Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Tanzania ni muungano wa nini na nini mkuu? Kua makini kwenye jibu Mu.lugo alikosea hili
Ndiyo maana Mizengo Pinda akauliza Tanganyika gani kwa sababu kwenye huu muungano kuanzia tarehe 26 April 1964 kulitokea Tanzania Bara na Zanzibar
 
Mimi naona jambo la muhimu kwa sasa ni kuangalia upya mfumo huu wa serikali mbili na kuufanyia marekebisho lakini mfumo wa sijui serikali Tatu,Nne ,Tano Mara shirikisho ni kujiongezea matatizo yasio ya msingi
na vipi ikiwa serikali moja, zanzbar iwe ni mikoa tu kama mtwara au kigoma.. hiyo imekaaje
 
Ukisikia janga la taifa ndio hili, Tunajua Tanganyika wamesha uza, maneno tuliyokuwa nchi imeuzwa ooo imeuzwa kumbe ni Tanganyika? Nashukuru sana Pinda kwa kufafanua, Tumesoma vitabu mzee tunaambiwa muungano ni watanganyika na Zanzibar na ninakumbuka zamani tulikuwa tunasherehekea uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 sio Tanzania Bara, Kweli leo nimeamini Tanzania hakuna wasomi maana tunadanywa hata kwenye Elimu,

nikijiuliza Zanzibar ni muunga vilevile, Unguja na Pemba, Mbona unguja ipo na Pemba Ipo kwanini Tanganyi ife? Zanzibar iwepo? Na kama Pinda anasema Tanganyi ipi tunataka? Yeye alizaliwa kwenye nchi inayotwa Tanganyika? Au Tanzania Bara? Maana kazaliwa kabla ya uhuru wa Tanganyika,

Jamani naomba niishie hapo maana nisije kutukana maana naona hapa hawa viongozi bado wanatuona ni wale wale wa kuambiwa ukichagua upinzania wataleta vita, yaaani bado wanatuona hatuna akili wametubebea, Wanachi wanataka Serikali tatu, ni maoni yao na wenyine muungano wa mkataba ni maoni yao, Sasa inakuwaje maoni ya CCM yawe mjadara? Na kwanini wajione hii nchi yao? Kuna maoni ya makanisa vyama vya Siasa vyote vilitoa maoni, jumuiya ya Waislamu, Sekta binafsi na makundi mbali mbali, wametoa kwa maandishi, je wote wasimamie kwenye maoni yao? Wasiifate tume ambayo ilikaa na kuyachambua maoni na kuona ni yapi yanafaa kuwepo? Kama wanataka basi tume ya katiba ilicho kifanya kiondolewe na waweke wanachotaka wao maana inaonekana tume walitutengenezea kwa danganya toto,
tusubiri tuone tutpata nini pale lakini sifikirii kupata kitu cha maana katika Bunge hili maana ccm kama watoto, oooo mara posho ndogo nina uhakika wanataka kuvuruga mchakato soi bure

aksante
 
Ukimwona muulize eti kama Zanzibar ni nchi yenye katiba na mipaka yake, je upande wa magharibi imepakana na nchi gani?

Mkuu Ntakasi atakuwa anaifahamu!
Pia atuambie JMT, hiyo "M" - Muungano inamaanisha nini na nini viliungana?
Asituletee Muunhano wa Mlugo
 
Mkuu ukisema tunadai TANGANYIKA tusioijua kwakuwa tumezaliwa hatukuikuta unamaanisha Historia ya Nchi yetu iliyo ktk vitabu na kumbukumbu mbalimbali ni uwongo?,km jibu ni historia yetu ni ya ukweli mjue wengi wetu tumeisoma na kuelewa na ndio maana wananchi wengi wamependekeza serikali tatu,na kama ni gharama hakuna chama kinacholipa ni wananchi wenyewe tutaigharamia hilo wengi waliliona na ndio sababu ya kuamua serikali TATU.
 
Sisi tunaitaka Tanganyika asoitaka yeye.
Wamesimamia kuua muungano kwa kuruhusu Zanzibar kuwa na katiba inayomuondolea rais wa muungano mamlaka kwenye masuala ya muungano dhidi ya Zanzibar,.saa hizi bila aibu wanaleta taarabu.
Sasa wanataka kutufanya tuamini nini zaidi ya usanii, tuitaka Tanganyika haijalishi ulikuwa umeoa au unalima au unadoma au unamiaka kumi.
Hili kosa liwafuate kote mtakapokuwa, msitulazimishe kuonekana vichaa kwa uzembe wenu mloutenda wa kulegeza misingi ya Muungano.
 
Hii nchi inakoelekea sio kuzuri, serikali bila aibu inalazimisha serikali 2 wakati wanajua wazi serikali ya Tanganyika haisurvive? Mbona Zanzibar wanakatiba yao, bendera yao na kila kitu cha msingi wanacho na bado wanatunyonya kwa kutumia raslimali zetu? Tunaitaka Tanganyika yetu! Wala hatuna haja na muungano wenu rudini pemba/unguja na waliopo zenj warudi kwao Tanganyika!
 
Namuunga mkono moja kwa moja eti mtu ana miaka 25 eti kwa sababu kapata tiketi ya kuingia bungeni kama mjumbe unasikia anasema serikali Tatu wakati hata wakati Tanganyika inapata uhuru hakuwepo,Pinda nakupongeza kwa msimamo wako thabiti

Hizi ni dalili za kupata katiba ya watanzania tena iliyonzuri sana kwa uma wote wa watanzania.

Hongera Pinda. Watanzania tupo nyuma yako

Ukiishi na kichaa utagundua kwamba kuna siku anazungumza ya maana utadhani kapona, kumbe ni hali ya kubahatisha tu! Ninyi watu huyu Pinda wenu mbona hakuna siku anayobahatisha? Ajabu munaunga mkono!

Kwa nafsi ya Uwaziri mkuu, ni kweli hajui rasimu, inaposema Tanganyika ina maana gani? Hilo nalo ni la kuwauliza wa TZ?
Munapomshangilia mtu huyu munadhani kapona au nanyi muko kundi moja?

Unahitaji kuwa mzee ili kujua umuhimu wa serikali ya Tanganyika? munapohitaji serikali mbili, munafahamu ni mbili za aina gani? Au munadhani kuna mwenye akili mwingine atakayewasaidia kuzipanga upya hizo mbili baada ya kuwa imeshindikana kwa miaka 50.

Kichaa anayesema tulizaliwa na kukuta serikali ya Tanzania, huyo waziri mkuu wenu alikuta ipi? Mbona kasahau mbona kasahau suti za vitenge na T-shirt nyeupe?

Serikali 3 zije, ikishindikana muungano ufe. Hatuhitaji ujanja wa ki-maimuna ktk muungano!
 
Ndiyo maana Mizengo Pinda akauliza Tanganyika gani kwa sababu kwenye huu muungano kuanzia tarehe 26 April 1964 kulitokea Tanzania Bara na Zanzibar
Na sisi tunamrudishia swali.

Je,Tanganyika ilikufa tarehe 26 April 1964?

Kama jawabu ni ndiyo basi hatutaki longolongo atuonyeshe tu hiyo document ya kifo cha Tanganyika.

Nafikiri katika uchaguzi ujao CCM wanahitaji kupumzishwa angalau kwa miaka mitano ili tuwaone wapinzani nao wana nini cha kutupatia katika miaka mitano hiyo.
 
Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana,” alisema Pinda.

Mbona Tanganyika ina ndugu wengi tena si wa kuoleana ni wa kuzaliana, mifano ni wamasai kati ya Tanganika na Kenya, Uganda, Burundi n.k


Hoja ya udugu haina mashiko
 
Mi nataka Serikali moja tu, tena iwe na vision ya kutuunganisha na si kutugawanya kama Pinda na CDM wanavyotaka.
 
Kunashida moja ya watanzania kutotaka kujielimisha na kutafuta ukweli ndiyo maana wengine hubeba jambo hata kama halijui undani wake.

Nchi zilizoendelea ni ushahidi wa kuwa na watu wenye akili.Tanzania haijaendelea kwa sababu watu wetu wengi sana hawana akili/hawajui namna ya kufikiri na kupata majibu ya matatizo yao.wengi wao walikaririshwa tu mambo shuleni anzia viongozi na wanao ongozwa.Katika hali kama hiyo katiba nzuri itatoka wapi?
 
Ha ha ha Pindaaaa.. 😉

Hivi kila 9 December huwa tuna sherehekea nini?

Tanzania ilizaliwa na Nchi ngapi??

Naona Viongozi wana-majibu kabla ya bunge kuanza..Inatisha sana..
 
Back
Top Bottom