Mizengo Pinda, Blandina Nyoni na Haji Mponda Wawajibike! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengo Pinda, Blandina Nyoni na Haji Mponda Wawajibike!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DALA, Feb 8, 2012.

 1. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 874
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 80
  Katika mazingira ya kawaida kabisa kwenye nchi yeneye uwajibikaji watu kama Mizengo Pinda, Haji Mponda, Blandina Nyoni na Anne Makinda wote wangejiuzulu mara moja nafasi zao!

  Inawezekana vipi kiongozi tena anayeongoza shughuli za serikali bungeni atumie ubabe kushughulikia matatizo na malalamiko ya madaktari eti wasiporudi kazini watakuwa wamejifuta kazi? Huyu ndo anayejiita mtoto wa Mkulima kweli asiyejua matatizo ya wakulima?

  Dkt Haji Mponda amepoteza hadhi ya kuwa waziri katika wizara ya afya kwa kushindwa kutoa majibu na suluhisho la matatizo ya madakitari! Inakuwaje tumefikia hatua hii ya kutokuchukua hata hatua alafu eti wanazunguka kila kona ya nchi kusherekea miaka 35 ya chukua chako mapema tena kwa gharama kubwa na karama za kufuru!

  Ingekuwa serikali yangu, ningeuda kama ya mtu mmoja tu wa kutathmini na kujua madhara ya kauli ya Mizengo Pinda, nafasi ya Blandina Nyoni na Haji Mponda na kisha kuwafikisha mahakamani!
  Tufike mahali tuseme ukweli JK ametufikisha pabaya zaidi na hii serikali yake isojuwa hata chembe cha uwajibikaji!

  Niko Jamvini!
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  mtoto wa mkulima utamuoneka bure; anatumwa cha kusema!!. hana hatia.
   
 3. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kama uliuwa kwenye akili yangu, nimeamka asubuhi nawaza hili suala la madoc na kauli za hawa watawala kwakweli nikasikia moyo wangu umeumia sana, nikajiuliza hivi watu kama misri walianza vipi maandamano mbona watanzania wagumu sana au hawaoni haya matatizo au tumezaliwa na uoga ndani yetu, kwakweli inaleta hasira za kimapinduzi, wazazi wetu wapata tabu kama wapo jangwani, watawalai wanachekelea kwa kauli za kibabe kama tupo vitani,..inatisha na tunako elekea kwa watawalai wa namna hii itatisha zaidi
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ni heri angeenda kulima kwao kuliko kuwepo nafasi ambayo wewe huna say.
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Actually Blandina ndio kikwazo katika sekta ya afya.. sijui anangoja nini kuachia ngazi
   
 6. m

  mahangu Senior Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nchi hii haina utawala bora ndugu yangu, si unaona akina Ngeleje wapo tu madarakani wakati wizara yake ilishachafuka kwa kuchangishs hela za kuwalainisha wabunge wapitishe bajeti yao? Jiulize Katibu Mkuu ( Jairo) angewezaje kufikiria kuwalainisha wabunge bila kupanga mipango hiyo na waziri wake? No good Governance in Africa!
  Wacha twende hivyo hivyo hata kama watu wanapoteza maisha kwa kukosa huduma za afya, wacha watu wale maisha. ulifikiria jana Mhe. rais angeenda kwenye ile hafla ya kuongea na Msumbiji kuhusu mambo ya ulinzi? Rais haingilii kati mgogoro wakati anajua fika PM ameshindwa, je anasubiri kutafuta nafasi mwisho wa mwezi kulionglea wakati watanzania wengine watakuwa wamekufa, wengine ugonjwa umeenea?
  Mungu tusaidie tusichague tena viongozi wasiojali maisha yetu
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Tunakubali kuwa kuna tatizo lakini kuwahukkumu wote kwa kapu la mgomo wa madaktari is not fair. Naanza kuona kama kunakuja political assassination exercise kwa baadhi yawatu hapa, to me most of them are innocent.

  Wamalize hili tatizo maisha yaendelee bwana.
   
 8. Glue

  Glue Senior Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hawa watu wanatakiwa wawajibike kwa wananchi. Na hakuna njia nyingine ya kuwajibika zaidi ya ya kujiuzulu nyazifa zao maramoja ili kuokoa maisha ya watanzania wanaoteseka kila kukicha.
   
 9. Glue

  Glue Senior Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Alafu jamani wanaharakati ili kutimiza adha hii ya kuwawajibisha hawa watu, tujongee pale LHRC tupange mikakati kwa pamoja.
   
 10. i

  isoko Senior Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duh balaa
   
 11. T

  Tanganyika2 Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ANGALIENI HALI ILIVYO MUHIMBILI HAPA:

  Hali inavyotisha Hospitali ya Taifa Muhimbili | Facebook
  NASIKIA KUNA WATU WANAKUTANA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY SASA HIVI JAMANI SHIME...
   
 12. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  tatizo nasikia ndani ya magamba na wabunge wa magamba hakuna mbadala.yaani utawawajibisha hao then nani ambaye ni msafi atachukua nafasi zao.wote magamba hayana mbadala labda JK akiamua kutoka nje ya mfumo wa magamba kuchagua wateule wake.Uwajibikaji ndani ya magamba HAKUNAGA :embarassed2:
   
Loading...