Mizengo pinda kuonana na madaktari ili kumaliza matatizo yao...

Hili siyo suala la Waziri Mkuu asiye na nguvu; hili ni suala la Rais na CCM kama chama tawala; Madaktari wasikubali kugereshwa kwa maneno ni lazima Rais ndiye akutane nao na CCM ibadilishe sera zake kwenye hili suala.

aha!wanafuata protocol!
 
Dr Ulimboka na wengine, kazeni uzi. Hakuna kukubali mpaka kitu kinatoka kwa maandishi. Tena siyo maandishi ya Blandina. Na isiwe kwa ahadi za Pinda et al.

Baada ya Pinda kuonyesha dharau awali kwa kutokutana na madaktari, Kikwete kaonyesha kubwa zaidi kwa kuonyesha anavyoweza kutumbua pesa ya Serikali. Tena si hiyo posho wanayotaka kama on-call allowance, yeye anatumia milioni 300 kwa siku 4 na msafara wake. Kikweta kagoma kabisa kujifunza nini matokeo ya kiburi cha Mwinyi na ushauri wa wakina Diria kwenda Uwanja wa Taifa kuangalia Isambe ya Kanda Bongoman na ulinganisho wa yanayojili sasa.
 
Hivi Pinda ana rekodi gani ya kujivunia tangu awe PM?

Jamaa anauzoefu wa kuwarudisha wahadhiri wa UDOM madarasani ila baada ya hapo chamoto wanakiona,wanafukuzwa mmoja baada ya mwingine...nasikia mpaka jamaa mmoja alikuwa mwenyekiti wao kapigwa chini mwaka jana mwishoni..madaktari muwe makini na huyu jamaa,anajua sana kuongea na kubembeleza watu.
 
Ni lazima aje na majawabu mezani na utekelezaji. Msikubali porojo.

Kila mmoja anaweza kuwa mwanasiasa hata kuwa rahisi wa nji lakini sio wote wanaweza kuwa madaktari.

kataeni kudharauliwa na kupuuzwa kiasi hcho.
 
Naamini asipokubaliana na madai yao wakati keshaidhinisha malipo ya Tsh 200,000/= kwa wabunge, patachimbika.
 
Pinda Pinda, utapanga kukutana na Madaktari au ulitakiwa uwe umesha kutana nao tangu last week?? Hembu acheni kunyanyasa watanzania maskini jamani, au kwa vile nyie mnajua kuwa ukipata maumivu kidodo tu ya uchovu wa safari unapelekwa Apollo? Si unajua kuwa kuna mgomo unaendelea na watanzania masikini hawapati hudma za afya? Unasema utapanga badala ya kutangaza kuwa unakuta nao kesho?? hembu muwe na haya ktk nyuso zenu jamani, ni aibu kubwa, yaani ni sawa na kutembea uchi mbele ya Wakwe zenu. Acheni aibu hiyo onana na madaktari kesho, Shame in you Serikali, lohh.
 
msikimbilie kutoa majibu/kumjibia mwacheni Pinda ajibu kisha tumhukumu

mbona ameshajibu! Ukiona mtu anatanguliza huruma ndo muanze kutatua matatizo huo ni uzushi. Huwezi kuniambia nisaidie wagonjwa sehemu ambayo haina gloves,dawa,syringe, xray,fluids ukategemea mi nikukubalie kirahisi. Ubovu wa hii serikali wanashindwa kusema pesa wametungua zote,wanafanya kazi ya kuchonganisha doctorz na wananchi. Madai yote ya madactari yapo tangu 2007,mwaka huu imeongezeka ya mgogoro wa intern. Kwani wao hawajui kwamba hospitali ni mbovu,hazina vifaa? Wameingia mikataba mibovu ya kuleta madaktari kutoka india kila mwaka wakija hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kutuibia, wanapelekana india kwa pesa kubwa ya serikali hata kwenda kutibiwa social phobia! Sasa hivi wanalipana posho za milion 10 kwa mwezi kwenda kupiga meza. Hizo pesa si zingenunua sophisticated instruments kwa ajili ya mnh? Ikipatikana chance ya kununua wananunua fourt hand kwa gharama ya brand new, nani muuaji kati yao na madoc? Hakuna kurudi nyuma mpaka hospitali ziboreshwe,maslahi yetu yazingatiwe,ili afya za mlipa kodi wa nchi hii iwe imara. Eti kazi ya wito, wito!!!!? Tupeni vitambulisho vinavyoonesha tunafanya kazi ya wito ili kila sehemu tuwe tunapata huduma bure. Na kwenye kikao akileta ujina tunamzomea mpaka ajione mavi!
 
kama kuna sehemu ambayo Pinda huwa anafanikiwa basi ni katika kunyamazisha mutiny (uasi). Hawa madaktari watamsikiliza tu, na sijui ni kwa nini
 
kama kuna sehemu ambayo Pinda huwa anafanikiwa basi ni katika kunyamazisha mutiny (uasi). Hawa madaktari watamsikiliza tu, na sijui ni kwa nini

unamaanisha doctors ni waasi? Ndo nyie mnavaa tisheti za chama mnatiwa vidole machoni mchana kweupe,mkiugua mnaishia kulalamika hakuna dawa hospitali!
 
Hili siyo suala la Waziri Mkuu asiye na nguvu; hili ni suala la Rais na CCM kama chama tawala; Madaktari wasikubali kugereshwa kwa maneno ni lazima Rais ndiye akutane nao na CCM ibadilishe sera zake kwenye hili suala.

Ha ha ha ..unajidai hujui kazi za waziri mkuu wa Tanzania au una obsession na rais wetu..(punguza vikao vya jumuiya) lol
 
The way nilivyokuwa namchukulia pinda hapo awali ni tofauti kabisa na ninvyomchukulia kwa sasa. Wakati anateuliwa kuwa PM kwa mara ya kwanza niliamini kuwa amepatikana PM makini, mwenye maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma. Kumbe sio kabisa, yani hakuna la maana alofanya la maana analoweza kujivunia tangu apewe mamlaka hayo muhimu. Labda afe ndo aanze kusifiwa kama ilivyo kawa, hasifiwi mtu akiwa hai hadi afe!
 
Kwanza kwa nini ajibu leo?
Lakini pia si walisema hakuna mgomo?! anyamaze tu basi kama alivyokuwa juzi na jana!!

Infact maDR wawe makini, jamaa anatafuta namna ya kubuy time tu wapate wasaa wa kuwagawanya. kuweni makini sana! After all jamaa hana meno!
 
Wamkatae huyu mleta porojo..maana hana jipya wangemtaka yule vasco da gama waongee nae na sio huyu asiye na meno "hadi rais atue"!!

Huyu Vasco Dagama [mkweree] amesepa kwani yeye hapendi mambo magumu magumu ndio maana amepeleka faili la posho za wabunge na hili la madaktari kwa Pinda!! Anafanya hivyo ili kuepusha lawama kama wakati ule wa Mwalimu alivyokuwa anamtumia Kawawa ili mambo yakiharibika lawama asipate yeye ingawa yeye ndio mwenye wajibu wa kuyashuhulukia mambo hayo!!
 
Back
Top Bottom