Mizimu inapata wapi nguvu za kuleta mvua?

Mtu au kiumbe chochote kikifa hakiwezi kusikia, kuona, kuhisi wala kujibu chochote.

Kwahiyo kuamini kuwa mizimu inaweza kuleta mvua au kufanya chochote ni Upumbavu na Ujinga.
Una ushahidi? Kwani MTU ni nini hasa? Je, unafikiri MTU ni hili boksi linalofukiwa au kuchomwa moto hata kuliwa na wanyama au kuozeana tu?
 
Shangaeni kwanza hizo dini zenu, Hao Miungu wenu mnaowaomba kwa majina ya vificho ambayo ni aina ya mizimu hiyo hiyo mnayoipinga.

Yesu kwa lugha ya kificho ni Zues/Azazel, ambaye ni aina ya mzimu wa wamisri wa kale, na huu mzimu ulikuja kubadirishiwa jina miaka ya 300 A.D na hao hao watu weupe.

bila kusahau hayo majina ya Allah, Yehovah, elishadai, Elohim hawa nao ni wale wale mizimu kama mizimu wengine.

mkae mkijua mtu akifariki hawi mzimu na hatowai kuja kuwa mzimu, bali imani ya kumuomba mtu aliyekufa ilikuja baada ya kuona matendo ya mtu huyo akiwa hai, hivyo hata akifa baadhi ya watu waliendelea kuamin mtu huyo ataweza kuwasikia walio hai kwa kumuomba awaunganishe na Nguvu za Miungu awasaidie kupeleka maombi hapa pia utaona ibada hizi za umizimu zipo hata kwa jamii za imani za ukristo(katoric mzimu wa bikra maria na watakatifu wengine).

Ni ngumu kutenganisha umizimu na dini, ushirikina, uchawi na uganga, haya mambo si mazuri maana yanaharibu jamii.

Mizimu ni aina ya viumbe wa kiroho ambao ni tofaut na binadamu/mtu, na viumbe hawa wana nguvu za kutenda muujiza wowote ule, iwe uponyaji, na miujiza kama hiyo ya mvua ama kuzuia majanga.

kila jamii imepitia hizo mbanga za kuabudu mizimu, ubaya ni pale jamii za wazungu, wahindi na waarabu walipoforce kuwaaminisha watu weusi waamini Imani za Mizimu yao kuwa ni bora kuliko imani za mizimu ya jamii za watu weusi, na hapa ndipo ugumu na ubaya ulipoanza.

hakuna imani iliyosahihi maana hizi zote zimeibuka baada ya watu kusaliti Asili ya Dunia ambayo inampasa mtu kutoabudu aina yoyote ya kiumbe iwe ni hivyo vinavyojiita Mungu, mizimu, majin ama mashetan,

hivi vyote ni viumbe vilivyoumbwa hapa hapa dunian na vilijipa majina na makufuru ili kumfanya mtu awe mtumwa wao, ila ukwel unabaki ni kwamba, Asili ya Uumbaji ndiyo ilipaswa kuabudiwa, na Asili hiyo haihusiani na dini wala aina yoyote ya Miungu yenu ya uongo, na asili hiyo watu tumeshaisahau baada ya ujio wa hii mizimu/Miungu kuwapotosha watu na ndipo majanga na matatizo yalipoanzia hapa, vita, njaa, mauwaji, magonjwa, na kila aina ya matatizo yamekuja baada ya kusaliti Asili ya Uumbaji.
1665108527662.jpg
 
Mtu au kiumbe chochote kikifa hakiwezi kusikia, kuona, kuhisi wala kujibu chochote.

Kwahiyo kuamini kuwa mizimu inaweza kuleta mvua au kufanya chochote ni Upumbavu na Ujinga.
Uliwahi kufa then ukafufuka?

Maana kama unajua kila kitu kuhusu after death experience!
 
Mimi mzee wetu alikuwa mgonjwa,tulihangaika nae sana tukajaambiwa aligombana na wazazi wake hivyo zilihitajika mbuzi 2,dume na jike ili zichinjwe kuwaomba hao wazazi wake yaani baba na mama yake,ambao walikwishfariki miaka mingi.basi zoezi lilifanyika la kutafuta hao mbuzi na kufanya hilo tambiko na baada ya wiki moja tu mzee alipona na mpaka leo ni mzima!nilichoona ni kuwa mizimu ipo na inafanya kazi
 
Mizimu haiombi bali inalinda ana inaharibu au inaonya na kuelekeza kupitia ndoto maono na matukio halisi
Hapa umesema ukweli mimi nimeshapewa instructions kupitia ndoto kama tatu hv lakn bahati mbaya sijaambulia maana ya hata moja
 
True kabisa

Juzi kuna mzee mmoja nilikua najadiriana nae Jambo, akaniambia tatizo vijana wa siku wanatanguliza sana usomi wao mbele, shida ndio inaanzia hapo, sikutaka kumfukua sana alikua anamaanisha nini ila nmeanza kumwelewa

Mfano juzi wahadhiri wa Chuo kikuu UDSM wanataka kufanya tafiti km uchawi upo au haupo, inaingia akilini kweli? Yaan umesoooma sasa umefika hatua ya kuanza kupingapinga kila kitu unachokiona unapinga tu, ila ukipigwa tukio unakimbilia kwa Mwamposa kukanyaga Mafura

Kuna watu ni sheeebzi type kabisa
Nane nane 2019 tulikuwa na mjapan ana PhD ya uchawi,sikutaka kumuhoji mengi na sikutaka kudadisi sana, sielewi thesis na hizo research alifanya kwa namna gani ila ni Doctor kabisa
 
Nane nane 2019 tulikuwa na mjapan ana PhD ya uchawi,sikutaka kumuhoji mengi na sikutaka kudadisi sana, sielewi thesis na hizo research alifanya kwa namna gani ila ni Doctor kabisa
True ila wapo nchi zilizoendelea huko wanatambuliwa kabisa na vyuo vipo

Nakumbuka kuna mwaka mmoja kuna mama simkumbuki jina ni Mtanzania ila alienda kusomea uchawi uko nje na akawa amemaliza masomo yake akarudi Tanzania, kwa hio huko nchi zingine ni taaluma km taaluma zingine tu
 
Fikiria unaota ndoto mara uko shuleni, mara uko kitaa na watu wengine kabisa mbali na hawa wa siku zote na kwenye ndoto hizo unaona ni Maisha tu ya kawaida mpaka pale utakapoamka. Kiukweli kuna dunia nyingine nje ya hii tulioizoea.
 
Kuna vitu Tuelewe kuwa Hatuabudu Mizimu ila we accept them as the historical connecter to one created us Kwa hiyo ukiona umeomba mzimu na kitu kimetokea Basi sio Yeye Ni yule aliyetuumba



Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Allah ndiye pekee mwenye kuleta mvua na muendeshaji wa mambo yote kaka...zingine porojo tu

[Qur an AR-RUM - 48 ]
Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapo wafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha.
 
Halafu mtu akifa anageuka kuwa mzimu, kesho mnaenda kumuomba alete mvua, huu upuuzi tumeupata wapi? Mfu anapata wapi Nguvu za kuleta mvua?
Ila Mzungu akimuita marehemu fulani Mtakatifu huwa mnaitikia "Utuombee". wakati hata huyo Mtakatifu naye pia ni Marehemu anaanzaje kukuombea wewe uliye hai?
Tuachane na utumwa wa kifikra, tujifunze kuheshimu na kuenzi vya kwetu.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom