Mizinga aina ya HIMARS (High Mobility Artillery Rockets System)

Nakwambia hivi siku ya kushehekea uhuru hapa ni maonyesho na ku test makombora hapa unakumbuka ile iliyo rushwa ikaenda kutua baharini pwani ya Carlifonia USA??
Marekani huwa hana show off ya silaha. Tangu nizaliwe sijawahi ona popote Marekani anafanya military parade, wakati fulani niliwahi waza hivi wanajeshi wa Marekani wanajua kweli kupiga gwaride sawasawa kama North Korea, China, India na Russia wanavyojua.

Na hapa tulizungumzia artillery systems na multiple rocket launchers sio nuclear missiles. Isitoshe Marekani haina mobile nukes kwenye maroli. Sio strategy yao badala yake wanazo nuclear attack submarines za Ohio class zipo 14 na kila moja inabeba nuclear missiles 24 za Trident II. Hizo ndio hukaa majini zikifanya shift muda wowote 24/4 zinasubiri yeyote ajichanganye. Urusi anazo Borei na Typhoon class zinabeba makombora mengi pungufu kidogo ya Ohio. Alafu sio lazima uwe na makombora mengi ya nyuklia, vita ikitokea hayatotumika mengi hivyo. Mradi uwe na survivability yake kubwa.
 
Wabongo kwa machinoo tu hamjambo. Yahani mnajua mambo ya ndani kabisa ya majeshi ya USA na Russian! Ajabu ya dunia

Kuonyesha silaha kwenye magwalide sio dili ni kama kuingizwa chaka. Hawawezi kujianika kihivyo. Funguka hacha kuklemu kila kitu
 
Kwamba umejibu kwa usahihi au lah...Sijui,ila nimependa namna nzuri ya kujibu ki uungwana...asante nimejifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo kwa machinoo tu hamjambo. Yahani mnajua mambo ya ndani kabisa ya majeshi ya USA na Russian! Ajabu ya dunia

Kuonyesha silaha kwenye magwalide sio dili ni kama kuingizwa chaka. Hawawezi kujianika kihivyo. Funguka hacha kuklemu kila kitu
Hapa umechangia nini mzee? Unajua hii comment yako tukiihamishia uzi wa Amber Ruty itapata mashiko uko. Haina msaada wowote kwenye uzi huu na haijaongeza value. Unaweza pinga kwa facts, kujazia au kurekebisha.

Ulichofanya hata darasa la pili anaweza
 
Huu Uzi nahisi wanao comment ni wajeda tu. Haiwezekani mtu wa kawaida tu ukawa unajisomea aina za makomborq na nguvu zake halafu basi tu iishie hewani.
Ila nawashukuru kuna elimu tunaipata hapa kutoka kwenu
 
America wanazo showoff sana tu
 
Niwashukuru sana wajuzi/wataalamu hakika Jamii forum kuna maarifa ya kutosha ukija kwa lengo la kujifunza hakina unajifunza napata nondo za kutosha.

Kuna jamaa mmoja nafwatilia anafanya PHd ya Military weapons anareport habari ya Ukraine & Russia jamaa anajua zana za Kivita mpaka raha,

Kumbe basi humu Jamii forum kumbe wajuzi wa mambo hayo wapo #Kongole

Hakuna Ushabiki humu tunataka kujifunza, nimepata extra knowledge.
 
Huyo tutakuwa tunamsoma wote. Nina waandishi nawasoma wengi wanafanya PhD ya mambo ya jeshi na usalama
 
Sina uhakika kama kuna tofauti kati ya HIMARS na MLRS. Naona kama zinadanya kazi za kufanana. Sina uhakika lakini
High Mobility Artillery Rocket System (HIMARS) ni aina ya Multiple Launching Rocket System (MLRS) yenye survivability kubwa kwenye mazingira magumu zaidi. Marekani wanapenda sana silaha zao kuzipa acronym nzuri na rahisi kutamka, za kuvutia. Kuna watu special kazi yao ni kutafuta maneno ambayo yakipangiliwa yanaleta maana ila ufupisho wake unakidhi.
 
Chief hii imekaaje, kama wanaona mpaka mahandaki hawajaona yale mahandaki ya 🇮🇷 IRAN au wameshawahi kuyaona na kuyafumua, (si mfuatiliaji wa ndank saana mambi haya, unaweza ongezea nyama katika hili)
 
Chief hii imekaaje, kama wanaona mpaka mahandaki hawajaona yale mahandaki ya 🇮🇷 IRAN au wameshawahi kuyaona na kuyafumua, (si mfuatiliaji wa ndank saana mambi haya, unaweza ongezea nyama katika hili)
Marekani na Iran hawapo kwenye vita kwahiyo hakuna sababu ya Marekani kuishambulia Iran.

Ni vizuri ukijua silaha au mbinu za adui usimwambie kuwa unajua. Wewe tafuta njia za kupambana nazo kimyakimya siku akitaka kuzitumia ashangae hazimpi matokeo yaleyale. Miaka ya Cold war CIA na MI6 waligundua cable ya mawasiliano kupitia Ujerumani Mashariki, hawakusema kabisa wakawa wanasikiliza taarifa zinazotoka Ujerumani Mashariki ambayo ilikuwa ya muhimu sana kwa Soviet Union. Baadae double agents wa CIA wakaiambia KGB kuwa huwa wanasikilizwa, KGB nayo haikuwaambia maadui kwamba tunajua mnatusikia, wala haikuacha kutuma taarifa. Ilianza kutuma taarifa nyepesi, za kimkakati na wa uongo kuwapumbaza, walikuja kuambiwa miaka ya baadae wakajiona wajinga.

Iran ana mahandaki mengi kati yake kuna yatakayokuwa yanajulikana (lazima yawepo) na yasiyojulikana. North Korea ana mahandaki mengi na kubwa zaidi lilipatikana na mamlaka za South Korea. USSR kwenye Cold war alikuwa na underground facilities kama Gola Yamantaw yenye kubeba zaidi ya watu 10,000 kwa miezi zaidi ya 6 na kila kitu humo ndani. Switzerland miaka ya Cold war ilikuwa na maandaki ya kutosha kuhifadhi raia wote nchi nzima na ziada 10% ya population. Sweden ilikuwa na ground facility ya kutunza meli za kivita pembeni na straight ya kwenda Urusi.

Hizi changamoto zililazimisha Marekani wakati wanatengeneza military satellites wajue namna ya kutambua ground kuna nini. Teknolojia inayotumika kupima madini na gesi kwa ndege ndio idea ilitoka hapo. Ukichimba shimo kubwa la km za mraba kadhaa chini na juu ukaacha udongo kwenye satellite wanaona kuna sehemu ardhi inakosa udongo. Labda uchimbe vichochoro ardhini kama vile vya Hamas ambavyo vinapitisha watu wawili wakibanana.

Na ndio maana kuna bunker buster bomb. Marekani wanayo inapiga na kupenya mita zaidi ya 50 za zege ndio inalipuka
 
Hizi ni propaganda kwa vifaa vya russia na teknolojia ingekuwa dhaifu marekan angeshamvamia urusi, biden alitereza tu ulimu, ikulu faster wakarekebisha... Kauli na kutegua endeleeni kuota
 
Trump alitaka kufanya military parade ikawa story kubwa sana kwenye media za US, nyingi zikimzungumzia anataka kuleta mambo ya Kiduku wa Korea Kaskazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…