Waziri Mkuu Pinda na Samweli Sitta wanamhujumu Rais Kikwete

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Waziri Sitta akiwa anatambua kabisa kwamba nchi ipo katika hali ya dharura, kutokana na mgomo wa mabasi, hajachukua hata hatua moja ya kushughulikia hali hii. Tulitegemea katika hali hii ya dharura, waziri mwenye dhamana ya uchukuzi angechukua hatua ya kubadilisha ratiba ya train ili angalau train zitoe huduma ya usafiri kwa wananchi katika kipindi hiki kigumu. Lakini cha kushangaza, train zimeendelea na ratiba zake za kawaida, huku ile ya Tazara hadi kigogo ikiamua kufanya safari moja badala ya mbili jana jioni.

Mgomo huu wa daladala na mabasi ya mikoani umesababishwa na uzembe wa Sitta. Sitta alijua kabisa kwamba mgomo ule wa kwanza uliahirishwa mnamo saa saba mchana baada ya ahadi za kisiasa za waziri mwenzake wa kazi na ajira, lakini yeye akijua kabisa kwamba ndiye mwenye dhamana ya usafiri nchi alikaa kimya. Hata pale madereva walipotangaza kufanya mgomo mwingine Sitta hakuchukua hatua zozote.

Mimi napata shida sana kumuelewa Sitta, ni kama vile anamhujumu Kikwete. Maana amepewa dhamana ya kuandaa katiba, akaivuruga tu kulingana na alivyojisikia yeye, alipokuwa wizara ya afrika mashariki alikuwa anatoa matamko ya hovyo hovyo tu ilimradi avuruge mambo. Ndiye huyu aliyediriki kusema Tanzania itaweza kuanzisha umoja na Burundi pamoja na Congo kwa kuwa Kenya, Uganda na Rwanda walikuwa wanafanya mambo bila kushirikisha Tanzania.

Lakini ameingia wizara ya uchukuzi, pia anafanya mambo hovyohovyo tu hata kama anajua anao uwezo wa kuyashughulikia. Najiuliza hivi mzee Sitta alishindwaje kutumia hata japo robo tu ya ubongo wake kufikiria kwamba mgogoro huu wa madereva ungeweza kuwa mkubwa kama usingeshughulikiwa? Jana anakuja eti na hoja ya kwamba ukosefu wa kamati ya kudumu ya maridhiano ndiyo sababu ya huu mgomo. Kwani tangu walipoanza malalamiko kule mwanzo kwanini hakuunda hiyo kamati. Sitta ni waziri Kimeo sana, inashangaza kuona kwamba anautaka na Urais. Mtu huwezi kushughulikia matatizo ya dharura ya nchi utawezaje kuwa Rais?

PINDA, SITTA WAENDELEA KUMUHUJUMU JK

Leo mgomo wa madereva wa mabasi na madaladala umeingia siku ya pili ukiendelea kupeleka mateso, maumivu, karaha na majuto yale yale kama ya jana kwa Wananchi.

Mgomo huu unaofanywa na madereva kupeleka vilio vya kwa serikali kwenda kusona na kutoa laki 5 kila baada ya miaka 3 ya ku renew leseni zao na pia pia kuiomba serikali kuisimamia mikataba yao ya uajiri kwa mabosi wao.

Madereva hao wanefikia hatua ya kugoma ili kutaka kukutana na Waziri mkuu Mizengo Kayanda Pinda ili atoe tamko la madai yao kutokana na kuchoshwa na wanavyonyanyaswa.

Badala ya Waziri mkuu Pinda kuamua kukutana na madereva aliamua kukutana na Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta tofauti kabisa na matarajio ya madereva.

Badala ya Pinda kuamua kutoa kauli ya kuamua hatma ya madai yao, akaamua kuunda tume licha ya kuwa alishapelekewa report zote za urasimu mkubwa wa SUMATRA. Huku ni kupoteza muda na kukoleza kwa matatizo na ukali wa mgomo huu.

Ikumbukwe tume hii iliyoundwa na Pinda itakuwa na kazi moja kubwa ya kutafuna mamilioni ya shilingi za walipa kodi wakati uchunguzi ulifanywa, kila kitu kipo wazi kilichokuwa kinasubiriwa na maamuzi magumu na sahihi kufanywa jambo ambalo Pinda ameonyesha siku zote kulikosa katika uongozi wake.

Mara baada ya Pinda kukosa uamuzi mgumu wa kumaliza tatizo hili la mgomo wa madereva aliamua kuhamisha na kuendeleza tatizo kwa kuunda tume na kisha yeye kwenda kupumzika (kulala) Mwanza na asubuhi ya leo amekwenda Musoma. Huku ni kukosa maamuzi magumu na sahihi yanayoashiria kutaka kumuhujumu Rais Kikwete ambaye naye yupo nje ya nchi ili aonekane nchi imemshinda kuiongoza.

PINDA nisaidie kujibu haya:

Hivi hiyo safari yako ya Mwanza na Musoma ina umuhimu kuliko:

1. Wagonjwa waliokwama kusafirishwa kwenda mikoani ktk hospitali za rufaa kwa ajili ya matibabu?

2. Walimu waliongojea ajila kwa miaka 3 juzi zimetoka wanatakiwa kureport vituo vyao vya kazi wamekwamia stand baada ya kuangaika uku na kule kukopa nauli kwa ndugu jamaa na marafiki sasa wameishia kituo cha madaladala hawajui kinachoendelea?

3. Wafanya kazi wanaotakiwa kwenda kuwahudumia watanzania ili kuweza kulipa kodi na kujikimu kimaisha?

4. Dawa na bidhaa zote zinazoitajika kufikishwa kwa watanzania ila zimekwama kwa kukosa huduma ya usafiri kwa siku ya pili mfululizo?

5. Walimu, madaktali ambao jana na leo wameshindwa kufika ktk vituo vyao vya kazi ili kuwahudumia watu?

6. Wafiwa waliokosa kusafiri kwenda kuwaaga wapendwa wao na kuwasindikiza japo kwa mara ya mwisho.

7. Wanafunzi wa kidato cha wanaofanya mitihani yao ya mwisho wanaochelewa kuingia katika vyumba vya mtihani kutokana na kukosa usafiri wa kuwapeleka shuleni

Ni wazi kuwa Pinda anamuhuju JK pasipo na shaka yeyote ile.

Tatizo halikuishia hapo! Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta naye pia aliendelea kukoleza moto wa mgomo kwa madereva ambao walimuona kupitia taarifa ya habari ya ITV kwa kuwasimanga na kuwatukana madereva kwa kuwaambia si wasikivu, majehuri na hawana maana kabisa. Lahaula!!

"Madereva siyo wasikivu na majehuri. Hii ni serikali umeitwa na Waziri mkuu unapuuza kisha unaendelwza mgomo hiki ni kiburi kwa hawa madereva kwani Serikali ina uwezo wa kuwanyang'anya leseni zao maana zinatolewa na Serikali" alisema Sitta.

Kauli ile iliwachukiza na kuwashanga madereva wengi kwani wao ndio waliokuwa wakitaka kuzungumza na waziri mkuu Pinda lakini Sitta alikuwa akiwakataza kukutana nao na leo hii anajibaraguza machoni kwa watu.

Kauli ile ya Sitta ilizaa msimamo wa kuendeleza mgomo wa madereva mpaka tume itakapoleta ripoti yake.

Wananchi wanazidi kuteseka, Taifa linazidi kupata madhara ya mgomo huo, yote hayo ni kwa sababu ya kauli ya Sitta ambaye siku zote amekuwa mstari wa mbele kumuhujumu JK kutokana na machungu aliyonayo ya kunyimwa Uwaziri mkuu.

Hizi hujuma za waziwazi ambazo zinafanywa na Pinda na Sitta kwa JK hazipaswi kuchekewa kwani zinatuletea athari kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
 
Jana nimemsikiliza, kiukweli Sitta ameonyesha ukosefu wa hali ya juu kabisa wa busara!. Taifa liko kwenye stand still, badala ya kutumia wisdom ya humility na sympathy, yeye ndio kwanza anazidisha threats na arrogance ya hali ya juu!.

Poor Sitta, ndio maana tangu mwanzo tulishauri kwa 2015, hatufai kabisa!. Angekuwepo Mwamba wa Kaskazi, huu mgomo wala usingetokea, ungeisha kuwa diffused zamani hata kabla haujatokea.

Pasco
 
Shida ya Sitta ni hiyo' amechoka sana'
yuko 'exhausted ' na anaonekana hataki kabisa kuwa disturbed...

sasa kwa kua anaamini kuna 'mkono wa mtu' which may be true ndo anazidi kuboronga kwa kutoa vitisho
wakati angeenda yeye mwenyewe tu kuongea nao.....
 
Kama huyu mnayesema anahujumiwa naye kashindwa Kuchukua hatua kwa anayemhujumu maana yake naye anawahujumu RAIA waliompa dhamana hiyo ya kuchukua hatua stahili
Jambo hili ni pana sana na athari zake ni kubwa sana kuliko hizi tuzionazo kwa macho. Ukweli ni kuwa mfumo wa utawala wetu uko exhausted kabisa na ni kwa neema ya MUNGU tuu kuwa kwa wakati kama huu anatuepusha na majanga makubwa.
Hebu tufikiri kidogo, jee likitokea janga kama LA Nepal hapa kwetu tunaweza kukabikiana nalo kwa serikali yenye utendaji kama huu?
 
Achana na habari ya nepali hili lililotokea la mgomo wa madereva lilijulikana litatokea,sasa suala la majanga ya kidunia hata kama unajua linaweza tokea huwezi jua mwaka wala siku.sita uwezo wake ni mdogo,yeye anawaza bandari na treni anafikiri haya mengine haya muhusu.
 
Jana nimemsikiliza, kiukweli Sitta ameonyesha ukosefu wa hali ya juu kabisa wa busara!. Taifa liko kwenye stand still, badala ya kutumia wisdom ya humility na sympathy, yeye ndio kwanza anazidisha threats na arrogance ya hali ya juu!.

Poor Sitta, ndio maana tangu mwanzo tulishauri kwa 2015, hatufai kabisa!. Angekuwepo Mwamba wa Kaskazi, huu mgomo wala usingetokea, ungeisha kuwa diffused zamani hata kabla haujatokea.

Pasco
ni kweli hiki kitu kipo? ukosefu wa busara kichwani (ubk)- ni ugonjwa au?
 
Jana nimemsikiliza, kiukweli Sitta ameonyesha ukosefu wa hali ya juu kabisa wa busara!. Taifa liko kwenye stand still, badala ya kutumia wisdom ya humility na sympathy, yeye ndio kwanza anazidisha threats na arrogance ya hali ya juu!.

Poor Sitta, ndio maana tangu mwanzo tulishauri kwa 2015, hatufai kabisa!. Angekuwepo Mwamba wa Kaskazi, huu mgomo wala usingetokea, ungeisha kuwa diffused zamani hata kabla haujatokea.

Pasco
Sitta ni mtu mwenye kiburi, majivuno, ubabe na asiyejali. Ni mtu mwepesi sana wa kupuuza hoja na malalamiko na hata vilio vya watu wengine kwa sababu ambazo si za kisomi wala wala hazina maslahi kwa wananchi. Anaweza kufanya jambo kwa sababu tu amejisikia kufanya. Kiujumla hana kabisa uwezo wa kiuongozi zaidi ya ubabe.
 
Achana na habari ya nepali hili lililotokea la mgomo wa madereva lilijulikana litatokea,sasa suala la majanga ya kidunia hata kama unajua linaweza tokea huwezi jua mwaka wala siku.sita uwezo wake ni mdogo,yeye anawaza bandari na treni anafikiri haya mengine haya muhusu.
Hata suala la trani ameshindwa kulitumia kwa busara. Tungetegemea jana abadilishe ratiba ya trani ili isafirishe watu kama hali ya dharura lakini amekaa tu anang'aa macho, hafikirii hata moja la kufanya ili kuiokoa hali ya nchi. Jamaa ni choka mbaya kwa kweli.
 
Kama huyu mnayesema anahujumiwa naye kashindwa Kuchukua hatua kwa anayemhujumu maana yake naye anawahujumu RAIA waliompa dhamana hiyo ya kuchukua hatua stahili
Jambo hili ni pana sana na athari zake ni kubwa sana kuliko hizi tuzionazo kwa macho. Ukweli ni kuwa mfumo wa utawala wetu uko exhausted kabisa na ni kwa neema ya MUNGU tuu kuwa kwa wakati kama huu anatuepusha na majanga makubwa.
Hebu tufikiri kidogo, jee likitokea janga kama LA Nepal hapa kwetu tunaweza kukabikiana nalo kwa serikali yenye utendaji kama huu?
Hili nalo neno Chakaza. Nafikiri mhujumiwa naye ni mhujumu aliyezoea kuhujumu wapiga kura wake. Sasa huyo hatuna haja naye tena, maana yeye tangu mwanzo ilishafahamika kwamba anahujumu kwa kuwa ni dhaifu. Lakini huyu Sitta uwezo anao lakini ni mpuuzi tu.
 
Last edited by a moderator:
Jana nimemsikiliza, kiukweli Sitta ameonyesha ukosefu wa hali ya juu kabisa wa busara!. Taifa liko kwenye stand still, badala ya kutumia wisdom ya humility na sympathy, yeye ndio kwanza anazidisha threats na arrogance ya hali ya juu!.

Poor Sitta, ndio maana tangu mwanzo tulishauri kwa 2015, hatufai kabisa!. Angekuwepo Mwamba wa Kaskazi, huu mgomo wala usingetokea, ungeisha kuwa diffused zamani hata kabla haujatokea.

Pasco

hahahahaha pasco wa LOWASA.
 
Team Lowasa mnakazi sana!! hizi sio zama za CCM tena ndugu.
 
Back
Top Bottom