiti kadogo, kupitia ndugu zake na namba zake za simu. Nilichobaini ni kwamba, wakati wote huo, hakukuwa na msiba wowote. Hny wangu huyo alikuwa anaendelea kuvinjari mitaa ya Dar akila Bata. Wana JF, aliyekuwa GF wangu (kwa sasa nimembwaga kwa sababu ya udanganyifu) ameua ndugu zake wawili ndani ya muda wa miezi mitatu, ili tu apate fedha za matanuzi.
Kufanya hivyo si vizuri jamani, kuweni wawazi tu.
 
hivi huyo alikuwa umemweka kama future girl wako.?? aisee hny wako ni mjinga sana aiseee ....
 
ina maana ni member wa JF Or/??

pole sana mapenzi noma
 
Pole sana, but inaonekana we ni mbahili ndio maana alikuwa anatumia mbinu za kuua ndugu zake..lol!
 
duh!!!
kama njaa huyo demu kapiliza mwajameni mweeee!!!!
 
Bora ulivopiga chini mapema. Hafai hata kuwa kijakazi wako.
 
Nilionana naye chuoni. Ukimtazama, huwezi kumdhania.

duuuuuh,bado yuko chuo au amemaliza? Maana bado anaaply ya vyuoni,cku c nyingi kuna mwingine atakuja hapa na mkasa wa chuoni tena,hawa wa vyuon umizwa kichwa aiseee
 
unamanisha member wa jf hawez kufanya tukio la ujambaz wa aina hiyo?

wanaweza kwa maana nao ni binadamu....kama vipi atupie no/avatar/na jina tumsaidie kumpa adabu
 
Mwingine anakuambia nina mimba yako na sijajianda kulea nipe hela ya kulitoa
 
Back
Top Bottom