Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,181
- 166,175
Ndugu Yohana Mashagala ametoa Ushahidi wa Nguvu ya asili kuleta mvua kijijini, baada ya mfungo, na maombi ya kanisani kushindwa kufungua milango ya mvua,
akanikumbusha juu ya Hekima za huyu mwamba wa kimarekani...
Waafrika Hatutaweza Kuamka hadi tutakaposoma Maandishi ya huyu Profesa..
Anaitwa Noam Chomsky, Mwanafalsafa na profesa wa Kimarekani, mwenye umri wa miaka 95, ambaye kwa sasa amepoteza uwezo wake wa kuzungumza na kuandika, na hivyo kulazimika kuachia kazi yake ya uandishi— chombo kile kile alichokitumia kufichua ukweli kuhusu mifumo ya dunia.
Katika maisha yake ya uandishi, aliacha nyuma tafakuri zenye nguvu sana kwa mtu mweusi, ikiwa ni pamoja na:
1. "Hakuna nchi maskini; kuna mifumo iliyofeli ya usimamizi wa rasilimali za nchi husika."
Hapa mtu mweusi hataelewa kabisa, hadi Nimfafanulie😁
2. "Hakuna atakayekuwekea ukweli katika akili yako; ni jambo ambalo ni lazima ulitafute na kuligundua mwenyewe."
Na hapa mfia dini za kimagharibi, za kizungu ndio kwanza ataanza kunichukia na kuniona adui yake, kwa kunukuu mstari huu..
3. "Kama unataka kumdhibiti mtu, muundie adui wa kufikirika ambaye anaonekana kuwa hatari zaidi yako, kisha ujionyeshe kama mkombozi wake. Wazungu wameumba Shetani wa kufikirika ili kuwachanganya Waafrika na kujifanya wao ni waokozi wa Afrika kupitia dini iliyojaa uongo."
Si maneno yangu, ni maneno ya huyu profesa..
4. "Mojawapo ya mafundisho ya wazi kabisa kutoka kwenye historia: haki haiombwi; inachukuliwa kwa nguvu."
Wale waoga, Wasiotaka kujihusisha na siasa kwa kuvunga wanalinda amani, kwa kuvunga kuwa dini na siasa haviingiliani, mzee wetu aliwafikia pia..
5. "Kuna sababu nyuma ya kupotosha historia kwa kuifanya ionekane kana kwamba ni watu wakuu pekee wanaoweza kutekeleza mambo makubwa. Hili huwafundisha watu kuamini kwamba hawana uwezo na lazima wasubiri mtu mkuu achukue hatua." wale wa kuomba makanisani Mungu awaletee amani na haki katika nchi yao bila wao kuchukua hatua, nanyi mzee wangu aliwafikia..
6. "Dunia ni mahali pa ajabu na pa kuchanganya. Ikiwa hujajitayarisha kuchanganyikiwa, basi unakuwa nakala tu ya mawazo ya mtu mwingine."
7. "Ili kuwadhibiti watu, unapaswa uwafanye waamini kuwa wao wenyewe ndio chanzo cha mateso yao, halafu ujionyeshe kama mkombozi wao."
8. "Magharibi siku moja watajutia mawazo yao ya juujuu yanayowatenganisha watu na asili yao halisi. Mtu lazima atafute dini sahihi na imani sahihi."
Nikagundua kuwa, hakika Waafrika Na ulimwengu kwa ujumla tulichezewa akili na kikundi cha watu wachache wasio na Nia njema..
Wakati Asili ya kidini ikikutaka upeleke sadaka hai, propaganda za kidini zinakutaka upeleke hela— Kuna uhusiano gani kati ya hela na sadaka?
Nikagundua baadae kuwa, matumizi ya fedha kama sadaka hai mbele za Mungu ni njia ya kututoa katika reli,
Ili tushindwe kupata Nguvu kamili yenye kutenda mara moja tunapokuwa na shida.
Tukutane kwenye Comment, kwa mwenye duku duku juu ya hekima ya huyu profesa..