Mizengo Pinda Waziri mkuu!


Hii Kali sana hahahahhaha umebariki week end yangu jamani....
 
Quite symbolic. Watu wanaanza majivu kuelekea pasaka, halafu Lowassa anafananishwa na yesu??? Hhahaa.
Ngoja nichukue biti ya Mr Yebo...
Kikwete umemfanya nini Lowassaaaaa, hana marketiiiii......
 

halafu,


kweli wikiendindo hii. nani original sasa au kila mmoja alifikiria hii kitu peke yake? lol
 


Outstanding post!! 🙂 🙂
 

I love JF. This has made my week end.
 
Duh,
Hawa wajomba kweli kibokooo!.... ama kweli JF jungu kuu!
 
Definetly..hii kali!Ni usanii wa hali ya juu!Hii inaonyesha kuna watu wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya nchi yetu kwa namna moja ama nyingine!Kwa wale wakristo..ni wazi wanaweza kuvutiwa na message..lakini at the same time ina maana Lowasa atafufuka kama Yesu?hopefully not!
 
NImeona maswali mazuri sana katika thread hii ambayo nadhani ni muhimu kupata jibu, naomba niongeze au nirudie baadhi:

1. Kwa nini EL alisisitiza kwamba yeye na MP wamefanana sana
2. Kwa nini wabunge wote wa CCM walimsifia EL na kusema ni shujaa etc baada ya ile aibu aliyopata?
3. Kwa nini MP alianza kumsifu EL nakusema ndiye aliyemkomaza?
4. Kwa nini MP alirudia sifa zake kwa EL baada ya kuchaguliwa na pia kutaja 'malezi' aliyopata chini ya Sumaye, Mkapa, Lowassa, etc
5. Kwa nini MP alisisitiza wasameheana?

Mimi sina majibu ya moja kwa moja lakini I am using my analytical skills na some information niliyopata from some insiders as follows:
- Mgawanyiko tulioona bungeni Alhamisi ilikuwa ni faction ya CCM asili na wengine walio nje ya Mtandao Maslahi wakionyesha makucha yao
- Alhamisi baada ya bunge kwisha kulikuwa na mvutano mkubwa sana kati ya kambi hizi mbalimbali. Walikuwa wana threaten tit for tat, kwani hizi story za EPA, Kiwira, Richmond, was leaked by different factions wakitaka kuonyesha kwamba the other awamu is more corrupt!
- MP alionekana ni mtu ambaye alikubalika na Mkapa camp, CCM asili camp na Mtandao camp.
- MP aliahidi kufunika mabaya yote, na alisema ya nyuma kuyasahau kwani ameahidi kuficha maovu yote ya CCM (Mkapa era, Kikwete era). Also ni kada mzuri wa chama, na kama kweli ni mtu wa usalama basi anafuata amri (he will not be a thinking man - not that EL appeared to be thinking).
- Mimi nadhani kilichobaki ni kujaribu kuelewa the politics behind kwa sababu watz tumezidi kuburuzwa na kuambiwa tusahau! Mimi sioni maendeleo yoyote in the coming years until 2010!
 
Susuviri,

Good analysis! M.K. Pinda is apparently the lesser of the devils, it is simply a well negotiated situation for impact mitigation!
 
Nimesisitiza kuwa tufurahi lakini bado tuwe makini..bado tuwe na mentality ya this is just the begining!Kikwete is very smart..inawezekana hii yote ni political game..kwamba walipanga matokeo..kwamba kujiuzulu huko kutaipunguzia serikali lawama za wananchi na pia kuonekana kuna uwajibikaji katika kipindi hiki ambacho Mr Kichaka anakaribia kutua bongo!Kujiuzulu ama kufutwa kazi haotoshi..haki itendeke kwa kuwahoji hao watuhumiwa wa ufisadi then wafikishwe kwenye vyombo vya sheria!Hii ni very important kuliko kujiuzulu kwa mtu yeyote yule!Kumbuka JK anajua namna ya kuwazuga wananchi..alimfuta kazi Balali..mambo powa..amepongezwa kwa sana!Sasa Lowasa hakuhojiwa..hivyo hawezi kushtakiwa..the same will happen with Balali!Narudia tena..KAMA KIKWETE ASIPOACHA VIINI MACHO MAMBO YARUDI PALEPALE!JUSTICE HAS TO PREVAIL!WAJIUZULU WANAVYOTAKA..ILA TUNATAKA HAKI..WAHOJIWE,WARUDISHE FEDHA WALIZOCHOTA,WARUDISHE MALI WALIZOIBA,WAFUTE MIKATABA WALIYOSAINI THEN SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE..THAT WILL THEN BE JUSTICE TO THE CITIZENS OF THE GREAT COUNTRY OF OURS!
 

I absolutely agree jmushi1, with everything you said except one thing that JK is very smart! He is NOT! What he is, is shrewd. They did not anticipate EL's resignation! I will tell you why.
- JK was allegedly planning different trips and preparing for Bush's trip when he was briefed by Speaker 6 that there's big trouble. They tried to mishmash the issue with that poorly executed excuse eti Spika anasafiri. Hivi naomba niulize kwanza wakati Bunge imeanza session after a loooong break na BUsh anakuja ni kweli Spika anaweza kuwa amepanga safari ya US? Hapana, they were trying to reposition themselves.
Walipoona Jumatano kwamba Mwakyembe ameweka kila kitu hadharani walijua mchezo kwisha! Ndipo alipoitwa na Shein aende Dodoma.
What happened is just damage control, nothing was planned. Viini macho walitaka kutuchezea na hiyo kamati ya uchunguzi wakijua hamna kitu lakini hawakutarajia that the committee will take themselves seriously (Damn these busy bodies Mwakyembe and co!)
Nakubaliana na wewe 100% kwamba wanafanya windowdressing and I have inside information that kila kukicha wanatafuta njia za 'kuwanyamizisha wapinzani' na 'kuwafurahisha wananchi'. Kitu cha kusikitisha ni vyema wangejivua fikra zao ambazo ni condescending and insulting wakidhani watanzania ni watoto.
I agree 100% - Richmond iendelee kujadiliwa bungeni na waanike. Ripoti kamili ya kamati iwekwe kwenye mtandao - it is public information!
 
Yote tisa, kumi ni pale ambapo Bush atajaribu kutamka "Jakaya Mrisho Kikwete, Ali Mohamed Shein and Mizengo Kayanza Pinda" back to back halafu baada ya dakika tatu ajaribu kutamka "Mwanamwema Shein"!!

Safi sana, ubantu udumu!!!
 

Kweli mkuu, lakini Pinda alikuwa naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaaa, wakati wa Sumaye alikuwa chini ya Ngwilizi, na kwa EL alikuwa full minister.

Kwa setting ya Richmond ilivyo, inaonekana EL alimudu ufusadi wa Richmond kwa kuwashinikiza watendaji na Viongozi wa Nishati na madni, wala si watu wake mwenyewe wizarani.

Ili tujue utendaji wa Pinda, lazima tutafiti aliyofanya TAMISEMI ndani ya uwezo wake. najaribu kutafuta hilo, ila hata wapinzani wamempa credit sana.
 

Mkuu, kamati imetoa mapendekezo. Haikuwa na mamlaka ya kumshitaki mtu. Ripoti ya kamati ilisema:

"Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mh. Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za kila siku za serikali na uongozi wa nchi kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuna wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile Vile ni wajibu wa bunge ambalo linathibithisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge."

Kamati pia imeliomba bunge kufikiria hatua dhidi ya wote waliohusika na utendaji mbovu.

Ninadhani ni wajibu wa bunge sasa katika mjadala unaoendelea kuilazimisha serikali kuandaa mashtaka dhidi ya watu hawa.
 
Niliposema kwamba ni very smart sikumaanisha kuwa ni smart kwenye kujali maslahi ya wananchi!Ni smart kwenye siasa za viini macho ambapo ameweza kujinasua kutoka kwenye uwajibikaji wa kashfa hizi baada ya kufanya mambo ambayo hakuna mtu aliyetarajia!Mambo ambayo yataleta gumzo na kumpa muda wa kuendelea kujipanga!kupunguza presha na kuendelea kujichotea mifwedha ya wafadhili!Bush pengine ataendelea kuwapa pesa kwasababu watajidai wameonesha uwajibikaji!Ni smart kwasababu mara zote kashfa zinapotokea yeye anachonganisha watu nakuendelea kuwafanya wacheze makida.. anasahaulika kuwa amehusika pia!Kwamba ana uwezo wa kucheza na siasa za viini macho kwa watanzania ambapo ameweza ku buy time!Ila nahisi kuna mahali atafikia atagonga mwamba..atakwama..kwasababu wananchi wamefunguka macho na wanataka kuona sheria inachukua mkondo wake zaidi ya kujiuzulu peke yake!wanantaka kuona fedha na mali zote zinarudishwa mikononi mwa wananchi!
BADO TUNAHITAJI ASIKILE VILIO VYA WANANCHI WAKATI HUU WA MISUKOSUKO!
Kwenda kwa spika marekani nafikiri ailikuwa aende kukutana na Balali..lakini Richmond ikambana!UWAJIBIKAJI SI TU KUJIUZULU..BALI PIA KUHOJIWA NA KURUDISHA MALI NA FEDA ZOTE!
 
HIZO KAMATI SOMETIME NI JANJA YA NYANI..WANAJUA EVERYTHING..Kikwete anabuy time kwasababu hana ubavu wa kuwashughulikia..hivyo anatafuta watu wengine kuwachonganisha..kama alivyofanya kwa wakina Mwema na Pinda!Sasa sijui watajibu nini mbele za wananchi kama wakishindwa kuwwleta hawa watuhumiwa mbele ya sheria!
 
Kwa maoni yangu..ninaweza kusema kuwa kuna sababu mbili ambazo zinaweza kuwa zilitumika na Kikwete kumteua Pinda;
Moja ni uzoefu wake kwenye masuala ya kisheria..hii itamsaidia kuwaleta mafisadi mbele ya sheria bila kuvunja sheria!Hapo wananchi tuko upande wake!
Sababu ya pili inatia shaka..Huyu Mh Pinda kwanza kabisa ni mjamaa..then usalama wa taifa!Hizo sifa zinamfanya kuwa ni mtu msiri na unayeweza kumtegemea kwenye kurudisha nidhamu na kurekebisha loop holes ambazo zilisababisha news za ufisadi na mikataba mibovu kuvuja!Huyu jamaa anajua mambo mengi sana!Ila taarifa zinadai kuwa anaonekana ana mawazo mengi sasa na kwakuwa ana sifa ya uadilifu..then anaona itakuwa mzigo mkubwa kuwashughulikia mafisadi ambao amekiri kuwa ni watu wake wa karibu..kama vile Chenge etc!Htaweza kuchukua ushauri mwingine zaidi ya ule wa Mzee Mwiru!Akiwa mjanja atachukua ushauri wa Butiku ambaye wanafahamiana vyema na walifanya kazi pamoja chini ya Mwalimu kwa muda mrefu!
 
Susu,

Angalia majibu yangu ndani ya nukuu yenye rangi ya chama (kijani)


Mpanda Merikebu alitoa hoja tuwe na tume kama ile ya Afrika Kusini: Truth and Reconcilliation. We are in desparate need of this otherwise we are not going to make progress and everyone will be looking to revenge or protect themselves!
 



Pongezi kutoka kwa wabunge







Mapaparazi hawakuwa nyuma katika kurekodi siku hii ya kumbukumbu laivu






Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisubiri kuapishwa kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma jana.
Wengine kutoka kulia ni Makamu wa Rais, Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar, Amani Karume,
Waziri Kiongozi wa Zanzibar,Shamsi Nahodha , Spika wa Bunge, Samwel Sitta, Waziri Mkuu Mstaafu,
Edward Lowassa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika









JK akimwapisha waziri mkuu mpya mh. Pinda Chamwino leo,
amekubali kuitetea Katiba kwa haki na uadilifu . Kazi iliyomshinda EL!


President Jakaya Kikwete swears in Mr Mizengo Pinda new Prime Minister at the Chamwino State lodge in Dodoma Saturday. Looking on on President Kikwete's right is the Chief Secretary, Mr Phillemon Luhanjo.







Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Rehani Pinda (shoto) akiongea na mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata katika sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilizofanyika ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma leo






JK akisalimiana na baba wa waziri mkuu mzee Xsavery Kayanza Pinda Ikulu ya Chwamino leo mara baada ya jk kumwapisha mwanae kuwa waziri mkuu. katika ni mama mzazi wa waziri mkuu bibi albetina kasanga.




Fadhila ya Punda .......... .........








Kaka Mikoba ndio hiyo


Michuzi Blog
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…