Siku hawa viongozi waliopo madarakani in this case pamoja na muheshimiwa Pinda, watapo kubali ukweli kuwa, nyerere ndie alyeifisadi hii nchi kwa maamuzi yake mabovu, yote kwa muono wangu, kwani sijaliona jema hata moja la nyerere. Hapo ndipo kutakuwa na mabadiliko ya kweli. Haya masalia ya warithi wa nyerere ndio yanayozidisha matatizo kwenye nchi hii, kwani ikiwa kiongozi yeyote ataetuongoza anamuona nyerere hakuifisadi nchi hii, ingawa alituwacha tu masikini wakutupwa, basi sijui, sijui kiongozi kama huyo anajuwa ufisadi ni nini! Simply, kinachotakiwa ni viongozi wenye muono tofauti na itikadi za kinyerere. Za kumfanya kila mmoja awe masikini, masikini wa kutupwa.
Leo Tanzania, miaka karibu hamsini baada ya uhuru, ukitazama huduma za afya unatamani kulia na wenyewe wenye nchi hata mafuwa wanakwenda kujitibu nje ya nchi, wote kuanzia nyerere mwenyewe mpaka leo. Maji, wakati nyerere anapewa hii nchi, tulikuwa tukinywa maji ya bombani bila kuchemsha, leo inawezekana hilo? Elimu, hatari tupu tunaona ni hao watoto wa wenye nchi ndio wanapelekwa kusoma nje ya nchi, kwa nini? elimu yetu ni duni na wanajuwa hilo. Aaah alimradi kila kitu hohehahe, kuanzia uongozi mpaka huduma zote, nyerere kaziacha nyang'a nyang'a na bado tunaimba kila siku "baba wa taifa" mimi nasema tuimbe "baba wa ufisadi". Pinda anatokea huko-huko, hakuna jipya ataloleta. Labda akubali kuwa nyerere ndie alikuwa muasisi wa ufisadi na fisadi mkuu wa kwanza aliyeitia nchi hii kwenye lindi la ufukara na umasikini na uomba-omba na ufisadi wa kina. Akilijuwa na kukiri hilo, hapo kweli tutaona mabadiliko.