Mizengo Pinda: Serikali ibadilishe mfumo wa Elimu na Watoto wasiendelee kudanganywa kwamba kuna ajira

Ajira zipo ila Ni kwa watu wachache,Sina imani Kama watoto wa viongozi na vigogo wa chama chetu pendwa Kama Ni wahanga wa ajira pia
 
Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kukosa ubunifu wa kutengeneza ajira. Kuwasukumia vijana kwenye ujasiliamali na kujiajiri hakutaweza kukidhi mahitaji ya wananchi kwani fursa zenyewe ni chache.
 
Mapoli, Ardhi yenye rutuba, ardhi yenye madini chini, mito, maziwa, bahari, mbuga za wanyama nk hivi vyote vinahitaji fikra pana ili kutanua uwanja na mwisho kutoa mamilioni ya ajira..

Mifuko ya hifadhi ya jamii inunue meli za uvuvi bahari kuu, izikodishe kwa private companies, ijenge viwanda vya kuprocess samaki ivikodishe kwa private companies, samaki fresh and processed wauzwe worldwide as Tanzania product..

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara itafute wawekezaji wajenge viwanda vya juice vikubwa Tanga na Pwani, wananchi wawezeshwe walime kibepari kufeed hivyo viwanda through out the year..the same to mbogamboga, maua nk..

Vitu vingi sana aisee Serikali inaweza kuvipromote na kusimamia na uwanja ukawa mkubwa kiasi cha kutengeneza mamilioni ya ajira..
Kuna siku nilinunua juice ya embe iko kwenye chupa, ughaibuni.

Sasa huwa naoenda kusoma chupa kujua zaidi kuhusu kinywaji.

Katika kusoma nikagundua ile juice ya embe imetengenezwa Egypt.

Nikawaza, Egyot ni nchi ambayo sehemu kubwa ni jangwa. Sehemu inayofaa kwa kilimo ni akama 3% ya ardhi ya nchi.

Na wana export juice ya maembe.

Sisi ardhi inayofaa kulima imejaa tele lakini sijawahi kuona juice ya Tanzania inauzwa ughaibuni.

Ukienda kwa majirani hapo Kenya tu, wanauza maua ya mamilioni ya dola kika siku. Mwaka 2017 Kenya ineuza maua ya US $ 800 million.

Mwaka huo huo, zao la biashara linaloongoza Tanzania, korosho, liliingiza US $ 530.

Maana yake korosho zetu zin
Mezidiwa vibaya sana na maua ya Kenya.

Sisi tumezidiwa nini hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda ameishauri serikali kubadili mfumo wa elimu ili wanafunzi wajikite katika stadi za ufundi na ujasiriamali.

Mzee Pinda ametahadharisha kuwa siyo vema watoto wakaendelea kudanganywa kuwa kuna ajira wakati kiuhalisia ajira ni chache sana.

Pinda alikuwa anafunga kongamano la wawekezaji mkoani Songwe.

Chanzo: ITV habari

My take: Nimeupenda ukweli wa Pinda, msema kweli ni mpenzi wa Mungu!
Lakini mzingira ya biashara siyo mazuri kutokana na sera ambazo hazidumu sera za majukwaani(nyuma ya mikamera) ni tatizo 'policy uncertanity' or regime uncertainty
 
Unamuonea mzee wa watu bure, maana kasema kwa Sasa ajira hazipo hivyo Basi mfumo wa elimu ubadilishwe ili watu pia wawe na uwezo wa kujiajir, hayo n mapendekezo yake Kama hutaki endelea kusoma Songhai empire yako ukimaliza kaitumie mtaani.
johnthebaptist,
Huyo mzee anachekesha ile mbaya, hakuna ajira huku yeye anajipendekeza kwa Magufuli kila siku ili apewe ulaji na serikali. Atuonyeshe watoto wake na wajukuu wanafanya wapi kazi ili tuone kama wamejiajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kukosa ubunifu wa kutengeneza ajira. Kuwasukumia vijana kwenye ujasiliamali na kujiajiri hakutaweza kukidhi mahitaji ya wananchi kwani fursa zenyewe ni chache.
Jk alijitahidi angalau kupunguza ila awamu ya kukaza vyuma ni sawa na kiwanda cha kuzalisha umasikini
 
Albert Einstein alisema kuwa "We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them"

Mizengo Pinda ni sehemu ya tatizo, hana haki ya kuwa sehemu ya majawabu ya unemployment. Halafu kutwa kulamba viatu vya JPM ili ampe ulaji kwa njia ya trip na uwenyekiti wa Bodi.
Vyuma vimewakazia Wamebaki kuimba mapambio hawawezi ishi nje ya kubebwa
 
Mwambieni Mzee Pinda atoe solution na sio kupiga blah blah, kama mtu aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa anapaswa kufikiri mara 1000 ya hapo aje na solution anayoweza hata kushauri taasisi za maamuzi..Tanzania bado haijawa nchi yakuwa na tatizo la ajira watu wasikimbie majukumi wafikiri na kuzitengeneza hizo ajira..
Solution yake yeye ni kubadlishwa kwa mfumo wa elimu ambao utamjenga mwanafunz kujitegemea yey kam yey katka ishu za ajira
 
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda ameishauri serikali kubadili mfumo wa elimu ili wanafunzi wajikite katika stadi za ufundi na ujasiriamali.

Mzee Pinda ametahadharisha kuwa siyo vema watoto wakaendelea kudanganywa kuwa kuna ajira wakati kiuhalisia ajira ni chache sana.

Pinda alikuwa anafunga kongamano la wawekezaji mkoani Songwe.

Chanzo: ITV habari

My take: Nimeupenda ukweli wa Pinda, msema kweli ni mpenzi wa Mungu!
Angemalizia kuwa zilizopo ni kwa ajili ya WATOTO WETU TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapoli, Ardhi yenye rutuba, ardhi yenye madini chini, mito, maziwa, bahari, mbuga za wanyama nk hivi vyote vinahitaji fikra pana ili kutanua uwanja na mwisho kutoa mamilioni ya ajira..

Mifuko ya hifadhi ya jamii inunue meli za uvuvi bahari kuu, izikodishe kwa private companies, ijenge viwanda vya kuprocess samaki ivikodishe kwa private companies, samaki fresh and processed wauzwe worldwide as Tanzania product..

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara itafute wawekezaji wajenge viwanda vya juice vikubwa Tanga na Pwani, wananchi wawezeshwe walime kibepari kufeed hivyo viwanda through out the year..the same to mbogamboga, maua nk..

Vitu vingi sana aisee Serikali inaweza kuvipromote na kusimamia na uwanja ukawa mkubwa kiasi cha kutengeneza mamilioni ya ajira..
Wana akili za aina hii sasa? Wao wanachojua ili waendelee kutawala inabidi wanunuwe wapinzani
 
Back
Top Bottom