Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,080
- 1,448
MZIGO MZITO UNAMPA MPAGAZI, JE WA NDANI UNAMPA NANI?
mzigo mzito mpe Mnyamwezi,
Kwa sababu ana uwezo wa nguvu za mwili.
Mzigo wa akili hakuna wa kukubebea
Na huo ndio mzigo unaochosha kuliko anaoubeba Mnyamwezi.
Huu hauonekani… lakini unakula nguvu kila sekunde.
Chuki.
Maumivu ya zamani.
Tamaa zilizofichikana.
Majuto yasiyoisha.
Watu wanacheka na wewe…
lakini ndani wanapigana vita usivyovijua.
Wengine hushindwa kuibeba kabisa…
wanakata tamaa ya maisha wanajiua.
Kuna hadithi ya watawa wawili walioweka nadhiri: “Hatutagusa mwanamke.”
Wakakutana na mwanamke hawezi kuvuka mto.
Mmoja akajizuia.
Wa pili akambeba, akamvusha, akamshusha… akaendelea na safari.
Baadae yule wa kwanza akasema hali ya kumgombeza mwenzie.
“Umevunja nadhiri!”
Jibu la Mtawa lilikuwa jepesi tu:
“Mimi nilimbeba pale mtoni nikamshusha…
WEWE BADO UNAMBEBA HADI SASA.”
Sio kila mzigo unaoonekana ndio mzito.
Mingi iko ndani… na ndiyo inaua kimya kimya.
Mzigo wa mwili anaweza kupewa Mnyamwezi…
lakini wa moyo ukikukamata, unakukandamiza peke yako.
Si kila anayenyamaza yuko sawa…
wengine wanatafuta nguvu ya kuvumilia siku iishe tu.
Usife na mzigo ambao ungeweza kuushusha kwa kusema.
Abuuabdillah ✍️
0744 883 353